HABARI

 

Monday, August 19, 2013

BARAZA LA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LAKUTANA

0 Comments
Baadhi ya wawezeshaji wakijadiliana jambo katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Baadhi ya washiriki wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Mmoja wa washiriki wa warsha katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba akijadili jambo Warsha ya wajumbw wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba ikiendelea [/caption] BARAZA la Mtandao wa Wanawake limekutana lililoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali limekutana kwa siku mbili kujadili masuala ikiwemo namna ya ushiriki wa wanawake katika mabaraza yanayojadili rasimu ya Katiba Mpya. Kwa mujibu wa vyanzo wa habari hizi washiriki hao walikutana kwa siku mbili, yaani Agosti 16 na 17 mwaka huu Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe wa warsha hiyo ni pamoja na Mchakato wa Katiba Mpya na Ushiriki wa Wanawake katika Hatua mbalimbali, ikiwemo uchambuzi wa rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Diana Kidala wa Jukwaa la Katiba na mada ya Umuhimu wa Kuwepo kwa Sauti za Wanawake katika Katiba Mpya iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya. Mada zingine zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe hao ni pamoja na Uwasilishaji wa Masuala Muhimu ya Kijinsia yaliyojitokeza katika rasimu ya Katiba Mpya ya Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi na ile ya Masuala Muhimu ya Wanawake ya Kuiimarishwa na Kuingizwa katika Katiba Mpya iliyowasilishwa na Vicky Lihiru kutoka ULINGO. Pamoja na mambo mengine pia wajumbe hao walijenga mikakati ya pamoja kuendeleza ushiriki wa mtandao katika hatua zinazofuata kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya yenye mrengo wa usawa wa jinsia nchini. Baraza hilo la wajumbe lilifungwa na Bi. Betty Minde kutoka KWIECO. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

0 Comments:

Post a Comment