Hivi Punde!

MBIO ZA BENDERA YA CCM ZAZINDULIWA IRINGA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa eneo la Ruaha Buyuni waliokuja kumpokea tayari kwa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
 Kinamama kutoka mkoa wa Iringa wakicheza ngoma ya kihehe wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
 Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia salaam walizokuwa wanapewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akisalimia wakazi wa Ruaha Buyuni wakati wa uzinduzi wa  wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa
 Wananchi akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa chama waliofika wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa.
 Viongozi wa Chama mkoani iringa wakifuatilia ratiba ya matukio mbali mbali yaliyopangwa wakati wa uzinduzi wa mbio za Bendera ya Chama Mkoani Iringa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifungua Bendera ya Chama tayari kwa kuanza kwa mbio za Bendera ya Chama .
 Vijana wakakamavu wa chama wakiwa wamebeba picha ya Mwenyekiti wa Chama ambayo itakimbizwa sanjali na Bendera ya Chama katika mkoa wa Iringa.

 Bendera na Picha ya Mwenyekiti ambazo lengo ni kuwakumbusha wana CCM kukilinda na kukitetea chama ikiwa pamoja na kuwaeleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa ndugu Emmanuel Mteming'ombe akitoa salaam za utangulizi wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa Ruaha Mbuyuni wakati wa uzinduzi wa mbio za Bendera ya chama mkoani hapo

 Katibu wa NEC Itikad na Uenezi akihutubia wakati wa Iringa ambapo aliwaambia mbio hizo zitawasaidia wakazi wa mkoa huo kuelewa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, kukilinda na kujenga chama.
 Katibu wa NEC akikabidhi mpira kwa moja ya timu zilizofanya vizuri.
 Katibu wa NEC akikabidhi vyeti vya kutambua mchango wa mabalozi wa nyumba kumi .

Bendera ya Chama ikiwa juu kama ishara ya kuwa mbio za Bendera zimeshaanza.Na Mpigapicha Maalum)

No comments