Hivi Punde!

ZIARA YA KINANA SIMIYU, AONYESHA MFANO WA VIONGOZI KUJICHANGANYA NA WANANCHI


  • ASEMA CCM HAITAKUBALI KUBURUZWA
  • ASEMA CHADEMA NI MANENO TU, HAICHANGII CHOPCHOTE KATIKA MAENDELEO
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari  wa shina namba 12 tawi la Isenge kata ya Dutwa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakichimba msingi wa ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari wa shina namba 12 Tawi la Isenge kata ya Dutwa.
 Balozi Joyce Safari wa shina namba 12 tawi la Isenge kata ya Dutwa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye shina lake.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amekaa pamoja na wakazi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa tawi la Isenge baada ya kutembelea shina namba 12 kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa juu ya umuhimu wa ushirikiano na mshikamano kwa wananchi na wanachama wa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge wakila chakula cha Asili aina ya Michembe pamoja na Balozi Joyce Safari wa Shina namba 12 kata ya Dutwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimimina maharage kwenye wali uliokuwa kwenye tayari kula na wananchi pamoja na viongozi wengine.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila pamoja na wananchi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa baada ya kushiriki nao ubebaji wa matofali na uchimbaji wa msingi wa nyumba ya Balozi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akipokea taarifa ya soko la mazao ya kilimo na mifugo la Igaganulwa kata ya Dutwa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na mmoja wa wafanya biashara katika soko la Igaganulwa kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia samaki aina ya furu katika soko la Igaganulwa alipokuwa ziarani wilaya ya Bariadi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi na wafanya biashara katika soko la Igaganulwa kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi ambapo aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kushirikiana na viongozi wao katika kutatua matatizo yao na kupanga kuleta maendeleo na kujiepusha na wanasiasa ambao mtaji wao ni maneno na si mipango ya maendeleo.

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman KInana akishiriki katika ujenzi wa Madarasa ya shule ya sekondari ya MAlambo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
 Kikundi cha Ngoma cha Maisha Furaha Group kikitumbuiza kwa ngoma ya Bugobogo katika viwanja vya sabasaba wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alihutubia.

 Mbunge wa Bariadi Ndugu Andrew Chenge akihutubia wakazi wa Bariadi wakati wa mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya sabasaba wilayani hapo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani pamoja na Mbunge wa Bariadi Ndugu Andrew Chenge wakiwasalimu wakazi Bariadi waliofurika kwenye viwanja vya sabasaba wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Bariadi na kuwaambia CCM imejipanga kutekeleza ahadi zake zaidi kuliko malumbano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Bariadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba .
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuwasha pikipiki moja kati ya pikipiki tano ambazo walikabidhiwa vijana wa Bodaboda mjini hapo. PICHA NA ADAM MZEE

No comments