HABARI

 

Wednesday, September 11, 2013

DIWANI TLP: SIASA SI UADUI

0 Comments

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na diwani wa TLP Ntabo Majabi kata ya MwendaKulima wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha afya kilichodhaminiwa na mgodi wa Buzwagi kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.


DIWANI wa Kata Mwendakulima Ntabo Majabi kupitia Tanzania Labour Party (TLP), amesema Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana ni kiongozi mwenye busara na hekima kubwa na ndio maana Rais Jakaya Kikwete amemua kumpa nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa anamjua vizuri.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha afya katika eneo hilo, alisema amefurahishwa na aina ya siasa ambazo zinafanywa na Kinana na yeye binafsi ametambua kuwa Katibu Mkuu huyo wa CCM anaouwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.

“Kinana wewe ni jembe, wakati unazungumza nilikuwa nimekaa mbali na kusikiliza lakini maelezo yako yamenifurahisha na ndio maana nimeamua kuja kukupa mkono.Kama nchi hii ingekuwa na makatibu wakuu wengi wa aina yako, tungepiga hatua hasa katika siasa za nchi hii.

“Pia niwaambie wananchi siasa si ugomvi, Kinana ameeleza vizuri, tunatakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya kuwatumikia wananchi.Nakupongeza mzee Kinana kwa maelezo yako yamenipa faraja licha ya kwamba mimi ni diwani kupitia TLP,”alisema.
Ndugu Kinana alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa CCM ndio yenye Serikali na diwani huyo licha ya kuwa TLP bado anatekeleza ilani ya CCM , hivyo wananchi nao wanatakiwa kutambua hakuna sababu ya kulumbana kwasababu tu ya mambo ya siasa.

0 Comments:

Post a Comment