Hivi Punde!

ILANI YA CCM 2015-2020

UMOJA NI USHINDI
Y A L I Y O M O
Utangulizi …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…. i
SURA YA KWANZA …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..….. 1
Hali ya Uchumi Mwaka 2010-2015 na Malengo ya Mwaka 2015-
2020...................................................................................................... 1
SURA YA PILI …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..… 6
Mafanikio na Malengo ya Sekta za Uzalishaji Mali...................... 6
SURA YA TATU…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…. 35
Sekta za Miundombinu na Huduma za Kiuchumi..................... 35
SURA YA NNE …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…. 81
Sekta ya Huduma za Jamii............................................................. 81
SURA YA TANO …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..… 110
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi................................................. 110
SURA YA SITA …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…. 119
Mazingatio Maalumu ya Ilani Kuhusu Zanzibar...................... 119
SURA YA SABA…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…. 204
Maeneo Mengine Muhimu........................................................... 204
SURA YA NANE …..…..…..…..…..…..…..…..…..…..…..… 229
Chama Cha Mapinduzi................................................................. 229

i
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI
MKUU WA MWAKA 2015
Utangulizi
1. Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili
ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wa kuwachagua Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar,
Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani
imeandaliwa ikiwa ni mkataba kati ya CCM na wananchi.
Ilani hii imeandikwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya 2025 na Mwelekeo wa Sera za CCM zenye lengo na
nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020).
2. Ilani hii ni tamko maalumu kwa wapiga kura kuhusu
nia ya CCM ya kuendelea kushika dola na kuwaongoza
Watanzania kwa njia ya kidemokrasia, na hasa kuendelea
kudumisha amani, umoja wa Kitaifa, usawa, ustawi wa
wananchi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kipindi kingine cha
miaka mitano.
3. Nia na uwezo wa CCM wa kuendelea kuongoza Taifa hili
unajidhihirisha katika uzoefu ambao tumeupata kwa miaka
38 tangu kuanzishwa kwake na kuwa madarakani, ambapo
katika kipindi chote hiki kimeiwezesha nchi yetu kupata
mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na
kijamii.
4. Katika miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM ikiwa
madarakani, itazielekeza Serikali zake kutumia nguvu
zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa
nne:- Kwanza kuondoa umaskini; pili kupunguza tatizo
la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; tatu kuendeleza vita
dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na
nne kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa
maisha ya wananchi na mali zao.
ii
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kupambana na Umasikini
5. Pamoja na mafanikio ya kukua kwa uchumi na ongezeko la
huduma za kijamii yaliyopatikana katika kipindi hiki, bado
ipo changamoto kubwa ya umasikini wa kipato na usio
wa kipato. Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 28.2 ya
Watanzania ni masikini. Wengi wa wananchi hao wanaishi
vijijini (asilimia 75) na wanategemea kilimo katika maisha
yao. Wapo pia wananchi masikini wanaoishi mijini ambao
wanaendesha maisha yao kupitia shughuli za biashara
ndogo ndogo zisizo rasmi.
6. Katika kupambana na changamoto hii, CCM itazielekeza
Serikali zake kuboresha maisha ya wananchi wote na
hususan wa vijijini, kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuhamasisha kilimo kupitia kauli mbiu ya Kilimo
Kwanza kwa kuwawezesha wakulima kupata
mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za
kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za
kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao;
(b) Kuongeza kasi ya kupima ardhi yao na kuwapatia hati
miliki za kimila ambazo watazitumia kama dhamana
ya kuwawezesha kupata mikopo ya kuendeleza
shughuli zao za kilimo, ufugaji na uvuvi;
(c) Kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma za kijamii
ikiwemo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa
nyumba bora; na
(d) Kuongeza kasi ya kurasimisha biashara na kuwapatia
wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia
biashara, leseni na fursa za kupata mikopo yenye
masharti nafuu.
7. Mafanikio ya utekelezaji wa masuala haya yote kwa pamoja
yanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo
mijini na vijinini, na hivyo kupunguza kwa kiwango
kikubwa hali ya umasikini nchini.
iii
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Ajira kwa Vijana
8. Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya changamoto
zinazolikabili Taifa letu na dunia yote kwa ujumla. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita yapo mafanikio
yaliyopatikana katika kuongeza ajira. Hata hivyo,
mafanikio katika upanuzi wa elimu ya Sekondari na Vyuo
yameongeza mahitaji ya ajira ya vijana wasomi kila mwaka
ikilinganishwa na nafasi zinazokuwepo.
9. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo jitihada za kulipatia
ufumbuzi tatizo la ajira nchini zitaendelezwa. Kipaumbele
kitakuwa katika kukuza na kuanzisha viwanda vidogo, vya
kati na vikubwa vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi
na vyenye kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi
wa ndani ya nchi na zile za kuuza nchi za nje. Aidha, kwa
upande wa Tanzania Zanzibar, mikakati ya kuongeza ajira
kwa vijana itazingatia mazingira maalamu ya fursa za
uchumi wa visiwa.
10. Katika kipindi cha 2015-2020, sekta za uzalishaji mali
kama kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda vikubwa na vidogo
na huduma za kiuchumi kama vile miundombinu ya
nishati, uchukuzi na ujenzi zitaelekeza mipango yao katika
kupunguza umasikini na kuanzisha ajira hususan kwa
vijana. Aidha, huduma za jamii za elimu, afya na maji
zitajielekeza kusaidia kuondoa umasikini na kuongeza
ajira.
Vita dhidi ya Rushwa
11. Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii
hazitaleta manufaa kwa wananchi na kuondoa umasikini
iwapo adui rushwa ataendelea kulitafuna Taifa letu.
Rushwa ni adui wa haki pia ni adui wa maendeleo na
ustawi wa wananchi, hivyo ni moja ya changamoto kubwa
inayoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla.
12. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza
Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa
kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya
iv
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za
haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa
Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na
taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa;
ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa
ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
13. Sambamba na kupambana na tatizo la rushwa, Serikali
pia zitatakiwa kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la
ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya
madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi
wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi
kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza
masuala yenye maslahi kwa umma.
Ulinzi na Usalama
14. Nchi yetu imepata mafanikio makubwa ya kuwa na amani
na utulivu tangu tupate uhuru mwaka 1961 na Mapinduzi
ya Zanzibar ya mwaka 1964. Imekuwa kimbilio la watu
wa Mataifa ya jirani kila wapatapo matatizo ya uvunjifu
wa amani katika nchi zao. Hata hivyo, siku za karibuni
vimeanza kuonekana viashiria vinavyoleta hofu ya usalama
wa wananchi, hasa vitendo vya mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi (Albino), kuuawa kwa vikongwe, ukatili
dhidi ya wanawake na watoto na tishio la vitendo vyenye
mwelekeo wa kigaidi.
15. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza
Serikali zake kuendelea kuimarisha vyombo vyote vya
ulinzi na usalama kwa kuviongezea raslimali fedha,
raslimali watu, maslahi, zana za kisasa na mafunzo. Aidha,
elimu kwa umma itatolewa ili kukomesha imani potofu za
kishirikina zinazosababisha mauaji ya albino na vikongwe
na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale
wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya mauaji ya
makundi hayo.
v
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Utekelezaji wa Ilani
16. Kazi kubwa ya Serikali za CCM katika kipindi cha miaka
mitano ijayo itakuwa ni kuendeleza mapambano dhidi ya
umasikini, ukosefu wa ajira, rushwa; na kudumisha umoja,
amani, ulinzi na usalama. Ili kutimiza azma hiyo, CCM
itazielekeza Serikali zake zisiwe kubwa, zenye watumishi
weledi, waadilifu na wawajibikaji. Serikali zisizo na urasimu
unaokwamisha na kuchelewesha maamuzi na utekelezaji.
Serikali zitakazongeza maradufu au hata zaidi ukusanyaji
wa mapato yake ili zijitegemee kadri inavyowezekana
kwenye bajeti zake.
17. Vile vile katika kipindi cha Ilani hii, Chama Cha Mapinduzi
kitaziagiza Serikali zake kuendeleza na kuimarisha mfumo
wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN na BRP) katika kutekeleza
Ilani na kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati na
kipaumbele unaozingatia nidhamu ya utekelezaji katika
muda uliopangwa, ufuatiliaji makini na wa kina, pamoja na
kupata ufumbuzi wa vikwazo na changamoto za utekelezaji.

1
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA KWANZA
HALI YA UCHUMI - MWAKA 2010 – 2015
NA MALENGO YA MWAKA 2015 – 2020
18. Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010–
2015, ililenga katika kutekeleza kipindi cha kwanza cha
Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010–2020
na kutekelezwa katika kipindi cha pili na cha mwisho cha
Serikali ya Awamu ya Nne chini ya uongozi wa Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Katika kipindi hiki, Serikali imetekeleza kwa mafanikio
makubwa Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya
2010–2020 kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025
na Malengo ya Milenia. Aidha, kutokana na mafanikio
hayo, Serikali imeweza kuendeleza na kuimarisha huduma
za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Hali ya Uchumi
19. Katika kipindi hiki, Serikali imeweza kutekeleza mipango
yake kwa ufanisi mkubwa licha ya changamoto zilizokuwa
zikijitokeza na kuleta mafanikio ya kiuchumi yafuatayo:-
(a) Ukuaji wa Pato la Taifa kwa kipindi cha miaka mitano
iliyopita, umekua kwa wastani wa asilimia 7 kwa
mwaka;
(b) Ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kutoka
wastani wa Shilingi bilioni 390 kwa mwezi mwaka
2010 na kufikia wastani wa Shilingi bilioni 850 kwa
mwezi, mwaka 2014/15;
(c) Misaada na mikopo ya Washirika wa Maendeleo
kwenye bajeti ya Serikali imepungua kutoka asilimia
42 mwaka 2005 hadi asilimia 8 mwaka 2015/2016;
2
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Mapato ya kodi yameongezeka kutoka Shilingi trilioni
5.74 mwaka 2010/11 na kufikia shilingi trilioni 7.42
mwaka 2014/15;
(e) Mfumko wa bei umeendelea kubakia tarakimu moja
(single digit) na umepungua kutoka wastani wa
asilimia 19.8 Desemba, 2011 hadi kufikia asilimia 4.8
Desemba, 2014 na asilimia 4.3 Machi, 2015.
(f) Bajeti ya Serikali imeongezeka kutoka Shilingi trilioni
4.18 mwaka 2010/2011 hadi Shilingi trilioni 22.49
mwaka 2015/2016; na
(g) Wastani wa pato kwa kila mwananchi limeongezeka
kutoka Shilingi 770,000 mwaka 2010 hadi wastani wa
Shilingi 1,675,232 mwaka 2014.
20. Sekta ya Fedha ndio kipimo kinachoweza kuonesha
viwango vya uchumi wa nchi vilivyofikiwa katika vigezo
mbalimbali kama vile Pato la Taifa, Ukuaji wa Uchumi na
Mfumko wa Bei. Maendeleo ya haraka katika nyanja hizo
yatategemea uimara na uwezeshaji wa sekta ya fedha.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii 2015-2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kutekeleza
yafuatayo na kuhakikisha kwamba:-
(a) Uchumi unaendelea kukua kwa kasi ya wastani wa
asilimia 8 au zaidi na kuinua ustawi wa Watanzania
kwa kuongeza mapato ya wananchi kufikia kiwango
cha wastani wa nchi ya uchumi wa kati na hivyo,
kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini; na
(b) Kunakuwepo utulivu wa uchumi jumla ambao ni
endelevu (sustainable macroeconomic stability) kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kudhibiti mfumko wa bei ili uendelee kubaki
kwenye tarakimu moja na hivyo kuzuia kasi ya
kupanda kwa gharama za maisha;
3
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kudhibiti nakisi ya bajeti ili iendelee kushuka na
kufikia kiwango kisichozidi asilimia 3 ya Pato la
Taifa ili pamoja na mambo mengine, Tanzania
iendelee kuwa kivutio kwa wawekezaji na
kupunguza gharama za kukopa kwa ajili ya
maendeleo ya nchi yetu;
(iii) Kusimamia Deni la Taifa liendelee kuwa himilivu
ili lisiwe mzigo kwa uchumi wetu bali liendelee
kuwa fursa na kichocheo cha maendeleo ya nchi
yetu;
(iv) Kuhakikisha thamani ya Shilingi yetu
inatengamaa ili kujenga imani ya uchumi wetu
kwa lengo la kuongeza shughuli za uwekezaji,
uzalishaji na biashara;
(v) Kuongeza mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi,
kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na
kuepuka kuagiza bidhaa zisizo za lazima kutoka
nje ya nchi; na
(vi) Kuendelea kuwa na mikakati itakayowezesha
kuwa na akiba ya fedha za kigeni zinazotosheleza
kuagiza bidhaa na huduma nje bila ya matatizo.
(c) Kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuongeza
vyanzo vipya vya mapato na kupanua wigo wa walipa
kodi ili kuongeza uwezo wa Serikali wa kugharimia
huduma za kijamii na kiuchumi;
(d) Kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma
kwa kuzingatia sheria na miongozo ya ununuzi wa
umma, ukaguzi na kusimamia mali za Serikali ili
Watanzania wote wanufaike na rasilimali zilizopo; na
(e) Kuimarisha Sekta ya Fedha kwa kuhakikisha wananchi
wananufaika kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuendelea kupanua huduma za fedha hadi
vijijini kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi;
4
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kuhamasisha wananchi wajiunge na huduma
za Bima ya Afya, Bima ya Maisha na Mifuko ya
Hifadhi za Jamii ili kujihakikishia kinga dhidi
ya majanga na maisha ya uzeeni na baada ya
kustaafu; na
(iii) Kuweka mazingira yatakayowezesha kushuka
kwa riba ya mikopo katika Taasisi za Fedha ili
kutoa fursa kwa wananchi kupata mikopo ya
muda mfupi na mrefu kwa riba nafuu.
(f) Kutekeleza Sera na Sheria za kusimamia mapato
yanayotokana na gesi asilia na mafuta ili kuhakikisha
fedha zinatumika kwa manufaa ya Wananchi wa
kizazi hiki na kijacho;
(g) Kuwawezesha wananchi kumiliki na kuwekeza
kwenye soko la mitaji na dhamana kwa:-
(i) Kuongeza ufanisi wa shughuli za minada kwa
njia ya simu na mtandao wa intaneti;
(ii) Kuelimisha umma kuhusu fursa za kujiongezea
kipato kupitia masoko ya mitaji na uwekezaji;
na
(iii) Kuendelea kutoa fursa kwa wajasiriamali
wadogo na wa kati ili waweze kunufaika na Soko
la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kupitia dirisha
maalumu la kukuza na kuimarisha masoko ya
wajasiriamali wadogo na wa kati.
(h) Kuboresha mfumo wa kifedha kati ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa manufaa ya pande
zote mbili za Muungano kwa kutekeleza yafuatayo:-
(i) Kuimarisha asasi zinazohusika na masuala ya
uhusiano wa kifedha kati ya SMT na SMZ;
5
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti
ya Fedha ya pamoja ili kuzidi kuimarisha
mshikamano na maelewano; na
(iii) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweka
utaratibu wa kuoanisha viwango vya kodi
ya forodha kati ya pande mbili za Jamhuri ya
Muungano.
6
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA PILI
MAFANIKIO NA MALENGO YA SEKTA ZA
UZALISHAJI
Kilimo na Ushirika
21. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Chama Cha
Mapinduzi kiliweka kipaumbele cha kuhakikisha kuwa
kilimo nchini kinakuwa endelevu na chenye tija ili
kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula; kuongeza
mapato ya wakulima; kuwa chanzo cha kuaminika cha
malighafi ya sekta ya viwanda; na kuendelea kuwa chanzo
kikuu cha ajira kwa wananchi. Kwa kutekeleza azma hiyo,
mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Bajeti ya Sekta ya kilimo imeongezeka kutoka Shilingi
bilioni 903.8 mwaka 2010/11 hadi Shilingi trilioni 1.08
mwaka 2014/15;
(b) Dirisha la kilimo limeanzishwa katika Benki ya
Rasilimali (TIB) kwa lengo la kutoa mikopo yenye
masharti nafuu kwa wakulima ili waweze kununua
pembejeo na zana za kilimo. Aidha, imeanzishwa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo mahususi kwa ajili ya
kutoa mikopo kwa wakulima;
(c) Katika kuimarisha huduma za ugani, udahili katika
vyuo vya kilimo umeongezeka kutoka wanafunzi
1,246 mwaka 2010/11 hadi 2,500 mwaka 2013/14.
Aidha, idadi ya maafisa ugani katika ngazi ya Vijiji na
Kata imeongezeka kutoka 5,184 mwaka 2010/11 hadi
9,558 mwaka 2013/14;
(d) Uzalishaji na usambazaji wa pembejeo bora za kilimo
umeimarishwa ambapo:-
(i) Uzalishaji wa mbegu bora umeongezeka kutoka
tani 10,477.17 mwaka 2005 hadi tani 32,340
mwaka 2014; usambazaji umeongezeka kutoka
7
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
tani 16,148.2 mwaka 2009/2010 hadi tani 35,352
mwaka 2013/14; na
(ii) Usambazaji wa mbolea umeongezeka kutoka
tani 302,200 mwaka 2009/2010 hadi tani 343,687
mwaka 2013/14.
(e) Matumizi ya matrekta madogo na makubwa
yameongezeka kutoka 11,223 mwaka 2010/11 hadi
16,412 mwaka 2013/14. Ongezeko hili limechangia
kuongozeka kwa eneo linalolimwa kwa matrekta
kutoka asilimia 12 mwaka 2010/11 hadi asilimia 14
mwaka 2013/14;
(f) Ruzuku ya mbolea na pembejeo imeongezeka kutoka
Shilingi bilioni 7.5 mwaka 2005/06 hadi Shilingi
bilioni 299.3 mwaka 2014;
(g) Kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula
kimeendelea kuongezeka kutoka tani milioni 12.83
mwaka 2009/10 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014/15.
Kwa ongezeko hilo Taifa limeweza kujitosheleza kwa
chakula;
(h) Katika juhudi za kuhifadhi mazao kwa ubora
unaostahili, jumla ya maghala 30 yenye uwezo
wa kuhifadhi kati ya tani 5,000 hadi 10,000
yamekarabatiwa. Aidha, ujenzi wa ghala lenye
uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 umekamilika katika
Wilaya ya Songea mwaka 2013/14 chini ya mpango
wa SAGCOT;
(i) Hatua za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo
cha mboga mboga na matunda zimechukuliwa kwa
kujenga Maeneo ya Hifadhi ya Mazao (Packhouse
and refeer container) katika Wilaya za Lushoto na
Korogwe. Aidha, mashine za kusindika na kusafisha
mafuta ya alizeti zimesambazwa kwa vikundi vya
wazalishaji na wasindikaji wadogo katika mikoa
inayolima alizeti nchini;
8
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(j) Mchakato wa kuanzisha Soko la Bidhaa (Commodity
Exchange) umeanza na imetungwa Sheria Na. 15 ya
Mwaka 2015. Soko hilo litamwezesha mkulima kuwa
na uhakika wa kuuza mazao yake na kupata bei nzuri;
(k) Hatua za kuimarisha soko la nafaka zimechukuliwa
kwa kuondoa zuio la kuuza nafaka nje ya nchi;
kuwezesha Wakala wa Taifa wa Chakula kununua
nafaka kutoka kwa wakulima kwa bei ya soko; na
kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi;
(l) Hatua za kuandaa mipango ya matumizi bora ya
ardhi kwa lengo la kuondoa migogoro katika maeneo
mbalimbali nchini zimeendelea kuchukuliwa kwa
kupima na kutoa hati miliki kwa wakulima vijijini; na
kwa wawekezaji wakubwa na wadogo. Jitihada hizo
zimewezesha upimaji wa jumla ya ekari 444,663.2 za
mashamba ya wakulima;
(m) Kilimo cha umwagiliaji kimepewa kipaumbele
kwa kupanua eneo la umwagiliaji ambapo Sheria
ya Umwagiliaji Na. 5 ya mwaka 2013 imetungwa
na kuanzisha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Aidha,
kutokana na utekelezaji wa Sera na Mikakati
mbalimbali, kilimo cha umwagiliaji kimechangia
asilimia 24 ya mahitaji ya chakula nchini; na
(n) Kwa muda mrefu Sekta ya Ushirika ilikabiliwa na
changamoto kadhaa ambazo zilidumaza jitihada za
kuendeleza ushirika. Ili kuondokana na changamoto
hizo, Sheria ya Vyama vya Ushirika ilifanyiwa
mabadiliko na kuanzisha Sheria mpya (Sheria Na. 6
ya mwaka 2013) ambayo imeanzisha Tume Huru ya
Maendeleo ya Ushirika.
9
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kilimo cha Umwagiliaji kinachotumia zana bora kitaongeza
tija kwa wakulima ambao ndio wengi nchini.
22. Katika kipindi cha mwaka 2015 - 2020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kutilia mkazo utekelezaji
wa Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo
(Agricultural Sector Development Programme – ASDP II)
pamoja na miradi ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa
Sasa (BRN) ili kufikia malengo makuu ya kukifanya
kilimo kuwa cha kisasa na cha kibiashara; chenye tija na
ambacho mazao yake yatakuwa yameongezewa thamani.
Lengo ni kuhakikisha kuwa Taifa linajitosheleza kwa
chakula; kuimarisha uchumi; kuongeza kipato cha
wakulima; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na
kuongeza ajira kwa kufanya yafuatayo:-
(a) Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za
kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji kwa kuzingatia
matumizi ya teknolojia ya kisasa hususan katika
kuboresha mifumo ya utoaji wa ruzuku na pembejeo
pamoja na kuwaunganisha wakulima na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo na taasisi nyingine za fedha;
10
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kanuni bora za
kilimo kwa kuongeza idadi ya maafisa ugani kutoka
9,558 waliopo sasa hadi kufikia 15,082 mwaka 2020;
na kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Kilimo na Mifugo
katika kila Kata nchini; na
(c) Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza
utegemezi wa mvua kwa kuongeza eneo la umwagiliaji
kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 hadi 1,000,000
mwaka 2020. Ili kufanikisha hilo, Serikali itafanya
mambo yafuatayo:-
(i) Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuwekeza
katika miundombinu ya umwagiliaji kwa
kujenga mifereji mikuu, mifereji ya kati na
kujenga mabwawa ya kuhifadhia maji kwenye
maeneo yenye ukame;
(ii) Kuhamasisha wakulima kupitia vyama vyao
vya umwagiliaji kuchangia katika ujenzi wa
mifereji midogo ya kuingiza maji mashambani
na kushiriki katika kutunza mifereji hiyo;
(iii) Kuwafundisha kulima kwa tija na ufanisi kwa
kutumia miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja
na kulima zaidi ya mara moja kwa mwaka;
(iv) Kukamilisha ujenzi wa skimu zote za umwagiliaji
zilizoanza kujengwa miaka ya nyuma;
(v) Kujenga, kukarabati na kuboresha skimu za
umwagiliaji za wakulima wadogo na wa kati
ili kuongeza uzalishaji na ufanisi wa matumizi
bora ya rasilimali maji;
(vi) Kujenga na kuimarisha mabwawa ya uvunaji
wa maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji wa
kilimo cha mpunga;
(vii) Kushirikisha sekta binafsi katika uwekezaji na
uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji; na
11
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(viii) Kuijengea uwezo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
ili iongeze kasi ya ujenzi wa miundombinu.
(d) Kuboresha mfumo wa utafiti wa kilimo nchini ili
matokeo ya tafiti hizo yawafikie wakulima kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kugundua na kutathmini aina za mbegu bora za
mazao mbalimbali zenye sifa ya kutoa mavuno
mengi, zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi
na zenye viinilishe vingi;
(ii) Kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali kwa
kushirikiana na taasisi za umma na binafsi ili
kutosheleza mahitaji ya uzalishaji wa mbegu
bora nchini;
(iii) Kutafiti magonjwa na visumbufu vya mimea
vinavyoathiri mazao hasa migomba, mihogo,
minazi, mahindi, mpunga, mboga na matunda
ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao nchini;
(iv) Kuchambua mifumo ya kilimo, kutoa teknolojia
za kurutubisha udongo na matumizi bora ya
mbolea na kuandaa ramani za ikolojia kwa kila
Kanda; na
(v) Kuboresha miundombinu ya utafiti na
kuwajengea uwezo watafiti ili kuongeza ufanisi
wa utafiti nchini.
(e) Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya kilimo
kwa kuendelea kupima mashamba ya wakulima na
kutoa hati miliki za kimila kwa wakulima wadogo
kwa lengo la kuondoa migogoro ya ardhi na kutumia
hati hizo kama dhamana ya kupata mikopo; na
(f) Kuwawezesha wakulima hususan vijana na
wanawake kujishughulisha katika kilimo kwa kufanya
yafuatayo:-
12
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Kuainisha na kupima maeneo ya ardhi ya kilimo
ili kuwawezesha wakulima kujiajiri katika sekta
ya kilimo hususan kilimo cha mazao ya mboga
mboga, matunda, maua, mbegu za mafuta na
nafaka;
(ii) Kuendelea kupima maeneo na kuyapatia hati
miliki ili kuwawezesha wakulima kushiriki
katika kuyaendeleza maeneo hayo kwa kutumia
hati miliki kama dhamana ya kupata mikopo
kutoka katika taasisi za fedha;
(iii) Kuwaunganisha wakulima (Vijana na
wanawake) na asasi za fedha kwa ajili ya kupata
mikopo ya pembejeo, zana bora na mashine za
usindikaji kupitia vyama vyao vya ushirika na
vikundi vya uzalishaji mali; na
(iv) Kuimarisha matumizi ya teknolojia
zitakazorahisisha kazi ili kuwapunguzia harubu
wanawake na vijana katika kilimo.
(g) Kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya
Kilimo kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kushirikisha sekta binafsi kujenga miundombinu
ya masoko na maghala bora ya kuhifadhia
mazao mbalimbali hususan vijijini kwa kutoa
elimu na kuondoa vikwazo vya utaratibu wa
Stakabadhi ya Mazao Ghalani;
(ii) Kuanzisha Soko la Bidhaa kwa mujibu wa Sheria
ya Soko la Bidhaa (Commodity Exchange Act)
Namba 15 ya mwaka 2015;
(iii) Kujenga masoko ya kimkakati katika maeneo ya
mipaka ya nchi ili kuwapa wakulima fursa ya
kuuza mazao yao nje ya nchi;
(iv) Kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya
ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya
13
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka
mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi
na uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu
juu ya uongezaji thamani na biashara.
(h) Kuhamasisha sekta binafsi na vyama vya ushirika
wa mazao kuanzisha viwanda vya kusindika mazao
ya kilimo hususan kwenye maeneo ya uzalishaji
wa mazao hayo kwa lengo la kuongeza thamani na
kuongeza ajira. Aidha, kuwawezesha wakulima
kupata majokofu ili kuhifadhi matunda na mazao
ya mboga mboga yanayoharibika haraka pamoja na
vifungashio.
Mifugo na Uvuvi
23. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya Mifugo
na Uvuvi imeimarishwa ili kuwaongezea wafugaji na
wavuvi kipato pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.
Mifugo
24. Katika kipindi hicho, Sekta ya Mifugo imepata mafanikio
yafuatayo:-
(a) Mashamba matano yenye uwezo wa kuzalisha
mitamba 5,000 kwa mwaka yameanzishwa. Aidha,
Kituo cha Uhamilishaji cha NAIC kilichopo Arusha
kimeimarishwa na kinazalisha mbegu bora za mifugo.
Vituo vipya vya Uhamilishaji vimeanzishwa katika
Mikoa ya Pwani, Dodoma, Mbeya, Katavi, Lindi na
Mwanza. Sekta binafsi imezalisha mitamba 10,000
mwaka 2013/14 na kusambazwa kwa wafugaji;
(b) Ruzuku ya dawa za kuogeshea mifugo imetolewa
ambapo lita 252,138 za dawa zenye thamani ya
Shilingi bilioni 4.2 zimenunuliwa na kusambazwa
katika Mikoa yote nchini;
(c) Ujenzi na ukarabati wa Vyuo vya Mifugo vya Mabuki,
Kikulula na Rorya umefanyika na kuwezesha mafunzo
14
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kwa wafugaji 2,000 pamoja na kutoa mafunzo kwa
Maafisa Mifugo 2,000 katika ngazi ya Astashahada na
Stashahada;
(d) Dozi milioni 7.1 za Chanjo ya Homa ya Mapafu ya
Ng’ombe, dozi 900 za chanjo ya Homa ya Bonde la
Ufa (RVF) na dozi milioni 12.8 za chanjo ya Sotoka
zimenunuliwa na kusambazwa katika mikoa
mbalimbali nchini;
(e) Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC)
kimefunguliwa huko Sumbawanga kwa ajili ya
kuhudumia Eneo Huru la Magonjwa; na
(f) Jumla ya wataalamu 900 wamesajiliwa ikiwa ni
pamoja na kusajili vituo vya kutolea huduma za
mifugo. Aidha, leseni 290 za Wakaguzi wa Nyama,
Wahamilishaji na Watalaamu wa Maabara za Mifugo
zimetolewa.
Ufugaji bora wenye tija kwa wafugaji ambao pia hupunguza
uharibifu wa mazingira.
15
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
25. Katika kipindi cha Ilani hii ya 2015-2020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali yake kuiendeleza Sekta ya
Mifugo kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuongeza uzalishaji wa mitamba kwenye mashamba
inakozalishwa na kuweka mazingira wezeshi kwa
Sekta Binafsi kuendelea kuzalisha mitamba ili
kuhamasisha ufugaji wa kisasa;
(b) Kutenga, kupima na kumilikisha wafugaji maeneo
ya ufugaji nchini ili kuongeza maeneo ya ufugaji
yaliyopimwa kutoka hekta milioni 1.4 za sasa hadi
hekta milioni 5.0 mwaka 2020;
(c) Kujenga miundombinu ya mifugo kwa kuongeza
idadi ya malambo kutoka 1,378 yaliyopo sasa hadi
2,000; na kujenga mabwawa katika mikoa yenye
mifugo mingi. Aidha, vitajengwa visima virefu 300,
majosho 50 na kuanzisha minada 164 ya mifugo katika
maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili ya ufugaji ili
kuzuia kuhamahama kwa wafugaji kunakosababisha
migogoro;
(d) Kutoa dhamana kwa vikundi vya wafugaji ili kupata
mikopo kwenye asasi za fedha, hususan vijana na
wanawake watakaokuwa kwenye vyama vya ushirika
vya ufugaji wa ng’ombe, kuku, mbuzi na uzalishaji
malisho pamoja na usindikaji wa mazao ya mifugo
(nyama, maziwa na ngozi);
(e) Kuanzisha mashamba darasa ya malisho katika kila
Halmashauri ya Wilaya ili wafugaji wa asili wajifunze
jinsi ya kuboresha na kuhifadhi malisho (feed banks)
hususan wakati wa kiangazi na ukame;
(f) Kueneza ufugaji wa mifugo bora kupitia mikopo ya
mifugo kwa wafugaji watakaojiunga katika vikundi
kupitia miradi ya kopa ng’ombe/mbuzi lipa ng’ombe/
mbuzi au kopa ng’ombe/mbuzi lipa maziwa;
16
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji wanaomiliki na
watakaomilikishwa ardhi ili kutumia hati zao kama
dhamana ya kupata mikopo kutoka asasi za fedha;
(h) Kuendelea kutoa elimu kuhusu matumizi ya
teknolojia ya uhamilishaji katika kuboresha koosafu
za mifugo nchini kwa kutoa huduma za uhamilishaji
kwa wafugaji kwa gharama nafuu kupitia ruzuku
itakayowekwa katika mbegu za uhamilishaji;
(i) Kuboresha huduma za uhamilishaji kwa kuimarisha
vituo vya uhamilishaji vya Taifa vya NAIC- Usa River
(Arusha) na Sao Hill (Iringa); na vituo vya Kanda vya
Kibaha (Mashariki), Lindi (Kusini), Mbeya (Nyanda
za Juu Kusini), Dodoma (Kati), Mwanza (Ziwa) na
Mpanda (Kusini Magharibi) ili kusogeza karibu
huduma ya uhamilishaji kwa wafugaji na kujenga
vituo vipya vya uhamilishaji vya Kanda vya Tabora
(Magharibi) na Tanga (Mashariki);
(j) Kuendelea kukuza na kuendeleza masoko ya mifugo
na mazao yake yanayozalishwa na wafugaji na
kujenga viwanda viwili (2) vya ngozi katika mikoa ya
Singida na Dodoma;
(k) Kuendelea kutoa ruzuku ya dawa za kuogesha mifugo
kiasi cha lita milioni 1.0 ili kuhakikisha kuwa majosho
2,428 yaliyopo nchini yanatumika kudhibiti kupe na
magonjwa wayaenezayo hususan ugonjwa hatari wa
Ndigana kali. Aidha, Serikali itatoa ruzuku ya Chanjo
ya Ndigana kali (ECF) na kushirikisha sekta binafsi
na wadau wengine kufufua majosho 150 na kujenga
majosho mapya 200 katika mikoa yenye mifugo mingi;
(l) Kuendelea kununua na kutoa chanjo za magonjwa ya
mlipuko yanayoathiri afya ya mifugo na binadamu
na kuwezesha biashara ya mifugo katika soko la
kimataifa, hususan Ugonjwa wa Homa ya Mapafu
ya Ng’ombe (CBPP), Homa ya Bonde la Ufa (RVF) na
Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR);
17
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(m) Kuendelea kuimarisha eneo huru la magonjwa
ya mifugo katika Kanda ya Kusini Magharibi na
kuanzisha vitalu huru vipya viwili (2) vya magonjwa
katika ranchi za Kongwa na Ruvu ili kukidhi matakwa
ya soko la kimataifa hivyo kuongeza ajira na Pato la
Taifa; na kuongeza thamani ya mifugo na mazao yake;
(n) Kuendelea kuzalisha chanjo za magonjwa ya mifugo
katika kituo cha Uzalishaji wa chanjo cha Kibaha
(Tanzania Vaccine Institute);
(o) Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo kwa
kuongeza udahili wa maafisa ugani kutoka 1,800 hadi
2,500 kwa mwaka katika vyuo vinane (8) vya Serikali
na kushirikisha vyuo 21 vya sekta binafsi kwa lengo la
kuongeza upatikanaji wa maafisa ugani katika ngazi
za vijiji na Kata ili kuimarisha huduma za mifugo;
(p) Kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vya
nyama na mazao mengine yatokanayo na mifugo
ikiwemo jibini na ngozi hususan katika maeneo yenye
mifugo mingi ili kuongeza thamani; na
(q) Kuitafutia ufumbuzi wa kudumu migogoro ya
wakulima na wafugaji.
Uvuvi
26. Kwa kuzingatia ukubwa wa maeneo na wingi wa rasilimali
za uvuvi tulizonazo, katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Usimamizi wa rasilimali za uvuvi Tanzania
Bara umeimarishwa ambapo vituo 25 vya doria
vimeanzishwa na kupewa zana za kisasa kwa lengo
la kudhibiti uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali
nchini;
(b) Vikundi vya usimamizi shirikishi wa rasilimali za
uvuvi 226 vimeanzishwa na kufanya idadi ya vikundi
hivyo kufikia 749, kati ya hivyo 511 vimesajiliwa na
18
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
vinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria
ndogo ya mipango kazi yake;
(c) Ujenzi na uboreshaji wa mialo ya kisasa ya kupokelea
mazao ya uvuvi umetekelezwa katika Kanda ya
Pwani ya Bahari ya Hindi (3), Ziwa Tanganyika (4) na
Ziwa Victoria (6). Aidha, mialo 19 ya ukanda wa Ziwa
Victoria imekarabatiwa;
(d) Vituo vya kuzalisha vifaranga wa samaki wa maji
baridi vimeanzishwa katika Mikoa ya Lindi, Kigoma,
Ruvuma, Tanga, Pwani, Geita na Morogoro. Vituo
hivyo kwa ujumla vina uwezo wa kuzalisha vifaranga
10,000,000 kwa mwaka;
(e) Sekta binafsi imeendelea kuhamasishwa kushiriki
katika uvuvi ikiwemo kuanzisha viwanda vya
kuchakata samaki. Hadi sasa kuna viwanda 48 vya
kuchakata samaki na maghala 84 ya kuhifadhia mazao
ya uvuvi; na
(f) Jumla ya vikundi 208 vya Kuweka na Kukopa
(VICOBA) vimeanzishwa ambapo wananchi 5,573
wamenufaika na hivyo kuwawezesha kuendesha
shughuli ndogo ndogo za uvuvi.
27. Katika kipindi cha Ilani hii ya 2015–2020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuiendeleza Sekta ya
Uvuvi kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuanzisha na kuimarisha vikundi na vyama vya
ushirika vya msingi vya wavuvi wadogo wadogo kwa
lengo la kuwakopesha vifaa vikiwemo zana za uvuvi
katika maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi,
maziwa na mito kwa kupunguza kodi na kuviwezesha
vikundi hivyo vikopesheke;
(b) Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi na Vyama
vya Ushirika itanunua meli tano za uvuvi zenye
uwezo wa kuvua samaki Bahari Kuu ambapo ajira
zaidi ya 15,000 kwa mwaka zitapatikana;
19
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kujenga bandari ya uvuvi katika ukanda wa Pwani
ambayo itawezesha meli zinazovua Bahari Kuu kutia
nanga kwa lengo la kuhaulisha samaki, kuuza samaki,
kutoa takwimu sahihi na huduma nyingine. Zaidi ya
ajira 30,000 zitapatikana na kuongeza pato kwa jamii
na Taifa;
(d) Kuimarisha miundombinu ya uvuvi kwa kujenga mialo
mitatu (Ziwa Victoria), minne (Ziwa Tanganyika)
na miwili (Ziwa Nyasa) na hivyo kuongeza idadi ya
mialo kutoka 39 hadi 48 na kuimarisha masoko ya
samaki ya Feri (Dar es Salaam), Kirumba (Mwanza)
na Muganza (Kagera) ili kuongeza thamani na ubora
wa samaki pamoja na kupunguza upotevu wa mazao
ya uvuvi kabla ya kumfikia mtumiaji;
(e) Kuimarisha hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu
18 pamoja na kuanzisha maeneo mengine sita (6)
na hifadhi katika maziwa makuu, hususan Victoria,
Tanganyika na Nyasa ili kuhakikisha kuwa mazalia
na makulia ya samaki yaliyoharibika yanarejeshwa
katika hali yake ya awali;
(f) Kurejesha mazalia na makulia ya samaki yaliyoharibika
kutokana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu
wa mazingira kwa kuweka matumbawe bandia na
kupanda mikoko katika bahari;
(g) Kushirikiana na Mashirika ya Umma yenye dhamana
ya uvuvi nchini, kuwavutia wawekezaji kuanzisha
viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya
mazao ya uvuvi, vyombo na zana za uvuvi;
(h) Kuboresha maeneo ya uvuvi kwa kutumia teknolojia
rafiki ya mazingira kwa kuweka vifaa vya kuvutia
samaki (Fish Aggregating Devices) baharini ili
kuwawezesha wavuvi wadogo kuyafikia maeneo
yenye samaki wengi na hivyo kuongeza upatikanaji
wa samaki;
20
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo kwa
kuongeza udahili wa maafisa ugani wa uvuvi kutoka
1,200 hadi 2,500 kwa mwaka na kuwezesha upatikanaji
wa Maafisa Ugani katika ngazi ya Kata ili kuimarisha
huduma za uvuvi na ufugaji wa samaki;
(j) Kuendeleza utafiti wa kurudishia samaki na
kupandikiza samaki ili kuongeza wingi katika
maziwa, mito na mabwawa, hususan Ziwa Victoria;
(k) Kuanzisha na kuimarisha vikundi na vyama vya
ushirika vya wafugaji wa samaki kwa lengo la kukuza
ufugaji wa samaki nchini;
(l) Kushirikiana na wadau wa ufugaji samaki ili kuongeza
uzalishaji wa samaki kwa kujenga mabwawa ya
kufugia samaki na kuongeza uzalishaji kutoka tani
10,000 hadi 50,000 kwa mwaka na kupanua wigo wa
ajira kwa vijana;
(m) Kuwawezesha wakulima wa mwani, hususan vikundi
vya akina mama na vijana wa mwambao wa pwani
katika kuongeza uzalishaji kutoka tani 12,000 hadi
tani 20,000 kwa mwaka, uzalishaji wa chaza wa lulu,
kaa, kamba na viumbe wengine wa baharini kwa
kuwapatia nyenzo na utaalamu;
(n) Kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo kupata vifaa
vya uvuvi kwa bei nafuu;
(o) Kuhamasisha uchimbaji wa mabwawa na ufugaji wa
samaki katika maeneo yenye ukame kwa lengo la
kuongeza lishe bora pamoja na kuongeza ajira kwa
vijana; na
(p) Kuendelea kupambana na uvuvi haramu ili uvuvi
uwe endelevu na wenye tija.
21
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Utalii
28. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kuhakikisha kwamba Sekta ya Utalii
inaimarishwa na kuendelezwa kwa kuwa ni moja ya sekta
zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa na
ajira kwa wananchi. Katika kipindi hicho, mambo yafuatayo
yamefanyika:-
(a) Ujenzi wa Chuo Kipya cha Utalii, Kampasi ya Bustani
umekamilika mwaka 2011 na kuwezesha idadi ya
udahili wa wanafunzi kuongezeka kutoka 138 mwaka
2005 hadi wanafunzi 289 mwaka 2014. Ili kuongeza
wataalam wa fani hii, Serikali imeruhusu taasisi
binafsi na wakala kutoa mafunzo ya utalii na ukarimu
katika ngazi ya Astashahada na Stashahada;
(b) Tanzania imefanikiwa kuviingiza vivutio vya utalii
kwenye soko la Kimataifa ambavyo ni Mlima
Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Bonde la Hifadhi
la Ngorongoro kuwa kati ya Maajabu Saba ya Asili ya
Afrika (New Wonders of Africa); na
(c) Makusanyo yatokanayo na shughuli za utalii
yameongezeka kutoka wastani wa Shilingi trilioni
2.98 mwaka 2012/13 hadi Shilingi trilioni 3.94 mwaka
2013/14.
29. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitasimamia utekelezaji wa mikakati ya
kukuza utalii nchini kwa kuhakikisha kwamba, Serikali
inatekeleza mambo yafuatayo:-
(a) Kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kutoka
1,102,026 mwaka 2015 hadi 2,000,000 mwaka 2020 kwa
kuwezesha Sekta Binafsi kuwekeza katika huduma
za miundombinu ya utalii pamoja na kuendeleza
Mkakati wa Kimataifa wa Utangazaji wa Utalii ili
kuwavutia watalii wengi zaidi;
22
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuongeza msukumo katika utalii wa kihistoria kwa
kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya malikale
na kuyatangaza maeneo hayo;
(c) Kuongeza bajeti ya Sekta ya Utalii ili kuutangaza utalii
ndani na nje ya nchi;
(d) Kuimarisha mafunzo ya Hoteli na Utalii hususan
katika ngazi ya shahada ili kuongeza ubora wa
watumishi wa huduma za Ukarimu na Utalii kwa
kukifanya Chuo cha Taifa cha Utalii kutoa mafunzo
ya ukufunzi;
(e) Kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii
wa ndani na kuweka mazingira yatakayowezesha
wawekezaji wa ndani kuendeleza biashara za utalii
pamoja na kuwajengea uwezo waongoza watalii;
(f) Kufanya jitihada za kufungua fursa za utalii katika
Kanda ya Kusini pamoja na kutumia fukwe zake;
(g) Kuendelea kujenga mazingira bora ya kuwawezesha
vijana kuanzisha kampuni za kutembeza watalii
katika maeneo mbalimbali ya utalii; na
(h) Kuhifadhi malikale kwa kuishirikisha jamii kutumia
Malikale kama chanzo cha kujipatia kipato kwa kutoa
elimu ya ujasiriamali, kutenga maeneo ya biashara,
kuishirikisha sekta binafsi na kutoa elimu ya uhifadhi
kwa umma.
Maliasili
30. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, pamoja na
changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Sekta ya
Maliasili, Serikali imechukua hatua za kuhakikisha kuwa
sekta hii inapewa msukumo wa kutosha ili iweze kuchangia
kikamilifu katika kuboresha maisha ya wananchi. Katika
kutimiza azma hiyo, Serikali imetekeleza yafuatayo:-
23
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Hatua zimechukuliwa za kuimarisha mahusiano
mema baina ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa na
wananchi wanaoishi karibu na hifadhi hizo kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Maeneo 16 yaliyokosa sifa ya kuendelea kuwa
maeneo ya hifadhi yamerejeshwa kwa mamlaka
za wananchi;
(ii) Vijiji vinavyopakana na hifadhi vimepatiwa
huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa madarasa, nyumba za walimu, barabara na
masoko; na
(iii) Jumla ya wanavijiji 7,320 wamepatiwa mizinga
ya nyuki 24,076 na kupewa mafunzo ya mbinu
za kisasa za ufugaji nyuki na kutafuta masoko
ya asali ikiwa ni pamoja kuwawezesha kushiriki
katika maonesho mbalimbali ndani na nje ya
nchi.
(b) Upandaji wa miti kwenye misitu ya jamii umeongezeka
ambapo wastani wa miti milioni 200 kwa mwaka
imepandwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
ambapo asilimia 65 ya miti yote iliyopandwa
imeendelea kukua vizuri.
31. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Serikali itaendelea
kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba Sekta ya Maliasili
inazidi kuimarika ili kuyafanya mazao yatokanayo na
maliasili hususan misitu na nyuki yanaendelea kuchangia
katika ukuaji wa uchumi, kuwaongezea wananchi kipato
na kuongeza fursa za ajira. Ili kufikia azma hiyo Chama
Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kujenga mahusiano mema baina ya
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa na wananchi wanaoishi
karibu na hifadhi hizo kwa namna ambayo wananchi
hao watanufaika na uwepo wa hifadhi hizo;
24
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na
maeneo ya jirani na hifadhi kwa kushirikisha wadau
katika kuhakiki mipaka ya maeneo ya hifadhi kwa
kuweka alama za kudumu; kuandaa mipango ya
matumizi bora ya ardhi; na kuzingatia utawala wa
Sheria katika kusimamia rasilimali za maliasili;
(c) Kuboresha miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba
na Vikosi dhidi ya ujangili na kuongeza vitendea kazi
vya kisasa kwa ajili ya doria na upelelezi nje na ndani
ya maeneo ya hifadhi;
(d) Kuendelea kutekeleza programu ya ufugaji nyuki ya
mwaka 2007–2016 ili kuwajengea uwezo wadau wake
kuzifahamu mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya
nyuki na pia masoko ya asali na nta ya ndani na nje ya
nchi;
(e) Kuendelea kuimarisha doria za ulinzi wa wananchi
dhidi ya wanyamapori kwa kuboresha mfumo wa
utoaji taarifa za wanyamapori waharibifu. Aidha,
Serikali itaboresha na kutoa kwa wakati kifuta
machozi kwa watu au familia zitakazoathirika kwa
kiwango kinacholingana na athari zitakazotokea;
(f) Kuongeza eneo la kupanda miti kutoka hekta 60,000
mwaka 2015 hadi hekta 130,000 mwaka 2020 na
kuhakikisha kwamba mbao zinazovunwa zinatumiwa
kwa ajili ya kutengeneza samani na matumizi mengine
hapa nchini badala ya kusafirisha magogo nje ya nchi;
(g) Kuweka utaratibu wa wazi utakaowawezesha
wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kufaidika na
rasilimali hizo;
(h) Kuanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
ambayo moja kati ya majukumu yake ni kuweka
utaratibu utakaotumika katika kutoa vibali vya
uvunaji wa raslimali za maliasili; na
25
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Kupambana na ujangili wa wanyama pori
wakiwemo Tembo na Faru.
Viwanda na Biashara
32. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Ilani ya Uchaguzi
iliweka msukumo mkubwa zaidi katika kuimarisha
uzalishaji katika viwanda vilivyopo na kujenga viwanda
vipya ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na michepuo
ya bidhaa, kuhimiza mauzo ya bidhaa ndani na nje ya
nchi na kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza
viwanda vya kimkakati kupitia mashirikia ya Umma ya
NDC na EPZA. Katika kipindi hicho mafanikio makubwa
yamepatikana ambayo ni pamoja na:-
(a) Ukuaji wa Sekta ya Viwanda:
(i) Sekta ya Viwanda imekua kutoka asilimia
7.7 mwaka 2010 hadi asilimia 7.9 mwaka
2013. Ukuaji huo umechangiwa kwa kiasi
kikubwa kutokana na kuimarika kwa uzalishaji
viwandani, hususan viwanda vya vinywaji,
saruji, bidhaa za chuma; na usindikaji wa mazao
ya kilimo;
(ii) Mwenendo wa mchango wa Sekta ya Viwanda
katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia
9.6 mwaka 2010 hadi asilimia 9.9 mwaka 2013;
na
(iii) Miradi mipya ya viwanda vilivyosajiliwa na
ujenzi kuanza katika kipindi husika imefikia
454.
(b) Ujenzi wa viwanda vinane vya Saruji ambao uko
katika hatua za mwisho za kukamilika ambavyo
vitawezesha Taifa kuongeza uzalishaji zaidi ya
maradufu na hivyo nchi yetu kuijitosheleza kwa
saruji na nyingine kuuzwa nje. Aidha, kukamilika
kwa viwanda hivi kutaifanya bei ya saruji kushuka
26
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na pia kuongeza ajira mambo ambayo yataendelea
kuboresha ustawi wa wananchi;
(c) Katika Kanda ya Ziwa, ujenzi wa Kiwanda cha Nguo
unaendelea. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa
kutumia kiwango kikubwa cha pamba inayozalishwa
katika ukanda huo hatua ambayo itahakikisha soko la
uhakika la pamba na kuongeza ajira kwa wakazi wa
eneo hilo na kwa Watanzania kwa ujumla;
(d) Ujenzi wa viwanda viwili vikubwa vya ngozi
unaoendelea katika mikoa ya Arusha na Shinyanga
ambapo utakapokamilika utafanya uuzaji wa ngozi
ghafi nje ya nchi kuwa historia. Ngozi na bidhaa za
ngozi zitauzwa nje ya nchi zikiwa zimeongezewa
thamani na hivyo kuongeza ajira; na
(e) Uzalishaji wa mbolea za NPK na MRP katika kiwanda
cha Minjingu umeongeza kutoka tani 75,000 hadi
kufikia tani 100,000 kwa mwaka.
(f) Mauzo ya Bidhaa za Viwandani:
(i) Mauzo kwenda soko la nchi wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
yameongezeka kutoka dola za Kimarekani
milioni 419 mwaka 2010 hadi dola milioni 450
mwaka 2013;
(ii) Mauzo kwenda soko la Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) yameongezeka
kutoka dola za Marekani 625 mwaka 2010 hadi
kufikia dola 1,209 mwaka 2013; na
(iii) Mauzo katika soko la Marekani kupitia Mpango
wa AGOA yameongezeka kutoka dola za
Marekani milioni 51 mwaka 2010 hadi dola
milioni 76 mwaka 2013.
27
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Maeneo Maalumu ya Uwekezaji:
(i) Mikoa 20 imetenga Maeneo Maalumu ya
Uwekezaji ili yawekewe miundombinu ya
msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga
viwanda na kufanya biashara katika maeneo
hayo; na
(ii) Sheria za Maeneo Maalumu ya Uzalishaji
kwa Mauzo Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu
ya Uchumi (SEZ) zimepitiwa ambapo vivutio
mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafuu ya kodi
vimebainishwa ili kuhamasisha ushiriki wa
Sekta Binafsi katika uwekezaji.
(h) Benki ya Rasilimali imeanzisha Dirisha Maalumu kwa
ajili ya kuwezesha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali
kupata mikopo kwa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda;
(i) Jumla ya makampuni 130 yamewekeza mitaji yenye
thamani ya Shilingi bilioni 2,041.6 mwaka 2014
ukilinganisha na Shilingi bilioni 126.6 mwaka 2010 na
kutengeneza ajira za moja kwa moja zilizotokana na
uwekezaji huo kufikia 31,923; na
(j) Ekari 107 zimepimwa katika Mkoa wa Dodoma
kwa ajili ya kuanzisha Vijiji vya Viwanda (Industrial
Villages) na kupata hati miliki (Title Deeds) ili
kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza
bidhaa za ngozi.
(k) Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI):
Katika kipindi cha mwaka 2010-2013, jumla ya mikopo
56,517 yenye thamani ya Shilingi bilioni 30.6 imetolewa
na kuwezesha upatikanaji wa ajira zipatazo 113,876
kupitia Mfuko wa Kuendeleza Wafanyabiashara
Wadogo (NEDF).
28
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mradi wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti
kinachojengwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
33. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015–2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuweka
nguvu kubwa katika kukamilisha utekelezaji wa Sera
ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu
(2010–2020) ambayo malengo yake ni kuiwezesha Sekta
ya Viwanda kuchangia katika kufikia malengo ya
maendeleo ya muda mrefu kama ilivyoanishwa katika
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Aidha, Utekelezaji wa
Ilani hii utakuwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Mpango
wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16-2020/21)
ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi wa viwanda.
Katika kipindi hicho, utaanza ujenzi wa viwanda mama
(basic industries) na kuimarisha viwanda vilivyopo lengo
likiwa ni kuhakikisha kwamba:-
(a) Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa
unaongezeka kutoka asilimia 9.9 mwaka 2013 hadi
asilimia 15 ifikapo mwaka 2020;
29
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Sekta ya Viwanda inaongeza ajira kufikia asilimia 40
ya ajira zote ifikapo 2020 kwa kuweka kipaumbele
cha kujenga viwanda vinavyotumia malighafi
zinazozalishwa hapa nchini kama vile kilimo, mifugo,
uvuvi na maliasili; Viwanda hivyo ni pamoja na
viwanda vya nguo, sabuni, korosho, matunda n.k.
(c) Kuandaa mikakati thabiti ya kuhamasisha sekta
binafsi kuanzisha viwanda vikubwa na vya kati na
kuweka utaratibu wa kuvilinda dhidi ya viwanda vya
nje;
(d) Kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha
kupunguza gharama za uwekezaji na uendeshaji wa
viwanda;
(e) Kuanzisha viwanda vya msingi vinavyotumia
malighafi ya chuma katika maeneo ya Liganga na
Mchuchuma;
(f) Sekta ya Viwanda inaongeza fursa za masoko hususan
yenye upendeleo wa ushuru wa forodha kama
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika, Utatu wa COMESA-EACSADC
na Umoja wa Ulaya, nchi rafiki kama India,
China, Japan na Marekani; na
(g) Kuendeleza kasi ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya
kati hasa vinavyosindika mazao.
(h) Kuhakikisha Benki ya Rasilimali (TIB) inapanua
wigo wa Dirisha Maalumu ili liweze kutoa huduma
zake kwenye maeneo yote nchini ikiwemo Tanzania
Zanzibar.
Madini
34. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendeleza juhudi katika kuhakikisha Sekta ya Madini
inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ajira.
Kutokana na juhudi hizo, mchango wa madini katika Pato
30
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.3 mwaka 2010
hadi asilimia 3.5 mwaka 2014. Kuimarika kwa sekta hii
kumetokana na kufanyika mambo yafuatayo:-
(a) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewezeshwa
kumiliki hisa kwenye migodi ya STAMIGOLD (100%),
Buchreef (45%), Buhemba (100%), Kiwira (100%),
Tanzaniteone (50%), Tulawaka (100%), NDC–Liganga
(20%), Mchuchuma (20%), Ngaka Coal Projects (30%)
na Mgodi wa Almasi wa Mwadui (25%);
(b) STAMICO imeanzisha Kampuni iitwayo Kyerwa
Tin Company Limited (KTCL) ili kununua madini
ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini
hayo huko Kyerwa. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla
ya tani 71.3 zimenunuliwa kwa gharama ya Shilingi
1,106,326,000. Aidha, tani 30 zimeuzwa kwa Dola za
Marekani 201,000;
(c) STAMICO imefanikiwa kupata kandarasi nne (4) za
uchorongaji na utafiti wa madini yenye thamani ya
Shilingi bilioni 1.35 ambapo jumla ya ajira mpya 78
zimepatikana kutokana na upatikanaji wa mashine za
kisasa za uchorongaji;
(d) Ofisi mbili za madini za Kanda zimeanzishwa; moja
katika Kanda ya Ziwa Nyasa inayohudumia Mikoa
ya Njombe na Ruvuma; na nyingine kanda ya Ziwa
ambayo inahudumia Mikoa ya Mara na Simiyu
ili kusimamia na kudhibiti biashara ya madini.
Kuanzishwa kwa ofisi hizo mpya kumeongeza idadi
ya ofisi za Kanda kufikia kumi (10) na hivyo kuongeza
ufanisi kwa wadau wa sekta hii; na
(e) Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umeendelea
kuwezeshwa kwa kupatiwa fedha na vitendea kazi ili
kuimarisha utendaji kazi wake. Katika kipindi hicho
Wakala wa Jiolojia amepata mafanikio yafuatayo:-
(i) Mfumo wa utunzaji, uchakataji, na usambazaji/
31
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
uuzaji wa takwimu na taarifa za upatikanaji
madini ili kuvutia uwekezaji umeboreshwa;
(ii) GST imejiunga na COSOTA ili kusajili
machapisho yake na kupewa haki miliki
(Copyright);
(iii) GST imejenga maabara ya kisasa ya kuchunguza
miamba na madini baada ya kununua vifaa
muhimu na vya kisasa; na
(iv) GST imefanikiwa kufanya ugani na uchoraji wa
ramani za upatikanaji wa madini (geological and
mineral occurrence mapping) kwa asilimia 92 ya
ardhi kavu ya Tanzania Bara.
(f) Idadi ya leseni za madini imeongezeka hadi kufikia
37,261 mwaka 2015 ambapo leseni za uchimbaji
mkubwa ni 15; uchimbaji wa kati ni 380; uchimbaji
mdogo ni 33,131; na leseni za utafutaji madini ni
3,735. Watanzania wanamiliki asilimia 70 ya leseni
hizo, wageni asilimia 25 na asilimia 5 ya leseni hizo
zinamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Wageni;
(g) Wachimbaji wadogo wametengewa maeneo 25 yenye
ukubwa wa kilometa za mraba 2,407 na jumla ya
leseni 8,800 zimetolewa kwenye maeneo hayo;
(h) Wachimbaji wadogo 10,000 wamepatiwa mafunzo ya
huduma za ugani (extension services) katika nyanja
za kutambua umbile na tabia ya mashapo, masuala
ya utunzaji wa mazingira, utambuzi wa madini na
uboreshaji wa uchenjuaji madini;
(i) Jumla ya Shilingi milioni 909.5 zimetolewa kwa
wachimbaji wadogo kama ruzuku;
(j) Mpango wa utunzaji mazingira katika maeneo ya
uchimbaji wa madini (Modern Environmental Protection
Plan) umeanzishwa na umewahamasisha wachimbaji
wadogo kutunza mazingira na kuepuka kuchafua
vyanzo vya maji;
32
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(k) Mikataba ya madini imepitiwa kwa lengo la kulinda
maslahi ya nchi ambapo baadhi ya vipengele
vimefanyiwa marekebisho ili mrahaba ulipwe kwa
kiwango cha asilimia 4 ya mauzo ghafi ya dhahabu
(gross value) badala ya asilimia 3 ya mauzo halisi
ya dhahabu (Net Back Value) iliyokuwa ikilipwa na
wawekezaji hapo awali;
(l) Migodi ya Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Geita
imeanza kulipa ushuru wa huduma (service levy)
kwa Halmashauri husika kwa kiwango cha asilimia
0.3 ya mapato ghafi ya migodi hiyo badala ya Dola
za Kimarekani 200,000 zilizokuwa zinalipwa kwa
mwaka;
(m) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)
imeanzisha madawati ya ukaguzi kwenye viwanja
vya ndege vya Kimataifa ili kudhibiti vitendo vya
utoroshaji wa madini nje ya nchi, hatua iliyowezesha
kukamatwa madini yenye thamani ya Shilingi bilioni
15; na
(n) Kamati Maalumu ya Kitaifa (National Local Content
Committee) imeundwa ili kusimamia mikakati
iliyowekwa na wadau kuhakikisha kuwa Makapuni
ya Madini yanaongeza kiwango cha manunuzi ya
bidhaa na huduma hapa nchini kwa lengo la kuongeza
ajira na soko la bidhaa za ndani.
35. Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali yake kutekeleza mambo yafuatayo
ili kuendelea kukuza Sekta ya Madini na kuongeza
mchango wake kwenye Pato la Taifa:-
(a) Kuweka na kusimamia mfumo thabiti wa kukagua
shughuli za migodi, kukusanya takwimu za madini
na kufuatilia maduhuli yatokanayo na madini kwa
malengo mapana ya kuongeza mapato ya Serikali;
(b) Kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti ya
kuvutia mitaji ya uwekezaji katika Sekta ya Madini,
33
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
hususan kwenye madini adimu (Rare Earth Elements
- REE);
(c) Kuhamasisha uzalishaji na masoko ya madini ya
viwandani;
(d) Kuweka miundombinu muhimu (umeme, simu, maji,
barabara) kupitia ushirikiano wa Serikali na Sekta
Binafsi (PPP) kwenye maeneo yenye uwezekano wa
kuanzishwa kwa migodi mikubwa mipya;
(e) Kuboresha mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni
za madini, na upatikanaji wa taarifa muhimu kwa
wadau kuhusu Sekta ya Madini;
(f) Kuimarisha udhibiti na usimamizi wa upatikanaji,
utunzaji, usafirishaji na matumizi ya baruti katika
shughuli za migodi;
(g) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) ili liweze kushiriki kikamilifu kwenye
shughuli za utafutaji, uchimbaji na utoaji huduma
katika Sekta ya Madini kwa niaba ya Serikali na
Watanzania wote;
(h) Kuendelea kuujengea uwezo wa kifedha na rasilimali
watu Wakala wa Jiolojia Tanzania ili uweze kufikia
kiwango bora zaidi katika ukusanyaji wa takwimu
na taarifa muhimu za kijiolojia na kijiofizikia
zitakazosaidia katika kuchochea kasi ya utafutaji
na upatikanaji wa mashapo ya madini hapa nchini
yanayoweza kuchimbwa kwa faida;
(i) Kuendelea kuujengea uwezo Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Tanzania na Ofisi za Madini Mikoani ili
zijiimarishe katika kukagua na kusimamia shughuli
za uzalishaji na biashara ya madini nchini, na hivyo
kuongeza manufaa yatokanayo na Sekta ya Madini
kwenye uchumi;
34
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(j) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli
za uongezaji thamani madini ili kukuza mchango wa
sekta hiyo katika Pato la Taifa;
(k) Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi
itakayowezesha kupunguza au kukomesha kabisa
vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi
na biashara haramu ya madini nchini;
(l) Kuweka na kutekeleza mikakati maalumu
itakayowezesha soko la Tanzanite hapa nchini
kuimarika zaidi na hivyo kuongeza manufaa
yatokanayo na madini hayo yanayopatikana Tanzania
pekee;
(m) Kuwawezesha wachimbaji wadogo kujiajiri kupitia
sekta hii kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuwatambua, kuwarasimisha na kuwapatia
maeneo ya uchimbaji madini;
(ii) Kuwapatia ruzuku, mafunzo, teknolojia na
maarifa ya kisasa kwa ajili ya kuendeleza
shughuli za uchimbaji;
(iii) Serikali kupitia STAMICO kwa kushirikiana na
wachimbaji wakubwa kuwawezesha kupata
mikopo na masoko; na
(iv) Kuendelea kuongeza na kuwekeza mtaji wa
Benki ya Rasilimali (TIB) ili iweze kutoa mikopo
kwa wajasiriamali wadogo.
(n) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika
masuala ya usalama, utunzaji wa mazingira na afya
migodini; na
(o) Kuhakikisha migodi yote mikubwa nchini inaendelea
inanunua huduma na bidhaa kutoka hapa nchini kwa
kiwango cha kuridhisha kwa kadri ya upatikanaji
wake.
35
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA TATU
SEKTA ZA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA
KIUCHUMI
Ardhi
36. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali imepata
mafanikio yafuatayo katika Sekta ya Ardhi:-
(a) Utawala wa Ardhi:
(i) Jumla ya vijiji 1,619 katika Halmashauri za
Wilaya 37 vimepimwa;
(ii) Jumla ya vijiji 5,558 vimepatiwa vyeti vya Ardhi
ya Kijiji;
(iii) Jumla vijiji 509 vimeandaliwa mipango ya
matumizi bora ya ardhi katika wilaya 69 nchini;
(iv) Jumla ya Hatimiliki za Kimila 348,000
zimetolewa; na
(v) Ofisi za Ardhi za Kanda zimeanzishwa na
kuimarishwa.
(b) Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi (2013-2033)
umeandaliwa na utekelezaji wake umeanza ambapo
Vijiji 509 vimeandaliwa mipango ya matumizi
ya ardhi katika wilaya 69 nchini na kufanya vijiji
vilivyoandaliwa mipango hiyo kufikia 1,560.
(c) Mipango Miji:
(i) Programu ya Kurasimisha na Kuzuia Makazi
Holela imeandaliwa mwaka 2012;
(ii) Elimu ya Urasimishaji na Kuzuia Makazi Holela
imetolewa katika mikoa mbalimbali;
36
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Dar es Salaam
zimetoa leseni za makazi 35,362 na kutoa Hati
2,204 za kumiliki Ardhi;
(iv) Huduma za upimaji na ramani zimepelekwa
katika ofisi mbalimbali za Kanda;
(v) Ili kupunguza msongamano katika miji
mikubwa nchini hususan Dar es Salaam na
Arusha, mipango kabambe ya kujenga miji
midogo ya Luguruni (ekari 156.53), Mji Mpya
wa Kigamboni (ekari 16,047) na Kawe (ekari
267.71) imekamilika. Aidha, miji midogo ya
Burka/Matevesi (ekari 579.2) na eneo la Usa
River (ekari 296) katika Jiji la Arusha itajengwa;
na
(vi) Mpango wa kuanzisha mji mpya wa kisasa wa
Kigamboni ili kukabiliana na ukuaji wa kasi
wa Jiji la Dar es Salaam umekamilika. Hatua
ambazo zimefikiwa katika uanzishwaji wa mji
huo wa kisasa ni:-
• Wakala wa kusimamia utekelezaji na
uendelezaji wa Mpango wa Mji mpya wa
Kigamboni (KDA) umeundwa;
• Rasimu ya Mpango Kabambe wa Mji mpya
wa Kigamboni imeandaliwa (Kigamboni
New City Master Plan – 2011 – 2031);
• Ujenzi wa daraja la Kigamboni na barabara
kiunganishi unaendelea chini ya usimamizi
wa Wizara ya Ujenzi;
• Eneo la upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam
katika Kata ya Vijibweni limebainishwa na
kazi ya uthamini inaendelea; na
• Utaratibu mpya wa uendelezaji wa Mji
wa Kigamboni umepitiwa na kuridhiwa
37
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na Kamati ya Wadau wa Kigamboni
ambapo Serikali itajihusisha zaidi na
uwekezaji katika kuweka/kujenga
miundombinu kama vile barabara, umeme
na maji. Wananchi wataruhusiwa kufanya
yafuatayo:-
- Kuwa waendelezaji wenyewe katika
eneo la mradi kwa kuzingatia Mpango
Kabambe wa kuendeleza Mji wa
Kigamboni; au
- Kuingia ubia na mwekezaji, ambapo
thamani ya ardhi ya mwananchi
itakuwa ndio mtaji wake; au
- Kulipwa fidia/kuuza eneo lake kwa
wawekezaji/Serikali kwa bei ya soko.
(d) Kazi ya kuanzisha Benki ya Ardhi (Land Bank) kwa
ajili ya wawekezaji wa ndani na nje imeendelea
kutekelezwa na jumla ya Shilingi bilioni moja
zimetengwa kwa ajili ya kianzio cha Mfuko wa Fidia ya
Ardhi (Land Compensation Fund). Aidha, mashamba
66 mkoani Morogoro yameainishwa kwa ajili ya
kuingizwa kwenye Hazina ya Ardhi na mashamba
112 mkoani Arusha yamekaguliwa na kupendekezwa
kuingizwa kwenye Hazina ya Ardhi;
(e) Baadhi ya Halmashauri za Miji na Wilaya nchini
zimewezeshwa kutumia mfumo wa teknolojia ya
kompyuta katika kutoa huduma za ardhi;
(f) Halmashauri za Miji na Wilaya zimeendelea
kujengewa uwezo kupitia Mfuko wa Mzunguko
(Plot Development Revolving Fund) wa kupima
viwanja na kuviuza kwa wananchi ambapo jumla ya
Halmashauri 14 zimeidhinishiwa mikopo ya jumla ya
Shilingi bilioni 2.67; na
38
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Hatua zifuatazo zimechukuliwa katika kuzijengea
uwezo Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji
ili kuhakikisha majukumu ya Sekta ya Ardhi
yanatekelezwa ipasavyo:-
(i) Kompyuta 100 kwa ajili ya matumizi ya shughuli
za Sekta ya Ardhi katika Halmashauri 100 hapa
nchini zimenunuliwa na kusambazwa;
(ii) Vifaa vya upimaji vimenunuliwa na kufikishwa
katika Halmashauri ya Manyoni (Total station
1), Jiji la Mbeya (Total station 1), Ofisi ya Mkoa
wa Mwanza (GPS 1 na Total station 1); na
(h) Pamoja na changamoto zinazoyakabili Mabaraza
ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, hatua zifuatazo
zimechukuliwa katika kushughulikia mashauri
yahusuyo ardhi na nyumba:-
(i) Mabaraza 39 ya wilaya mbalimbali yamepatiwa
watumishi, samani na vitendea kazi;
(ii) Mabaraza mapya 10 yameanzishwa katika
wilaya za Nzega, Manyoni, Kilosa, Tunduru,
Mpanda, Kyela, Muleba, Ngara, Karagwe na
Ngorogoro hivyo kufanya mabaraza yanayotoa
huduma kufikia 49; na
(iii) Hatua za kinidhamu zimeendelea kuchukuliwa
dhidi ya wenyeviti wa mabaraza ya wilaya
waliokiuka maadili ya umma.
(i) Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kushirikiana na
sekta binafsi limeendelea kujenga nyumba kwa ajili
ya makazi na mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(i) Ujenzi wa majengo ya biashara 81 na nyumba za
makazi 5,900 umekamilika;
(ii) Ujenzi wa majengo 50 ulioshirikisha sekta
binafsi umekamilika; na
39
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Ardhi yenye ukubwa wa ekari 4,642 katika
maeneo mbalimbali nchini imenunuliwa kwa
ajili miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba.
(j) Wakala wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi
(NHBRA) umefanya yafuatayo:-
(i) Utafiti kuhusu mashine za kufungamana
(interlocking press machine), kofia, mashine za
“hydraform”, majaribio ya sampuli ya udongo,
ujenzi wa zege na kofia za vigae vya kuezekea
ulifanyika na matokeo ya utafiti huo yameenezwa
katika Halmashauri za Wilaya za Namtumbo,
Karatu, Monduli, Simanjiro, Sumbawanga,
Bariadi, Kilombero, Rungwe na Halmashauri za
Manispaa za Temeke, Kinondoni, Ilala, Tabora,
Iringa, Dodoma na Halmashauri ya Jiji la Tanga;
na
(ii) Jumla ya mashine za kufyatulia matofali 1,105
ziligawiwa kwa Halmashauri mbalimbali
nchini.
(k) Uanzishwaji wa vyama vya Ushirika wa Nyumba
umeendelea kuhamasishwa ili kuwezesha wananchi
wa kipato cha chini kunufaika na mikopo ya nyumba
ambapo:-
(i) Vijana 150 wamepewa mafunzo ya teknolojia ya
ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu
katika ofisi za Wakala, katika Mkoa wa Kagera
(vijana 55) na Jiji la Dar es Salaam (vijana 95);
(ii) Mwongozo kuhusu kuanzisha na kusimamia
vyama vya Ushirika wa Nyumba umeandaliwa;
na
(iii) Jumla ya mashine 656 za kufyatulia matofali
yanayofungamana zimetolewa kwa
Halmashauri 163 ambapo kila Halmashauri
ilipatiwa wastani wa mashine nne.
40
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(l) Ujenzi wa mtandao wa upimaji nchini wenye alama
640 za madaraja mbalimbali umekamilika kwa asilimia
98;
(m) Upimaji wa njia za kuingia katika bandari (port
approaches) za Dar es Salaam na Zanzibar
umekamilika;
(n) Kampuni ya Dhamana ya Mikopo ya Nyumba (The
Tanzania Mortgage Refinancing Company) imeanzishwa
kwa lengo la kutoa mikopo ya muda mrefu kwa benki
za biashara ili nazo zitoe mikopo ya nyumba ya muda
mrefu kwa wananchi ambapo mafanikio yafuatayo
yamepatikana:-
i. Benki za biashara 20 zimetoa mikopo ya muda
mrefu yenye riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba kwa wananchi 3,598;
ii. Mfuko wa Mikopo Midogo Midogo ya Nyumba
(Housing Micro-finance Fund) umeanzishwa chini
ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Aidha, mtaji
wa Shilingi bilioni 36 zimetengwa kwa ajili ya
Mfuko wa Dhamana ya Mikopo ya Nyumba
(TMRC);
iii. Mwongozo kuhusu sifa za taasisi za fedha
zinazostahili kupata mkopo kutoka TMRC
umeandaliwa; na
iv. Mpango wa kutoa elimu kwa umma kuhusu
Sheria, Kanuni na Taratibu za mikopo ya
nyumba umeandaliwa.
(o) Ujenzi wa Nyumba na Majengo ya Serikali:
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015, Serikali
kupitia Wakala wa Majengo (TBA) imendelea na ujenzi
wa ofisi za Serikali, nyumba za viongozi na mradi
wa nyumba 10,000 kwa ajili ya watumishi wa umma
katika mikoa mbalimbali nchini. Ujenzi wa majengo
41
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ya umma umekuwa ukizingatia mahitaji maalumu ya
watu wenye ulemavu.
37. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuendelea kutekeleza
mipango ya kuendeleza ardhi katika maeneo yafuatayo:-
(a) Utawala wa Ardhi
(i) Kujenga mfumo utakaorahisisha umilikishaji
wa ardhi na uhifadhi wa kumbukumbu za ardhi
kwa kukamilisha ujenzi wa Mfumo Unganishi
wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi (Integrated
Land Management Information System);
(ii) Kuimarisha huduma za ardhi katika Kanda
kwa kujenga majengo manane (8) ili kusogeza
huduma za ardhi karibu na wananchi katika
Kanda za Nyanda za Juu Kusini (Mbeya),
Ziwa (Mwanza), Kaskazini (Moshi), Magharibi
(Tabora), Kati (Dodoma), Kusini (Mtwara),
Kanda ya Mashariki, na Kanda ya Dar es Salaam
inayohudumia mkoa wa Dar es Salaam;
(iii) Kuimarisha utoaji wa huduma za ardhi katika
Kanda nane (8) za Ardhi nchini kwa lengo la
kuongeza kasi ya utoaji wa Hatimiliki za Kimila
nchini;
(iv) Kuzijengea uwezo Halmashauri za Miji na
Wilaya kwa kuzipatia mafunzo, vifaa, rasilimali
fedha na wataalamu ili ziweze kupima viwanja
na mashamba nchini;
(v) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Fidia ya Ardhi
ili uweze kufidia ardhi itakayotwaliwa kwa
matumizi ya umma na uwekezaji;
(vi) Kufanya uhakiki wa mashamba pori
yasiyoendelezwa kwa kipindi kirefu na kugawa
upya kwa wananchi;
42
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(vii) Kuanzisha Baraza la Taifa la Ushauri la Ardhi
(National Land Advisory Council) ili kuwezesha
ardhi kutumika kwa ufanisi;
(viii) Kutoa elimu kwa umma juu ya Sheria za Ardhi,
Sheria ya Mipangomiji, Sheria ya Mipango
ya Matumizi ya Ardhi na Sheria zingine
zinazohusiana na utawala wa ardhi;
(ix) Kuimarisha huduma ya utatuzi wa migogoro
ya ardhi kwa kuanzisha Mabaraza mapya 100
ya Ardhi na Nyumba kwenye wilaya zenye
migogoro mingi ya ardhi;
(x) Kuhakikisha maafisa ardhi wasio waaminifu
wanashughulikiwa; na
(xi) Kuanzisha akiba ya ardhi (land bank).
(b) Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya
ardhi nchini
(i) Kuendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa
Matumizi ya Ardhi;
(ii) Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya
vijiji 7,500 na mipango ya matumizi ya ardhi ya
Wilaya 25;
(iii) Kukamilisha upimaji wa mipaka ya vijiji vyote
nchini;
(iv) Kuwapatia wananchi hatimiliki za kimila
2,500,000 pamoja na kujenga masjala za ardhi
250 katika ngazi za Wilaya na Vijiji; na
(v) Kuwapatia wananchi hati miliki 2,000,000
pamoja na kusajili nyaraka nyingine za kisheria.
43
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Nyumba
(i) Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu
na kwa masharti nafuu;
(ii) Kuwaelimisha wananchi kuzielewa sheria
za mikopo ya nyumba ili wazitumie kupata
mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya kujenga au
kununua nyumba na kuhamasisha mabenki na
asasi nyingine za fedha zitoe mikopo ya nyumba
ya muda mrefu na yenye riba nafuu;
(iii) Kuweka utaratibu utakaowezesha kuanzisha
Benki ya Nyumba ya Taifa;
(iv) Asasi za Serikali kwa kushirikiana na sekta
binafsi zitajenga nyumba za gharama nafuu
zisizopungua 50,000;
(v) Kuwawezesha wanavijiji kujiunga kwenye
vikundi vya ujenzi vitakavyopatiwa elimu ya
jinsi ya kujenga nyumba bora vijijini;
(vi) Kuliwezesha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
kuwa Mwendelezaji Miliki Mkuu (Master Estate
Developer);
(vii) Kupunguza kodi kwenye vifaa vya ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu hususan vijijini;
(viii) Kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika
vya ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu;
(ix) Kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujenga
nyumba bora kwa kutumia vifaa vya ujenzi vya
gharama nafuu; na
(x) Kujenga nyumba za watumishi wa umma na
majengo ya serikali yenye kuzingatia mahitaji
maalumu ya watu wenye ulemavu kwa:-
44
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Kuanza ujenzi wa majengo yatakayotumika
kama Ofisi kwa Taasisi za Serikali ili
kuipunguzia Serikali gharama ya kodi
kubwa ya pango katika soko huria;
• Kuendelea na mradi wa ujenzi wa nyumba
10,000 kwa ajili ya watumishi wa umma
ambapo asilimia 50 zitajengwa katika
maeneo ya vijijini; na
• Kuboresha karakana 6 za kutengeneza
samani za ofisi na nyumba za Serikali ili
kupunguza gharama za uagizaji wa samani
kutoka nje ya nchi.
(xi) Kukamilisha utungaji wa Sera ya Taifa ya
Nyumba (Housing Policy).
(xii) Kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti na Uendelezaji
wa Miliki (Real Estate Regulatory Authority)
ambayo pamoja na majukumu mengine
itasimamia udhibiti wa kodi za pango kwa
nyumba za makazi na biashara.
(d) Mipango Miji na Vijiji
(i) Kukamilisha uandaaji wa Mipango Kabambe
(Master Plans) kwa miji mikuu yote ya mikoa;
(ii) Kuhimiza ujenzi wa miji ya pembezeno (Satilite
cities) katika jiji la Dar es Salaam pamoja na
miji mingine ili kufanya miji hiyo ikue kwa
kuzingatia mipango miji;
(iii) Kuendelea kujenga mji mpya wa Kigamboni
(Kigamboni New City) kwa kuzingatia matakwa,
maslahi na ushiriki wa wananchi wa Kigamboni;
(iv) Kuendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya
Kurasimisha Makazi yaliyopo katika maeneo
ambayo hayajapimwa kwa lengo la kuyapanga
45
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na kuyapima viwanja katika miji ya Dar es
Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga, Morogoro na
Mbeya. Program hii itatoa hatimilki za Makazi;
(v) Kuendeleza maeneo yaliyoiva (re-development
scheme) ya Kipawa, Namanga, Vingunguti,
Manzese, Buguruni, Msasani Bonde la Mpunga
na Kawe, Jijini Dar es Salaam.
(e) Upimaji na Ramani
Upimaji wa ardhi na utayarishaji wa ramani ni chanzo
muhimu cha taarifa zinazohitajika katika kubuni na
kutayarisha mipango ya matumizi ya ardhi kwa sekta
mbalimbali. Hadi sasa ni sehemu ndogo tu ya ardhi
ya nchi imepimwa, hivyo ili kuifanya ardhi kuchangia
katika kukuza Pato la Taifa, kutoa fursa za ajira na
kuvutia uwekezaji ipo haja ya kuongeza kasi ya
upimaji wa ardhi.
Katika kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(i) Kuendeleza upimaji wa ardhi katika maeneo ya
mipaka ya nchi ili kuimarisha ulinzi na usalama;
(ii) Kuimarisha alama za mipaka kati ya Tanzania
na nchi jirani za Kenya, Burundi, Zambia,
Malawi, Uganda, Rwanda, Msumbiji na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo;
(iii) Kujenga kituo cha kupokea picha za anga
(Satellite Receiving Station) kitakachojengwa
katikati ya nchi (Chuo Kikuu cha Dodoma)
ambacho kitawezesha utayarishaji wa ramani
za msingi (base maps), kupanga na kuongeza
kasi ya kupima ardhi kwa ajili ya matumizi
mbalimbali; na
(iv) Kuzijengea uwezo wa rasilimali watu na
fedha Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji
na kuzipatia zana za kisasa za kupima ardhi
46
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na usanifu wa ramani na kuwapatia mafunzo
stahiki watalaamu wa ardhi.
Usafirishaji na Uchukuzi
38. Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafiri na
usafirishaji umechochea kukua kwa shughuli za kiuchumi
ambazo zimewezesha pia kuongeza ajira nchini. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea
kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi na ukarabati
wa miundombinu ya barabara, reli, madaraja, vivuko na
viwanja vya ndege ambao umekuwa msingi wa kukua kwa
uchumi wetu na shughuli nyingine za kijamii. Tanzania
imepiga hatua kubwa katika sekta hii na kuifanya kuwa
moja kati ya nchi zenye mtandao mzuri wa miundombinu
ya usafiri hususan barabara katika Bara la Afrika.
(a) Barabara
Nchi yetu ina mtandao wa barabara wenye jumla ya
urefu wa kilometa 35,000 zinazojumuisha kilometa
12,786 za barabara kuu na kilometa 22,214 za barabara
za mikoa.
Katika kipindi cha miaka kumi cha uongozi wa Serikali
ya Awamu ya Nne, barabara zenye urefu wa jumla ya
kilometa 13,753 zimekuwa katika hatua mbalimbali
za ujenzi ambapo jumla ya barabara zenye urefu wa
kilometa 4,691 zimekamilika kujengwa kwa kiwango
cha lami na barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa
2,358 zimeendelea kujengwa katika kiwango cha lami.
Aidha, jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa
3,419 zimefanyiwa upembuzi na usanifu kwa ajili ya
ujenzi. Barabara hizo ni kama zilivyoanishwa:-
47
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Barabara ambazo zimekamilika kujengwa kwa
kiwango cha lami:
• Korogwe – Handeni (km 65)
• Dumila – Rudewa (km 45)
• Lwanjilo – Chunya (km. 36)
• Tanga – Horohoro (km 65)
• Masasi – Mangaka (km 54)
• Minjingu – Babati - Singida (km 222)
• Mwandiga – Manyovu (km 60)
• Handeni – Mkata (km 54)
• Barabara ya Kilwa/Dsm (km 12)
• Barabara ya Mandela/Dsm (km 16)
• Msimba – Ikokoto – Mafinga (km 219)
• Arusha – Namanga (km 105)
• Chalinze – Segera –Tanga (km 245)
• Isaka – Ushirombo (km 132)
• Rau Madukani – Mawela – Uru Njari (km
12.5)
• Tunduma – Sumbawanga (km 230)
• Sehemu ya Bonga – Babati (km 19.2)
• Dodoma – Iringa (km 260)
• Puge – Tabora (km 56)
• Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.30)
• Tabora – Ndono (km 42)
• Uvinza – Kidahwe (km 77)
• Daraja la Malagarasi na Barabara zake (km
48)
• Namtumbo – Songea (km 70)
• Peramiho – Mbinga (km 78)
• Ujenzi kwa sehemu ya Mwenge – Tegeta
(km 12.9)
• Segera – Korogwe (km 20)
48
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Korogwe – Mkumbara (km 76
• Arusha – Minjingu (km 104)
• Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85)
• Banana – Kitunda – Kivule – Msongola (km
3.2)
• Msoga – Msolwa (Chalinze Bypass) Km 10)
• Barabara ya Mafia (Mafia Access Road) (km
14)
• Barabara ya Dodoma University (km 12)
(ii) Barabara ambazo zipo katika hatua mbalimbali
za ujenzi:
• Mziha – Turiani – Magole (km 84.6)
• Dumila – Kilosa (km 63)
• Dumila – Turiani - Handeni (km 174)
• Bariadi – Lamadi (km 71.8)
• Mbeya – Chunya – Makongolosi (km 115)
• Makofia – Msata (km 64)
• Kisarawe – Maneromango (km 54)
• Ushirombo – Lusahunga (km 110)
• Kwa Sadala – Masama (km 12.2)
• Kibosho Shine – Kwa Raphael – International
School (km 43)
• Kirua Nduoni – Marangu Mtoni (km 31.5)
• Kahama Mjini (km 5)
• Bunda – Kisorya – Nansio (km 93)
• Dodoma – Babati (km 261)
• Sumbawanga – Kinyani – Nyakanazi (km
562)
• Nzega – Tabora (km 116)
• Manyoni – Itigi – Tabora (km 264)
• Mangaka – Mtambaswala (km 65)
49
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Mto wa Mbu – Loliondo – Mugumu – Nata-
Makutano (km 452)
• Tunduru – Namtumbo (km 194)
• Tabora – Urambo (km 90)
• Uyovu – Bwanga – Biharamulo (km 112)
• Kisesa – Usagara (km 17)
• Kyaka – Bugene (km 59)
• Segera – Same – Himo (km 261)
• Arusha – Moshi – Himo – Holili (km 140)
• Nyanguge – Musoma – Sirari (km 262)
• Katumba – Mbambo – Tukuyu (km 80)
• Kaliua – Kazilambwa (km 56)
• Barabara ya Kibamba – Monganzila (km
4.0)
• Barabara ya KIA – Mererani (km 26)
• Mafinga – Igawa (km 137.9)
• Mwigumbi – Maswa – Bariadi (km 100)
• KAMATA – Bendera Tatu (km 1.3)
• Ardhi – Makongo – Goba (km 9)
(iii) Barabara ambazo zimefanyiwa upembuzi
na usanifu na baadhi ya maeneo ujenzi kwa
kiwango cha lami unaendelea:
• Makurunge – Saadan – Pangani – Tanga
(km 178)
• Rujewa – Madibira – Mafinga (km 151)
• Matai – Kasesya (km 50)
• Mbinga – Mbamba Bay (km 66)
• Kamwanga – Sanya Juu (km 75)
• Makambako – Songea (km 295)
• Mtwara – Masasi (km 200)
• Sanya Juu – Bomang’ombe (km 25)
50
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Tabora – Mbambali – Bukene – Itobo –
Kahama (km 149)
• Lupilo – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo –
Londo – Kitanda (km 96)
• Ifakara – Mahenge (km 67)
• Kibondo – Mabamba (km 35)
• Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala –
Oldeani Jct (km 328)
• Omugakorongo – Kigarama – Murongo
(km 105)
• Mpemba – Isongole (Tanzania/Malawi)
(km 49)
• Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe (km
74)
• Makofia – Mlandizi – Vikumburu (km 148)
• Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 162)
• Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyankulu –
Kahama (km 428)
• Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (km 412)
• Mtwara – Newala – Masasi (km 209)
• Handeni – Kiberashi – Kondoa – Singida
(km 460)
• Kibaha – Mapinga (km 23)
• Geita – Bukoli – Kahama (km 107)
• Mbande – Kongwa Jct – Mpwapwa (km 50)
• Njombe – Makete (km 109)
• Nata – Fort Ikoma (km 141)
• Ipole – Koga – Mpanda (km 255)
• Dsm (Port) – TAZARA – JNIA – Pugu (km
29)
• Outer ring road (Pugu – Kinyerezi – Mbezi
(Morogoro) – Mpiji Magore – Bunju (km 34)
• Barabara ya Dar es Salaam – Chalinze –
Morogoro (km 200)
51
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Sehemu ya Dar es Salaam – Chalinze (km
100) “Express way”
• Musoma – Makojo – Busekela (km 92)
• KAMATA – Bendera Tatu (km 1.3)
• Ardhi – Makongo – Goba (km 9)
• Daraja jipya la Selander (DSM)
• Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa
(km 430)
• Barabara ya Nyamirembe Port – Katoke
(km 50)
• Barabara ya Murugarama – Rulenge –
Nyakahura (km 85)
• Barabara ya Ipole – Rungwa (km 172)
• Barabara ya Uongozi Institute (km 8.8)
• Barabara ya Mwanangwa – Misasi – Salawe
– Kahama (km 149)
(b) Madaraja
(i) Ujenzi wa daraja la Kilombero umeanza.
(ii) Ujenzi wa daraja la mto Mwatisi (Morogoro)
umekamilika.
(iii) Ujenzi wa daraja la mto Malagalasi Kigoma,
umekamilika.
(iv) Ujenzi wa daraja la Kigamboni ili kuunganisha
Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam umekamilika
kwa zaidi ya asilimia 80.
(v) Ujenzi wa daraja la Nangoo (Masasi), Ruhekei
(Mbinga) na Mbutu (Igunga) umekamilika.
(vi) Ujenzi wa daraja la Rusumo (Kagera)
umekamilika.
(vii) Ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu la
Mabatini (Mwanza) umekamilika.
52
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(viii) Ujenzi wa daraja la Sibiti (Singida) unaendelea.
(ix) Upembuzi yakinifu na usanifu wa daraja la
Ruhuhu (Ruvuma) umekamilika.
(x) Ujenzi wa daraja la Kavuu (Katavi) unaendelea.
(c) Vivuko
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) imenunua vivuko vinane kwa ajili ya kutoa
huduma katika maeneo mbalimbali Nchini.
(i) Msangamkuu (Mtwara)
(ii) Rusumo (Kagera) na
(iii) Ilagala (Kigoma)
(iv) Kahunda – Maisome
(v) Kahunda – Musoma – Kinesi
(vi) Kahunda – Kisorya – Rugezi
(vii) Dar es Salaam – Bagamoyo
(d) Kupunguza Msongamano katika Jiji la Dar es
Salaam
Ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la
Dar es Salaam, Serikali imefanya mambo yafuatayo:-
(i) Usanifu wa kina umekamilika kwa makutano
ya TAZARA na Ubungo kwa ajili ya kujenga
barabara za juu; na
(ii) Serikali inaendelea kupanua mtandao wa
barabara kwa kujenga na kukarabati barabara
zifuatazo:-
• Mbezi (Morogoro road) – Malambamawili –
Kinyerezi – Banana (km 14.0)
53
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Tegeta Kibaoni – Wazo – Goba – Mbezi
mwisho (km 20.0)
• Tangi Bovu – Goba (km 9.0)
• Kimara – Baruti – Msewe – Changanyikeni
(km 2.6)
• Kimara – Kilungule – External Mandela
road (km 9.0)
• Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Kigogo
Round about (km 6.4)
• Kigogo Round about – Bonde la Msimbazi –
Twiga/Msimbazi (km 2.7)
• Tabata Dampo – Kigogo – Ubungo Maziwa
(km 2.25)
• Old Bagamoyo – Garden Road (km 9.0)
Usanifu umekamilika
• Jet Corner – Vituka – Devis Corner (km 6)
ujenzi umekamilika
(iii) Ujenzi wa awamu ya kwanza ya miundombinu
ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit
– BRT): Kimara – Kivukoni, Fire-Kariakoo na
Magomeni – Morocco (km 20.9) unaendelea.
39. Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, Chama
Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuendelea
kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja,
vivuko, nyumba na majengo ya Serikali kwa lengo la
kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za
kijamii. Aidha, kipaumbele katika ujenzi wa barabara
kitazingatia barabara zinazounganisha nchi yetu na nchi
jirani; barabara zinazounganisha mikoa; na barabara
zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi
kama vile Liganga, Mchuchuma n.k. Ili kutimiza azma
hiyo Serikali itafanya mambo yafuatayo:-
54
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuimarisha Mfuko wa Barabara (Tanzania Road
Fund)
(i) Kubuni vyanzo vipya na kuimarisha ukusanyaji
wa mapato yatokanayo na vyanzo vya sasa ili
kuongeza mapato;
(ii) Kubuni/kuboresha mfumo wa ufuatiliaji na
tathmini ili kuhakikisha kwamba thamani na
ubora wa kazi unaendana na fedha zilizotumika
(value for money); na
(iii) Kuanzisha wakala/taasisi itakayosimamia kazi
za ujenzi na matengenezo ya barabara za miji
na majiji na Halmashauri ambazo ziko chini ya
TAMISEMI.
(b) Masuala ya Kisera
Ili kupunguza umasikini, kuwawezesha wananchi
kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo, Serikali
itashughulikia masuala yafuatayo:-
(i) Kuunganisha makao makuu ya mikoa ambayo
bado haijaunganishwa kwa barabara za lami
na kujenga barabara kuu zote zinazounganisha
Tanzania na nchi jirani kwa kiwango cha lami;
(ii) Kuhakikisha kuwa makao makuu ya Wilaya
ambazo bado barabara zake hazipitiki majira
yote zinafanyiwa ukarabati angalau kwa
kiwango cha changarawe na kuzifanya zipitike
majira yote ya mwaka;
(iii) Kupunguza umaskini kwa kushirikisha
kikamilifu vikundi vya wananchi katika kazi
za matengenezo madogo madogo ya barabara
kama vile kazi za kufyeka nyasi, kuzibua mifereji
na kufanya usafi wa barabara zinazopita katika
maeneo yao; na
55
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iv) Makandarasi wazalendo wanaoonesha nia
ya kushiriki katika kazi kubwa za ujenzi wa
barabara watapatiwa dhamana na Serikali
ili kuwajengea uwezo na kuwapatia fursa za
kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za sekta
ya ujenzi.
(c) Kukamilisha ukarabati wa barabara zote
unaoendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami
ambao umekwishaanza katika barabara kuu na
barabara za mikoa:-
(i) Kukamilisha Ujenzi (km 2,439.35)
• Sumbawanga - Matai - Kasanga (km 56 kati
ya km 112)
• Mziha - Turiani - Magole (km 75 kati ya km
84.6)
• Dumila - Kilosa (km 18 kati ya km 63)
• Dumila – Turiani - Handeni (km 174)
• Bariadi - Lamadi (km 13 kati ya km 71.8)
• Mbeya - Chunya - Makongolosi (km 56 kati
ya km 115)
• Bagamoyo - Makofia - Msata (km 7 kati ya
km 64)
• Kisarawe - Maneromango (km 48 kati ya
km 54)
• Kibosho Shine - Kwa Raphael - International
School (km 24 kati ya km 43)
• Kirua - Nduoni - Marangu Mtoni (km 16
kati ya km 31.5)
• Nyamuswa - Bunda - Kisorya - Nansio (km
117 kati ya km 117.5)
• Babati - Dodoma (km 195.15 kati ya km 251)
56
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Sumbawanga - Kanyani - Nyakanazi (km
483.7 kati ya km 562)
• Nzega - Tabora (Puge) (km 20.5 kati ya km
116)
• Manyoni - Itigi - Tabora (km 113 kati ya km
264)
• Mangaka - Mtambaswala ( km 65)
• Makutano - Nata - Mugumu (km 125)
• Kyaka - Bugene (km 28 kati ya km 59)
• Tunduru - Namtumbo (km 194)
• Tunduru - Mangaka (km 137)
• Mwigumbi - Maswa - Bariadi (100)
• Tabora - Urambo (km 8.8 kati ya km 90)
• Uyovu - Bwanga - Biharamulo (km 112)
• Kisesa - Usagara (km 17)
• Mganza - Kasenda (km 4.2)
• Katumba - Mbambo - Tukuyu (km 80)
• Kidahwe - Kasulu (Kanyani) (km 50)
• Kikusya - Ipinda - Matema Beach (km 39.5)
• KIA - Mererani (km 26)
• Mwanga - Kikweni - Lomo (km 7.5 kati ya
km 22.5)
• Kaliua - Kazilambwa (km 42 kati ya km 56)
• Singida - Sepuka - Ndago - Kizaga (75 kati
ya km 89)
• Dodoma University Road (km 12)
57
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kukamilisha Ukarabati (km 517.2)
• Ushirombo - Lusahunga (km 67 kati ya km
110)
• Kawawa Jct - Mwenge (km 4.3)
• Segera - Same - Himo (km 131 kati ya 285)
• Nyanguge - Musoma - Sirari (km 177 kati ya
km 262)
• Mafinga - Igawa (km 137.9)
(d) Kuanza ujenzi mpya na ukarabati wa barabara
kwa kiwango cha lami
(i) Kuanza ujenzi (km 5,427.0)
• Njombe - Makete (km 109)
• Nata - Fort Ikoma (km 30)
• Mto wa Mbu - Loliondo (km 213)
• Sanya Juu - Bomang’ombe (km 25)
• Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 359)
• Matai - Kasesya (km 50)
• Sanya Juu - Kamwanga (km 75)
• Rujewa - Madibila - Mafinga(km 151)
• Makurunge - Saadani - Pangani - Tanga (km
178)
• Mbinga - Mbamba bay (km 66)
• Mtwara - Mingoyo - Masasi (km 200)
• Mpemba - Isongole (Tanzania/Malawi) (km
49)
• Makongolosi - Rungwa - Mkiwa (km 412)
• Mtwara - Newala - Masasi (km 209)
• Kibaha - Mapinga (km 23)
58
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Geita - Bukoli - Kahama (km 107)
• Mbande - Kongwa Jct - Mpwapwa (km 50)
• Ipole - Rungwa (km 172)
• Njombe (Kibena) - Lupembe - Madeke
(Mfuji) Morogoro/Njombe Boarder (km
125)
• Njombe - Ndulamo - Makete - Kitulo -
Isyonje(km 205)
• Itoni - Ludewa - Manda (km 211)
• Dar es Salaam - Chalinze - Morogoro express
way (km 190)
• Musoma - Makojo - Busekera (km 92)
• Tabora - Mambali - Bukene - Itobo - Kahama
(km 149)
• Lupilo - Malinyi - Kilosa kwa Mpepo -
Londo - Kitanda (km 296)
• Ifakara - Mahenge (km 67)
• Kibondo - Mabamba (km 35)
• Kolandoto - Lalago - Mwanhuzi - Matala -
Oldeani Jct (km 328)
• Mugakorongo - Kigarama - Murongo (km
105)
• Soni - Bumbuli - Dindira - Korogwe (km 74)
• Makofia - Mlandizi - Vikumburu (km 148)
• Handeni - Kiberashi - Kondoa - Singida (km
460)
• Pugu - Kifuru - Mbezi Mwisho - Mpiji
Magoe - Bunju (km 34)
• Kisarawe - Mlandizi (km 52)
• Kiboroloni - Tsuduni - Kidia (km 10.8)
59
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• TPC - Mabogini - Kahe (km 11.4)
• Nyamirembe Port - Katoke (km 50)
• Iringa - Ruaha National Park (km 104)
• Njombe (Ramadhani) - Iyayi (km 74)
• Mziha – Handeni (km 68)
• Kilosa – Mikumi (km 72.8)
(ii) Kuanza Ukarabati (km 1,055.12)
• Arusha - Moshi - Himo-Holili (km 140)
• Makambako - Songea (km 295)
• Mtwara - Mingoyo - Masasi (km 200)
• Lusahunga - Rusumo (km 92)
• Nyakasanza - Kobero (km 60)
• Mlandizi - Chalinze (km 53)
• Mbeya -Tunduma (km 110)
• Igawa - Uyole (km 105.12)
(e) Kuzifanyia upembuzi na usanifu wa kina km
6,530.7 barabara zifuatazo:-
• Kibaoni - Majimoto - Inyonga (km 162)
• Mpanda - Ugala - Kaliua - Ulyankulu - Kahama
(km 428)
• Arusha - Kibaya - Kongwa (km 430)
• Bugene - Kasulo (BENACO) (km 124)
• Mbeya - Igawa (km 116)
• Mbeya - Tunduma (km 104)
• Murshaka – Murongo (km 125)
• Kilindoni – Ras Mkumbi (km 55) - Mafia
• Morogoro - Dodoma (km 263)
• Mwanza - Mwanza/Shinyanga (km 102)
60
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Mwanangwa - Misasi - Salawe - Kahama (km
149)
• Kibaoni - Majimoto - Kasansa - Muze -
Kilyamatundu (km 200)
• Magu - Bukwimba - Ngudu - Jojiro (km 64)
• Tarime - Mugumu (km 87)
• Njombe - Iyayi (km 74)
• Amani - Muheza (km 34)
• Nyahunge – Sengerema (km 68)
• Mugakorongo - Rwambaizi – Murongo (km 125)
• Morogoro (Bigwa) - Mvuha (km 78)
• Morogoro Kibena -Lupembe-Mfuji (Morogoro/
Njombe Boarder) (km 125)
• (Bigwa) - Kisaki (km 151)
• Kamanga - Sengerema (km 35) (Mwanza)
• Geita - Nzera - Nkome (km 54) (Geita)
• Upanuzi wa (Tegeta) - Bagamoyo (km 57)
• Kibada - Kimbiji (km 29.2)
• Murugarama - Rulenge - Nyakahura (km 85)
• Karatu - Mbulu - Haydom - Singida (km 190)
• Ba r i a d i - K i s e sa-Mwandoya-Ngoboko-
Mwanhuzi-Sibiti-Mkalama-Iguguno (km 289)
• Mika - Utegi - Shirati (km 44)
• Chimala - Matamba - Kitulo (km 51)
• Upanuzi wa Kitonga Escarpment (km 10)
(Iringa)
• Babati - Orkesumet - Kibaya (km 225)
• Kongwa – Mbuyuni NARCO JCT – Kibaya –
Orkemet (km 340)
61
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Mbulu - Magugu (Mbuyu wa Mjerumani) (km
63)
• Mafinga - Mgololo (km 77.6)
• Nyololo - Igowole - Mtwango (km 40.4)
• Igowole - Kasanga - Nyigo (km 54.5)
• Madaba - Mundindi (Liganga) - Mkiu (km 46)
(Ruvuma)
• Kilwa - Liwale (km 258)
• Liwale - Nachingwea - Ruangwa (185)
• Kitai - Lituhi (km 93)
• Babati (Dareda) – Dongobesh (km 60)
• Mhutwe - Kamachumu - Muleba (km 53)
• Uru – Mamboleo – Materuni (km 10.2)
• Kongwa Ranch - Kiteto - Simanjiro - KIA (km
483)
• Mto wa Mbu - Longido - Karatu - Ngorongoro
(km 300)
• Sanya Juu – Longido (km 65)
• Madaba – Mavanga – Ludewa (km 40)
• Likuyufusi – Mkenda (km 124)
(f) Madaraja
(i) Kukamilisha ujenzi wa madaraja sita (6)
yafuatayo:-
• Kilombero na barabara za maingilio km 9
• Kigamboni na barabara za maingilio km 10
• Kavuu (Katavi)
• Sibiti (Singida)
• Lukuledi II (Lindi)
• Ruvu Chini (Pwani)
62
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kuanza ujenzi / Ukarabati wa madaraja saba
(7) yafuatayo:-
• Ruhuhu (Ruvuma)
• Momba (Rukwa)
• Kirumi (Mara)
• Selander (daraja jipya) (DSM)
• Magara (Manyara)
• Wami Chini (daraja jipya) (Pwani)
• Pangani (Tanga)
(iii) Kuanza usanifu wa madaraja matatu (3)
yafuatayo:-
• Daraja la Simiyu (Mwanza)
• Mzinga (DSM) na
• Mlalakuwa (DSM)
Muonekano wa Daraja la Kigamboni litakapokuwa limekamilika
kujengwa. Ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80.
63
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Kupunguza msongamano wa magari katika Jiji
la Dar Es Salaam kwa kufanya yafuatayo:-
Kuanza ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) kwenye
makutano ya barabara maeneo yafuatayo:-
• TAZARA
• Ubungo
• Chang’ombe
• Uhasibu
• KAMATA
• Morocco
• Mwenge
• Magomeni
• Tabata
Kuanza na kukamilisha ujenzi wa barabara na reli
ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la
Dar es Salaam:-
(i) Kukamilisha Ujenzi (km 80.1)
• Mbezi - Malamba Mawili - Kinyerezi -
Banana ( km 14)
• Tegeta Kibaoni - Wazo Hill - Goba - Mbezi/
Morogoro Road (km 16.2 kati ya km 20)
• Tangi Bovu - Goba (km 5.2 kati ya km 9)
• Kimara Baruti - Msewe - Changanyikeni
(km 2 kati ya 2.6)
• Kimara Kilungule - External Mandela Road
(km 8.8 kati ya 9)
• Kigogo Round About - Bonde la Msimbazi -
Twiga/Msimbazi Jct.km(km 0.5 kati km 2.7)
64
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Tabata Dampo - Kigogo (km 1.6 kati ya km
2.25)
• Kibamba - Mlonganzila (km 8 kati ya km 12
• Upanuzi wa barabara ya Kimara - Kibaha
na Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji
(km 23.8 kati ya km 25)
(ii) Kuanza Ujenzi (km 58.8)
• Upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki
(Morocco - Kawe Round About) na Garden
Road ( km 9.1)
• Banana - Kitunda - Kivule – Msongola (km
14.7)
• Ardhi - Makongo - Goba (km 9)
• Upanuzi wa barabara ya Uwanja wa Ndege
(JNIA) - Pugu (km 8)
• Upanuzi wa barabara ya Mbagala -
Kongowe – Mwandege (km 4)
• Upanuzi wa barabara ya DSM Port
-TAZARA - Uwanja wa Ndege (JNIA) (km
14)
(iii) Kuanza ujenzi wa miundombinu ya mradi wa
mabasi yaendayo haraka (BRT) Awamu ya Pili
(II) na ya Tatu (III):-
• Awamu ya II: Barabara ya Kilwa na Kawawa
(km 19.3)
• Awamu ya III: Barabara za Nyerere, Uhuru,
Bibi Titi Mohamed na Azikiwe (Km 23.6)
(iv) Kuanza ujenzi wa reli ya usafirishaji wa abiria
katika jiji la Dar es Salaam.
65
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(h) Miradi ya kupunguza msongamano katika majiji na
miji mingine yenye jumla ya km 102 kama ifuatavyo:-
• Usagara - Kisesa (km 17) (Mwanza)
• Shabiby - Arusha road Round about (km 1.6)
(Dodoma),
• Uyole - Songwe (km 40) (Mbeya)
• Iringa Bypass (km 7)
• Upanuzi wa barabara Mwanza - Mwanza
Airport (km12),
• Upanuzi wa Babara ya Arusha Mjini - Kisongo
(km 8.8),
• Babati Bypass (km. 12)
• Utofu - Majani Mapana - Duga Mwembeni (km
4) (Tanga)
(i) Vivuko
Kuimarisha usafiri wa majini katika mito, maziwa na
bahari ili kufanya barabara kuwa na kiunganishi cha
uhakika kwa kutekeleza miradi ifuatayo:-
(i) Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo - Busisi
Mkoani Mwanza;
(ii) Kuanza ujenzi wa kivuko kipya cha Rugezi -
Kisorya mkoani Mwanza;
(iii) Kuanza ujenzi wa kivuko kipya cha Pangani -
Bweni mkoani Tanga;
(iv) Upanuzi wa jengo la abiria wa kivuko cha
Magogoni - Kigamboni upande wa Kigamboni;
na
(v) Kuanza ujenzi wa Kivuko kipya cha Magogoni –
Kigamboni.
66
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Uchukuzi
40. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha
huduma za usafiri na usafirishaji wa reli, majini na usafiri
wa anga na mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Mashirika ya Reli
(i) Shirika la Reli nchini (TRL) limeendelea
kuimarishwa kwa kufanya yafuatayo:-
• Kununua na kukarabati vifaa mbalimbali
(vichwa vya treni, mataruma, na mitambo
ya kunyanyulia mabehewa);
• Kutandika reli za ratili 80 kwa yadi kutoka
Kitaraka hadi Malongwe (kilometa 89);
• Ujenzi wa Madaraja makubwa matatu ya
stesheni za Kilosa na Gulwe; na stesheni za
Bahi na Kintinku; na
(ii) Kwa upande wa shirika la TAZARA,
vichwa vya treni vya njia kuu vipya sita
(6); mabehewa ya mizigo 90; vipuri vya
matengenezo ya vichwa vya treni vitatu (3);
na ukarabati wa mitambo ya kunyanyulia
mizigo vinne (4) vimenunuliwa na ukarabati
umefanyika. Aidha, mazungumzo kati ya
Serikali ya Tanzania na Zambia yanaendelea
ili kuboresha shirika hilo.
(b) Ujenzi wa Reli Mpya
Upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Reli mpya
ya Dar es Salaam-Kigali (Rwanda) na Msongati
(Burundi) kwa kiwango cha kimataifa (standard
gauge) umekamilika. Aidha, upembuzi yakinifu na
usanifu kwa ajili ya ujenzi wa reli kwa kiwango cha
kimataifa kutoka Isaka hadi Mwanza umekamilika.
67
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Bandari
(i) Huduma za uchukuzi kwenye maziwa
zimeendelea kuimarishwa kwa kuboresha
bandari za Kigoma, Mbamba Bay, Mwanza,
Bukoba na Nansio; ikiwa ni pamoja na kuondoa
mchanga katika bandari ya Kigoma, kukarabati
chelezo, kufunga maboya ya kuongozea meli,
kununua Mobile Grove Crane tani 35, kununua
mtambo wa kuondoa mchanga majini (dreadger)
na upembuzi yakinifu wa Bandari Kavu ya
Katosha. Aidha, uthamini wa eneo la Kibirizi
kwa ajili ya kujenga maegesho ya vyombo
vidogo vidogo vya majini umekamilika;
(ii) Bandari ya Dar es Salaam imeendelea
kuboreshwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
boya la mafuta (SPM) na ununuzi wa vifaa vya
kuhudumia mizigo. Aidha, upembuzi yakinifu
wa kuboresha gati namba 1-7 na utafiti wa ujenzi
wa gati (RoRo) kwa ajili ya kuhudumia meli za
magari; ujenzi wa mfumo wa kuhamisha mizigo
(conveyor system) na maghala (silo) kwa ajili ya
kuhudumia shehena ya Kichele umekamilika.
(iii) Eneo la Msanga Mkuu lenye hekta 2,623 kwa
ajili ya uendelezaji wa Bandari ya Mtwara
na shughuli za EPZ limetengwa na kazi ya
upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa
Bandari hiyo umekamilika; na
(iv) Ujenzi wa gati jipya la kisasa katika bandari ya
Kilindoni-Mafia umekamilika.
(d) Viwanja vya Ndege
(i) Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili
ya kuboresha na kupanua jengo la pili la abiria
katika Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere
umekamilika;
68
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Songwe umekamilika na kuanza kutoa huduma
za usafiri wa anga. Aidha, ujenzi wa jengo
kubwa la abiria na uzio wa kiwanja unaendelea
kukamilishwa;
(iii) Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Kiwanja
cha Ndege cha Mtwara umekamilika. Aidha,
matengenezo katika jengo la abiria na barabara
ya kurukia na kutua ndege umekamilika;
(iv) Mradi wa kuboresha Kiwanja cha Ndege cha
Kigoma awamu ya kwanza umekamilika. Aidha,
upanuzi na ukarabati wa kiwanja hicho awamu
ya pili chini ya ufadhili wa Benki ya Uwekezaji
ya Ulaya umekamilika;
(v) Kazi za upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha
Ndege cha Bukoba kwa kiwango cha lami
kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege;
barabara ya kiungo na maegesho ya magari
imekamilika. Aidha, ujenzi wa jengo la abiria
lipo katika hatua za mwisho za ujenzi; na
(vi) Ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Mafia kwa kiwango cha lami umekamilika.
(e) Hali ya Hewa
Utambuzi wa hali ya hewa ni muhimu kwa shughuli
za kiuchumi zikiwemo za kilimo, uvuvi, usafiri
hususan usafiri wa anga na majini. Utambuzi wa
hali ya hewa ni muhimu pia kwa shughuli nyingine
za kijamii ikiwa ni pamoja na kuweka tahadhari za
majanga. Ili kuimarisha huduma za utambuzi wa hali
ya hewa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
yamefanyika mambo yafuatayo:-
(i) Rada mbili za utabiri wa hali ya hewa zenye
ubora wa kimataifa zimenunuliwa na kufungwa
katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza;
69
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kituo cha kutoa taarifa za hali ya hewa kwa
watumiaji wa maeneo ya Ziwa Victoria
kimeanzishwa mkoani Mwanza. Ili kuhakikisha
kwamba taarifa za hali ya hewa zinawafikia
wananchi na wadau wengine kwa wakati,
taarifa za hali ya hewa sasa zinatolewa kwenye
vyombo vya habari vikiwemo simu na mitandao
ya kijamii; na
(iii) Vituo vitatu vya hali ya hewa (synoptic stations)
vya Kilwa Masoko, Mpandeni Songwe vimeanza
kufanya kazi. Aidha, upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina wa Kituo Kikuu cha Hali ya
Hewa umekamilika.
41. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya mambo
yafuatayo:-
Miundombinu ya Huduma za Reli
(a) Kwa kushirikiana na sekta binafisi kuanza ujenzi wa reli
zifuatazo kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge):-
(i) Dar es Salaam – Tabora – Kigoma/Mwanza
(ii) Uvinza – Msongati (Burundi) na Isaka – Kigali
(Rwanda)
(iii) Mtwara – Songea – Mbamba Bay na matawi ya kwenda
Mchuchuma na Liganga
(iv) Tanga – Arusha – Musoma
(v) Kaliua – Mpanda – Karema
(b) Kuijengea uwezo Kampuni ya Reli Tanzania kwa kuongeza
idadi ya vichwa vya treni, mabehewa ya mizigo na abiria ili
kuimarisha utendaji wake ikiwa ni pamoja na kuimarisha
karakana za Morogoro, Tabora na Dar es Salaam;
70
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kukamilisha Sheria mpya ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania
na Zambia (TAZARA) itakayosaidia kubadilisha mfumo wa
uendeshaji wa Shirika kwa lengo la kuboresha huduma za
abiria na mizigo; na
(d) Kuendelea kuboresha usafiri wa reli jijini Dar es Salaam
kwa lengo la kupunguza msongamano.
Usafiri wa Majini
Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuendelea kuboresha
huduma za uchukuzi katika Bandari za mwambao kwa kufanya
yatuatayo:-
(a) Kuanza ujenzi wa gati Na. 13 na 14 katika Bandari ya Dar es
Salaam;
(b) Kukamilisha uboreshaji wa gati Na. 1 – 7 ili kuimarisha
utoaji wa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam;
(c) Kuanza ujenzi wa gati la kushusha magari (RoRo) katika
Bandari ya Dar es Salaam;
(d) Kuanza ujenzi wa bandari mpya za Bagamoyo na Mwambani
Tanga;
(e) Kuanza na kukamilisha ujenzi wa magati manne (4) ya
ziada katika Bandari ya Mtwara;
(f) Kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamisati ili kuboresha
usafirishaji wa kwenda na kutoka Mafia;
(g) Kuendelea kuboresha Bandari ya Mwanza, upanuzi
wa Bandari ya Musoma na ujenzi wa magati ya Ntama,
Lushamba na Kiyamkwiki;
(h) Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya bandari
za Ziwa Nyasa na Tanganyika ili kuimarisha huduma
zitolewazo kwa kujenga magati ya Kagunga, Kasanga,
Kibirizi, Itungi na Kiwira;
(i) Kuboresha mfumo wa uondoshaji mizigo katika Bandari ya
Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza kiwango cha utendaji
71
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kwa kuweka mfumo wa “electronic window System” na
kufunga mita za kupima mafuta; na
(j) Kujenga na kukamilisha meli mbili za abiria na mizigo
katika Ziwa Tanganyika, meli moja ya abiria na mizigo
katika Ziwa Victoria na meli nyingine ya abiria na mizigo
katika Ziwa Nyasa.
Usafiri wa Anga
Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuendelea kuboresha huduma
za usafiri wa anga kwa kufanya yatuatayo:-
(a) Kukamilisha mpango kabambe wa usafiri wa anga;
(b) Kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza ya Jengo la
Tatu la Abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kuanza ujenzi wa
awamu ya pili ya Jengo la Tatu la JNIA;
(c) Kuanza na kukamilisha ujenzi vya Viwanja vya Ndege vya
Shinyanga na Sumbawanga kwa kukarabati barabara ya
kutua na kuruka ndege kwa kiwango cha lami;
(d) Kujenga na kukamilisha awamu ya pili ya Viwanja vya
Ndege vya Tabora na Kigoma;
(e) Kuanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato kwa
kiwango cha Kimataifa;
(f) Kukamilisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza
hususan jengo la abiria na kufikia kiwango cha kimataifa;
(g) Kuanza awamu ya pili ya mradi wa ujenzi, ukarabati na
upanuzi wa Viwanja vya Ndege kumi na moja (11) vya mikoa
vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina vya
Lindi, Kilwa Masoko, Songea, Singida, Lake Manyara,
Tanga, Iringa, Njombe, Simiyu, Musoma na Moshi; na
(h) Kuhamasisha uwekezaji wa Sekta ya Umma na Binafsi
(PPP) ili kuimarisha huduma za Shirika la Ndege la Taifa.
72
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Huduma za Hali ya Hewa
Kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa kwa kufanya
yatuatayo:-
(a) Kuanza ujenzi wa kituo kikuu cha utabiri wa hali ya hewa
nchini; na
(b) Kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa nchini ili
kufikia kiwango cha kimataifa kwa kununua rada za hali ya
hewa zisizopungua tano.
Nishati
42. Kwa kutambua umuhimu wa nishati kwa maendeleo ya
Taifa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imechukua hatua za kuhakikisha kuwa nishati ya kutosha
inapatikana kwa lengo la kukidhi mahitaji ya viwanda,
taasisi zinazotoa huduma na wananchi kwa ujumla. Nguvu
kubwa imeelekezwa katika kuhakikisha kwamba nishati
ya umeme inasambazwa kwa gharama nafuu ili kuwaletea
unafuu wa maisha wananchi hasa wale wanaoishi maeneo
ya vijijini. Katika kutimiza azma hiyo:-
(a) Mipango ya kuunganisha gridi ya Taifa na nchi jirani
imeendelea kutekelezwa kwa lengo la kuimarisha
biashara ya umeme. Miradi muhimu ambayo
utekelezaji wake unaendelea ni pamoja na:-
(i) Mradi wa Rusumo wa megawati 80 kwa ajili ya
Rwanda-Burundi-Tanzania;
(ii) Mradi wa usafirishaji umeme wa gridi ya
Kaskazini-Mashariki wa usafirishaji umeme kati
ya Ethiopia-Kenya –Tanzania; na
(iii) Mradi wa Zambia - Tanzania-Kenya (ZTK
Interconnector).
(b) Kiwango cha uunganishwaji umeme kwenye
Mikoa na Wilaya ambako gridi ya Taifa haijafika
nchini kimeongezeka kutoka asilimia 5 mwaka 2010
73
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
hadi asilimia 36 mwaka 2015. Aidha, kiwango cha
uunganishwaji umeme vijijini kimeongezeka kutoka
asilimia 5 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2014
kupitia utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi
Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini wenye
miradi midogo 41 katika mikoa 16 ya Tanzania Bara
(Arusha, Dodoma, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro,
Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Pwani,
Rukwa, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga) ambapo
jumla ya wateja wapya 209,237 wameunganishiwa
umeme hadi kufikia Disemba, 2014;
(c) Ukiritimba wa TANESCO wa kuwa mzalishaji na
msambazaji pekee wa umeme umeondolewa na sasa
sekta binafsi imeruhusiwa kushiriki katika kuzalisha,
kusambaza na kuuza umeme;
(d) Ujenzi wa bomba la gesi lenye urefu wa km 542 kutoka
Mnazi Bay (Mtwara) hadi Dar es Salaam umekamilika.
Aidha, ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi katika eneo
la Somanga Fungu, Kinyerezi Dar es Salaam na Tegeta
umefikia wastani wa asilimia 96;
(e) Jumla ya futi za ujazo trilioni 55.08 za gesi
imegunduliwa nchini hadi kufikia mwaka 2015;
(f) Jumla ya nyumba za makazi 812, nyumba za ibada
27, shule 6 na zahanati 8 zimepatiwa umeme wa jua
pamoja na jumla ya taa za mitaani 200 katika vijiji
10 kutoka Wilaya za Mlele, Kongwa na Uyui kupitia
Mradi wa Maendeleo ya Nishati (Tanzania Energy
Development and Access Expansion – TEDAP); na
(g) Mradi wa usambazaji gesi asilia katika Jiji la Dar
es Salaam ili kukidhi mahitaji ya sekta mbalimbali
umeshaanza ambapo maandalizi ya ujenzi wa
miundombinu ya kusambaza gesi yamekamilika na
kwa sasa shughuli za upanuzi zinaendelea.
74
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
43. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya 2015–2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuongeza
kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati ili kuendelea
kukuza Sekta hiyo na kuongeza mchango wake kwenye
Pato la Taifa kwa kutekeleza yafuatayo:-
Umeme
(a) Kuongeza uzalishaji wa umeme ili kuhakikisha wananchi
wanafikiwa na huduma hii kulingana na Sera ya Nishati
ya Taifa. Kwa kutekeleza miradi iliyoainishwa kwenye
Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme (Power
System Master Plan – 2009-2033) ili kukidhi mahitaji ya
umeme nchini, kipaumbele kitatolewa katika rasilimali za
makaa ya mawe, maji (hydro), gesi asilia na nishati jadidifu
(renewable energy) ambapo lengo ni kufikia MW 4,915 mwaka
2020 kutoka MW 1,308 mwaka 2015; na
(b) Kukamilisha na kuimarisha mtandao wa usafirishaji na
usambazaji umeme (National Grid) unaounganisha nchi
nzima kwa kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa njia
za kusafirisha umeme kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji
wa umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi yetu.
Miradi hiyo ni pamoja na:-
(i) Mradi wa Backbone wa kV 400 unaounganisha mikoa
ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga wenye urefu
wa km 670;
(ii) Mradi wa Makambako-Songea wa kV 220, ambao
unaunganisha mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma
km 250; na
(iii) Mradi wa Kaskazini-Mashariki (North-East)
unaounganisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga,
Kilimanjaro na Arusha. Aidha, mradi mwingine
muhimu ni ule wa Kaskazini-Magharibi (North-West),
ambao unaunganisha mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa
na Kigoma.
75
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kuendelea kusambaza umeme wenye uhakika mijini na
vijijini kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuendelea kuongeza bajeti ya Wakala wa Kusambaza
Umeme Vijijini (REA) ili kuhakikisha upatikanaji wa
umeme wenye uhakika;
(ii) Kukamilisha utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango
kabambe wa kupeleka umeme vijijini (REA Turn-Key
Projects Phase II) yenye lengo la kuunganisha wateja
250,000 utakapokamilika; na
(iii) Kuanzisha REA (III) ambayo ina malengo yaafuatayo:-
• Kuongeza wigo wa usambazaji umeme kutoka
REA I na II zilipoishia;
• Kufikisha umeme kwenye shule zote za
sekondari, hospitali na vyanzo vya maji;
• Kuongeza idadi ya vijiji ambavyo vinafikiwa na
umeme; na
• Kupeleka umeme maeneo yote ambayo si tija
kwa TANESCO kuwekeza.
(iv) Kuongeza kiwango cha uunganishaji umeme
(connection level) kutoka asilimia 36 mwaka 2015 hadi
asilimia 60 ifikapo mwaka 2020; na
(v) Kutekeleza miradi ya kuunganisha gridi ya Taifa
na gridi za nchi jirani ambapo miradi ya Zambia-
Tanzania-Kenya, Burundi-Rwanda-Tanzania na
Tanzania-Kenya-Ethiopia itahusika.
Mafuta na Gesi Asilia
44. Kwa kuzingatia ugunduzi wa kiwango kikubwa cha gesi
asilia na matarajio ya upatikanaji wa mafuta, Chama Cha
Mapinduzi kitaendelea kuielekeza Serikali kusimamia
sekta hii kwa kuzingatia Sera na Sheria mbalimbali
zilizopo zitakazowezesha nchi kunufaika na rasilimali hii
76
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Pamoja na kutekeleza
Sera na Sheria hizo, malengo muhimu katika kipindi cha
mwaka 2015 hadi 2020 ni pamoja na:-
(a) Kuwezesha na kusimamia ujenzi wa miundombinu
muhimu ya gesi asilia na mafuta nchini pamoja na
kukamilisha Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi
Asilia (Natural Gas Utilisation Master Plan);
(b) Kuhakikisha wananchi wanaopakana na
miundombinu ya gesi na ambako bomba la gesi
linapita wanashiriki na kunufaika na gesi;
(c) Kuwawezesha wananchi kwa ujumla washiriki na
wanufaike na fursa zinazotokana na uchumi wa gesi;
(d) Kuendeleza mradi wa kugeuza gesi kuwa katika
hali ya vimiminika (Liquefied Natural Gas - LNG) ili
kuwezesha mauzo ya gesi asilia ndani na nje ya nchi;
(e) Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kushiriki
katika sekta ndogo ya mafuta na gesi kwa kuzingatia
Sera na Sheria zilizopo;
(f) Kuendelea kuhamasisha utafutaji wa mafuta na gesi
asilia;
(g) Kuendelea kusomesha vijana wa Kitanzania katika
ngazi mbalimbali za vyuo vikuu, VETA, kulingana na
mahitaji ya rasilimali watu katika Sekta ya Mafuta na
Gesi; na
(h) Kuendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu
muhimu ya mafuta na gesi nchini ili kuleta ufanisi na
tija katika kuvuna na kutumia mafuta na gesi asilia.
(i) Kwa kutambua umuhimu wa nishati ya mafuta,
Serikali:-
(i) Itahakikisha hifadhi za kimkakati zenye uwezo
wa kukidhi mahitaji ya mafuta kwa nchi yetu na
nchi jirani zinajengwa Dar es Salaam, Tanga na
Zanzibar;
77
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Itahamasisha sekta binafsi kutumia fursa ya
kijiografia kuigeuza Dar es Salaam kuwa soko
kubwa la mafuta ya jamii ya petroli kwa ukanda
wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara;
(iii) Itahakikisha wakati wote sehemu zote za
nchi zinapata mafuta yenye ubora unaokidhi
viwango na kwa bei inayoakisi gharama halisi
kupitia Taasisi zake (TPDC, EWURA na Wizara
ya Nishati na Madini); na
(iv) Itahimiza matumizi ya gesi ya Petroli (Liquefied
Pretroleum Gas -LPG) na gesi asilia katika
matumizi ya nyumbani na viwandani ili
kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na hivyo
kuhifadhi mazingira.
Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati
45. Kwa kuzingatia kwamba gesi asilia na makaa ya mawe
ni rasilimali zinazoisha (depletable), na kwa kuzingatia
madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Chama Chama
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuwekeza nguvu kubwa
katika kuzalisha nishati jadidifu kwa kufanya yafuatayo:-
(a) Kuzalisha umeme wa jua usiopungua MW 180;
Joto ardhi MW 200 kwa kuzigatia uwezo uliopo wa
kuzalisha hadi MW 5000;
(b) Kuzalisha umeme MW 100 kwa kutumia nguvu za
upepo kufikia mwaka 2020; na
(c) Kufanya tafiti ili kubaini na kupanga vyanzo mbadala
kwa miaka ijayo ili kuepusha Taifa kukosa nishati ya
umeme.
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
46. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imekuwa
katika jitihada za kuendeleza utekelezaji wa mipango
na mikakati mbalimbali kwa lengo la kuinua Sekta ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ili kufikia maendeleo
78
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ya kijamii na kiuchumi. Katika kipindi hicho, mafanikio
yafuatayo yamepatikana:-
(a) Kuimarisha Utendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kwa kuhakikisha:-
(i) Sheria ya Tume imepitiwa upya ili kuipa
COSTECH mamlaka ya kiudhibiti pamoja na
kutambua mchango wa ubunifu; na
(ii) COSTECH imeanzisha taasisi za kuwakuza
wajasiriamali wa TEHAMA ikiwemo ya Dar
Teknohama Incubator (DTBi) ambapo matokeo
yake yamechangia kuanzishwa kwa mfumo wa
MAXMALIPO.
(b) Jumla ya watafiti 517 wamesomeshwa katika ngazi ya
shahada ya Uzamili na Uzamivu katika vyuo vikuu
vya hapa nchini katika kipindi cha mwaka 2010 hadi
2014;
(c) Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 wagunduzi
11 walipewa Tuzo ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(TASTA). Aidha, Taasisi nane (8) zilipewa Tuzo za
Utafiti wa Sayansi na Teknolojia (NARST) na Taasisi
mbili (2) zimepatiwa Tuzo za Mazingira (NAEM);
(d) Ujenzi wa awamu ya I na II ya Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano wenye urefu kilometa 7,560 umekamilika
na umesaidia watoa huduma kufikisha huduma za
mawasilianao kwa wananchi kwa uharaka zaidi,
uhakika na kwa gharama nafuu. Kuwepo kwa mkongo
mmoja unaomilikiwa na Serikali umepunguza
gharama za huduma ya mawasiliano ambapo:-
(i) Gharama kwa mtumiaji wa mwisho zimeshuka
kutoka Shilingi 147 kwa dakika mwaka 2009
hadi Shilingi 67 kwa dakika mwaka 2014; na
(ii) Ada ya kuunganisha simu za mikononi imeshuka
kutoka Shilingi 115 kwa dakika mwaka 2009
hadi Shilingi 34.92 kwa dakika mwaka 2014.
79
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Mfumo wa kusimamia mawasiliano umewekwa
ili kubaini takwimu zinazopita katika mitandao ya
mawasiliano kwa kutambua mapato na miamala ya
fedha, kufuatilia na kugundua mawasiliano ya ulaghai
na kutambua taarifa za laini za simu na za kifaa cha
mawasiliano;
(f) Zoezi la kuhamisha matangazo kutoka mfumo wa
Analojia kwenda katika utangazaji wa Digiti awamu
ya kwanza limekamilika; na
(g) Idadi ya wananchi wanaomiliki simu za kiganjani
imeongezeka kutoka milioni 2.9 mwaka 2005 hadi
milioni 32.01 mwaka 2015.
47. Mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda ambavyo
Taifa linataka yafanyike ili kuleta mageuzi ya uchumi,
yatawezekana kwa kuwekeza vema katika ujenzi wa
msingi imara wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za
uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali
yatasaidia uchumi wetu kukua kwa kasi na kuwapunguzia
wananchi umasikini pamoja na kuongeza ajira.
Sekta ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika
kipindi cha miaka mitano ya Utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2015-2020, itaweka
msisitizo mkubwa wa vipaumbele kama ifuatavyo:-
(a) Kuanzisha vituo vya ubunifu ili kukuza makampuni
ya TEHAMA yanayoibukia kwa lengo la kuongeza
ajira kwa vijana;
(b) Kuandaa mazingira bora ya kusambaza matokeo ya
utafiti na teknolojia kwa watumiaji katika sekta za
uzalishaji hususan kilimo, mifugo, uvuvi na afya;
(c) Kuendeleza matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika
tiba ya saratani na kuongeza vituo kutoka vituo viwili
(2) vya sasa hadi sita (6) vitakavyohudumia kanda
mbalimbali nchini, vituo vinne vitakavyoongezwa ni:
80
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Hospitali ya Rufaa Mbeya, Mnazi Mmoja (Zanzibar),
KCMC pamoja na Dodoma;
(d) Kuunganisha katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
baadhi ya shule za msingi, shule zote za sekondari,
ofisi zote za wakuu wa wilaya/polisi (OCD), hospitali
zote za wilaya, vyuo vikuu vyote na vituo vya posta
65 ili kuweza kutumia fursa za TEHAMA hususan
Elimu Mtandao, Maktaba Mtandao na Afya Mtandao;
(e) Kuanzisha kituo mahiri cha huduma za TEHAMA kwa
kushirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kuhawilisha
teknolojia na kutoa ajira kwa Watanzania;
(f) Kufikisha huduma za mawasiliano ya simu za
viganjani kwa wananchi wote kupitia Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika vijiji vyote
vya Tanzania Bara na Zanzibar;
(g) Kuendelea kuweka mazingira bora ya ushindani
kwenye Sekta ya Mawasiliano ili wananchi wengi
waweze kumudu gharama za mawasiliano ya simu;
(h) Kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia
1.0 ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) kwa ajili ya utafiti,
maendeleo na maonyesho ya matokeo ya utafiti;
(i) Kuwalinda watumiaji wa simu za mikononi dhidi ya
dhuluma, wizi na uhalifu wa mitandao; na
(j) Kuongeza idadi ya watumiaji mitandao (internet)
kutoka milioni 9.0 mwaka 2015 hadi kufikia milioni
20.0 mwaka 2020.
81
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA NNE
SEKTA YA HUDUMA ZA JAMII
48. Huduma bora za jamii kama afya, elimu, maji na
nyinginezo ni nyenzo muhimu katika kuondoa umasikini
na kuharakisha maendeleo ya wananchi. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita, Serikali chini ya uongozi wa Chama
Cha Mapinduzi imeendeleza jitihada za kuhakikisha
kwamba wananchi wanaendelea kunufaika na huduma
hizo. Kwa hivyo, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani
hii 2015-2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali
kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi
kilichopita ili wananchi waendelee kunufaika na huduma
za jamii ambazo ni za msingi katika jitihada za kuboresha
maisha yao.
Afya
49. Ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora inayowawezesha
kuzalisha mali na kutoa huduma mbalimbali, katika kipindi
cha mwaka 2010-2015, Serikali iliendelea kuyapa kipaumbele
maeneo yaliyoainishwa katika MKUKUTA na Malengo ya
Milenia ambapo mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Vituo vya kutolea huduma ya Afya vimeongezeka
kutoka 6,260 mwaka 2010 hadi vituo 7,014 mwaka
2015. Pia kuna kliniki 89 zinazohamishika (huduma
za mkoba) katika mfumo wa utoaji wa huduma
za wazazi, meno, macho, moyo na sukari ambazo
huendeshwa na madaktari bingwa;
(b) Udahili wa wanafunzi watarajali umeongezeka kutoka
7,013 mwaka 2010 hadi wanafunzi 11,192 mwaka 2015
katika Vyuo vya Afya na Ustawi wa Jamii;
(c) Waajiriwa wapya wa kada za afya wameongezeka
kutoka 7,471 mwaka 2010 hadi waajiriwa 9,345 mwaka
2014;
82
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kupitia mpango wa hati punguzo, vyandarua
8,753,438 vyenye viuatilifu kwa ajili ya kaya zenye
watoto chini ya miaka mitano, vyandarua 7,785,787
kwa ajili ya wajawazito na vyandarua 4,960,111
kwa ajili ya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja
vimesambazwa bure kwa lengo la kuboresha tiba
ya malaria, kudhibiti mbu na kutoa kinga. Aidha,
vyandarua 26,371,329 viligawiwa kwa wananchi bila
malipo kupitia kampeni zilizolenga watoto chini ya
miaka mitano na ngazi ya Kaya. Matokeo yake ni:-
(i) Vifo vitokanavyo na malaria vimepungua
kutoka 33 mwaka 2010 hadi 12 kwa kila watu
1,000 mwaka 2014; na
(ii) Idadi ya watu waliopatikana na malaria
imepungua kutoka watu 310 mwaka 2010 hadi
161 kwa kila watu 1,000 mwaka 2014.
(e) Mpango wa Upuliziaji wa viuatilifu ukoko katika kuta
ndani ya nyumba ili kuua mbu wanaoeneza malaria
umetekelezwa kwa mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara
na Geita ambapo zaidi ya kaya 1,440,000 zenye watu
6,500,000 zilinufaika;
(f) Ujenzi wa kiwanda cha viuadudu (bio-larvicides)
katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa lengo la
kuzalisha viuadudu kwa ajili ya kudhibiti viluwiluwi
vya mbu nchini umekamilika ambapo Kata za Jiji la
Dar es Salaam zimeanza kunufaika;
(g) Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) ilitoa huduma
za kibingwa za mkoba kwa wagonjwa 513 ambapo
wagonjwa 116 walifanyiwa upasuaji katika Hospitali
ya Rufaa ya Mbeya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro;
(h) Hospitali za Rufaa za Mikoa 24 zimeunganishwa
kwenye mtandao wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano
ili kutoa huduma za afya kwa njia ya mtandao;
83
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Vifaa vya kujimudu kwa watu wenye ulemavu ikiwa
ni pamoja na shime sikio, viti mwendo, mashine za
nukta nundu na fimbo nyeupe kwa ajili ya makazi
17 ya wazee, wasiojiweza na vyuo viwili vya ufundi
vimenunuliwa. Jumla ya wazee 1,750 walipatiwa
huduma katika makazi 17 yanayomilikiwa na Serikali
na 24 yanayomilikiwa na wakala wa hiari;
(j) Bohari ya Dawa (MSD) imeendelea kushirikiana na
Sekta Binafsi katika kuhakikisha kuwa dawa na vifaa
tiba vinapokosekana katika bohari zake, Mshitiri/
Mnunuzi wa Sekta Binafsi anakuwa tayari kuwezesha
upatikanaji wa dawa hizo kwa ajili ya vituo vya
kutolea huduma za afya nchini;
(k) MSD imeanza kupeleka shehena za dawa moja kwa
moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili
kuboresha usambazaji dawa na kupunguza gharama;
(l) Jumla ya Wataalamu 1,553 wa Sekta ya Afya katika
ngazi ya Halmashauri wamepata mafunzo ya uingizaji
na utumiaji wa taarifa kupitia mfumo wa elektroniki ili
kufanikisha upatikanaji wa takwimu za afya ambapo
jumla ya kompyuta 133 kwa ajili ya Halmashauri na
Mikoa; na kompyuta 189 kwa ajili ya matumizi ya
mfumo wa hospitali za Mikoa na Wilaya zilitolewa;
(m) Watanzania 4,010,844 sawa na asilimia 9.2 wamejiunga
na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kufikia mwaka
2015. Aidha, asilimia 19.2 ya Watanzania wamefikiwa
na huduma za bima kwa kujumuisha mifuko yote ya
Bima za Afya;
(n) Huduma za matibabu ya kibingwa na uchunguzi
zimeimarishwa. Huduma hizo ni pamoja na upasuaji
mkubwa wa moyo; upasuaji wa mgongo na ubongo;
kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya
figo; kuanzishwa kwa huduma ya matibabu ya dharura
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Emergency
Medicine); na kununua mashine za mionzi. Aidha,
84
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
hadi sasa jumla ya wagonjwa 671 walipata huduma
ya upasuaji mkubwa wa moyo; wagonjwa 211
walifanyiwa upasuaji maalumu: ubongo 29, mgongo
107, 56 waliwekewa viungo bandia vya nyonga na 19
viungo bandia vya goti; na
(o) Mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya
Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa Mama kwenda
kwa Mtoto umeanzishwa. Hadi sasa akina Mama
walioanzishiwa tiba ya maisha ni 72,207 kati ya
mama wajawazito wenye VVU watarajiwa 97,908.
Mpango huu umewezesha kiwango cha maambukizi
kupungua kutoka asilimia 8 mwaka 2010 hadi asilimia
5 mwaka 2015.
Moja ya ghala la Bohari Kuu ya Dawa kwa ajili ya kuhifadhi
Dawa katika Kanda
50. Kwa kuzingatia dhamira ya kuwa na wananchi wenye afya
bora watakaoweza kushiriki katika shughuli mbalimbali
za kiuchumi na kutoa huduma katika miaka mitano ijayo,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuendelea
kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora za
afya kwa kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendeleza utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa
Afya ya Msingi (MMAM) wenye lengo la kuimarisha
na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa
kuhakikisha kwamba:-
85
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Lengo la kila kijiji kuwa na Zahanati, Kata kuwa
na Kituo cha Afya na Wilaya kuwa na Hospitali
linaendelea kutekelezwa katika maeneo ambayo
huduma hizi hazijakamilika pamoja na kujenga
hospitali za wilaya katika wilaya zote mpya;
(ii) Hospitali za Rufaa za Mikoa zinaendelea
kuimarishwa na kukamilisha ujenzi kwa mikoa
mipya na ile ambayo haina hospitali hizi;
(iii) Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika
Sekta ya Afya kwa kupitia sera ya ubia baina ya
Sekta ya Umma na Binafsi (PPP);
(iv) Hospitali za Rufaa za Kanda zitaendelea
kuimarishwa na kujenga hospitali nyingine tatu
kwa ajili ya Kanda ya Kusini, Kati na Magharibi;
(v) Kudahili wanafunzi 15,000 katika Vyuo vya Afya
na Ustawi wa Jamii ifikapo mwaka 2020 ikiwa
ni jitihada za kutosheleza mahitaji ya rasilimali
watu katika sekta hii;
(vi) Kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu
katika vyuo vya mafunzo ya afya na kushirikisha
Sekta Binafsi katika uendeshaji wa vyuo;
(vii) Kuajiri wataalamu zaidi wa afya kutoka ndani
na nje ya nchi pamoja na kuboresha mazingira ya
kazi kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma
za afya. Aidha, hospitali za wilaya zitaendelea
kuimarishwa kwa kuzipatia madaktari,
wauguzi, dawa na vifaa tiba vya kutosha;
(viii) Kutoa motisha kwa watumishi ambao wanafanya
kazi katika maeneo yenye mazingira magumu
ili kuwajengea ushawishi wa kuendelea kutoa
huduma za afya katika maeneo hayo; na
86
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ix) Kujenga nyumba za watumishi karibu na vituo
vya kutolea huduma.
(b) Kuimarisha mapambano dhidi ya malaria kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kuwagawia wananchi vyandarua vyenye
viuatilifu 22,360,386 bila malipo;
(ii) Kutekeleza mpango wa upuliziaji wa viuatilifu
ukoko katika kuta za nyumba ili kuua mbu
wanaoeneza malaria katika mikoa ya Kigoma
na Lindi;
(iii) Kuendelea kutekeleza mpango wa kuangamiza
viluwiluwi vya mbu kwa kutumia viuadudu
vya kibailojia katika Kata za Jiji la Dar es Salaam;
na
(iv) Kununua na kusambaza dawa za malaria katika
vituo vyote vya kutolea huduma nchini.
(c) Kuimarisha upatikanaji wa huduma za dharura na za
kawaida kwa wagonjwa kupitia vituo vya huduma za
afya hapa nchini. Huduma hizi ni pamoja na magonjwa
ya saratani, mishipa ya fahamu, mapafu, figo, huduma
za magonjwa ya moyo, upasuaji mbalilmbali ikiwamo
upasuaji wa mifupa;
(d) Hospitali ya Taifa Muhimbili itaendelea kutoa huduma
za kibingwa za mkoba katika Hospitali za Rufaa za
Kanda;
(e) Kuunganisha hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya
na hospitali nyinginezo kwenye mfumo wa matibabu
mtandao (telemedicine);
(f) Halmashauri za Wilaya zitaelekezwa kutenga bajeti
kwa ajili ya kununulia vifaa vya kujimudu kwa lengo
la kuwawezesha watu wenye ulemavu;
87
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Bohari ya Dawa itakamilisha ujenzi wa maghala ya
kisasa ya kuhifadhia dawa katika mikoa ya Tanga,
Tabora, Mtwara na Dar es Salaam. Aidha, Serikali
itaendelea kushirikisha Sekta Binafsi kuwezesha
upatikanaji wa dawa pale zinapokosekana katika
Bohari ya Dawa;
(h) Kuongeza Washitiri Binafsi 17 katika mikoa tisa kwa
ajili ya ununuzi wa dawa pale ambapo hazipo Bohari
ya Dawa;
(i) Kuunganisha mifumo ya ukusanyaji na utoaji taarifa
za afya ili kufikia lengo la kuwa na mfumo mmoja
unaokusanya na kutoa taarifa za afya nchini. Aidha,
mfumo wa ukusanyaji taarifa kwa njia ya simu za
mkononi utasambazwa nchi nzima;
(j) Kuweka utaratibu utakaowezesha wananchi kuwa na
Bima ya Afya ili kumudu gharama za matibabu;
(k) Kuimarisha huduma za matibabu ili kupunguza
gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kununua mashine za mionzi (LINAC machine)
kwa ajili ya tiba ya saratani;
(ii) Kununua vifaa vya kisasa na kuwajengea uwezo
wataalam ili kuhudumia wagonjwa wengi wa
moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na
hospitali za rufaa za Kanda;
(iii) Kununua mashine za mionzi (CT-Scan, MRI)
kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji wa
mgongo na ubongo; na
(iv) Kuimarisha mtandao wa Hospitali za Taifa
pamoja na Huduma za Ubingwa wa Juu
zikiwemo zile za upasuaji wa moyo; huduma
kwa wagonjwa wa saratani; upasuaji wa ubongo
na mishipa ya fahamu na upasuaji kupitia tundu
88
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
dogo kwa kutumia kifaa maalumu ikiwa ni
pamoja na kuchuja damu na kupandikiza figo
kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
(l) Kupanua huduma za matibabu mtandao
(telemedicine) pamoja na zile za kutumia mtandao
wa simu pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi
yatakayowawezesha kutoa huduma za kibingwa.
Aidha, vituo vingine vya saratani vitaongezwa katika
hospitali ya KCMC na hospitali ya rufaa ya Mbeya ili
kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi;
(m) Kukamilisha ujenzi wa hospitali za Mloganzila,
Mtwara na Chuo Kikuu cha Dodoma;
(n) Kukarabati na kuimarisha huduma za kibinadamu
katika vituo vya kutolea huduma za ustawi wa jamii
vikiwemo makazi 17 ya wazee, mahabusi saba za
watoto walio katika mkinzano na sheria pamoja na
shule moja ya maadilisho;
(o) Kuimarisha upatikanaji wa haki na huduma za
makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu
wa ngozi (albinism) na watoto wanaoishi mitaani
ikiwa ni pamoja na kuanzisha Kamati za Ulinzi wa
Mtoto katika Halmashauri zote;
(p) Kukamilisha Sera ya Huduma za Ustawi wa Jamii
pamoja na Mkakati wake wa Utekelezaji. Aidha,
Halmashauri zitahakikisha wazee wanatambuliwa na
kupewa matibabu bure katika hospitali za Serikali;
(q) Kuimarisha Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa
kuzingatia vipaumbele vya Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuzijengea uwezo Hospitali na Vituo vya Afya ili
kutoa huduma kamili ya Afya ya Uzazi na Mtoto
pamoja na upasuaji kwa mama wajawazito;
89
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kuanzisha Benki za Damu katika Mikoa
itakayoanza kutekeleza mpango wa kutoa
huduma kamili ya afya ya uzazi na mtoto.
Vilevile, huduma za uzazi wa mpango zitapewa
kipaumbele;
(iii) Kuzijengea uwezo Zahanati na Vituo vya Afya
katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu
na Kigoma kutoa huduma ya msingi ya dharura
ya Afya ya Uzazi na Mtoto;
(iv) Kutoa huduma za mkoba (mobile clinic) hasa
maeneo ya vijijini; na
(v) Kuendelea kutekeleza mpango wa kutokomeza
maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa Mama
kwenda kwa Mtoto.
Elimu
51. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha,
kuimarisha na kupanua Elimu ya Awali hadi ya Chuo Kikuu
kwa lengo la kuhakikisha kwamba elimu katika ngazi zote
inakuwa na ubora unaostahili ili kuwawezesha vijana na
makundi mengine kumudu ushindani wa soko la ajira
ambalo wigo wake umepanuka ndani na nje ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki. Katika kipindi hicho, yamepatikana
mafanikio yafuatayo:-
(a) Elimu ya Awali
(i) Idadi ya shule za msingi zenye madarasa ya
Elimu ya Awali imeongezeka kutoka shule
10,612 mwaka 2010 hadi shule 14,783 ambayo
yana walimu 13,600 mwaka 2015;
(ii) Stashahada ya Elimu ya Awali ya miaka miwili
katika vyuo 19 vya serikali imeanzishwa kwa
lengo la kupata walimu wenye weledi wa juu
katika ngazi ya Elimu ya Awali; na
90
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Idadi ya matundu ya vyoo imeongezeka kutoka
128,847 mwaka 2006 hadi 157,162 mwaka 2013.
(b) Elimu ya Msingi
(i) Katika kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa
walimu wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na
Sayansi, vigezo vya kujiunga na mafunzo ya
ualimu vimepandishwa hadhi kutoka ufaulu
wa daraja la nne hadi kuanzia ufaulu wa daraja
la kwanza mpaka daraja la tatu kwa waliofaulu
masomo hayo;
(ii) Kupitia mpango wa kuwajengea uwezo walimu
na mwanafunzi, jumla ya walimu 9,814 katika
Halmashauri 40 wakiwemo walimu 3,272 wa
somo la Hisabati na 3,272 wa somo la Kiingereza
wamejengewa uwezo wa kuyamudu masomo ya
Hisabati, Sayansi na Lugha. Aidha, Stashahada
ya Elimu ya Msingi imeanzishwa katika
vyuo vinne (4) UDOM, Morogoro, Bustani na
Marangu vyenye uwezo wa kudahili walimu
tarajali 713 kwa mwaka ili kuandaa walimu
mahiri watakaofundisha Elimu ya Msingi;
(iii) Maslahi ya walimu yameendelea kuboreshwa
kulingana na ukuaji wa uchumi;
(iv) Madai mbalimbali ya walimu yameendelea
kulipwa baada ya kuhakikiwa;
(v) Ruzuku ya Wanafunzi (Capitation Grants)
imeendelea kutolewa kwa ajili ya ununuzi wa
vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule
zote za Serikali nchini;
(vi) Stashahada ya Elimu ya Msingi katika vyuo
vitatu (3), Stashahada ya Juu ya Elimu masomo
ya Sayansi katika vyuo vitatu (3), Stashahada
ya Juu ya Elimu masomo la Lugha katika chuo
kimoja (1) na Stashahada ya Elimu ya Michezo
91
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
katika chuo kimoja (1) zimeanzishwa ili kuweza
kuandaa walimu mahiri watakaofundisha Elimu
ya Msingi kwa kuwajengea uwezo wa kumudu
maarifa na stadi muhimu katika kutekeleza
mitaala kwa ufanisi;
(vii) Uandikishaji wa watoto wa miaka 7-13
umeongezeka kutoka wanafunzi 6,499,581
mwaka 2005 hadi wanafunzi 7,679,877 mwaka
2013;
(viii) Idadi ya uandikishaji wa wanafunzi wenye
ulemavu imeongezeka kutoka wanafunzi 27,422
mwaka 2009 hadi wanafunzi 31,488 mwaka
2013;
(ix) Jumla ya shule za msingi 7,165 sawa na asilimia
37.4 zilikaguliwa mwaka 2013 kwa lengo la
kuboresha kiwango cha elimu;
(x) Idadi ya walimu walioajiriwa imeongezeka
kutoka 135,013 mwaka 2005 hadi 189,487 mwaka
2013;
(xi) Uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi
umeimarika kutoka uwiano mwalimu mmoja
kwa wanafunzi 56 (1:56) mwaka 2005 hadi
uwiano wa mwalimu mmoja wanafunzi 43
(1:43) mwaka 2013;
(xii) Uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umeboreshwa
kutoka kitabu kimoja wanafunzi saba (1:7)
mwaka 2010 kufikia wastani wa kitabu kimoja
wanafunzi watatu (1:3) mwaka 2014;
(xiii) Idadi ya nyumba za walimu imeongezeka
kutoka 38,448 mwaka 2006 hadi 161,007 mwaka
2013; na
(xiv) Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na Elimu ya
Sekondari (Kidato cha Kwanza) imeongezeka
92
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kutoka wanafunzi 403,873 sawa na aslimia 84.3
mwaka 2010 hadi 451,392 mwaka 2015 sawa na
asilimia 100.
(c) Elimu ya Sekondari
(i) Idadi ya walimu wa sekondari imeongezeka
kutoka 40,517 mwaka 2010 hadi walimu 80,529
mwaka 2014 na hivyo kufikia uwiano Kitaifa wa
mwalimu mmoja kwa wanafunzi 22 (1:22);
(ii) Walimu wa masomo ya Sayansi za Jamii
wameongezeka hadi kufikia 52,816 mwaka
2014 na hivyo kuwa na ziada ya walimu 2,960
ikilinganishwa na mahitaji ya walimu 49,856 wa
fani hizo;
(iii) Walimu wa Sayansi na Hisabati wameendelea
kupatiwa mafunzo ili kuboresha fani hizo
ambapo vifaa vya maabara na kemikali vyenye
thamani ya Shilingi milioni 327.7 vimenunuliwa
na kusambazwa. Aidha, jumla ya vitabu
milioni 4,485,530 vya sayansi vimenunuliwa na
kusambazwa katika shule mbali mbali nchini;
(iv) Hadi kufikia mwaka 2014, kupitia Mpango
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu
ya pili (MMES II), mafunzo ya Sayansi na
Hisabati yametolewa kwa walimu 9,004 katika
mzunguko wa mada za mwanzo na walimu
7,863 kwa mzunguko wa mada za pili na walimu
182 wameanza mzunguko wa mada za tatu; na
(v) Idadi ya maabara imeongezeka kutoka 1,478
mwaka 2005 hadi 4,237 mwaka 2015 na maabara
5,974 zipo katika hatua mbalimali za ujenzi.
93
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa
shule za Sekondari wakati wa uzinduzi wa moja ya Maabara
zilizokamilika kujengwa.
(d) Elimu ya Ualimu
(i) Mafunzo tarajali ya walimu wa Shule za Msingi
watakaofundisha masomo mawili yameanza
kutolewa ambapo wanachuo 1,964 wa Diploma
ya Juu ya Elimu ya Sekondari na wanachuo 178
wa Diploma ya Sayansi wa Shule za Msingi
wamedahiliwa kwa mwaka 2014/15 katika
Chuo Kikuu cha Dodoma;
(ii) Kati ya mwaka 2010 na 2015, wakufunzi 331
wa Vyuo vya Ualimu walipatiwa mafunzo ya
namna ya kutumia TEHAMA katika kufundisha
na kujifunza. Aidha, vyuo vyote vya ualimu (34)
vimepatiwa kompyuta na hivyo kuwapatia fursa
wakufunzi kuandaa mada zao na maandiko
mengine kwa kutumia teknolijia hiyo;
94
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Jumla ya Shilingi bilioni 4.3 zimetumika
kukarabati miundombinu ya vyuo vya Ualimu
Patandi, Bustani na Vikindu ili kuboresha
mazingira ya kujifunzia na kufundishia; na
(iv) Maabara za Vyuo vya Ualimu vyenye mchepuo
wa Sayansi zimeboreshwa kwa kuzinunulia
vifaa vyenye thamani ya Shilingi milioni 379.8
katika maabara na kemikali za masomo ya
Sayansi (Fizikia, Kemia na Biolojia) katika vyuo
saba vya Ualimu vya Korogwe, Kleruu, Butimba,
Songea, Tukuyu, Monduli na Morogoro.
(e) Elimu ya Juu
(i) Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu wa
mwaka 2010 umeandaliwa na utekelezaji
wake umechangia wanafunzi wa kidato cha
sita wanaojiunga na Vyuo Vikuu kuongezeka
kutoka wanafunzi 34,564 mwaka 2009/2010
hadi wanafunzi 40,452 mwaka 2014/2015 sawa
na asilimia 14.6;
(ii) Utaratibu wa utoaji na urejeshwaji mikopo
kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu umeboreshwa
ambapo:-
• Dawati la Mikopo limeanzishwa katika kila
Chuo;
• Idadi ya wanafunzi ambao wamepata
mikopo imeongezeka kutoka wanafunzi
72,035 mwaka 2009/2010 hadi kufikia 99,928
Mwezi Machi, 2015 sawa na ongezeko la
asilimia 27.9; na
• Utaratibu wa urejeshaji wa makopo
umeendelea kuboresha ambapo hadi kufikia
tarehe 31 Machi, 2015 jumla ya Shilingi
bilioni 75.57 zemerejeshwa kati ya Shilingi
bilioni 165.0 ya mikupuo inayopaswa kuwa
95
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
imerejeshwa. Makusanyo haya ni asilimia
45.4 ya kiwango kinachopaswa kuwa
kimekusanywa.
(iii) Bajeti kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu
imeendelea kuongezeka kutoka Shilingi
bilioni 186.48 mwaka 2010 hadi Shilingi bilioni
328.313,44 mwaka 2015 sawa na ongezeko la
asimia 43.2;
(iv) Ujenzi na ukarabati wa majengo mapya 25
kwa ajili ya kumbi za mihadhara, maabara na
ofisi za wafanyakazi katika vyuo vikuu vya
UDSM, OUT, DUCE, MUCE, SUA, DIT na ARU
umekamilika na utaongeza nafasi za kusomea
wanafunzi hadi kufikia 47,622;
(v) Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika Vyuo
Vikuu imeongezeka kutoka wanafunzi 139,638
mwaka 2010 hadi kufikia wanafunzi 218,959
mwaka 2014 sawa na asilimia 36.2;
(vi) Idadi ya wanafunzi wa kike wanaosoma Elimu
ya Juu imeongezeka kutoka wanafunzi 53,376
kati ya wanafunzi 141,671 waliodahiliwa mwaka
2010/11 hadi kufikia wanafunzi 78,800 kati
ya wanafunzi 218,959 waliodahiliwa mwaka
2014/2015;
(vii) Taasisi 23 za Elimu ya Juu kati ya 32
zimeunganishwa katika Mkongo wa Taifa ili
kuimarisha ufundishaji na uendeshaji wa elimu
kwa njia ya mtandao hadi kufikia mwaka 2015;
(viii) Chuo Kikuu Huria na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam vimeanza kutoa mafunzo kwa njia ya
masafa baada ya kuunganishwa na Mkongo wa
Taifa na kuwezesha wahadhiri kutoa elimu kwa
njia ya masafa na kuweza kuwafikia wanafunzi
wengi mikoani; na
96
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ix) Idadi ya Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki
vimeongezeka kutoka 19 mwaka 2010 hadi 49
mwaka 2015.
(f) Elimu ya Mafunzo ya Ufundi
(i) Vyuo vya Ufundi Stadi vimeongezeka kutoka
vyuo 672 mwaka 2010 hadi kufikia vyuo 755
mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la aslimia 12.35;
(ii) Vyuo vya Elimu ya Ufundi vimeongezeka
kutoka 240 mwaka 2010 hadi 473 mwaka 2014
ikiwa ni ongezeko la asilimia 97.08;
(iii) Udahili wa wanachuo katika Vyuo vya Ufundi
Stadi umeongezeka kutoka wanachuo 78,586
mwaka 2010 hadi kufikia wanachuo 145,511
mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 85.16;
(iv) Udahili katika vyuo vya Elimu ya Ufundi na
Mafunzo umeongezeka kutoka wanachuo
85,040 mwaka 2010 hadi wanachuo 113,080
mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.81;
na
(v) Udahili wa wasichana katika Vyuo vya Ufundi
Stadi umeongezeka kutoka 52,154 mwaka 2010
hadi 56,849 mwaka 2014. Aidha, udahili wa
wasichana katika vyuo vya Elimu ya Ufundi
umeongezeka kutoka 38,698 mwaka 2010 kufikia
53,891 mwaka 2014.
(g) Elimu ya Watu Wazima yenye Manufaa
(i) Idadi ya wanafunzi wa Elimu Masafa na Ana
kwa Ana (ODL) imeongezeka kutoka wanafunzi
5,767 mwaka 2005 hadi kufikia wanafunzi 9,399
mwaka 2013; na
(ii) Jumla ya watu wazima 907,771 (wanaume
434,466 na wanawake 473,305) wamejiunga na
97
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Elimu ya Watu Wazima na kujifunza Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK), na kujifunza fani
nyingine za kilimo, ufundi, ufugaji na usindikaji
wa bidhaa mbalimbali ambapo wameweza
kuongeza fursa za kujiajiri.
52. Elimu ya kisasa na hasa yenye mwelekeo wa Sayansi na
Teknolojia ina nafasi ya pekee katika kufanikisha ujenzi
wa msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea.
Kwa kutambua ukweli huu, CCM inaipa kipaumbele
Sekta ya Elimu umuhimu wa kipekee ili kuiendeleza sekta
hii. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020),
CCM itahakikisha Serikali inasimamia Utekelezaji wa
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kuandaa mfumo, muundo na taratibu nyumbufu za
kutoa Elimu ya Awali na Elimumsingi (1+6+4) bila
malipo ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa darasa
la Elimu ya Awali unaongezeka kutoka asilimia
45 mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2020;
(ii) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa Darasa
la Kwanza unaongezeka kutoka asilimia 95
mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2020; na
(iii) Uandikishwaji rika lengwa la Wanafunzi wa
Kidato cha Kwanza unaongezeka kutoka
asilimia 60 mwaka 2015 hadi asilimia 80 mwaka
2020.
(b) Kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa
elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa
kutambua sifa zinazopatikana katika mifumo na
taasisi tofauti ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Asilimia 20 ya wahitimu wa Elimumsingi
wanaendelea na masomo katika ngazi za
Sekondari ya Juu na asilimia 80 kuendelea na
98
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
elimu au mafunzo ya ufundi katika ngazi ya
cheti, stashahada au shahada kulingana na sifa,
vipaji au vipawa;
(ii) Asilimia 80 ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari
ya Juu kujiunga na Elimu ya Juu ya Taaluma
na asilimia 20 kuendelea na Elimu ya Ufundi,
katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada
kulingana na sifa; na
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu wa Elimu au Mafunzo
ya Ufundi na Taaluma wanapata ajira kwa
kujiajiri au kuajiriwa.
(c) Kudurusu na kuhuisha muundo wa mitaala ili elimu
katika ngazi mbalimbali ikamilike kwa muda wenye
tija na itilie maanani matokeo ya kusoma yenye
kujenga ujuzi, maarifa ya kujitegemea, weledi na
kuwawezesha wahitimu kumudu na kufanya kazi
mbalimbali za kuajiriwa au kujiajiri;
(d) Kuhuisha vigezo na utaratibu wa kuhakiki, kusimamia
na kupima utekelezaji wa mitaala katika shule na
taasisi za elimu na mafunzo katika ngazi zote ili
kuhakikisha kwamba:-
(i) Ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya
Msingi unaongezeka kutoka asilimia 57 mwaka
2015 hadi asilimia 90 mwaka 2020 na asilimia
ya wanafunzi wanaoendelea na Kidato cha
Kwanza kuongezeka kutoka asilimia 55.5 hadi
asilimia 100;
(ii) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha Nne
unaongezeka kutoka wastani wa asilimia 69.8
mwaka 2015 hadi asilimia 90.0 mwaka 2020 na
ufaulu wa daraja la I – III unaongezeka kutoka
wastani wa asilimia 30.8 hadi asilimia 50.0; na
(iii) Idadi ya wataalamu wenye ujuzi wa juu
wanaongezeka kutoka asilimia 3 hadi asimilia
99
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
10 mwaka 2020, ujuzi wa kati kutoka asilimia
13 hadi 30 na ujuzi wa chini kupungua kutoka
asilimia 84 hadi 60.
(e) Kuimarisha ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na
mafunzo ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada
kwenye sekta ambazo zinachangia kwa kiasi
kikubwa kukua kwa uchumi;
(ii) Programu tatu (3) au zaidi za mafunzo
zinaanzishwa zenye kukidhi mahitaji na kuleta
maendeleo ya kijamii na kiuchumi kulingana na
mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa;
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu katika ngazi zote wawe
katika mrengo wa sayansi, ufundi, hisabati na
teknolojia;
(f) Kuandaa na kutumia utaratibu wa upatikanaji na
usambazaji wa vitabu vya kiada na ziada kwa ngazi
zote za elimu na mafunzo ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Uwiano wa kitabu cha kiada kwa mwanafunzi
katika Elimumsingi unaongezeka kutoka 1:3
mwaka 2015 hadi 1:1 mwaka 2020;
(ii) Asilimia 50 ya fedha za ruzuku ya uendeshaji
wa shule zinatumika kuchapisha na kusambaza
vitabu vya kiada; na
(iii) Uwiano wa vitabu vya ziada kwa kila somo kwa
mwanafunzi katika Elimumsingi kuwa 1:10.
(g) Kuandaa utaratibu, kuimarisha mfumo wa udahili na
kutumia fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya
nchi kwa makundi yote ya jamii kwa usawa katika
ngazi zote hususan katika ufundi, hisabati, sayansi na
teknolojia ili kuhakikisha kwamba:-
100
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Asilimia 100 ya wahitaji wa mikopo kwa ajili ya
kusomea fani ya udaktari wanapata mikopo;
(ii) Ufadhili wa nafasi 500 za masomo ya fani ya
udaktari zinapatikana kila mwaka ili kupunguza
pengo la uhaba wa madaktari nchini;
(iii) Asilimia 100 ya wale wenye mahitaji maalumu,
vipaji na vipawa wataotambulika watapata
fursa za kuendelea na masomo katika ngazi
mbalimbali; na
(iv) Shule moja maalumu ya Ufundi (Specialized
Technical Schools) au zaidi inaanzishwa kila
mkoa ambayo itadahili wanafunzi wenye vipaji
mbalimbali na kuwaendeleza kwenye fani
mbalimbali zenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
(h) Kuandaa mpango wa kuwawezesha walimu na
wanafunzi kutumia TEHAMA katika kufundishia na
kujifunzia ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Asilimia 80 ya walimu wanaandaliwa na
kutumia TEHAMA kufundishia katika ngazi
zote; na
(ii) Asilimia 70 ya taasisi zote zinazotoa elimu na
mafunzo zinaunganishwa katika Mkongo wa
Taifa.
(i) Kuhuisha miongozo ya Elimu na Mafunzo ili kuondoa
vikwazo vinavyosababisha mwanafunzi kushindwa
kukamilisha mzunguko wa elimu au mafunzo ili
kuhakikisha kwamba:-
(i) Mdondoko katika Elimumsingi unapungua
kutoka wastani wa asilimia 8.2 mwaka 2015
hadi asilimia 2 mwaka 2020;
(ii) Wasichana wote wa Elimumsingi wanaoacha
shule kwa sababu ya kupata ujauzito
wataendelea na masomo; na
101
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Wanafunzi wanaomaliza mzunguko wa elimu
katika ngazi ya Elimumsingi wanaongezeka
kutoka asilimia 67 mwaka 2015 hadi asilimia 95
mwaka 2020.
(j) Kuandaa walimu, wakufunzi na wahadhiri mahiri
hususan katika masomo ya hisabati, lugha, sayansi,
teknolojia na ufundi ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Uondokaji wa walimu, wakufunzi na wahadhiri
unapungua kutoka wastani wa asilimia 0.8
mwaka 2015 hadi asilimia 0.2 mwaka 2020;
(ii) Tatizo la uhaba wa walimu wapato 24,000 wa
masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za
Sekondari linapungua kwa kutoa mafunzo kwa
walimu 5,000 wa masomo hayo kila mwaka; na
(iii) Idadi ya wahadhiri wanaongezeka kutoka
wahadhiri 6,880 mwaka 2015 hadi wahadhiri
10,000 mwaka 2020.
(k) Kuandaa mpango kabambe wa kuongeza udahili katika
taasisi za elimu na mafunzo kwa kuzingatia mahitaji
ya rasilimali watu na ujuzi kwa maendeleo ya Taifa na
soko la ajira hususan ujuzi unaohitajika au kuhusiana
na sekta zinazokua haraka na zinazojitokeza mfano
mafuta, gesi na madini ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi
Shirikishi cha Mwalimu J.K. Nyerere (Butiama)
unakamilika na kuanzisha na kukamilisha
ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Madini
Shinyanga;
(ii) Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha
Mkoa wa Kagera utafanyika;
(iii) Udahili katika vyuo vya Ufundi Stadi
unaongezeka kutoka wastani wa wanafunzi
150,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi 700,000
mwaka 2020;
102
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iv) Udahili katika vyuo vya Ufundi vya Kati
unaongezeka kutoka wastani wa wanafunzi
30,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi 285,600
mwaka 2020; na
(v) Udahili katika ngazi ya shahada unaongezeka
katika vyuo vya elimu ya Juu kutoka wastani wa
wanafunzi 60,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi
117,000 mwaka 2020.
(l) Kushirikiana na wadau katika kuimarisha mfumo wa
ugharimiaji wa elimu ya mafunzo ikiwemo mikopo na
ruzuku ili uwe endelelevu na wenye vyanzo anuai;
(m) Kuweka utaratibu wa ada na michango mbalimbali
katika shule na vyuo binafsi ili kusimamia kwa ufanisi
masuala ya ada na michango;
(n) Kuandaa utaratibu wa ushirikiano baina ya Sekta ya
Umma, Binafsi na Jamii katika kugharamia maendeleo
ya elimu na mafunzo katika ngazi zote ili kuhakikisha
kwamba:-
(i) Mchango wa Sekta Binafsi katika kudahili
wanafunzi katika vyuo vya Ufundi ngazi ya kati
unaongezeka kutoka asilimia 21 mwaka 2015
hadi asilimia 25 mwaka 2020; na
(ii) Mchango wa Sekta Binafsi kudahili wanafunzi
katika ngazi ya shahada unaongezeka kutoka
asilimia 35 mwaka 2015 hadi asilimia 40 mwaka
2020.
(iii) Bajeti ya Sekta ya Elimu na Mafunzo inaongezeka
kutoka asilimia 17.6 mwaka 2015 hadi asilimia
25 ya bajeti ya Serikali mwaka 2020;
(iv) Bajeti ya Elimumsingi inaongezeka kutoka
asilimia 71 mwaka 2015 hadi asilima 75 ya Bajeti
ya Sekta ya Elimu na Mafunzo mwaka 2020;
103
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(v) Bajeti ya Elimu ya Ufundi na Elimu ya Juu
inaongezeka hadi kufikia asilimia 25 ya Bajeti ya
Sekta ya Elimu na Mafunzo ifikapo mwaka 2020;
na
(vi) Kuendelea kusimamia Sera ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi ya mwaka 2015 ambayo inaifanya
elimu ya Msingi hadi Sekondari kuwa ya lazima
na bila ya malipo.
(o) Kuanzisha Tume ya Walimu itakayosimamia
Maendeleo na Maslahi ya Walimu wote Nchini.
Maji
53. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kutekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta
ya Maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma
ya maji safi na salama kwa wananchi wote hususan wale
ambao wanaishi maeneo ya vijijini. Katika kipindi hicho
yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana:-
(a) Serikali imeendelea kuimarisha huduma za maji Vijijini
kwa kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu
ya maji, hali iliyochangia upatikanaji wa huduma ya
maji safi na salama Vijijini kuongezeka kutoka asilimia
53.5 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 67.7 mwaka
2015;
(b) Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali
yenye lengo la kuboresha huduma ya maji safi na
salama Mijini. Kutokana na jitihada hizo, kiwango
cha upatikanaji maji kwa wakazi wa Miji Mikuu ya
Mikoa kimeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2005
hadi asilimia 86 mwaka 2014. Aidha, katika jiji la Dar
es Salaam pamoja na Miji ya Bagamoyo na Kibaha,
kiwango cha upatikanaji maji kimeongezeka kutoka
asilimia 55 hadi asilimia 68 katika kipindi hicho.
(c) Maabara za maji 16 na Kituo cha Utafiti cha kuondoa
madini ya fluoride cha Ngurdoto kilichoko Arusha
104
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
zimejengewa uwezo kwa kuzipatia dawa za kufanyia
uchunguzi, mashine pamoja na usafiri. Aidha,
maabara za maji katika mikoa ya Kigoma, Singida,
Shinyanga na Bukoba zimekarabatiwa;
(d) Wananchi wameendelea kushirikishwa katika
utekelezaji wa miradi ya maji vijijini ambapo vyombo
vya watumiaji maji (COWSOs) 520 vimeundwa katika
Halmashauri mbalimbali nchini; na
(e) Usimamizi wa rasilimali za maji umeendelea
kuimarishwa na yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(i) Jumuiya 91 za Watumiaji Maji zimeundwa; na
(ii) Maeneo 26 ya vyanzo vya maji yametathminiwa
na kuzungushiwa uzio pamoja na maeneo ya
maji chini ya ardhi ya Maisaka na Makutupora.
(f) Ujenzi wa mabwawa manne ya Nyambele (Bunda),
Kinyambwiga (Bunda) Nyashitanda (Misungwi) na
New Sola (Maswa) umekamilika na yamekabidhiwa
kwa wananchi;
(g) Mradi wa maji wa Kahama/Shinyanga umekamilika
ambapo upanuzi wa mradi unaendelea katika maeneo
ya Vijiji vilivyoainishwa pamoja na Miji iliyopo
katika Wilaya hiyo. Aidha, Mji wa Ngudu, wilayani
Kwimba tayari umeunganishwa kwenye mradi huo
na wananchi wanapata maji; na
(h) Upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya majitaka
umefanyika katika Miji ya Moshi, Tanga, Arusha,
Mbeya, Iringa, Songea, Tabora, Mwanza, Morogoro,
Dar es Salaam na Dodoma.
105
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya
maji mkazi wa Nachingwea mara baada ya kuzindua mradi
wa maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 unaojumuisha
Wilaya za Nachingwea na Masasi Mkoani Mtwara.
54. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi
kilichopita, bado zipo changamoto mbalimbali katika
kutekeleza miradi ya maji nchini. Katika kipindi cha
miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali kukabiliana na changamoto hizo kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kuboresha huduma ya maji vijijini kutoka asilimia
67.7 mwaka 2015 hadi asilimia 85 mwaka 2020 kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kuendelea kutekeleza lengo la kuwapatia
wananchi waishio vijijini huduma ya maji safi,
salama na ya kutosha kama yalivyo Malengo ya
Milenia;
106
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Kujenga vituo vya kuchotea maji 93,051
vitakavyohudumia watu 23,262,876 ambavyo
vitaongeza idadi ya watu wanaopata huduma
ya maji safi na salama kutoka 20,022,283 mwaka
2015 hadi kufikia 43,285,159 mwaka 2020 sawa
na asilimia 53.7; na
(iii) Kuhamasisha ujenzi wa miundombinu ya
kuvuna maji ya mvua katika majengo ya Serikali,
asasi za umma na binafsi na nyumba za watu
binafsi.
(b) Kuboresha huduma ya Maji Mijini kwa kufanya
yafuatayo:-
(i) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika
Jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 68 mwaka
2015 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020;
(ii) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika
miji mikuu ya mikoa kutoka asilimia 86 mwaka
2015 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020;
(iii) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika
miji mikuu ya wilaya, miji midogo na maeneo ya
miradi ya Kitaifa kutoka asilimia 57 mwaka 2015
hadi kufikia asilimia 90 mwaka 2020; na
(iv) Kujenga Bwawa la Kidunda ili kuboresha
huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam.
(c) Kukamilisha miradi mikubwa ya maji na kuhakikisha
vijiji vyote vilivyopo kando kando ya miradi hiyo
mikubwa vinanufaika. Miradi hiyo ni:-
(i) Mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda
Nzega, Tabora na Igunga;
(ii) Mradi wa Maji wa Chalinze awamu ya tatu;
(iii) Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe;
na
107
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iv) Miradi ya Maji katika miji mikuu ya mikoa
mipya ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavi.
(d) Kupanua na kuboresha miradi ya maji ya kitaifa
ifuatayo:-
(i) Mradi wa Wanging’ombe, Maswa, Mugango-
Kiabakari, Handeni Trunk Main (HTM),
Chalinze, Makonde na Kahama-Shinyanga; na
(ii) Mradi wa kutoa maji kutoka Mto Ruvuma
kwenda Mji wa Mtwara ili kukidhi mahitaji ya
maji katika ukanda huo kutokana na ongezeko
la watu na shughuli za uwekezaji baada ya
kugundulika kwa gesi asilia.
(e) Kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabwawa katika
mikoa yenye ukame kama ifuatavyo:-
(i) Ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua
kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mifugo
na kilimo katika mikoa ya Dodoma, Singida,
Tabora, Mara, Simiyu, Arusha, Shinyanga,
Manyara na maeneo mengine yenye ukame;
(ii) Ujenzi wa mabwawa manane ya kimkakati kwa
ajili ya kuhifadhi mazingira, kuzuia mafuriko na
matumizi mengine; na
(iii) Kukamilisha ukarabati wa mabwawa ambayo
tayari yamekwisha jengwa.
55. Shughuli nyingine zitakazofanyika ili kuboresha
huduma ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini ni kama
ifuatavyo:-
(a) Kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwenye
vijiji vinavyozunguka maziwa ya Tanganyika, Nyasa
na Victoria;
(b) Kuendelea na uchimbaji wa visima vya maji na
kutumia pampu za maji zinazotumia nishati ya jua;
108
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kuiwezesha Sekta Binafsi kutoa huduma ya maji safi
kwa mfumo wa ubia na Sekta ya Umma;
(d) Kuendelea kuhamasisha wananchi kuunda Jumuiya
za Watumia Maji Vijijini katika Mabonde yote ya
maji nchini ifikapo mwaka 2020 ili kuwashirikisha
wananchi kikamilifu katika kupanga, kujenga,
kuendesha na kumiliki miradi ya maji;
(e) Kujenga na kukarabati Maabara za Maji kwa ajili ya
kusimamia ubora wa maji nchini na kutoa taarifa za
hali ya ubora wa maji kila mwaka;
(f) Kuziongezea uwezo wa kiutendaji taasisi
zinazoshughulika na Sekta ya Maji ambazo ni Chuo
cha Maji, Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa
Mabwawa na Bohari Kuu ya Maji ili kuongeza ufanisi
wa taasisi hizo;
(g) Kuendelea kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika
matumizi endelevu na usimamizi bora wa rasilimali
za maji shirikishi;
(h) Kuweka mfumo madhubuti na endelevu wa utunzaji
wa vyanzo vya maji na udhibiti wa uchafuzi wa
vyanzo hivyo;
(i) Kufanya tafiti za upatikanaji maji chini ya ardhi katika
maeneo mbalimbali nchini ili kuendeleza rasilimali
hiyo kwa matumizi mbalimbali;
(j) Kuimarisha mtandao wa ukusanyaji takwimu za
rasilimali za maji kwa ajili ya kupata taarifa sahihi
za hali ya rasilimali za maji nchini ili kuwezesha
mgawanyo mzuri wa maji na kupunguza migogoro
baina ya watumia maji; na
(k) Kuanzisha Mfuko wa Maji wa Taifa (National Water
Investment Fund) kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa
miradi nchini.
109
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Majitaka
(a) Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya uondoshaji
majitaka nchini.
(b) Kuiwezesha Sekta Binafsi kutoa huduma ya majitaka kwa
mfumo wa ubia na Sekta ya Umma.
110
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA TANO
UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
56. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kwa kuanzisha na kuendesha
programu za kukabiliana na changamoto za umasikini kwa
wananchi na ukosefu wa ajira hususan kwa vijana ambapo
mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Dhamana ya mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni
10.5 imetolewa na kuwanufaisha wananchi 10,646
katika vikundi 300 kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo
Mwanza, Mtwara, Mbeya, Rukwa, Singida, Dodoma,
Manyara, Ruvuma, Tanga, Kagera na Lindi;
(b) Kuanzishwa kwa mafunzo ya ujasirimali kwa
vijana wahitimu wa Vyuo Vikuu yenye lengo la
kuwawezesha kujiajiri kwa kutumia fursa zilizopo
badala ya kutegemea ajira za sekta rasmi;
(c) Kampuni 1,728 zimesajiliwa kwa ushirikiano na
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambapo
Kampuni 786 zilipata kiasi cha shilingi bilioni 7.8 kama
mitaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya
kiuchumi;
(d) Mfuko wa Ufundi na Utafiti umeanzishwa kwa
ushirikiano na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ambapo
kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 zilitolewa kwa vyuo tisa
vya Elimu ya Juu kati ya vyuo 49 vilivyotuma maombi
kwa ajili ya vifaa vya kufundishia;
(e) Uhamasishaji wa kuanzisha Ushirika wa Kuweka na
Kukopa (SACCOS na VICOBA) umewezesha SACCOS
kuongezeka kutoka 1,875 mwaka 2005 hadi 9,468
mwaka 2013. Idadi ya VICOBA imeongezeka hadi
kufikia 23,000 mwaka 2015 vyenye wanachama 700,000
na mtaji wa Shilingi bilioni 86. Aidha, wanachama wa
111
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SACCOS na vikundi vingine vya kijamii milioni 1.6
wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali. Kati ya hao,
wanawake ni asilimia 53 na wanaume ni asilimia 47.
(f) Shirikisho la Mafundi Seremala limeanzishwa kwa
lengo la kuboresha uzalishaji wa samani ili kukidhi
mahitaji ya soko la ndani na nje;
(g) Mfuko wa Uwezeshaji Wajasiriamali Wadogo
umeboreshwa na mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(i) Mikopo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 25.1
mwaka 2010 hadi kufikia bilioni 57.7 mwaka
2014 na kunufaisha wajasiriamali 95,336. Aidha,
urejeshaji wa mikopo umefikia asilimia 93.8; na
(ii) Mfuko umeongeza ajira 650,000 na kuzijengea
uwezo asasi ndogo ndogo za kifedha 590.
Aidha, wajasiriamali 8,665 wamepatiwa ujuzi
wa kuendesha biashara zao.
(h) Mfuko wa Udhamini wa Wafanyabiashara Wadogo na
wa Kati kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa
Mauzo ya Bidhaa Nje, umeongezewa mtaji kutoka
Shilingi bilioni 6 mwaka 2010 hadi shilingi bilioni
30.81 mwaka 2014. Aidha, mfuko umetoa dhamana
ya Shilingi milioni 448.59 ambapo asilimia 80 ya
dhamana imetumika kuwezesha shughuli za kilimo,
kuhamasisha uundaji wa mfumo wa Stakabadhi za
Mazao Ghalani na kuchochea watu wengi kufanya
biashara ya mauzo ya nje; na
(i) Mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 50.03
imetolewa kwa wajasiriliamali chini ya mpango wa
uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuongeza ajira.
Mikopo hiyo imetolewa kupitia Benki za CRDB na
NMB na kuwanufaisha wajasiriamali 74,701.
112
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
57. Kwa kutambua kwamba kuwawezesha wananchi
kiuchumi ni hatua ya msingi katika kujenga Taifa
lililoimarika kiuchumi na lenye lengo la kujitegemea,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha kuwa shughuli zote zenye mwelekeo wa
ushirika zinapewa msukumo stahiki kwa kuhamasisha
na kusimamia kwa nguvu uanzishaji wa vikundi vya
ushirika kama vile SACCOS na VICOBA; Vyama vya
Mazao, Ufugaji na Uvuvi hasa ikizingatiwa kuwa
ushirika ndiyo silaha kuu ya wanyonge na nguzo kuu
ya ujenzi wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea;
(b) Kuweka mfumo wa kuvitambua, kuvisajili na
kuviwezesha vikundi vyote vyenye mwelekeo wa
ushirika na ujasiriamali;
(c) Kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha
kwamba fursa ya mikopo kwa ajili ya mitaji
inapatikana bila ya urasimu na kwa masharti nafuu
na kuwafikia wananchi wengi mijini na vijijini;
(d) Kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji
kama Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa
ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia
Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) katika
vijiji husika;
(e) Kusaidia wafanyabiashara wadogo kwa kufanya
yafuatayo:-
(i) Kutenga maeneo mahsusi katika kila
Halmashauri kwa ajili ya biashara ndogo ndogo;
(ii) Kuondoa kero na malalamiko kuhusu ushuru
na kodi zinazotozwa na Halmashauri ambazo
zinakwamisha jitihada za wafanyabiashara
wadogo kujikwamua kimaisha;
113
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Kuwarasimisha wafanyabiashara wadogo
ili biashara zao zitambuliwe kisheria kwa
kuwapatia leseni, mafunzo ya ujasiriamali na
kuwaunganisha na asasi za fedha ili wapate
mikopo yenye masharti nafuu;
(iv) Kuanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara
Ndogo na za Kati;
(v) Kuanzisha mfuko mkubwa wa kitaifa wa
wajasiriamali wadogo na wa kati kwa
kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na
asasi nyingine za fedha;
(vi) Kuweka utaratibu utakaozitaka Halmashauri
kutenga asilimia 30 ya thamani ya manunuzi
yake kwa ajili ya biashara, kampuni au vikundi
vinavyomilikiwa na vijana/wanawake; na
(vii) Kuhakikisha kazi za ujenzi unaogharamiwa na
Serikali katika maeneo ya vijijini kwa mfano
ujenzi wa barabara, shule na zahanati zinatolewa
kwa vikundi vya vijana na wanawake katika
maeneo husika.
(f) Kuhamasisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika
uwekezaji kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ubia
baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na
kukamilisha marekebisho ya Sera na Sheria ya
Uwekezaji na pia kuandaa Sera ya Maendeleo
ya Sekta Binafsi;
(ii) Kuondoa vikwazo vya kuanzisha na kuendesha
biashara kwa kupitia upya Sheria, Kanuni na
Taratibu za biashara ili kuvutia uwekezaji
kutoka ndani na nje ya nchi; na
(iii) Kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika
miradi ya ubia na sekta ya umma pamoja na
114
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kuandaa mazingira rafiki ya biashara kwa lengo
la kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Urasimishaji Mali za Wanyonge:
58. Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ulianzishwa kwa
lengo la kuwawezesha wananchi na kuwapa nguvu
ya kiuchumi hasa wanyonge mijini na vijijini kwa
kuwawezesha kumiliki ardhi na kufanya biashara katika
mfumo rasmi wa kisasa unaoendeshwa kwa mujibu wa
Sheria. Hivyo, kupitia urasimishaji rasilimali na biashara,
MKURABITA ni nyenzo muhimu ya uwezeshaji
wananchi kiuchumi, kupunguza umasikini na kuongeza
ajira nchini. Katika kipindi cha miaka mitano ya Ilani hii
ya 2015-2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali
kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuongeza kasi ya utambuzi, usajili na umiliki wa ardhi
pamoja na kuendeleza urasimishaji wa rasilimali za
wananchi, kuwashirikisha na kuwawezesha kutumia
rasilimali zao kama dhamana ya kupata mitaji;
(b) Kutekeleza mipango ya matumizi bora ya ardhi
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ardhi
wakiwemo Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi
Bora ya Ardhi na Halmashauri za Miji, Majiji na
Wilaya ili kukamilisha kazi ya upimaji wa mipaka ya
vijiji vyote na kuwahamasisha wananchi kuchangia
upimaji wa mashamba yao na kuwapatia hati miliki
za kimila;
(c) Kuanzisha chombo cheye nguvu ya kisheria
kitakachoratibu shughuli za urasimishaji rasilimali za
wananchi; na
(d) Kuanzisha Mfuko Maalumu wa kugharamia shughuli
za urasimishaji ambao utaziwezesha Halmashauri
za Wilaya, Miji na Majiji kukopeshwa kwa masharti
nafuu. Mfuko huu utaendeshwa kwa utaratibu wa
Dhamana ya Benki (Bank Guarantee Scheme).
115
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kuwawezesha Vijana Kujiajiri
59. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuongeza
ajira kwa vijana kwa kuanzisha na kuendesha programu
za kukabiliana na ongezeko kubwa la vijana wanaofuzu
Elimu ya Msingi, Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu kila
mwaka wanaohitaji ajira ambapo mafanikio yafuatayo
yamepatikana:-
(i) Takriban vijana milioni 16 wameajiriwa katika sekta
mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka 2011
hadi 2015;
(ii) Mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya
Shilingi bilioni 5.8 imetolewa kwa SACCOS 244 na
vikundi vya vijana 667 katika kipindi cha 2014/15;
(iii) Jumla ya vijana 35,000 wamepewa mafunzo ya
ujasiriamali ambapo kati yao, vijana 11,500 walikuwa
wahitimu wa elimu ya juu; na
(iv) Wahitimu 325 wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine,
wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na
kuwezeshwa kupata mitaji kupitia ushirikiano wa
Serikali na Umoja wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha
Kilimo Sokoine (SUGECO).
60. Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa vijana
ambao ni kundi kubwa la nguvukazi. Changamoto
zinazowakabili ni pamoja na ukosefu wa ajira, elimu na
maarifa ya kisasa katika uzalishaji mali, mitaji, biashara
na ujasiriamali. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani
hii, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya
yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini
zinaendelea kutenga, kurasimisha, kupima na
kuyawekea miundombinu maeneo maalumu ya
vijana kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali katika
116
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
sekta mbalimbali hususan kilimo, ufugaji, madini,
viwanda vidogo, uvuvi, mawasiliano na biashara;
(b) Kuziwezesha SACCOS za vijana katika Halmashauri
zote nchini kupata mikopo kutoka kwenye benki na
taasisi nyingine za fedha;
(c) Kuwajengea uwezo vijana kutumia TEHAMA katika
kuboresha uzalishaji mali, ufanisi, viwango na
kutafuta masoko katika shughuli zao za uchumi;
(d) Kuwawezesha vijana wanaohitimu Elimu ya Juu na
Vyuo vya Ufundi kuunda makampuni kulingana na
fani zao kwa lengo la kuwapatia mitaji na nyenzo
kupitia taasisi za fedha na mifuko mingine ya
uwezeshaji;
(e) Kuhamasisha na kuweka mazingira yatakayowezesha
vijana wajasiriamali wadogo kujiunga na Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii ili kuweza kupata mikopo na
kunufaika na mafao mengineyo yatolewayo na mifuko
hiyo;
(f) Kuviwezesha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
(FDCs) ili viweze kutoa mafunzo ya ujasiriamali, stadi
za maisha, ujasiri, uongozi na TEHAMA kwa vijana;
(g) Kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinaanzisha
vituo maalumu ili kuwawezesha vijana kupata sehemu
ya kujifunza kwa vitendo shughuli mbalimbali
za ujasiriamali na kupata taarifa mbalimbali za
maendeleo;
(h) Kuwawezesha vijana wanaohitimu Vyuo Vikuu na
Vyuo vya Kati kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi
mbalimbali kwa lengo la kuwapatia uzoefu na maadili
ya kazi ili waweze kuajirika au kujiajiri wenyewe; na
(i) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini
zinaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana kwa mujibu wa Sheria ili
117
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye masharti
nafuu.
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi
61. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jitihada za
kuwaendeleza wanawake zimeendelea kuchukuliwa kwa
kutunga Sera, Sheria na Programu mbalimbali zenye lengo
la kuongeza fursa za kiuchumi na kuwajengea uwezo wa
kitaaluma, kibiashara, mbinu za kupata mitaji, masoko
pamoja na mikopo.
62. Fursa hizo zimewawezesha wanawake kujiajiri katika
shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kuinua vipato
vyao na vya familia.
63. Kwa kutambua kuwa uwezeshwaji wa wanawake
kiuchumi umeleta maendeleo na mabadiliko makubwa
kwa wanawake, familia na Taifa kwa ujumla na kwa
kutambua kuwa wanawake ndio wazalishaji wakuu wa
chakula na walezi wa familia, Chama Cha Mapinduzi,
katika miaka mitano ijayo, kitaielekeza Serikali
kuendelea kuwaendeleza wanawake kiuchumi kwa
kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu,
elimu ya ujasiriamali na biashara ili kuwawezesha
kuongeza ajira, ujuzi wa kujiajiri, fursa za kipato na
kujikimu;
(b) Kuwahamasisha kuanzisha na kujiunga katika
vikundi vya uzalishaji mali, vikundi vya kuweka
na kukopa (SACCOS na VICOBA) na kuwawezesha
kimtaji ili kupanua shughuli zao za uzalishaji mali;
(c) Kuwahamasisha kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii ili kuweza kupata mikopo na kunufaika na
mafao mengineyo yatolewayo na mifuko hiyo hasa
mafao ya uzazi na elimu;
118
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini
zinaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Wanawake kwa mujibu wa Sheria ili
kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye masharti
nafuu; na
(e) Kuondoa kero na malalamiko ya wanawake
wajasiriamali hasa mama lishe, wauza mbogamboga,
wauza maandazi/vitumbua kuhusu maeneo ya
kufanyia biashara, ushuru na kodi zinazotozwa na
Halmashauri ambazo zinakwamisha jitihada zao za
kujikwamua kimaisha.
119
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA SITA
MAZINGATIO MAALUMU YA ILANI
KUHUSU ZANZIBAR
Mwenyekiti wa CCM Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati)
akiwatambulisha Mgombea wa CCM wa Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli (kulia) na
Mgombea wa CCM wa Urais wa Zanzibar Ndugu Ali Mohamed Shein
Utangulizi
64. Katika Sura hii, Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015 - 2020, inaelezea na kuainisha maeneo
muhimu ya Sera za CCM, kwa kuzingatia mazingira
maalumu ya Zanzibar. Kwa kutambua na kuridhika na
Sera hizo ambazo zinazingatia maslahi mapana ya Taifa
letu yaani haki, umoja, mshikamano, uwazi na uwajibikaji,
Wazanzibari wameendelea kuiunga mkono CCM na kuipa
ridhaa ya kuongoza Serikali ya Mapinduzi kwa kuichagua
katika chaguzi zote zilizopita.
65. Katika kipindi cha mwaka 2010 - 2015 cha Awamu ya Saba
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi
wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Zanzibar imeendelea kupiga
hatua kubwa ya maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii.
120
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
MAFANIKIO NA MALENGO YA KIUCHUMI
66. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi mahiri
wa Dkt. Ali Mohamed Shein imeweza kutekeleza kwa
mafanikio makubwa, Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka 2010 - 2015 na kuendelea kuimarisha umoja
wa kitaifa na utoaji wa huduma mbalimbali za kiuchumi
na kijamii. Baadhi ya mafanikio hayo ya kujivunia ni kama
yafuatayo:-
Hali ya Uchumi
67. Katika miaka mitano iliyopita Sekta ya Uchumi imepata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Kukuza Uchumi:
(i) Pato la Taifa limeongezeka kutoka thamani ya
Shilingi bilioni 1,050.8 mwaka 2010 hadi kufikia
thamani ya Shilingi bilioni 2,138.5 mwaka 2014.
Kiwango cha ukuaji wa uchumi kiliongezeka
kutoka asilimia 4.3 mwaka 2010 hadi asilimia 7.0
mwaka 2014;
(ii) Mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 6.1
mwaka 2010 hadi asilimia 5.6 mwaka 2014;
(iii) Pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka
shilingi 856,000 sawa na dola za Kimarekani
613 mwaka 2010 na kufikia shilingi milioni 1.56
sawa na Dola 939 mwaka 2014;
(iv) Kiwango cha thamani ya bidhaa zilizosafirishwa
nje, kiliongezeka kutoka shilingi bilioni 18
mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 133.6
mwaka 2014; na
(v) Kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani
kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 181.379
mwaka 2010/2011 hadi shilingi bilioni 330.7
mwaka 2013/2014.
121
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Maeneo Huru ya Kiuchumi
(i) Mpango Mkuu wa Matumizi ya Ardhi (Land
Use Plan) wa eneo Huru la Kiuchumi la Fumba,
umekamilika. Jumla ya hekta 3,000 zimewekewa
mipaka na kugawanywa katika eneo la vijiji vya
asili (hekta 1,310), eneo la uwekezaji (hekta 743)
na eneo la akiba (hekta 947). Aidha, maandalizi
ya kulifungua kiuchumi Eneo Huru la Kiuchumi
la Micheweni, yanaendelea.
(ii) Hadi kufikia mwaka 2014, jumla ya miradi 165,
yenye mtaji wa thamani ya Dola za Kimarekani
milioni 526.7 imeidhinishwa kuwekezwa na
Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar
(ZIPA) ikilinganishwa na miradi 33 mwaka 2010
yenye mtaji wa thamani ya Dola za Kimarekani
milioni 115.2. Miradi 63 kati ya hiyo, ni ya
wawekezaji Wazalendo, na 90 ni ya wageni.
Miradi hiyo yote inazalisha ajira zipatazo 6,658
kwa wananchi.
(c) Uwakilishi wa Sekta Binafsi:
Baraza la Biashara la Zanzibar limeanzishwa na
kushiriki katika majadiliano ya ubia wa uwekezaji
kwa maendeleo ya viwanda na mashirikiano kwa
ajili ya wote (Smart Partneship Dialogue). Miongoni
mwa yaliyojadiliwa katika vikao hivyo ni pamoja na
kuimarisha mapato, kukuza Pato la Taifa na Faharisi
ya Bei ya mtumiaji.
(d) Mazingira Bora ya Kiuchumi:
Sheria ya Fedha na Uwekezaji imefanyiwa mapitio
ili iendane na mazingira halisi ya kiuchumi na kutoa
nafasi zaidi ya kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo
nchini. Kutokana na hatua hizo, wawekezaji kutoka
nje wameweza kujitokeza na kuwekeza katika miradi
ya maendeleo.
122
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Kupambana na Umasikini:
(i) Mifuko ya mikopo kwa wananchi na
wafanyabiashara wadogo wadogo, yaani
Mfuko wa Kujitegemea na Mfuko wa JK & AK
imeunganishwa pamoja na kuanzishwa mfuko
mmoja tu (Mfuko wa Kuwawezesha Wananchi
Kiuchumi). Mfuko huo umezinduliwa ukiwa
na mtaji wa shilingi bilioni 2.31. Aidha, mikopo
1,603 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.45,
imetolewa katika shehia 305 Unguja na Pemba
na kutoa ajira za moja kwa moja 20,614,
zilizowahusisha wanawake 11,873 na wanaume
8,741;
(ii) Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF II) umekamilika
ambapo miradi 656 yenye thamani ya Shilingi
bilioni 9.4 imetekelezwa. Kati yake miradi 324
ni ya Unguja na 332 ni ya Pemba. Miradi hiyo
inahusu shughuli za kijamii, uvuvi (ununuzi wa
boti na zana za kuvulia) pamoja na mapambano
dhidi ya UKIMWI.
(iii) Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF III) umeanza katika
Shehia 40 za Unguja na Pemba (Unguja 20 na
Pemba 20) ambapo miradi 103 (Unguja 68 na
Pemba 35) yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.1
imeanzishwa. Miradi hiyo inahusu ujenzi wa
skuli za maandalizi, ujenzi wa matuta ya kuzuia
maji ya bahari, hifadhi ya mazingira na ukarabati
wa njia za ndani. Jumla ya kaya masikini 6,598
zimenufaika na miradi hiyo.
(iv) Vikundi vya kiuchumi 250 na wajasiriamali
6,000 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali,
wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu 250, ili
kubadili mitazamo yao na kuwajengea uwezo
wa kujiajiri wao wenyewe; na
123
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(v) Kituo cha kulelea wajasiriamali kimeanzishwa.
Kituo hicho ni cha kwanza na cha aina yake
katika ukanda wa Afrika Mashariki na kinatoa
mafunzo katika fani za Uchumi, TEHAMA,
Utalii na Usindikaji wa Mazao ya Biashara.
Kukuza Uchumi
68. Katika kipindi kilichopita (2010 -2015), Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM,
imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi na
kuimarisha huduma za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaendeleza
mafanikio hayo na kuandaa Mipango ya kipaumbele ili
kufanikisha huduma za kilimo, utalii endelevu pamoja
na kujenga mazingira bora ya biashara na kuimarisha
huduma za jamii kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kufanya mapitio ya Mpango wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umasikini (MKUZA) na kuandaa mkakati
mpya wa utekelezaji wa Mpango huo (MKUZA III) na
Dira ya Maendeleo ya Zanzibar (Vision 2020);
(b) Kujenga mazingira yatakayowezesha uchumi wa
Zanzibar kufikia kiwango cha uchumi wa nchi zenye
kipato cha kati, kiwango cha ukuaji wa uchumi kufikia
wastani wa asilimia 10, mfumuko wa bei kubaki katika
tarakimu moja na wastani wa pato la kila mwananchi
kuongezeka kutoka kiwango cha sasa cha wastani wa
dola za Kimarekani 939 (shilingi 1,340,000) hadi dola
1950 (shilingi 3,500,000) ifikapo mwaka 2020;
(c) Kuendeleza udhibiti wa mapato na nidhamu katika
matumizi ya Serikali, kuziba mianya ya uvujaji wa
mapato ya Serikali na kuanzisha Msimamizi wa
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu; na
(d) Kupunguza utegemezi kwa Wahisani wa Maendeleo,
misamaha ya kodi isiyo na tija kwa Taifa na kuongeza
kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka
Shilingi bilioni 330.7 mwaka 2013/2014 hadi kufikia
124
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Shilingi bilioni 800 ifikapo mwaka 2020/21 na
kushusha kiwango cha nakisi ya Bajeti ya Serikali
kutoka uwiano wa asilimia 8 ya Pato la Taifa mwaka
2014/2015 hadi kufikia asilimia 7 ifikapo mwaka
2019/2020.
Mchango wa Sekta Binafsi
69. Sekta Binafsi hutoa mchango mkubwa katika kukuza
uchumi na maendeleo ya Taifa. Katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita (2010-2015), Mamlaka ya Uwekezaji
Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), iliidhinisha jumla ya
miradi 35 yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni
1.06 na kutengeneza ajira 1,365. Ili kuongeza mchango wa
Sekta Binafsi katika kukuza Uchumi wa Zanzibar, Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM,
itatekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Mwongozo na Sheria
ya Ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi na kuharakisha utekelezaji wa miradi yenye
tija inayopendekezwa kufanyika;
(b) Kukamilisha utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji
wa mji mpya wa kisasa katika Maeneo Huru ya
Uchumi ya Fumba na Micheweni, na kuweka vivutio
kwa wawekezaji wa Sekta ya Viwanda; na
(c) Kujenga mazingira endelevu ya kuwawezesha
kimtaji wawekezaji wa ndani na kuwaunganisha na
wawekezaji wa nje pamoja na kuvishawishi Vyombo
na Taasisi za Fedha nchini, kuwapatia mikopo yenye
riba na masharti nafuu na kupunguza urasimu na
vikwazo katika biashara, ukiwemo mlolongo wa
leseni na kodi.
125
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kupambana na Umasikini
70. Ili kuongeza nguvu na kasi ya kupambana na umasikini
katika kipindi kilichopita (2010-2015), Mfuko wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi umeanzishwa. Kwa kupitia mfuko
huo wananchi wengi hususan vijana, wanawake na
wafanyabishara wadogo wadogo wameweza kupatiwa
mitaji (mikopo) na kujikwamua kiuchumi. Katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaendeleza
jitihada hizo na kuielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Uwezeshaji wa
Wananchi Kiuchumi ili kuongeza uwezo wake wa
kutoa mikopo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara
wadogo, kuimarisha Kituo cha Kulelea Wajasiriamali
na kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ili
kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuondokana na
umasikini;
(b) Kuendelea kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi
vya ushirika na hasa ushirika wa uzalishaji mali,
vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS), VICOBA
pamoja na BENKI NDOGO vyenye wanachama wengi
na kuleta tija kwa jamii;
(c) Kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
ili kukamilisha Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini (TASAF III) na kubuni programu
nyingine za kusaidia jamii kupambana na umasikini;
na
(d) Kuendelea kuimarisha na kusimamia Mfuko wa
Maendeleo ya Jimbo na kuhakikisha kwamba, fedha
za mfuko huo zinatumika kwa lengo lililokusudiwa
na hususan kuimarisha huduma za jamii.
(e) Kuzihamasisha asasi za kifedha nchini kuanzisha
dirisha maalumu kwa ajili ya kuwapatia mikopo
yenye masharti nafuu wanawake na vijana. Aidha,
idara maalumu ya mikopo itaanzishwa ili kusimamia
majukumu yafuatayo:-
126
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Asasi za
Mikopo Nafuu (Micro-Finance Policy) ili
kuwawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika
na huduma za kifedha kwa masharti nafuu;
(ii) Kutoa mikopo 5,000 yenye thamani ya shilingi
bilioni 2.5 itakayowanufaisha jumla ya wananchi
50,000 kutoka makundi mbalimbali ya jamii
hususan wanawake, vijana na walemavu Unguja
na Pemba;
(iii) Kuimarisha huduma za mikopo kwa kutumia
njia mbalimbali ikiwemo teknolojia ya mitandao
ya simu ili kupunguza gharama na muda wa
upatikanaji na urejeshaji wa fedha za mikopo;
na
(iv) Kuongeza kiwango cha dhamana ya Serikali
katika benki kutoka shilingi milioni 100 hadi
shilingi milioni 500 ili ziweze kuwahudumia
wajasiriamali 50,000.
(f) Kuanzisha jumla ya vituo kumi vya huduma za
biashara, kimoja kwa kila Wilaya ili kuongeza tija
katika shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara
wadogo.
Sekta za Uzalishaji Mali
Kilimo
71. Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 31 katika Pato la Taifa
(GDP) na kuwawezesha wananchi walio wengi kujikimu
kimaisha na kuwapatia uhakika wa chakula na lishe bora.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya Kilimo
imepata mafaniko yafuatayo:-
(a) Sera ya Masoko na Bidhaa za Kilimo imepitishwa na
kuanza kutumika. Sheria ya kuanzishwa kwa Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar, Sheria ya Haki Miliki
za Wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea,
127
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Sheria ya Uhifadhi na Utibabu wa Mimea na Sheria ya
Uhakika wa Chakula na Lishe zimepitishwa;
(b) Mashamba darasa 1,200 ya wakulima yameanzishwa.
Wakulima 2,800 wa zao la mpunga na 1,500 wa
zao la muhogo na mboga mboga wamepatiwa
mafunzo. Jumla ya tani 674,334 za mazao ya chakula
zimezalishwa mwaka 2014 ikilinganishwa na tani
346,535 zilizovunwa mwaka 2013. Ongezeko hilo ni
sawa na asilimia 95;
(c) Jumla ya matrekta mapya 45 yamenunuliwa, matrekta
makongwe 37 yamefanyiwa matengenezo na mashine
za kuvunia mpunga 14 zimenunuliwa. Eneo la
uzalishaji wa zao la mpunga limeongezeka kutoka
hekta 10,000 mwaka 2010 hadi hekta 34,000 mwaka
2015. Kiwango cha uzalishaji wa zao hilo kimeongezeka
kutoka tani 20,000 hadi tani 33,655. Idadi ya kaya
zinazojishughulisha na kilimo imeongezeka kutoka
10,000 mwaka 2010 hadi 70,000 mwaka 2014;
(d) Mafunzo ya nadharia na vitendo yametolewa kwa
wakulima 400 juu ya mbinu za kilimo bora cha
mpunga wa umwagiliaji. Wakulima 2,000 (700 Pemba
na 1,300 Unguja) walipatiwa mafunzo juu ya mbinu
bora za uzalishaji mpunga;
(e) Eneo la kilimo cha umwagiliaji limeongezeka kutoka
hekta 600 mwaka 2010, hadi hekta 800 mwaka 2014.
Jumla ya hekta 200 za miundombinu ya umwagiliaji
maji zimeimarishwa. Kiwango cha uzalishaji wa
mpunga wa kumwagilia maji kimeongezeka kutoka
tani 2 mwaka 2010 hadi tani 4 kwa hekta mwaka 2014;
(f) Matumizi ya pembejeo kati ya mwaka 2010 hadi 2015
yameongezeka kutoka tani 13 hadi 750 za mbegu tani
203 hadi 1,500 za mbolea na lita 10,000 hadi 30,000
za dawa ya kuulia magugu. Wakulima 61,500 wa
mpunga wa kumwagilia maji na wa kutegemea mvua
wamepatiwa ruzuku ya bei za pembejeo (asilimia 75);
128
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Vikundi 33 vya wakulima 652 (wanawake 345 na
wanaume 307) vimeanzishwa na kupatiwa mafunzo
ya kilimo cha mbogamboga na matunda;
(h) Chuo cha Kilimo cha Kizimbani kimeimarishwa. Idadi
ya wanafunzi wa ngazi ya cheti imeongezeka kutoka
300 mwaka 2010 hadi 741 mwaka 2014. Mafunzo
ya Stashahada katika fani ya uzalishaji mifugo na
uzalishaji wa mazao na kilimo mjumuisho yameanza
kufundishwa;
(i) Kituo cha Utafiti cha Kizimbani kimepandishwa
hadhi kuwa Taasisi kamili ya Utafiti wa Kilimo.
Ujenzi wa maabara mpya ya utafiti wa zao la mpunga
na ukarabati wa maabara ya udongo na maabara ya
usarifu wa mazao umekamilika. Mbegu nne mpya za
muhogo na mbili za viazi vitamu vyenye viini lishe na
kustahamili ukame zimegunduliwa;
(j) Jumla ya miche 3,500,000 ya mikarafuu imeoteshwa
katika vitalu mbalimbali vya Serikali. Kati ya hiyo
miche 2,216,328 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.4
imetolewa kwa wakulima bila ya malipo. Kiwango
cha uzalishaji wa karafuu kimeongezeka kutoka tani
2,673 mwaka 2010 hadi kufikia tani 5,340 mwaka 2014.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50;
(k) Jumla ya tani 11,477 za karafuu zenye thamani ya
dola za Kimarekani milioni 130.82 zimesafirishwa
na kuuzwa nje ya nchi. Bei ya kuuzia karafuu kwa
wakulima imeongezeka kutoka shilingi 5,000 hadi
shilingi 14,000 kwa kilo moja. Bei hiyo ni sawa na
asilimia 80 ya bei ya karafuu katika soko la dunia; na
(l) Jumla ya miche ya minazi mirefu 89,200 (Unguja
52,900 na Pemba 36,300) imeoteshwa na kupandwa
katika kipindi cha 2010 hadi 2014.
129
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia zao la karafuu
alipotembelea katika shamba la Bw.Said Sinani (hayupo
pichani) Chumbageni - Kusini Pemba akiwa katika ziara
maalum
72. Kwa kutambua kwamba bado zipo changamoto
zinazowakabili wakulima walio wengi, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015 - 2020), Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, chini ya uongozi wa CCM itaendelea kuzipatia
ufumbuzi changamoto hizo kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni
za kilimo bora kwa kuzingatia Mpango Mkuu wa
Umwagiliaji Maji pamoja na programu ya mapinduzi
ya kilimo na usimamizi wa raslimali za misitu;
(b) Kuongeza idadi ya Mabwana/Mabibi shamba kutoka
172 mwaka 2014 hadi kufikia mmoja kwa kila Shehia
ifikapo mwaka 2020 na kuendeleza mafunzo kwa
wakulima na kutilia mkazo matumizi ya Kanuni za
Kilimo Bora katika uzalishaji wa mazao ya chakula na
biashara pamoja na matumizi ya zana za kisasa;
130
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maji kwa
kuzingatia Mpango Mkuu wa Kilimo cha Umwagiliaji
maji na kuimarisha eneo la hekta 2,105 za miundombinu
ya umwagiliaji maji katika bonde la Cheju, Kilombero,
Chaani, Mlemele na Makwararani;
(d) Kuongeza uzalishaji na ubora wa zao la karafuu
pamoja na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara
hususan manjano, hiliki, tangawizi, pilipilimanga,
kungumanga, kilimo cha alizeti na kuanzisha mazao
mapya ya biashara;
(e) Kuimarisha vituo vya huduma na udhibiti wa maradhi
ya mazao, wadudu waharibifu pamoja na ukaguzi na
karantini dhidi ya maradhi na wadudu waharibifu wa
mimea na mifugo ili kudhibiti maradhi ya mimea na
mifugo nchini;
(f) Kuendeleza utafiti wa mbegu bora za mazao ya
chakula, biashara, mboga mboga na matunda na
kuhakikisha kwamba, matumizi ya takwimu na
matokeo ya utafiti huo yanawafikia wakulima na
kutumika kufanya maamuzi;
(g) Kukiimarisha Chuo cha Kilimo Kizimbani ili kuongeza
idadi ya wataalamu wa kilimo na mifugo nchini kwa
kukifanya kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo
Kikuu cha Taifa (SUZA);
(h) Kuhamasisha Sekta Binafsi kujenga viwanda vya
usarifu wa mazao ili kuongeza thamani na ubora
wa mazao ya mboga na matunda, nazi na karafuu
ili kukuza kipato cha wakulima na kurahisisha
upatikanaji wa soko;
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi ya Taifa
ya Chakula ili kujikinga na balaa la njaa na ukosefu
wa chakula na lishe; na
(j) Kuwawezesha wakulima kumudu gharama za
matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi wa
131
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
matumizi ya ardhi na uzalishaji wenye tija kupitia
utekelezaji wa programu ya kuwawezesha wakulima
wa vijijini.
Ufugaji
73. Umuhimu wa ufugaji bora na wa kisasa unazingatia haja
ya kuongeza tija na ubora wa mazao ya mifugo kutokana
na uhaba wa ardhi, ongezeko la idadi ya watu na kupanuka
kwa shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya Mifugo imepata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Wafugaji 23,393 wa ng’ombe, mbuzi na kuku
wametembelewa na kupatiwa ushauri wa kitaalamu
pamoja na mbinu za ufugaji wa kisasa. Pia vituo vya
wafugaji 570 vimeanzishwa ili kutoa mafunzo kwa
wafugaji;
(b) Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita
4,343,351 mwaka 2010 hadi 27,243,351 mwaka 2014.
Aidha, jumla ya wafugaji 40 wamepatiwa mafunzo ya
usindikaji wa mazao ya maziwa. Uzalishaji wa mayai
umeongezeka kwa asilimia 14 kutoka 164,270,132
mwaka 2010 hadi 186,870,292 mwaka 2014;
(c) Huduma za upandishaji wa ng’ombe kwa
sindano zimeimarishwa. Jumla ya ng’ombe 6,400
wamepandishwa kwa kutumia mbegu za kisasa;
(d) Vituo vya huduma za utibabu wa mifugo vimefanyiwa
ukarabati na kupatiwa madawa. Watoa huduma za
msingi 42 na madaktari wasaidizi 90, wamepatiwa
mafunzo Unguja na Pemba;
(e) Kiwanda kikubwa cha usarifu maziwa cha Azam
Dairy kimeanzishwa huko Fumba na tayari kimeanza
uzalishaji. Kiwanda hicho kitatoa ajira 200. Aidha,
kiwanda kingine cha kusarifu kuku kimeanzishwa
huko Maruhubi; na
132
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(f) Wafugaji wameshajiishwa na kupatiwa mafunzo
juu ya matumizi ya samadi kama chanzo cha nishati
mbadala na kupatiwa utaalamu wa kutumia na
kutunza mitambo ya Biogesi. Jumla ya mitambo 32
imejengwa Unguja na Pemba.
74. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020),
SMZ chini ya uongozi wa CCM itaendelea kuhimiza na
kuimarisha ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa
na nyama, mbuzi pamoja na kuku wa nyama na mayai
ili kuongeza tija na kipato cha wafugaji kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Programu
mbalimbali za elimu kwa wafugaji ili kuwawezesha
wafugaji wadogo kutekeleza kanuni za ufugaji wa
kisasa na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo na
kukidhi mahitaji na viwango vya soko la ndani na nje;
(b) Kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za kinga
na tiba za mifugo na kuwapatia wafugaji huduma
ya upandishaji wa ng’ombe kwa sindano ili kupata
mbegu bora pamoja na kuhamasisha sekta binafsi
kutoa huduma za afya na pembejeo za mifugo;
(c) Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ili kuwekeza
katika sekta ya mifugo na viwanda vya usindikaji wa
mazao ya mifugo; na
(d) Kuongeza uwezo wa kitaaluma kwa wafanyakazi wa
sekta ya mifugo.
Uvuvi na Mazao ya Baharini
75. Uvuvi na uzalishaji wa mazao ya bahari ni moja ya shughuli
muhimu za kiuchumi zinazofanywa na wananchi wengi
wanaoishi pembezoni mwa mwambao wa bahari. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta ya
Uvuvi imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Vikundi 167 vya wavuvi wadogo wadogo na vikundi
48 vya Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari vimeanzishwa
133
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na kupatiwa mafunzo pamoja na msaada wa vifaa
mbalimbali vya uvuvi. Leseni za uvuvi 32,500
zimetolewa na vyombo 10,210 vimesajiliwa ambapo
tani 148,535 za samaki zenye thamani ya shilingi
bilioni 572.5 zimevuliwa;
(b) Vikundi 144 vya Uvuvi na Ufugaji wa Viumbe vya
Baharini (samaki, kaa na majongoo) vikiwemo vile vya
ufugaji wa chaza na lulu vimeanzishwa na kupatiwa
mafunzo, vitendea kazi pamoja na vifaranga vya
samaki 33,081. Mabwawa sita (6) ya mfano (mashamba
darasa) ya kufugia samaki yamejengwa Unguja na
Pemba na wajasiriamali 59 wa mazao ya baharini
walipelekwa China ili kupata mafunzo ya ufugaji wa
mazao ya baharini;
(c) Kanuni za Usimamizi wa Maeneo ya Hifadhi
zimeandaliwa na kuchapishwa katika Gazeti Rasmi
la Serikali. Kanuni hizo zinahusu maeneo ya zamani
ya MENAI, MIMCA na PECCA pamoja na maeneo
mapya ya Tumbatu na Changuu - Bawe. Pia ulinzi
shirikishi umeimarishwa kwa kuanzisha kitengo cha
kusimamia maeneo yote ya hifadhi za baharini na
kuanzisha Kamati za Doria Vijijini;
(d) Kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi ya Bahari
(IMS) na Kampuni ya ununuzi wa mwani ya Birr,
utafiti umefanywa juu ya uwezekano wa kulima
mwani aina ya “cottonii” kwenye kina kirefu cha
maji huko Fundo, Shumba Mjini, Mkia wa Ng’ombe,
Tumbe na Makangale Pemba na kubaini mafanikio
mazuri. Jumla ya tani 51,687 zenye thamani ya shilingi
bilioni 18.7 zimezalishwa na kusafirishwa nje ya nchi;
(e) Ili kuwaendeleza wakulima wa mwani, jumla ya
vihori 100 vimetolewa kwa njia ya mkopo. Vihori
hivyo vimetolewa kwa vikundi 50 vya Wanawake
wanaolima mwani kwa wingi katika vijiji 10 vya
Unguja ili kurahisisha usafirishaji wa mwani kutoka
134
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
baharini. Vile vile, mashine za kukaushia mwani na
matunda kwa nguvu za jua zimeanza kutumika; na
(f) Idadi ya leseni za uvuvi wa Bahari Kuu imeongezeka
kutoka 23 mwaka 2009/2010 hadi 77 mwaka
2013/2014. Mapato yatokanayo na leseni hizo, nayo
yameongezeka kutoka shilingi billion 1.12 mwaka
2009/2010 hadi kufikia shilingi bilioni 3.30 mwaka
2013/2014.
Wakulima wa zao la Mwani wakivuna zao hilo katika kijiji
cha Kojani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
76. Kwa kutambua mchango mkubwa wa uvuvi na mazao
ya baharini katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar na
kipato cha mwananchi, Chama Cha Mapinduzi katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020) kitaielekeza
SMZ kuendeleza uvuvi na mazao ya baharini kwa kasi
zaidi kwa kutekeleza yafuatayo:-
135
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria za Uvuvi
ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali za bahari na
uhifadhi wa mazingira na kuendeleza jitihada za
kuwahamasisha wavuvi wadogo kuanzisha vikundi
vya ushirika na kuwapatia mafunzo na mikopo nafuu
ya zana za kisasa ili kuongeza mapato yao;
(b) Kuandaa Mpango na mazingira ya kuvutia Sekta
Binafsi kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu,
utengenezaji wa boti za uvuvi, ujenzi wa vyumba
vya baridi (cold rooms) pamoja na viwanda vya
kusindika samaki. Aidha, wavuvi hasa vijana
watahamasishwa na kupatiwa mafunzo na zana za
kisasa zitakazowawezesha kuvua katika kina kirefu
cha maji;
(c) Kuendelea kununua vihori 500 vya kubebea mwani na
kuvisambaza kwa wakulima wa mwani 3,000 Unguja
na Pemba ili kuongeza uzalishaji wa mwani na
kuhamasisha wafugaji wa samaki, chaza, kaa, kamba
na majongoo ili kuendeleza uzalishaji wa mazao hayo
na kusimamia utafutaji wa masoko;
(d) Kuendelea kusimamia mpango shirikishi wa maeneo
ya hifadhi ya bahari yakiwemo maeneo ya Tumbatu,
Chumbe-Bawe, Menai na MIMCA kwa Unguja na
Kisiwa Panza, Kokota na Mwambe kwa PECCAPemba;
na kuhakikisha kwamba, jamii inayozunguka
maeneo hayo inanufaika na uhifadhi huo; na
(e) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa pamoja
zitaandaa Sera ya Uvuvi wa Bahari Kuu ili kuvutia
wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza katika
Sekta ya Uvuvi wa bahari kuu, kujenga viwanda vya
kusindika samaki, kuanzisha Chuo cha Mafunzo ya
Uvuvi na kujenga Bandari ya Uvuvi.
136
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Maliasili
77. Visiwa vya Unguja na Pemba vimesheheni utajiri wa
maliasili ambazo ni kivutio kikubwa cha watalii. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya Maliasili
imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Mpango wa Matumizi ya Misitu, Sera ya Misitu
na Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Rasilimali
za Misitu umeandaliwa ili kuimarisha udhibiti na
uhifadhi wa maliasili zikiwemo rasilimali za misitu,
maliasili zisizorejesheka, wanyama pori pamoja
na bayoanuai. Aidha, wananchi wameshirikishwa
kikamilifu katika usimamizi na uhifadhi wa maeneo
tengefu ya Jozani na Ngezi pamoja na misitu ya asili
ya Masingini, Msitu Mkuu na Kiwengwa.
(b) Ushirikishwaji wa wananchi umefanyika katika
utunzaji na uhifadhi wa wanyama adimu walio katika
hatari ya kutoweka hususan Kima Punju, Popo wa
Pemba na Paa Nunga. Maeneo mapya ya hifadhi ya
Kima Punju huko Muyuni na Jambiani yameanzishwa.
Jumla ya mikataba 50 ya usimamizi wa misitu ya jamii
na matumizi endelevu ya maliasili imefikiwa kati ya
Serikali na wananchi. Chini ya mikataba hiyo, kaya
4,500 zimepatiwa majiko ya gesi bila ya malipo; na
(c) Wananchi wamehamasishwa kuanzisha miradi ya
ufugaji wa nyuki ambapo jumla ya mizinga ya kisasa
3,000 imesambazwa kwa wafugaji na kupatiwa fursa
ya soko la ndani na nje ya nchi.
78. Ili kuendeleza zaidi sekta ya maliasili, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaielekeza SMZ
kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Misitu
na Uhifadhi wa Raslimali zisizorejesheka na kutoa
taaluma ya udhibiti wa raslimali hizo kwa jamii;
137
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuimarisha maeneo ya hifadhi na usimamizi wa
wanyama pori walio katika hatari ya kutoweka
wakiwemo Paa Nunga, Kima Punju na Popo wa
Pemba ili kuongeza idadi ya wanyama hao na
kuimarisha utalii wa kimaumbile (eco-tourism);
(c) Kusimamia matumizi endelevu ya rasimali za misitu
ya jamii na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa asali
kutoka tani 5 mwaka 2014, hadi kufikia tani 10 mwaka
2020; na
(d) Kuendeleza kazi ya uatikaji na usambazaji wa miche
ya misitu na kuhamasisha upandaji na utunzaji wa
miti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (katikati)
akijumuika na wananchi wa kikundi cha kuhifadhi Mazingira
Fuoni Kibondeni katika upandaji wa miti ya mikoko ili
kutunza mazingira ya eneo hilo wakati akiwa katika ziara ya
kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya CCM
138
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mazingira na Mabadiliko Tabianchi
79. Mazingira ni suala mtambuka ambalo linagusa sekta
mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Aidha, upo uhusiano
tegemezi kati ya mazingira na maendeleo na kwamba
uharibifu wa mazingira si tu husababisha umasikini,
bali umasikini nao husababisha uharibifu wa mazingira.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, yamepatikana
mafanikio kutokana na utunzaji na uhifadhi wa mazingira
kama ifuatavyo:-
(a) Sera ya Mazingira ya mwaka 1992 imefanyiwa
mapitio na Sera Mpya ya Mwaka 2013 imezinduliwa.
Ili kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa mazingira,
Sheria ya Mazingira ya Mwaka 1996 imefanyiwa
marekebisho na Sheria Mpya ya Mazingira ya Mwaka
2015 pamoja na Kanuni ya Usimamizi wa Maliasili
zisiorejesheka na Kanuni ya Marufuku ya Mifuko ya
Plastiki zimepitishwa;
(b) Jumla ya miradi 221 imefanyiwa ukaguzi wa
kimazingira na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
Miradi mingine 32 ya uwekezaji imefanyiwa tathmini
ya kimazingira na kupatiwa vyeti vya mazingira;
(c) Jumla ya miche 6,020,861 ya misitu na miti ya
matunda imesambazwa na kupandwa katika maeneo
mbalimbali yakiwemo maeneo yaliyoathirika kwa
uchimbaji wa mchanga, uchimbaji wa kifusi na
matofali ya mawe; na
(d) Utafiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi
umefanyika. Maeneo 148 (Unguja 25 na Pemba 123)
yamebainika kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi
kwa kuingiwa na maji ya chumvi kutokana na
kupanda kwa kina cha bahari.
80. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itaielekeza SMZ kuendeleza udhibiti wa hifadhi ya
mazingira kwa kutekeleza yafuatayo:-
139
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuendelea kusimamia Sera na Sheria ya Mazingira na
ushirikishwaji wa jamii katika utunzaji na uhifadhi
wa mazingira kwenye maeneo yao;
(b) Kufanya tathmini za athari za Kimazingira, ukaguzi
wa Kimazingira na ufuatiliaji wa Kimazingira katika
maeneo mbalimbali ya nchi;
(c) Kusimamia mabadiliko ya tabianchi na elimu kwa
wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira;
(d) Kuanzisha vituo viwili vya usarifu wa taka ngumu
(Unguja 1 na Pemba 1) kwa lengo la kuhifadhi
mazingira na kuzalisha ajira kwa vijana; na
(e) Kukamilisha ujenzi wa ukuta katika kingo za barabara
ya Mizingani ili kuzuia athari za mmomonyoko wa
ardhi unaosababishwa na bahari.
Utalii
81. Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye historia na vivutio
mbalimbali vya utalii zikiwemo fukwe za kuvutia, misitu
ya asili, wanyama adimu, magofu na urithi wa kimataifa wa
Mji Mkongwe. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
Sekta ya Utalii imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Sheria ya Kamisheni ya Utalii imefanyiwa marekebisho
na Kanuni za Sheria ya Kamisheni ya Utalii na ile ya
Chuo cha Utalii zimepitishwa na kuanza kutumika.
Chini ya sheria hio mpya (Sheria Na. 7/2012) Kamati
za Utalii za wilaya zimeanzishwa;
(b) Ofisi ya Uwakala wa Utangazaji Utalii nchini India
imeanzishwa na masoko mapya ya utalii ya India,
China, Uturuki na Urusi yameibuliwa. Kutokana na
hatua hizo, watalii 1,863 kutoka India, 2001 kutoka
China na 840 kutoka Uturuki walipokelewa;
(c) Idadi ya watalii walioingia Zanzibar imeongezeka
kutoka 132,836 mwaka 2010 hadi 310,500 mwaka
2014. Kukamilika kwa ujenzi wa chumba cha chini ya
140
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
bahari katika hoteli ya Manta Reef huko Makangale
Pemba ni moja ya kivutio kikubwa cha watalii;
(d) Utafiti wa kiikolojia kwenye Ngome ya Mazrui –
Chwaka na Tumbe (Pemba) na Ngome Kongwe
na Forodhani (Unguja) umefanyika. Maeneo
mapya manane (8) ya kihistoria yakiwemo Kiumbi,
Kiwengwa, Muyuni, Dimani, Mwanampambe, Mwana
wa Mwana, Tazari na kijiji kilichozama Mkumbuu
yameibuliwa. Jengo la Makumbusho ya Hamamni
Baths yamefanyiwa ukarabati ili kulirudisha katika
hali yake ya awali;
(e) Uhakiki wa hoteli na kuzipangia madaraja umefanyika.
Hoteli 71 zilifikia vigezo vilivyowekwa na Jumuiya ya
Afrika Mashariki zikiwemo hoteli za nyota tano 16,
nyota nne tisa, nyota tatu 43 na nyota mbili sita; na
(f) Chuo cha Maendeleo ya Utalii kimeimarishwa. Jumla
ya wahitimu 983 (wanawake 386 na wanaume 597)
wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada
na Stashahada. Walimu sita wamepatiwa mafunzo ya
juu.
141
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Watalii wanaotembelea katika Visiwa vya Zanzibar hupata
fursa za kutembelea maeneo ya Historia na vivutio vya Utalii
ndani ya Zanzibar na vitongoji vyake. Kama wanavyoonekana
Watalii hawa waliofika Zanzibar wakipata historia ya
Nyumba ya Marcury ilioko katika mtaa wa Shangani ndani
ya mji Mkongwe wa Unguja.Wageni wengi wanaotembelea
Zanzibar hufika katika nyumba hii ikiwa katika medali ya
historia ya Zanzibar
82. Ili kuendeleza Sekta ya Utalii na kuifanya iwe endelevu
na kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa
Zanzibar, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-
2020), CCM itaielekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kufanya mapitio ya Sera ya Utalii na kusimamia
utekelezaji wa Sheria na Kanuni zinazohusiana na
sekta hii pamoja na kuandaa mpango wa kukusanya
taarifa na takwimu za idadi ya hoteli na taarifa
nyingine ili kufahamu thamani halisi ya mchango wa
sekta kwenye Pato la Taifa;
(b) Kuendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kuanzisha
miradi ya ujenzi wa hoteli za kitalii hususan hoteli
za daraja la kwanza na kuongeza idadi ya watalii
142
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
wanaoingia Zanziabr kutoka 310,500 mwaka 2014
hadi 500,000 mwaka 2020;
(c) Kuimarisha kikosi maalumu cha ulinzi na
ushirikishwaji wa wananchi kwa kuanzisha vituo
vitatu vya utoaji taarifa zikiwemo za uhalifu ili
kuimarisha usalama wa watalii wanaotembelea
Zanzibar;
(d) Kuendeleza utalii wa kumbukumbu za kihistoria,
kiutamaduni na kimaumbile wenye kutunza
mazingira na kuibua maeneo mapya likiwemo jengo
la “Living Stone House”(Kinazini), jengo la Tip
Tip (Forodhani), jengo la Baraza la Kutunga Sheria
“Legislative Council” (Mnazi Mmoja) na jengo la
Mwinyimkuu (Dunga) ili kuongeza idadi ya watalii
na muda wa kukaa nchini;
(e) Kuendeleza jitihada ya kuvitangaza vivutio vya
utalii kwa kuanzisha Kitengo cha Masoko, Ofisi tatu
za kutangaza utalii, kuanzisha masoko kwa njia
shirikishi na mtandao na kufanya utafiti ili kuibua
masoko mapya hasa katika Bara la Asia na Mashariki
ya Kati;
(f) Kuimarisha bidhaa na huduma za utalii kwa
kuanzisha vituo 10 vya huduma na bidhaa za utalii
zinazotokana na asili ya Mzanzibari sambamba na
utoaji wa huduma kwa watalii katika bustani nane za
kimaumbile zitakazozalisha ajira 1,000;
(g) Kuihamasisha jamii kushiriki katika utalii wa ndani
na kutoa mafunzo kwa vijana 680 ili kuwawezesha
kujiajiri wenyewe kupitia Sekta ya Utalii na
kutengeneza ajira 100,000 za moja kwa moja na zisizo
za moja kwa moja; na
(h) Kukiunganisha Chuo cha Utalii na SUZA ili kutoa
mafunzo ya Shahada ya Utalii.
143
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Viwanda na Biashara
83. Uchumi wa viwanda una nguvu kubwa ya kuziwezesha
sekta nyingine za uchumi kuingia katika mkondo wa uchumi
wa kisasa. Aidha, Sekta ya Biashara ina umuhimu mkubwa
kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa wananchi. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta ya
Viwanda na Biashara imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Sera ya Biashara imefanyiwa mapitio na Sheria Mpya
ya Utoaji Leseni za Biashara na Usajili imepitishwa.
Aidha, sheria ya kusimamia mwenendo wa biashara
na kumlinda mtumiaji, sheria ya mizani na vipimo na
sheria ya biashara zimefanyiwa mapitio;
(b) Miradi 817 ya viwanda na ya wajasiriamali
imekaguliwa na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
Wazalishaji wadogo wadogo 189 (Unguja 119 na
Pemba 70) wamepatiwa mafunzo juu usindikaji
mazao, ujasiriamali, kuongeza thamani ya mazao na
mbinu za kuendeleza biashara zao. Vikundi 500 vya
wajasiriamali vimeweza kushiriki katika maonesho ya
Kikanda na Kimataifa;
(c) Sheria mpya ya Biashara imepitishwa. Chini ya Sheria
hiyo, Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) na Alama
ya Utambulisho (logo) na Alama ya Ubora wa Bidhaa
(Standard Mark) ambayo itaonesha ubora wa bidhaa
hizo pia imeanzishwa ili kusimamia ubora wa bidhaa
zinazozalishwa na kuingizwa nchini na kukuza
masoko ya ndani na nje;
(d) Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kimepatiwa
mwekezaji na kimefanyiwa ukarabati mkubwa pamoja
na kupatiwa mashine mpya na kuimarisha mashamba
ya miwa. Jumla ya wafanyakazi 350 wameajiriwa na
usindikaji wa sukari tayari umeanza;
(e) Kiwanda cha Makonyo huko Pemba kimeimarishwa
kwa kupatiwa mashine mpya ya kupimia ubora wa
mafuta ya mimea (Gas Chromolography) na mashine ya
144
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kuwekea mafuta kwenye ujazo mdogo. Kiwanda pia
kimeingia makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya
Land ya Japan ili kuuza mafuta ya mimea katika soko
la Japan;
(f) Mradi wa Tasnia Chapa (Branding) umeanzishwa ili
kuilinda na kuipa hadhi zaidi karafuu ya Zanzibar
na kuitangaza Zanzibar kupitia bidhaa nyingine za
viungo zikiwemo mdalasini, pilipili hoho na pilipili
manga; na
(g) Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) limefanyiwa
mabadiliko makumbwa ambapo:-
(i) Zao la karafuu halikubinafishwa na mpango wa
kuliendeleza umetayarishwa;
(ii) Magendo ya karafuu yamepungua sana
kutokana na ushirikishwaji wa wananchi; na
(iii) Sheria ya maendeleo ya karafuu na Mfuko wa
Maendeleo ya Karafuu umeanzishwa.
84. Ili kuendeleza shughuli za viwanda na biashara na kuinua
Uchumi wa Zanzibar, katika kipindi cha miaka mitano
ijayo (2015-2020), CCM itaielekeza SMZ kuchukua hatua
zifuatazo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uendelezaji wa
Viwanda Vidogo na vya Kati na kuandaa vivutio kwa
ajili ya uwekezaji wa viwanda vikubwa;
(b) Kuandaa mkakati wa kuendeleza Sekta Binafsi
pamoja na programu ya kuwakuza wawekezaji wa
ndani na wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati
(SME’s) kwa kuwapatia mafunzo, mitaji na huduma
za kiufundi ili kuzalisha bidhaa bora zenye kukabili
ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi;
(c) Kuendeleza viwanda chini ya Maeneo Maalumu ya
Kiuchumi (SEZ) na kuwavutia wawekezaji wenye
mitaji mikubwa kuwekeza katika miundombinu
145
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ya viwanda vinavyozalisha ajira kwa wingi,
vikiwemo viwanda vya kushona nguo, usindikaji
mazao, usindikaji samaki na viwanda vya kusarifu
(kuchakata) mazao ya kilimo na mifugo;
(d) Kufanya mapitio ya Sera ya Biashara ya Mwaka 2006,
kuandaa Sera Mpya ya Biashara na kuanzisha chombo
maalumu cha kuwaendeleza wajasiriamali wadogo
na kufanya utafiti juu ya gharama za biashara kwa
lengo la kuchochea ukuaji wa biashara na kuondosha
urasimu katika utoaji wa leseni;
(e) Kuimarisha utengamano wa kikanda (EAC, SADC,
IOR, ACP) na kuhamasisha matumizi ya fursa za
masoko ya EAC, SADC na AGOA na kuandaa Mkakati
wa Kukuza Mauzo ya Nje (Zanzibar National Export
Strategy);
(f) Kuanzisha na kuendeleza ujenzi wa Kiwanja cha
Maonyesho ya Biashara cha Kimataifa na kuhamasisha
ushiriki wa wajasiriamali wa Zanzibar katika
Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ndani na nje ya
nchi;
(g) Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi,
uchambuzi na usambazaji wa taarifa za masoko na
kufanya utafiti wa masoko na bei ili kupanua wigo wa
mahitaji ya masoko mbalimbali. Aidha, wajasiriamali
watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo na mbinu
za kuweza kuyafikia masoko hayo; na
(h) Kusimamia utekelezaji wa Taasisi ya Viwango
ya Zanzibar (ZBS) na kukamilisha mkakati wa
utambulisho wa karafuu ya Zanzibar na uhamasishaji
matumizi ya tasnia malibunifu (Intellectual Property
Right) ili kuendeleza tija.
146
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Vyama vya Ushirika
85. Vyama vya Ushirika bado vina nafasi muhimu katika
kuwaunganisha na kuwawezesha wananchi kubadili
maisha yao na kujiendeleza kiuchumi. Aidha, Vyama vya
Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) ni nyenzo ya
kuwapatia wananchi mitaji kutokana na michango yao na
mikopo kutoka katika vyombo na taasisi za fedha. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), utekelezaji
wa Sera na Sheria ya Vyama vya Ushirika imefanyika na
kupata mafanikio yafuatayo:-
(a) Vyama vipya vya Ushirika 749 vimesajiliwa zikiwemo
SACCOS 16, na vyama vya uzalishaji mali na huduma
826. Idadi ya vyama vya ushirika imefikia 2,493 vikiwa
na jumla ya wanachama 39,664 Unguja na Pemba;
(b) Vyama vya ushirika 485 vimefanyiwa ukaguzi wa
hesabu na ripoti za ukaguzi huo kuwasilishwa kwenye
Mikutano Mikuu ya vyama hivyo. Aidha, Vyama vya
Ushirika 2,243 vimefanyiwa ukaguzi wa kawaida ili
kutathmini hali ya uendeshaji, utekelezaji wa sheria
na uandishi wa vitabu vya hesabu;
(c) SACCOS 203 zimefanyiwa uthamini na kupangiwa
madaraja ya ubora. Mtaji wa SACCOS hizo
umefikia shilingi bilioni 3.5. Jumla ya SACCOS 17
zimeunganishwa na taasisi mbalimbali za fedha na
kuweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi
bilioni 3 ili kuimarisha mitaji katika biashara zao; na
(d) Jumla ya wanachama 13,953 wakiwemo wanawake
8,923 na wanaume 5,030 wamepatiwa mafunzo ya aina
mbalimbali juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika.
Aidha, Sekta ya Ushirika imeweza kutoa ajira binafsi
6,835 (wanawake 2,948 na wanaume 3,887) kutokana
na Vyama vya Ushirika 88.
86. Ili kuendeleza Sekta ya Ushirika, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaielekeza SMZ
kutekeleza yafuatayo:-
147
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuifanyia mapitio Sera ya Vyama vya Ushirika na
kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya
Ushirika na upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia
kuandaa mipango na kuleta mageuzi katika Sekta ya
Ushirika na kuimarisha uchumi wa Taifa;
(b) Kufanya usajili wa vyama vipya vya ushirika 600 vya
uzalishaji (kilimo, mifugo, viwanda vidogo vidogo,
uvuvi na huduma) pamoja na SACCOS 50 kubwa;
(c) Kuziimarisha SACCOS na Asasi Ndogo za Fedha
kwa kuzipatia mafunzo ya kitaaluma, uongozi na
kuwaongezea mitaji ili ziweze kutekeleza shughuli
zake kwa ufanisi kwa lengo la kuongeza ajira;
(d) Kuwapatia mafunzo ya uongozi na uendeshaji
wanachama 15,000 wakiwemo viongozi 3,000 na
wanachama 12,000 wa vyama vya ushirika na
kuvifanyia ukaguzi vyama 3,000 vya ushirika; na
(e) Kusimamia uanzishaji na kuviimarisha vyama vikuu
vitatu vya kisekta (kilimo na masoko, kazi za mikono
na huduma) ili kujenga sauti ya pamoja na utoaji wa
huduma muhimu za kisekta katika kuendeleza Vyama
vya Ushirika vya Msingi.
Sekta za Miundombinu ya Kiuchumi
87. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta
ya Miundombinu imepata mafanikio yafuatayo:-
Barabara
(a) Jumla ya Kilomita 656 (Unguja Km. 430 na Pemba 226)
za barabara za lami zilizokwishajengwa zimefanyiwa
matengenezo;
(b) Ujenzi wa barabara ya Mfenesini hadi Bumbwini (Km.13) na
barabara ya Welezo hadi Dunga (Km. 12.75) kwa kiwango
cha lami umekamilika. Vile vile, Kilomita 108.9 za barabara
za Pemba zimejengwa kwa kiwango cha lami;
148
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Jumla ya Kilomita 124.7 za barabara za Unguja zimejengwa
kwa viwango mbalimbali. Kilomita 18 zimejengwa kwa
kiwango cha lami Km. 14 kwa kiwango cha changarawe,
Km. 12 ujenzi bado unaendelea na km 80.7 zimefanyiwa
upembuzi yakinifu na ubunifu wa michoro; na
(d) Kwa upande wa Pemba, jumla ya Km. 203.4 za barabara
zimejengwa kwa viwango mbalimbali. Kilomita 103.0
zimejengwa kwa kiwango cha lami, Km. 60.3. kwa kiwango
cha changarawe na Km. 40.1 zimefanyiwa upembuzi
yakinifu pamoja na michoro.
Barabara mpya ya Amani – Mtoni ambayo ilifunguliwa rasmi
na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wakati
wa maadhimisho ya kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
88. Ili kuendeleza kazi ya kuimarisha miundombinu ya
barabara, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-
2020), CCM itahakikisha kuwa SMZ inatekeleza kazi
zifuatazo:-
149
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuendeleza kazi ya utunzaji na matengenezo
ya barabara zilizokwisha kujengwa na kufanya
marekebisho katika maeneo yanayotuama maji ya
mvua na kuathiri ubora wa barabara hizo;
(b) Kukamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa
barabara ya Jendele–Cheju–Kaebona (km 11.7) na
Koani –Jumbi (km 6.3) kwa Unguja na barabara ya Ole
– Kengeja (Km 35), Mkanyageni – Kangani (Km 6.5),
Finya – Kicha (Km 8.8) na Mgagadu - Kiwani (Km 7.6)
kwa Pemba;
(c) Kujenga jumla ya kilomita 160.8 za barabara kwa
kiwango cha lami Unguja na kilomita 51.1 za barabara
kwa kiwango cha lami huko Pemba kwa mpango
ufuatao:-
(i) Unguja
• Matemwe – Muyuni (Km 7.6)
• Kichwele – Pangeni (Km 4.8)
• Kinduni – Kichungwani – Kitope (Km 3.5)
• Umbuji – Uroa (Km 6.9)
• Fuoni – Kombeni (Km 8.6)
• Jozani – Charawe – Ukongoroni – Bwejuu
(Km 23.3)
• Mkwajuni – Kijini (Km 9.4)
• Pale – Kiongole (Km 4.6)
• Malindi Port – Kinazini – Mtoni – Bububu
(Km 11.2)
• Creek road – Mkunazini – Mnazimoja (Km
1.3)
• Tunguu – Fuoni – Magomeni – Kariakoo –
Mkunazini (Km 16.3)
• Welezo – Amani - Ng’ambo (Km 2.9)
• Mtoni – Amani – Kiembesamaki (Km 8.5)
150
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
• Airport – Kiembesamaki – Kilimani -
Mnazimmoja (Km 6.6)
• Bububu – Mahonda – Mkokotoni (Km 31)
• Kizimbani – Kiboje (Km 7.2)
• Melitano - Kwarara (Km 1)
• Kijitoupele – Fuoni – Mambosasa (Km 2.5)
• Sharifumsa – Mwanyanya - Bububu Skuli
(Km 3.6)
(ii) Pemba
• Chake – Wete (Km 22.1)
• Mkoani – Chake (Km 27)
• Mji wa Wete (Km 2)
(d) Kuendeleza kazi ya uwekaji wa taa za kuongoza
magari kwa kuweka taa sita (Unguja nne (4) na Pemba
mbili (2) ili kupunguza msongamano wa magari katika
baadhi ya maeneo ya miji hususan Zanzibar, Wete na
Chake Chake Pemba; na
(e) Kuimarisha Karakana Kuu ya Serikali kwa
mashirikiano na Sekta Binafsi ili kuongeza ufanisi
na utoaji wa huduma bora za kiufundi kwa Taasisi
mbalimbali za Serikali na watu binafsi.
Bandari
89. Bandari ni mlango mkuu wa biashara na chachu ya ukuaji
wa uchumi wa Taifa na wananchi kwa jumla. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), mafanikio
yaliyofikiwa kwenye eneo la bandari ni kama ifuatavyo:-
(a) Shirika la Bandari kwa kushirikiana na Kampuni ya
AZAM MARINE limejenga majengo ya kuhudumia
abiria likiwemo jengo la Watu Mashuhuri (VIP) katika
Bandari ya Malindi, pamoja na kuimarisha huduma
nyingine za abiria;
151
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Eneo la kuhifadhia makontena lenye ukubwa wa
kilomita za mraba 6,000 katika Bandari ya Malindi
limefanyiwa matengenezo ili kuongeza ufanisi. Aidha,
vifaa na mitambo mipya ya kisasa imenunuliwa;
(c) Matengenezo makubwa yamefanyika katika gati
ya Mkoani Pemba. Kiungo cha gati hiyo ambacho
kiliathirika kutokana na nguvu za mawimbi ya meli
pia kimefanyiwa matengenezo;
(d) Ili kuimarisha gati ndogo ya Mkokotoni, kazi ya
uchunguzi wa athari za kimazingira imekamilika.
Aidha, mpango wa ujenzi wa gati hiyo tayari
umeandaliwa; na
(e) Kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa
Bandari mpya ya Mpigaduri imekamilika. Mjenzi wa
Bandari hiyo, Kampuni ya China (Harbour Engineering
Company) ameteuliwa na fedha kwa ajili ya ujenzi huo
tayari zimepatikana.
90. Ili kuendeleza na kuimarisha bandari katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha
kwamba, SMZ inatekeleza kazi zifuatazo:-
(a) Kukamilisha ujenzi wa bandari mpya ya kuhudumia
mizigo katika eneo la Mpigaduri na kuiendeleza
Bandari ya Malindi kwa kuongeza vifaa vya huduma
kwa abiria pamoja na mizigo;
(b) Kuimarisha na kuendeleza Bandari ya Mkoani-Pemba
kwa kuipatia vifaa vya kisasa vya kuhudumia abiria
na mizigo. Aidha, kwa kushirikiana na Sekta Binafsi,
gati ya Wete itaimarishwa;
(c) Kuimarisha gati ya Mkokotoni kwa kukamilisha kazi
ya ujenzi wa jeti kwa ajili ya huduma za usafiri wa
wananchi wa Tumbatu na usafirishaji wa mizigo kwa
majahazi; na
152
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kuliimarisha Shirika la Meli ili lijiendeshe kibiashara
na kununua meli nyingine mpya ya abiria na moja ya
mafuta.
Usafiri wa Baharini
91. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Sheria ya kuanzisha Shirika la Meli la Zanzibar
imefanyiwa mapitio na sheria mpya imepitishwa.
Mpango wa mageuzi ya kimuundo na uendeshaji
umeanza kutekelezwa. Jumla ya meli mbili za Shirika
hilo; M V. Maendeleo na M V.Ukombozi zimefanyiwa
matengenezo makubwa;
(b) Serikali imenunua meli mpya ya abiria na mizigo yenye
uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo ili
kuimarisha huduma za usafiri kwa wananchi hususan
kati ya Kisiwa cha Unguja na Pemba;
(c) Ofisi ya Mrajisi wa Meli na Mamlaka ya Usafiri
wa Baharini “Zanzibar Maritime Authority” (ZMA)
imeimarishwa. Kwa kushirikiana na SUMATRA na
mamlaka hiyo imeweza kufanya ukaguzi wa mara
kwa mara wa vyombo vya baharini na kupunguza
kwa kiasi kikubwa ajali za mara kwa mara za vyombo
vya baharini; na
(d) Wawekezaji wa ndani na nje wameendelea
kushajiishwa ili kuwekeza katika sekta ya usafiri wa
baharini. Jumla ya kampuni 23 tayari zimewekeza
katika sekta ya usafiri wa baharini.
92. Ili kuendeleza na kuimarisha usafiri wa baharini, katika
kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itahakikisha
kwamba, SMZ inaendelea kusimamia Utekelezaji wa
Sheria na Kanuni za usafiri wa baharini ili kupunguza
ajali za vyombo vya baharini kwa kuimarisha utendaji wa
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (ZMA).
153
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Usafiri wa Anga
93. Uimara wa Sekta ya Usafiri wa Anga huchangia kwa kiasi
kikubwa ukuaji wa Sekta ya Utalii, biashara na kukuza
uchumi wa nchi. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
(2010-2015), yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Ujenzi wa jengo jipya na eneo la maegesho ya ndege
umeanzishwa ili kukiimarisha Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Abeid Amani Karume. Kazi ya ujenzi
wa maegesho na njia za kurukia ndege umekamilika;
(b) Ujenzi wa uzio wenye urefu wa kilomita 8.59
unaozunguka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Abeid Amani Karume umekamilika; na
(c) Hali ya usalama katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Abeid Amani Karume imeimarishwa.
Vifaa vya ukaguzi vikiwemo“walk through doors, x
- ray machine, hand held metal na under search mirrors”
vimenunuliwa. Pia wafanyakazi wa kada mbalimbali
wamepatiwa mafunzo yanayohusiana na kazi zao.
94. Ili kuiendeleza Sekta ya Usafiri wa Anga katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015-2020) CCM itahakikisha
kwamba, SMZ inatekeleza kazi zifuatazo:-
(a) Kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria katika
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani
Karume (AAKIA) ili kuongeza idadi ya abiria
wanaotumia kiwanja hicho, kiwango cha mizigo na
kuongeza mapato ya Serikali;
(b) Kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za
abiria, ndege na mizigo katika Kiwanja cha Ndege cha
Karume-Pemba ikiwemo kuongeza urefu na uwekaji
wa taa katika barabara ya kurukia na kutulia ndege,
huduma za umeme na kukamilisha ujenzi wa uzio; na
(c) Kuendelea kuwapatia mafunzo na vifaa vya kisasa
wafanyakazi wa viwanja vya ndege vya Unguja na
154
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Pemba pamoja na kuimarisha huduma za zimamoto
na usalama wa viwanja vya ndege.
Nishati
95. Sekta ya Nishati hususan umeme, ni nyenzo muhimu katika
kukuza uchumi na maendeleo ya jamii. Aidha, matumizi ya
nishati ya umeme hurahisisha shughuli nyingi za kiuchumi,
kuongeza kasi ya uzalishajimali na kuwawezesha wananchi
kujiajiri wao wenyewe. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Sera ya Nishati imeanzishwa na Mpango Mkakati wa
utekelezaji wa Sera hiyo umeandaliwa. Aidha, Sheria
ya Udhibsiti wa huduma za Maji na Nishati (ZURA)
imepitishwa;
(b) Mradi wa ujenzi wa njia ya pili ya umeme inayopita
chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni-Tanzania Bara
hadi Fumba-Unguja (Mradi wa MCC) umekamilika
na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme
kutoka Megawati 45 hadi kufikia Megawati 145 kwa
Unguja;
(c) Kazi ya ujenzi wa njia ya umeme ya megawati 20
inayopita chini ya bahari kutoka Tanga hadi Pemba
(Mradi wa NORAD) imetekelezwa na kumaliza kabisa
tatizo la umeme katika kisiwa hicho;
(d) Njia kubwa ya Umeme yenye urefu wa kilomita 5.2
imejengwa katika vijiji vya Kibonde Maji na Pongwe
kwa Unguja na Kivugo na Kichuwani kwa Pemba.
Aidha, vijiji 129 vimefikishiwa huduma ya umeme
Unguja na Pemba sawa na asilimia 105 ya lengo
lililowekwa (vijiji 123);
(e) Vyanzo vya nishati mbadala ya umeme ukiwemo
umeme wa jua, mawimbi ya bahari, upepo na gesi
asilia vimefanyiwa uhakiki. Kampuni kutoka Italia
imeteuliwa kuanza utafiti katika maeneo hayo; na
155
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(f) Vijana 32 wanaendelea kupatiwa mafunzo katika vyuo
mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuwatayarisha kwa
ajili ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi asilia.
96. Ili kuimarisha Sekta ya Nishati ambayo inajumuisha
umeme, nishati mbadala, mafuta na gesi asilia katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), SMZ chini ya
uongozi wa CCM itatekeleza kazi zifuatazo:-
(a) Umeme na nishati mbadala:
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya
Nishati ya Mwaka 2009 na kuendeleza juhudi za
upatikanaji wa umeme na nishati mbadala;
(ii) Kuimarisha shughuli za usimamizi wa huduma
za umeme na usambazaji wa nishati hiyo mijini
na vijijini vikiwemo visiwa vidogo vidogo
vinavyoishi watu; na
(iii) Kuimarisha Shirika la Umeme Zanzibar
(ZECO) kwa lengo la kuliwezesha kujiendesha
kibiashara.
(b) Mafuta na Gesi Asilia:
(i) Kuandaa Sera na Sheria ya Mafuta na Gesi
Asilia;
(ii) Kuendeleza jitihada za kuwajengea uwezo
watendaji pamoja na kuhamasisha vijana
kujiunga na masomo ya fani ya Mafuta na Gesi
Asilia; na
(iii) Kuandaa mpango shirikishi utakaohakikisha
kwamba wananchi wananufaika na kupata fursa
za kiuchumi na kijamii kutokana na shughuli za
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.
156
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Ardhi
97. Ardhi ni raslimali muhimu katika ujenzi wa uchumi wa
Taifa. Aidha, moja ya malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar
ya tarehe 12 Januari 1964, ni kuondoa umiliki wa ardhi
mikononi mwa wachache na kuhakikisha kwamba ardhi
yote ya Zanzibar inamilikiwa na wananchi wenyewe na
kuwawezesha kuondokana na umasikini, dhuluma na
ubaguzi wa kitabaka. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010-2015), mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Sera Mpya ya Ardhi imeandaliwa na utoaji wa Hati
Mpya za Matumizi ya Ardhi na kuzibadilisha zile
za zamani imetekelezwa katika Shehia 20 Unguja na
Pemba;
(b) Jumla ya maeneo 3,541 katika Shehia 22 za Unguja
na Pemba yamesajiliwa na Mrajis wa Ardhi.
Vile vile, nyumba, viwanja na mashamba 22,746
yametambuliwa Unguja na Pemba. Hati Mpya za
Ardhi 1,310 na viwanja 1,691 zimetolewa kwa ajili
ya matumizi mbalimbali na mikataba 223 ya ardhi
imetolewa kwa wawekezaji;
(c) Mapitio na utayarishaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa
wa Matumizi Bora ya Ardhi (National Land Use Plan)
na utayarishaji wa Mpango Kabambe (Master Plan)
ya Mji wa Zanzibar imetekelezwa;
(d) Kazi ya kufanya mapitio na marekebisho ya ramani ya
Zanzibar pamoja na miji ya Zanzibar, Chake Chake,
Wete na Mkoani pamoja na visiwa vidogo vidogo
imetekelezwa. Ramani mpya ya Kisiwa cha Unguja na
Pemba tayari zimechapishwa na kuanza kutumika;
(e) Kazi ya utambuzi wa umiliki wa ardhi katika maeneo
ya ukanda wa pwani na fukwe imetekelezwa. Jumla
ya wamiliki 1,600 wametambuliwa katika Kijiji cha
Nungwi na 1,000 katika Kijiji cha Paje. Maeneo ya
Chwaka kwa Unguja na Michenzani kwa Pemba
pia yamepimwa. Kazi ya utambuzi wa umiliki wa
157
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ardhi katika maeneo ya miji kwa majaribio (Pilot) pia
imefanyika. Jumla ya wamiliki 6,000 wametambuliwa
na kusajiliwa; na
(f) Idadi ya Mahakimu katika Mahakama za Ardhi
imeongezeka kutoka watatu (3) hadi sita (6) na
Washauri (Assessors) kutoka 19 hadi 27. Hatua hiyo
imeongeza ufanisi na kasi ya kusikiliza mashauri
yanayohusiana na migogoro ya ardhi na kuyatolea
uamuzi. Mahakama ya Ardhi ya Mkoa wa Kaskazini
Unguja na Kusini Pemba pia zimeanzishwa.
98. Ili kuendeleza Sekta ya Ardhi, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha kuwa, SMZ
inatekeleza malengo yafuatayo:
(a) Kuendeleza kazi ya Usajili wa Ardhi katika maeneo
yote ya Unguja na Pemba kwa mujibu wa Sera na
Sheria ya Ardhi. Aidha, ramani zote za visiwa vya
Unguja na Pemba zitaendelea kufanyiwa mapitio na
marekebisho kwa mujibu wa mahitaji na mabadiliko
yatakayojitokeza;
(b) Kuendeleza kazi ya upimaji wa viwanja na utoaji wa
Hati kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kiuchumi
na kijamii kwa kuzingatia Mpango wa Kitaifa wa
Matumizi Bora ya Ardhi (National Land Use Plan)
pamoja na ramani ya mji na za miji; na
(c) Kuendeleza jitihada za kupunguza migogoro ya
ardhi kwa kuimarisha huduma za Mahakama za
Ardhi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba. Aidha,
jamii itaelimishwa juu ya umuhimu wa kutambua
na kufuata Sheria mbalimbali za ardhi ikiwemo
utambuzi, upimaji na usajili.
158
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Sekta za Huduma za Jamii
Elimu
99. Elimu ni moja ya haki ya msingi kwa kila mwananchi na
nyenzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta
ya Elimu imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Elimu ya Maandalizi:
(i) Idadi ya Skuli za Maandalizi zimeongezeka
kutoka 238 mwaka 2010 hadi 279 mwaka 2015.
Ujenzi wa Skuli za Maandalizi za Tunduni,
Kama, Potoa, Jongowe na Konde umekamilika
na skuli ya maandalizi ya Machomane-Pemba
imefanyiwa ukarabati mkubwa; na
(ii) Idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 29,732
(15,216 wasichana na 14,516 wavulana) mwaka
2010 hadi 38,808 (19,654 wasichana na 19,154
wavulana) mwaka 2015. Idadi ya walimu 382
wamepatiwa mafunzo ya kusomesha ngazi ya
Elimu ya Maandalizi.
(b) Elimu ya Msingi:
(i) Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwanakwerekwe
umekamilika. Idadi ya skuli imeongezeka
kutoka 299 mwaka 2010 hadi 359 mwaka 2015.
Madarasa mapya 563 yamejengwa, madawati
7,955, viti 2,371 na meza 2,329 zimechongwa na
kusambazwa katika madarasa hayo Unguja na
Pemba;
(ii) Idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa
la kwanza imeongezeka kutoka 38,743 (19,163
wasichana na 19,580 wavulana) mwaka 2010
na kufikia 43,062 (21,129 wasichana na 21,933
wavulana) mwaka 2015. Walimu wa ngazi ya
cheti 949 wameajiriwa na kupelekwa katika
skuli za msingi Unguja na Pemba;
159
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Mazingira ya skuli za msingi yameimarishwa
kwa kukarabatiwa na kujengwa njia rafiki ili
kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kuingia
madarasani kwa urahisi. Jumla ya wanafunzi
203 wenye mahitaji maalumu wameandikishwa
na kuanza Elimu ya Msingi; na
(iv) Jumla ya skuli 248 za msingi zimepatiwa
kompyuta mbili kila moja kwa ajili ya kuhifadhi
kumbukumbu na skuli 20 zimepatiwa maabara
za kuhamishika (mobile lab) na pia skuli 25
zimepatiwa vifaa vya kuunganisha mawasiliano
(bridge IT) Unguja na Pemba.
(c) Elimu ya Sekondari:
(i) Idadi ya wanafunzi wa Sekondari (kidato
cha 1-4) imeongezeka kutoka 78,165 (41,804
wasichana na 36,361 wavulana) mwaka 2012
hadi 79,662 (43,544 wasichana 36,118 wavulana)
mwaka 2014;
(ii) Idadi ya Skuli za Sekondari imeongezeka
kutoka 194 mwaka 2010 hadi 213 mwaka 2014.
Skuli mpya 19 zimejengwa na madarasa mapya
263 yamejengwa katika skuli mbalimbali za
Sekondari Unguja na Pemba;
(iii) Skuli kongwe 6 za Sekondari zimefanyiwa
ukarabati mkubwa. Skuli hizo ni Hamamni,
Forodhani na Tumekuja kwa Unguja na Utaani,
Fidel-Casro na Uweleni kwa Pemba. Ujenzi wa
ghorofa ya pili ya Skuli ya Sekondari ya Donge
unaendelea. Aidha, nyumba za walimu 27
zimejengwa katika skuli mbalimbali Unguja na
Pemba; na
(iv) Jumla ya walimu 10 wamepatiwa mafunzo nje
ya nchi, 450 wamepatiwa mafunzo ya kuinua
uwezo wao wa kufundisha masomo ya Hisabati
160
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na Sayansi na wafanyakazi wa kada nyingine
za elimu 2,867 wameendelezwa kwa kupatiwa
mafunzo katika vyuo mbalimbali katika ngazi
ya cheti, stashahada, shahada ya uzamili na
uzamivu.
Jengo la Skuli ya Secondary ya Faraja lililofunguliwa na
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi
Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra
shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
(d) Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima:
(i) Kituo cha Elimu Mbadala cha Rahaleo
kimeendelea kutoa mafunzo katika fani
tofauti. Idadi ya wanafunzi katika kituo hicho
imeongezeka kutoka 246 (wanawake 67 na
wanaume 179) mwaka 2011 hadi 305 (wanawake
73 na wanaume 232) mwaka 2015; na
(ii) Jumla ya vikundi vya kiuchumi 250 na
wajasiriamali 6,000 wamepatiwa mafunzo ya
ujasiriamali kupitia madarasa ya Elimu ya Watu
Wazima, Unguja na Pemba.
161
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Kuimarisha Huduma za Maktaba:
(i) Ujenzi wa Maktaba Kuu ya Zanzibar
umekamilika. Zabuni ya ujenzi wa Maktaba
Kuu, Tawi la Pemba, pia imetangazwa na Shirika
la Huduma za Maktaba limeanzishwa; na
(ii) Jumla ya maktaba nane (8) za jamii
zimeanzishwa katika maeneo ya Chumbuni,
Welezo, Kiembesamaki, Mpapa, Uzini,
Fumba, Bweleo na Tumbatu kwa upande wa
Unguja kwa mashirikiano na jumuiya isiyo
ya kiserikali (MJUKIZA). Aidha, wananchi
wamehamasishwa kuanzisha Maktaba za Jamii
katika maeneo wanayoishi.
(f) Vyuo vya Elimu ya Juu:
(i) Idadi ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha
Taifa (SUZA), Zanzibar University (ZU) na
Univesity Collage of Education Zanzibar
(UCEZ) imeongezeka kutoka 3,624 mwaka 2010
hadi 6,038 mwaka 2014. Ongezeko hilo ni sawa
na asilimia 67;
(ii) Ujenzi wa Chuo Kikuu cha SUZA huko Tunguu
umekamilika. Majengo mapya manne (4)
yamejengwa na kuwekewa samani, kompyuta
na vifaa vya maabara. Idadi ya wanafunzi
waliodahiliwa imeongezeka kutoka 1,972
(wanawake 853 na wanaume 1119) mwaka 2010
hadi 2,078 (wanawake 1,244 na wanaume 834)
mwaka 2015. Wahitimu wa fani mbalimbali
nao wameongezeka kutoka 524 (wanawake 347
na wanaume 177) mwaka 2010 hadi 749 (418
wanawake na wanaume 331) mwaka 2015; na
(iii) Idadi ya wanafunzi wanaodhaminiwa na Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu imeongezeka kutoka
1,022 (wanawake 534 na wanaume 488) mwaka
162
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
2010 hadi 2,658 (wanawake 1,372 na wanaume
1,286) mwaka 2015.
(g) Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu:
(i) Ujenzi wa Chuo cha Ualimu cha Benjamin
William Mkapa, kilichopo Mchangamdogo,
Wete Pemba umekamilika. Mafunzo ya ualimu
yametolewa katika Chuo cha Kiislamu Mazizini
Unguja, Chuo cha Kiislamu Kiuyu na Chuo cha
Benjamin William Mkapa huko Pemba;
(ii) Jumla ya walimu 4,031 wamemaliza mafunzo
kati yao 238 wamemaliza mafunzo ya ngazi ya
Cheti cha Elimu Jumuisho, 951 wamemaliza
ngazi ya Stashahada ya Elimu ya Sekondari,
1,823 wamemaliza ngazi ya stashahada ya
Elimu ya Msingi na walimu 1,019 wamemaliza
Mafunzo ya Ualimu wa Dini na Kiarabu;
(iii) Chuo Kikuu cha SUZA kimeanzisha Diploma
ya Sayansi ya Ualimu yenye wanafunzi 102
na Diploma ya Uongozi yenye wanafunzi 100.
Aidha, hatua za awali za kutayarisha mtaala wa
ualimu Cheti ngazi ya Maandalizi zimeanza;
(iv) Kitivo cha Tiba (Faculty of Medicine)
kimeanzishwa na sasa wanafunzi 66 wa mwaka
wa kwanza na wa pili wanendelea na masomo;
(v) Jumla ya walimu 2,481 wamepatiwa mafunzo
ya ualimu kwa njia ya Elimu Masafa kwa
kupitia Vituo vya Walimu (TCs) na kuweza
kupandishwa daraja na kukidhi vigezo vya
kufundisha ngazi ya Elimu ya Msingi; na
(vi) Mradi maalumu umeanzishwa ili kuendeleza
mafunzo ya walimu wa sayansi na hisabati.
Programu ya Maendeleo ya Walimu (Teachers
Advancement Programme - TAP) imeanzishwa na
kufanikiwa kutoa mafunzo kwa walimu Unguja
163
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
na Pemba. Pia vituo vya ualimu vya Dunga
na Kiembesamaki vimepatiwa kompyuta kwa
ajili ya kurahisisha uwekaji wa kumbukumbu
kupitia mradi huu.
(h) Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali:
(i) Ujenzi wa Vituo vya Elimu ya Amali
vya Mkokotoni-Unguja na Vitongoji-
Pemba umekamilika. Mafunzo ya Amali
yametolewa katika Kituo cha Mkokotoni na
Mwanakwerekwe-Unguja na Vitongoji-Pemba.
Jumla ya wanafunzi 3,130 (936 wanawake na
2,194 wanaume) wamepatiwa mafunzo ya
Elimu ya Amali katika vyuo hivyo;
(ii) Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume,
ambayo hutoa mafunzo ya fani mbalimbali
za ufundi imeimarishwa. Ukarabati wa
miundombinu ya maji na umeme pamoja na
karakana ya uhunzi umefanyika. Idadi ya
wanafunzi katika Taasisi hiyo imeongezeka
kutoka 237 (wanawake 55 na wanaume 182)
mwaka 2010 hadi 1,308 (wanawake 250 na
wanaume 1,058) mwaka 2015; na
(iii) Ujenzi wa madarasa manne (4) katika Skuli
ya Ufundi ya Kengeja-Pemba umekamilika
na kupatiwa huduma ya umeme na vifaa vya
kisasa vya kufundishia pamoja na karakana.
100. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020),
SMZ chini ya uongozi wa CCM itaendeleza jitihada za
kusimamia ukaguzi ili kuendeleza ubora wa elimu katika
ngazi zote pamoja na kutekeleza yafuatayo:-
(a) Elimu ya Maandalizi
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Makuzi na
Malezi ya Mtoto na kuongeza kiwango cha
164
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
uandikishaji kutoka asilimia 31 Mwaka 2014
hadi kufikia asilimia 50 mwaka 2020;
(ii) Kuwahamasisha wananchi na Sekta Binafsi
kuongeza idadi ya madarasa pamoja na kujenga
skuli za Maandalizi hususan katika maeneo ya
vijijini; na
(iii) Kuimarisha mazingira rafiki ya skuli kwa mtoto
kujifunza kwa kutekeleza Programu ya Lishe
katika skuli 40 za Maandalizi na kuanzisha
vituo 150 vya Tucheze Tujifunze katika Wilaya
ya Kaskazini “A” na Kaskazini “B” Unguja na
Micheweni na Mkoani-Pemba.
(b) Elimu ya Msingi
(i) Kuongeza kiwango halisi cha uandikishaji
wanafunzi kutoka asilimia 83.7 mwaka 2013
hadi kufikia asilimia 100 mwaka 2020;
(ii) Kujenga Skuli za Msingi 10 za ghorofa (Unguja 6
na Pemba 4) katika maeneo yenye upungufu na
msongamano mkubwa wa wanafunzi;
(iii) Kuimarisha Programu ya Lishe katika Skuli za
Msingi zilizo katika mazingira magumu; na
(iv) Kutekeleza lengo la kutoa elimu bila malipo
katika elimu ya msingi kwa kutowachangisha
wazee michango yoyote.
(c) Elimu ya Sekondari
(i) Kuongeza kiwango cha uandikishaji kutoka
asilimia 60 mwaka 2014 hadi asilimia 80 mwaka
2020;
(ii) Kukamilisha ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya
Kibuteni na Donge Unguja; na Mkanyageni,
Pemba. Aidha, mabweni (dakhalia) ya kulala
wanafunzi katika skuli zilizo mbali na makaazi ya
165
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
wananchi hususan Skuli ya Sekondari ya Mtule,
Matemwe na Chwaka-Tumbe yatajengwa;
(iii) Kukamilisha ujenzi wa skuli 20 na ujenzi wa
madarasa 500 na kuimarisha Elimu ya Sayansi
na Hisabati kwa wanafunzi wa Sekondari; na
(iv) Kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) na ufundishaji wa somo la kompyuta
katika Skuli zote za Sekondari sambamba na
kuzipatia idadi ya kompyuta za kutosha.
(d) Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali
(i) Kukamilisha ujenzi wa Makao Makuu ya
Mamlaka ya Mafunzo ya Amali na kujenga
Kituo cha Mafunzo ya Amali huko Makunduchi
Unguja na Daya Mtambwe-Pemba;
(ii) Kuviimarisha vituo vya Mafunzo ya Amali
kwa kuvipatia vifaa vya kisasa ili viweze kutoa
mafunzo kwa njia ya vitendo na nadharia ikiwa
pamoja na kuimarisha mitaala ya mafunzo
kwa kuanzisha fani zinazoendana na mahitaji
ya soko la ajira ili kuwawezesha vijana wengi
zaidi kujiajiri hususan Sekta ya Utalii, Uvuvi na
Kilimo; na
(iii) Kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la madarasa
katika Taasisi ya Sayansi ya Karume ili kuongeza
idadi ya vijana wanaojiunga na Taasisi hiyo na
kupatiwa stadi mbalimbali za maisha.
(e) Mafunzo ya Ualimu
(i) Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya ualimu kazini
na vyuoni kwa ngazi ya Cheti na Diploma kwa
walimu 5,000 ifikapo mwaka 2020;
(ii) Kuviimarisha Vituo vya Walimu (TCs) vilivyopo
sasa kwa kuvipatia vifaa vya kujifunzia,
166
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kufundishia na TEHAMA; na kuendeleza
mashirikiano kati ya vituo hivyo na taasisi
mbalimbali zinazotoa mafunzo ya ualimu; na
(iii) Kutoa motisha kwa walimu wanaofanya kazi,
kuhamasisha walimu kujiendeleza kielimu kwa
kuwapatia ruzuku za masomo na kuwapandisha
daraja kazini.
(f) Elimu ya Juu
(i) Kuanzisha Awamu ya Pili ya ujenzi wa Chuo
Kikuu cha Taifa (SUZA); kujenga Chuo Kikuu
kipya katika eneo la Dole; na kuimarisha
mashirikiano na Vyuo Vikuu mbali mbali vya
ndani na nje ya nchi na kutoa fursa za masomo
ya Elimu ya Juu nje ya Zanzibar;
(ii) Kuongeza nafasi za masomo katika Elimu ya
Juu na kuimarisha Mfuko wa Bodi ya Mikopo ili
kuongeza idadi ya wanafunzi watakaonufaika
kutoka 2,658 mwaka 2015 hadi kufikia 22,404
mwaka 2020; na
(iii) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike
wanaojiunga na Elimu ya Juu hususan katika
fani za sayansi, ufundi, udaktari na teknolojia.
(g) Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima
(i) Kuendeleza jitihada za kuhamasisha vijana
kujiunga na madarasa ya Elimu Mbadala ili
kuwawezesha kujiajiri; na
(ii) Kuimarisha utoaji wa Elimu Endelevu kwa watu
wazima na kuongeza idadi ya watu wanaojua
kusoma, kuandika na kuhesabu kutoka asilimia
85.7 na kufikia asilimia 90 mwaka 2020.
167
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(h) Elimu Mjumuisho
(i) Kukamilisha Sera ya Elimu Mjumuisho na
kuimarisha miundombinu na mazingira ya
skuli ili kukidhi mahitaji ya utoaji wa Elimu
Mjumuisho na stadi za maisha; na
(ii) Kuimarisha uwezo wa walimu wa Elimu
Mjumuisho kwa kuwapatia mafunzo jumla ya
walimu 500 na kuandaa Kamusi ya Lugha ya
Alama.
(i) Michezo na Utamaduni katika Skuli
Kufufua na kuendeleza Michezo na Utamaduni
kwa wanafunzi wa skuli za Msingi na Sekondari na
kuanzisha somo la michezo katika Skuli teule sita za
Sekondari nne (4) Unguja na Pemba mbili (2).
(j) Uhifadhi wa Kumbukumbu za Kihistoria na
Mambo ya Kale
(i) Kuendeleza utekelezaji wa Mpango wa Uhifadhi
wa Mambo ya Kale na kuanzisha Taasisi ya
Nyaraka na Kumbukumbu za Kale pamoja na
vituo vya kuhifadhia kumbukumbu katika kila
Mkoa; na
(ii) Kusimamia uendeshaji, utunzaji na matengenezo
ya Makumbusho ya Mnazi Mmoja, Beit-Ajab,
Kasri ya Forodhani, Jengo la Kale la Mtoni pamoja
na kuendeleza ukusanyaji wa kumbukumbu
na nyaraka za Serikali kutoka katika taasisi
mbalimbali za Serikali na kuzihifadhi katika
mfumo wa komputa.
(k) Nyumba za Walimu
Kujenga jumla ya nyumba 40 za Walimu, Unguja (24)
na Pemba (16) na kukamilisha nyumba zote ambazo
ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
168
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(l) Huduma za Maktaba
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maktaba
ya Zanzibar na kukamilisha ujenzi wa jengo
la Maktaba Kuu Pemba, kuanzisha Maktaba
za Jamii katika maeneo wanayoishi pamoja na
kuendeleza uhamasishaji wa wananchi kupenda
kutumia maktaba; na
(ii) Kuendeleza mafunzo ya Ukutubi na kuongeza
idadi ya vitabu katika maktaba zote.
Afya
101. Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa wananchi, CCM
imeendelea kusimamia Utekelezaji wa lengo la kufikisha
huduma za afya karibu na wananchi wote mijini na vijijini.
Huduma za afya zinapatikana katika kila sehemu isiyozidi
kilomiti 5 Unguja na Pemba. Aidha, katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta ya Afya imepata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Utekelezaji wa Sera ya Afya:
Sera ya Afya ya mwaka 1999 imefanyiwa mapitio na
Sera mpya ya mwaka 2011 imeandaliwa na kuanza
kutumika. Aidha, Sheria ya Afya ya Jamii na Sheria
ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepitishwa. Chini ya
sheria hii, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
imeimarishwa na kupewa nguvu za kisheria.
(b) Kuimarisha Huduma za Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja:
Ili kufikia lengo la kuifanya Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja kuwa Hospitali ya Rufaa, hatua
mbalimbali za kuimarisha huduma katika Hospitali
hiyo zimetekelezwa kama ifuatavyo:-
(i) Idadi ya madaktari (MD) imeongezeka hadi
kufikia 82 wakiwemo madaktari bingwa sita.
169
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mashine ya uchunguzi wa moyo (ECG na
Echocardiography) imenunuliwa na daktari
bingwa mzalendo wa maradhi ya moyo
amepatikana;
(ii) Kwa mashirikiano na taasisi ya Maendeleo ya
Elimu ya Upasuaji wa Ubongo (Neurosurgical
Education and Development) ya Spain, jengo jipya
la Kitengo cha Upasuaji wa Uti wa Mgongo
(Neorosurgical Unit) limejengwa pamoja na
ununuzi wa vifaa vipya vya upasuaji wa
mgongo na vichwa maji. Aidha, tiba kwa njia
ya mawasiliano ya mtandao (telemedicine)
imeanzishwa;
(iii) Idara zote muhimu za maabara (microbiology,
parasitology, aematology, biochemistry,
histopathology and blood trasfusion) zimefanyiwa
matengenezo makubwa na kufikia kiwango
cha utendaji kinacholingana na maabara
nyingine za Afrika Mashariki. Jumla ya vipimo
67 vinafanyika ikilinganishwa na vipimo 30 vya
hapo awali;
(iv) Huduma ya uchunguzi wa maradhi ya Kifua
Kikuu kwa kutumia mashine ya kisasa (Gene
expert) yenye uwezo mkubwa wa kugundua
vimelea vya maradhi hayo kwa haraka zimeanza
kutolewa;
(v) Sehemu ya matibabu ya meno na macho
zimeimarishwa na kuweka vifaa vipya vya
matibabu;
(vi) Ukarabati mkubwa umefanyika katika Kitengo
cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Chumba cha
Upasuaji (theatre) na Wodi ya Wazazi pamoja na
kuwekewa vifaa vya kisasa; na
170
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(vii) Ujenzi wa ghala jipya la kuhifadhia dawa
(Bohari Kuu ya Dawa) huko Maruhubi na Kituo
cha Damu Salama huko Sebleni umekamilika.
(c) Hospitali ya Kivunge:
Jumla ya nyumba 12 za wafanyakazi zimejengwa,
Chumba cha Upasuaji, Wodi za Watoto na Sehemu
ya Wagonjwa wa Nje (OPD) zimejengwa. Aidha,
mashine za upasuaji na mashine ya mionzi (Utra
Sound) zimenunuliwa na Kitengo cha Huduma za
Dharura kimeanzishwa.
(d) Hospitali ya Wete:
Ili kuipandisha hadhi Hospitali ya Wete kuwa
Hospitali ya Mkoa, maabara mpya, wodi ya akina
mama na sehemu ya kuhifadhia maiti zimejengwa.
Aidha, wodi ya wanaume, kliniki ya watoto, vyoo
na ghala ya kuhifadhia dawa zimefanyiwa ukarabati
mkubwa na mashine ya mionzi (Utra Sound) pamoja
na mashine ya kupimia moyo zimenunuliwa.
(e) Hospitali ya Mkoani:
Ili kuipandisha daraja Hospitali ya Abdalla Mzee-
Mkoani na kuwa Hospitali ya Mkoa, mpango wa
kuijenga upya hospitali hiyo umeandaliwa. Katika
kutekeleza mpango huo, malipo ya fidia kwa wananchi
wote waliyobomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi
wa majengo mapya tayari yamefanyika na kazi ya
ujenzi wa hospitali hiyo unaendelea.
(f) Hospitali ya Micheweni:
Kazi ya utanuzi na matengenezo ya majengo ikiwemo
Wodi ya Wazazi, Chumba cha Upasuaji na Chumba
cha Maabara mpya ya kisasa umekamilika. Aidha,
ujenzi wa Chumba cha Upasuaji unaendelea.
171
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Kuimarisha Huduma za Kinga na Tiba:
(i) Uwiano wa daktari kwa kutoa huduma
kwa wananchi sasa umefikia daktari mmoja
anahudumia watu 9,093 (1:9093) badala ya watu
31,836 (1:31,836);
(ii) Jumla ya madaktari wazalendo 37 wameajiriwa.
Idadi ya madaktari na wataalamu wa afya
imeongezeka kutoka 3,634 mwaka 2010 hadi
4,618 mwaka 2014. Ongezeko hilo ni sawa na
asilimia 26;
(iii) Elimu ya Afya kwa Umma imeendelea
kutolewa kwa njia mbalimbali. Mkazo mkubwa
umewekwa katika kuelimisha wananchi
kuhusu maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya
kuambukiza. Jitihada maalumu zimechukuliwa
juu ya kinga na tahadhari kuhusu maradhi ya
EBOLA; na
(iv) Jumla ya wafanyakazi 142 wa kada mbali mbali
wamepelekwa masomoni ndani na nje ya nchi
wakiwemo Madaktari 9, Wasaidizi Madaktari
12, Wauguzi 96 na wengiene wasiokuwa wa
kada za afya.
(h) Mapambano dhidi ya Malaria:
(i) Ili kuendeleza mapambano dhidi ya malaria,
mradi wa “Maliza Malaria Zanzibar”
umeendelea kutekelezwa. Kupitia mradi huo,
nyumba 57,385 sawa na asilimia 96 ya lengo
lililowekwa zilipulizwa dawa ya kuua mbu wa
malaria. Zoezi hilo limefanyika katika Wilaya
zote za Unguja na Pemba;
(ii) Vyandarua 717,000 viligawiwa kwa wananchi
(vitatu kwa kila kaya) na vingine 30,474
vilisambazwa kwa kupitia katika vituo
172
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
vinavyotoa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto
Unguja na Pemba; na
(iii) Jumla ya wagonjwa 28,982 (7,618 wakiwa chini
ya umri wa miaka 5 na 21,364 wakiwa zaidi ya
miaka 5) walichunguzwa katika vituo mbalimbali
vya afya na asilimia 1.4 waligundulika kuwa na
vimelea vya malaria na kutibiwa. Jitihada hizo
zimewezesha kiwango cha ugonjwa wa malaria
kuendelea kushuka kutoka asilimia 0.06 mwaka
2010 hadi asilimia 0.03 mwaka 2014.
(i) Mapambano dhidi ya UKIMWI:
(i) Jitihada za kuelimisha jamii juu ya umuhimu
wa kupima afya zao na kupiga vita unyanyapaa
dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
(VVU) zimeendelezwa. Ili kuendeleza jitihada
hizo, jumla ya shilingi 51,471,765 zimetolewa
kwa Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI (ZAPHA+);
(ii) Wahudumu wa afya 150 na waelimishaji rika
40 wamepatiwa mafunzo ya kuelimisha jamii
mbinu za kujikinga na UKIMWI, kupiga vita
unyanyapaa na udhalilishaji wa kijinsia. Jumla
ya wananchi 3,881 kutoka katika Shehia 118 za
Unguja na Pemba wamefikiwa na kupatiwa
elimu hiyo. Vile vile vijana 300 wamepatiwa
mafunzo ya Stadi za Maisha;
(iii) Jumla ya wananchi 61,921 wamejitokeza kupima
afya zao (wanawake 32,477 na wanaume 29,444).
Kati yao 966, sawa na asilimia 1.56 waligundulika
kuwa wanaishi na Virusi vya UKIMWI (VVU)
wanawake 520 (asilimia 54) na wanaume 446
(asilimia 46);
(iv) Idadi ya wagonjwa wanaopata huduma ya dawa
za ARVs, imeongezeka kutoka 2,341 mwaka
2010 hadi 4,669 mwaka 2014 sawa na asilimia 99;
173
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(v) Huduma za tiba na kuzuia maambukizi ya
mama kwenda kwa mtoto zimetekelezwa. Idadi
ya vituo vinavyotoa huduma ya ushauri nasaha
na upimaji wa VVU imeongezeka kutoka 87
mwaka 2012, hadi 91 mwaka 2014; na
(vi) Matokeo ya jitihada hizo, kiwango cha
maambukizi ya VVU bado kimeendelea kuwa
asilimia 0.6.
(j) Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na Ukoma:
(i) Ili kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu na
Ukoma, matibabu ya maradhi hayo kwa
wananchi yameendelea kutolewa na kampeni
maalumu ya ulishaji dawa kwa jamii imeendelea
kutekelezwa. Vijiji 24 vya Unguja na Pemba
vimefikiwa kwa njia ya mikutano na wananchi
314 waligunduliwa kuwa na maambukizi ya
ugonjwa wa Kifua Kikuu kati yao 223 (asilimia
71) wanapatiwa dawa wakiwa nyumbani kwao
na chini ya uangalizi wa familia zao; na
(ii) Jumla ya wananchi 97 waligundulika kuwa na
maradhi ya Ukoma kati yao sita (6) wakiwa
na ulemavu wa daraja la pili. Hatua ya
kuwapatia mafunzo juu ya ugonjwa wa Ukoma
wananchi 169 ambao ni jamaa za wagonjwa hao
imetekelezwa.
(k) Huduma za Afya ya Mama na Mtoto:
(i) Jumla ya Vituo vya Afya 84 vinatoa huduma za
ziada ikiwemo kuzalisha, maabara na huduma
za meno. Huduma ya Afya ya Uzazi (kwa njia
ya kawaida au upasuaji) na Afya ya Mama na
Mtoto hutolewa bila ya malipo katika hospitali
zote na Vituo vya Afya. Vituo vyote hivyo
vinafaidika na upatikanaji wa dawa chini ya
mpango maalumu (Zanzibar Integrated Logistic
System); na
174
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(ii) Juhudi za kuwapatia watoto chanjo zimeendelea
kutekelezwa ili kupunguza idadi ya vifo vya
watoto ambapo asilimia 96.75 ya watoto wote
wenye umri chini ya miaka 15 wamepatiwa
chanjo hizo. Chanjo ya BCG imefikia asilimia
148, Polio 95, Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda
na Uti wa mgongo asilimia 101 na Surua asimilia
77.
(l) Kuendeleza Huduma ya Tiba Asili
Baraza la Tiba Asili limeanzishwa na waganga 193
wamesajiliwa. Jumla ya maduka ya dawa za asili 39,
kliniki za tiba asili na tiba mbadala 18 zimeanzishwa
na wasaidizi waganga 125 wamesajiliwa.
(m) Chuo cha Sayansi ya Afya:
(i) Jumla ya wanafunzi 821 wa taaluma mbalimbali
za afya wamehitimu mafunzo. Aidha, kwa
kushirikiana na Chuo cha MATANZAS cha
Cuba, wanafunzi 38 (19 wanaume na 19
wanawake) wa kada ya udaktari wamehitimu
na kuongeza idadi ya madaktari wazalendo
wanaotoa huduma katika hospitali za Unguja
na Pemba. Aidha, masomo ya kujiendeleza kwa
wafanyakazi wenye cheti kwa muda mrefu
na ambao hawakupata fursa ya kujiendeleza
kielimu katika fani zao yameanzishwa; na
(ii) Jumla ya wanafunzi 183 wamejiunga na mafunzo
hayo kwa mwaka 2013/2014 na wanafunzi 11
wanaendelea na mafunzo ya Elimu Masafa
kupitia AMREF.
102. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), Chama
Cha Mapinduzi kitaielekeza SMZ kuiendeleza zaidi Sekta
ya Afya kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendeleza ushirikishwaji wa wananchi na Sekta
Binafsi ili kuchangia maendeleo ya afya kwa
kuzingatia MKUZA na Dira ya 2020;
175
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuendelea kuifanya Hospitali ya Mnazimoja kuwa ya
Rufaa kwa kuongeza huduma za matibabu ya saratani
na kuimarisha huduma za uchunguzi na ununuzi
wa vifaa kama “Magnetic Resonance Imaging” (MRI),
DNA na kuongeza idadi ya madaktari bingwa wa fani
mbalimbali;
(c) Kujenga Hospitali ya kisasa ya Rufaa katika eneo la
Binguni Unguja, kukamilisha ujenzi wa Hospitali
ya Abdalla Mzee na kuimarisha Hospitali ya Wete-
Pemba ili zifikie daraja na kiwango cha Hospitali za
Mkoa. Aidha, Hospitali za Vijiji (Cottage Hospitals) za
Micheweni na Vitongoji (Pemba) na Makunduchi na
Kivunge (Unguja) zitaendelea kuimarishwa ili zifikie
daraja na kiwango cha Hospitali za Wilaya;
(d) Kuendeleza jitihada za kuimarisha Huduma ya Afya
ya Mama na Mtoto kwa kujenga majengo mapya ya
Wodi ya Wazazi na Wodi ya Watoto katika Hospitali
Kuu ya Mnazimoja pamoja na kuvifanyia ukarabati
vituo 19 vya Afya ya Msingi na kuvipatia vifaa vya
kisasa Unguja na Pemba ili kupunguza kiwango cha
vifo vya mama na mtoto;
(e) Kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI,
Kifua Kikuu na Ukoma na maradhi mengine ya
kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na
kuimarisha jitihada za utoaji wa elimu ya afya kwa
wananchi ili kupunguza ongezeko la maradhi ya
Saratani, Kisukari na Shinikizo la Damu;
(f) Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Taaluma za
Sayansi ya Afya na watumishi wa Sekta ya Afya kwa
kuwapatia mafunzo ya ndani na nje ya nchi wakiwemo
madaktari wa fani ya Udaktari Bingwa katika fani ya
maradhi ya wanawake, mifupa, watoto, maradhi ya
moyo na usingizi;
(g) Kuendelea kutambua umuhimu wa tiba asili na tiba
mbadala katika jamii na kuimarisha ushirikiano na
176
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Baraza la Tiba Asili katika utendaji wake wa kazi;
(h) Kuhamasisha upatikanaji wa chakula na lishe bora
katika kila kaya ili kupunguza utapiamlo mkali kwa
watoto kutoka asilimia 24 mwaka 2014 hadi asilimia
12 mwaka 2020;
(i) Kuendeleza tafiti mbalimbali katika maeneo ya Afya
ya Mama na Mtoto, maradhi ya kuambukiza na
yasiyo ya kuambukiza pamoja na mifumo ya utoaji
wa huduma za afya;
(j) Kuimarisha huduma za matibabu kwa wagonjwa
walioathirika na madawa ya kulevya na afya ya
akili na kujenga kituo maalumu kwa waathirika wa
madawa ya kulevya;
(k) Kuimarisha upatikanaji, ugawaji, usambazaji na
udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi (Reagents)
vyenye ubora na usalama katika ngazi zote;
(l) Kuandaa Sheria ya Uanzishaji wa Mfuko wa Bima ya
Afya na kusimamia utekelezaji wa mfuko huo; na
(m) Kuimarisha na kusimamia mfumo wa taarifa za Afya
ili ziweze kutumika katika kutoa maamuzi katika
ngazi zote.
Maji
103. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
SMZ chini ya uongozi wa CCM imeimarisha huduma za
usambazaji na ugawaji wa maji safi na salama kwa wananchi
ambapo mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Mradi wa maji Mkoa wa Mjini Magharibi, Awamu ya Pili
umetekelezwa. Ujenzi wa matangi makubwa mawili huko
Kinuni na Dole na uchimbaji wa visima vitano (Kizimbani
(3) na Msikiti Mzuri (2) pamoja na ulazaji wa mabomba
yenye urefu wa kilomita 21 umekamilika. Aidha, kiwango
cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kimefikia
asilimia 87.7;
177
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kazi ya ujenzi wa
matangi ya maji Matemwe (lita 3,000,000) na Nungwi
(lita 3,000,000) pamoja na ulazaji wa mabomba kwenye
maeneo yote ya mradi imekamilika. Kiwango cha
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika
mkoa huo kimefikia asilimia 71.68;
(c) Kwa Mkoa wa Kusini Unguja, kazi ya ujenzi wa
matangi ya maji ya Machui (lita 1,500,000) na Tunguu
(lita 1,200,000) pamoja na ulazaji wa mabomba kwenye
maeneo ya mradi imekamilika. Aidha, kiwango cha
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika
Mkoa huo kimefika asilimia 76.45;
(d) Kazi ya ujenzi wa matangi ya maji ya Ndagoni (lita
1,000,000), Vikunguni (lita 300,000), Vitongoji-Ali
Khamis Camp (lita 300,000), Kambini Bahanasa (lita
1,000,000) na Wambaa (lita 500,000) pamoja na ulazaji
wa mabomba katika maeneo yote ya miradi ya Mkoa
wa Kaskazini na Kusini Pemba imekamilika. Aidha,
kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na
salama katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kimefikia
asilimia 56.42 na Mkoa wa Kusini Pemba asilimia
74.08; na
(e) Jumla ya mita 3,007 zimefungwa katika nyumba za
makazi na maeneo ya biashara Unguja na Pemba ili
kupunguza kiwango cha upotevu wa maji.
104. Ili kuendeleza sekta ya maji na kuimarisha huduma
za usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itaielekeza SMZ kufanikisha yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha usambazaji wa huduma ya
maji safi na salama kwa wananchi kutoka asilimia 87
mwaka 2015 hadi asilimia 97 mwaka 2020 kwa Mijini
na kutoka asilimia 70 mwaka 2015 hadi asilimia 85
kwa vijijini;
178
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuendeleza utekelezaji wa mradi wa uimarishaji
wa miundombinu ya maji katika Mkoa wa Mjini
Magharibi na ufungaji wa mita kwa wateja ili kudhibiti
upotevu wa maji;
(c) Kuendeleza jitihada za kuhuisha miundombinu ya
maji ili kupunguza upotevu wa maji, kuhifadhi,
kutunza na kulinda vyanzo vya maji pamoja na
maeneo ya hifadhi ya maji; na
(d) Kuendelea kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu
wa uhifadhi, utumiaji na uchangiaji wa huduma ya
maji safi na salama na kufanya utafiti wa matumizi ya
Nishati ya Jua katika visima na vyanzo vya maji.
Makazi
105. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa
CCM imefanya juhudi kubwa za kuendeleza ujenzi wa
nyumba bora kwa ajili ya makazi ya wananchi Unguja na
Pemba. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-
2015), huduma za makazi zimeboreshwa na kupatikana
mafanikio yafuatayo:-
(a) Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Nyumba, Sheria
ya kuanzisha Shirika la Nyumba la Zanzibar ya
mwaka 2014 imepitishwa ili kuwapa fursa wananchi
waliopangishwa nyumba za maendeleo mijini na
vijijini kuuziwa sehemu ya majengo hayo;
(b) Kazi ya kuufanyia mapitio Mpango Kabambe (Master
Plan) wa mji wa Zanzibar ili kuanzisha maeneo
maalumu ya ujenzi wa nyumba za ghorofa hususan
katika maeneo ya mijini na kuwashajihisha wawekezaji
kuwekeza katika Sekta ya Nyumba imefikia katika
hatua za mwisho; na
(c) Ujenzi wa Nyumba ya Maendeleo huko Bambi
(Mpapa) umekamilika. Jumla ya nyumba (fleti)
24 zimekabidhiwa kwa wananchi wakati wa
179
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
106. Ili kuendelea kuwawezesha wananchi kupata nyumba
na makazi bora, CCM katika kipindi cha miaka mitano
ijayo (2015-2020), itahakikisha kuwa SMZ inasimamia
utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba na Sheria
“Condominium” pamoja na kuhamasisha Sekta Binafsi
kuanzisha miradi ya makazi kwa njia ya ubia (PPP).
Mamlaka ya Mji Mkongwe
107. Katika kuendeleza Mji Mkongwe, Mamlaka imefanya
ukaguzi wa kitaalamu ili kubaini nyumba zilizo katika
hali mbaya ya uchakavu na kuziingiza katika kanzidata
(database) pamoja na kuwashauri wamiliki au wapangaji
wa nyumba hizo kuzifanyia ukarabati unaohitajika ambapo
majengo 267 yamefanyiwa ukarabati bila kubadili uhalisia
wake.
108. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itahakikisha kuwa, SMZ inaendelea kuchukua hatua za
uhifadhi wa Mji Mkongwe ili uendelee kuwa kivutio cha
utalii na chanzo cha ajira kwa wananchi kwa kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kuhifadhi na kuuendeleza Mji Mkongwe wa Zanzibar
ili uendelee kubaki katika uasili wake na katika orodha
ya Miji ya Urithi wa Dunia;
(b) Kuendelea kuyahifadhi na kuyafanyia ukarabati
majengo yote ya kihistoria ndani ya eneo la Mji
Mkongwe kwa kushirikiana na Sekta Binafsi;
(c) Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya
umuhimu na thamani ya kuulinda, kuuhifadhi na
kuendeleza Mji Mkongwe kwa maslahi ya kizazi cha
sasa na cha baadaye; na
(d) Kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa ukuta wa
ukingo wa bahari katika eneo la Mizingani.
180
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Maeneo mengine ya kipaumbele
Utamaduni na Michezo
109. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta
ya Utamaduni na Michezo imepata mafanikio makubwa.
Michezo
110. Michezo ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha
mila na silka njema za jamii. Michezo huimarisha afya na
kujenga udugu na mashirikiano miongoni mwa wananchi
na Mataifa mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Mabaraza ya Michezo ya Wilaya yameimarishwa na
kupatiwa mafunzo juu ya usimamizi wa shughuli za
michezo;
(b) Timu ya Taifa na vilabu mbalimbali vimepata fursa ya
kushiriki katika mashindano mbalimbali ya Kitaifa na
Kimataifa;
(c) Timu ya vijana wenye ulemavu wa akili imeshiriki
katika mashindano ya olimpiki (Special Olympics)
yaliyofanyika nchini Ugiriki;
(d) Uwanja wa Amani umewekewa nyasi bandia.
Aidha, studio ya kisasa ya kurekodia filamu/muziki
imeanzishwa huko Rahaleo na pia Kituo cha Michezo
huko Dole (Dole Academy) kimejengwa ambapo zaidi
ya vijana 3,000 wameanza kukitumia na kupata fursa
ya kushiriki katika mashindano ya ndani na nje ya
nchi; na
(e) Uwanja wa mpira wa Gombani Pemba nao
umeimarishwa kwa kuwekewa taa, kujengwa paa
jipya, njia ya kukimbilia (running track) pamoja na
kiwanja cha michezo ya ndani.
181
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
111. Ili kuiendeleza Sekta ya Michezo, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaielekeza SMZ
kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuhamasisha jamii kushiriki katika michezo kwa lengo
la kuimarisha afya zao na kuendeleza Michezo ya Asili
hususan mchezo wa Ng’ombe na mashindano ya resi
za ngalawa na kutumia sanaa za aina mbalimbali ili
kujiajiri wao wenyewe kwa lengo la kupambana na
umasikini;
(b) Kukiimarisha Kituo cha Michezo cha Dole (Dole
Academy) ili kuendeleza michezo ya aina mbalimbali
kwa vijana na kuanzisha mfumo wa michezo ya
kulipwa na kushiriki mashindano ya Kimataifa;
(c) Kujenga viwanja vya michezo katika Wilaya tano
(5) na kuwapatia mafunzo na vifaa vya kisasa vijana
ili kuwaongezea ujuzi na uzoefu wa michezo kwa
kutumia walimu wa ndani na nje ya nchi;
(d) Kukifanyia matengennezo makubwa kiwanja cha
michezo cha “Mao Tse Tung” ili kiweze kutumika kwa
shughuli za michezo na sherehe za kitaifa; na
(e) Kuvipatia vyama vya michezo vya watu wenye
ulemavu fursa stahiki ili waweze kushiriki kikamilifu
katika kuendeleza michezo ikiwemo michezo ya
kulipwa.
Utamaduni
112. Utamaduni ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha
mila na silka njema za jamii. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010-2015), yamepatikana mafanikio yafuatayo:-
(a) Sera na Sheria zinazoongoza Utamaduni zimefanyiwa
mapitio ili kukidhi matarajio na mahitaji ya wakati na
sheria mpya ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu
na Utamaduni imetungwa. Chini ya sheria hiyo, Bodi
ya Sensa ya Filamu na Baraza la Sanaa la Zanzibar
vimeunganishwa;
182
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Utafiti wa Urithi wa Utamaduni usioshikika
umefanyika na matokeo ya utafiti huo kuhifadhiwa
Kimataifa na kuingizwa katika orodha ya UNESCO
ya tamaduni zinazohifadhiwa. Sambamba na hatua
hiyo, matokeo ya utafiti huo pia yamerejeshwa kwa
wananchi wa maeneo husika ili kuzitumia kama
sehemu ya ajira na kupambana na umasikini; na
(c) Hatua ya ukaguzi wa kazi za sanaa ili kulinda
na kuhifadhi mila, desturi na silka za Mzanzibari
imetekelezwa. Aidha, Kamusi za lahaja za Kipemba,
Kimakunduchi na Kitumbatu zimechapishwa na
kusambazwa kwa wananchi.
113. Ili kuendeleza Sekta ya Utamaduni, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itaielekeza SMZ
kutekeleza mambo yafuatayo:-
(a) Kuandaa Sera ya Urithi wa Utamaduni na kufanya
utafiti maalumu katika visiwa visivyoishi watu
ili kubaini aina ya utalii unaoweza kufanyika na
kuongeza fursa za ajira kwa wananchi;
(b) Kuimarisha lugha ya Kiswahili na kuzifanya lahaja za
Kiswahili za Zanzibar kuwa chimbuko la Kiswahili
fasaha. Jumla ya machapisho mapya 10 ya vitabu
na majarida 15 ya kuimarisha lugha ya Kiswahili
yatatolewa kwa lengo la kuwawezesha watumiaji
wenyeji na wageni kukitumia Kiswahili fasaha katika
nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii;
(c) Kuihamasisha jamii ili kuuenzi, kuulinda na
kuudumisha utamaduni wa Mzanzibari na kushiriki
katika uandaaji wa matamasha 50 ya utamaduni;
(d) Kuwapatia mafunzo walimu 150 wa utamaduni na
wasanii 500 ili kuwawezesha kutumia sanaa zao
kwa mambo yenye manufaa kwa wananchi na yenye
kuzingatia maadili ya jamii; na
183
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Kuendeleza teknolojia za jadi kwa kutoa mafunzo
kwa mafundi 75 ili ziweze kuwanufaisha wananchi
kiuchumi na kuirithisha teknolojia hiyo kwa kizazi
kipya.
Vyombo vya Habari
114. Vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kutoa habari,
kuburudisha na kuelimisha jamii juu ya matukio na masuala
mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya nchi na kuchangia
katika kukuza na kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), Sekta
ya Habari imepata mafanikio yafuatayo:-
(a) Mageuzi makubwa ya kisera na kisheria yamefanyika
ili kuiwezesha Zanzibar kuachana na mfumo wa
matangazo ya Analogia na kuingia katika mfumo wa
Dijitali. Aidha, Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC)
limeanzishwa ambapo Redio, Televisheni na Gazeti la
Serikali (Zanzibar Leo) vimeunganishwa. Hatua hizi
zimeongeza ubora wa matangazo na ufanisi katika
vyombo vya habari;
(b) Studio za Televisheni (Unguja na Pemba) zimepatiwa
vifaa na mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo.
Waandishi wa habari 114 (wanawake 78 na wanaume
36) wamepatiwa mafunzo ya Shahada ya Uzamivu
(PhD), Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza,
Stashahada na Astashahada;
(c) Jumla ya vituo vipya tisa (9) vya Radio za FM na
Televisheni sita (6) vimeanzishwa;
(d) Chuo cha Uandishi wa Habari kimepatiwa jengo jipya
huko Kilimani pamoja na vifaa vya kisasa, walimu
wenye ujunzi na kuanzisha mafunzo ya lugha ya
Kichina. Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na Chuo
hiki imeongezeka kutoka 75 mwaka 2010 hadi 180
mwaka 2014; na
184
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali kimehamishwa kutoka eneo la zamani la
Saateni na kupelekwa katika majengo mapya huko
Maruhubi. Aidha, kiwanda kimepatiwa mitambo
mipya na ya kisasa ya uchapaji (Digital Printing
Machine) na kuanza kutekeleza majukumu yake kwa
ufanisi mkubwa.
115. Kwa kutambua uzito wa jukumu la Vyombo vya Habari,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), SMZ
chini ya uongozi wa CCM itahakikisha kuwa Uhuru wa
Vyombo vya Habari unaendelea kuimarishwa na vyombo
hivyo vinatekeleza wajibu wake kwa weledi na kuzingatia
maadili ya kazi zao kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA na kuendeleza
mageuzi katika Sekta ya Habari ili kuongeza ufanisi
na weledi katika tasnia hii;
(b) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar
(ZBC) kwa kulipatia mitambo, vifaa vya kisasa na
vitendea kazi pamoja na fursa za mafunzo ndani na
nje ya nchi kwa wafanyakazi 600 wa kada mbalimbali;
(c) Kuendeleza jitihada za kukiimarisha Chuo cha
Uandishi wa Habari ili kiwe chachu ya kuendeleza
tasnia ya habari na chimbuko la kuibua na kuendeleza
vipaji vya uandishi; na
(d) Kuimarisha mfumo wa uendeshaji wa Kiwanda cha
Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
kwa kukiongezea mitambo na vifaa vya kisasa na
wataalamu.
Huduma za Uokoaji
116. Huduma za Uokoaji ni muhimu kwa jamii hasa pale
yanapozuka maafa na majanga mbalimbali. Katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita (2010-2015) mafanikio yafuatayo
yamepatikana:-
185
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(i) Sera ya Maafa ya mwaka 2011 imeandaliwa na
Mpango wa elimu ya kukabiliana na Maafa
kwa wananchi umetekelezwa;
(ii) Kamati ya Maafa ya Zanzibar, Wilaya na Shehia
277 zimeendelea kuimarishwa na kupatiwa
mafunzo ya msingi ya kukabiliana na maafa; na
(iii) Kikosi Maalumu cha Uzamiaji kimeanzishwa na
wananchi wamehamasishwa kuanzisha Vikosi
na Jumuiya za Uokozi katika maeneo yao.
117. Ili kuimarisha Huduma za Uokoaji, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha kuwa
SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Kukabiliana na
Maafa na kuanzisha Kamisheni ya Kukabiliana na
Maafa;
(b) Kuanzisha na kusimamia Mfuko wa Kukabiliana na
Maafa pamoja na kuimarisha juhudi za kuelimisha
jamii katika kukabiliana nayo; na
(c) Kurahisisha uratibu na upatikanaji wa rasilimali fedha
na mawasiliano ya moja kwa moja na asasi nyingine
za ndani na nje ya nchi katika shughuli za uokoaji.
Madawa ya Kulevya
118. Madawa ya kulevya ni moja ya changamoto kubwa
zinazowakabili wananchi wengi hasa vijana. Madawa
ya kulevya yameathiri sana afya za watumiaji na
kudhoofisha nguvu kazi na uchumi wa Taifa letu. Aidha,
utafiti umethibitisha kwamba upo uhusiano mkubwa
kati ya matumizi ya madawa ya kulevya na maambukizi
ya virusi vya ukimwi (VVU). Katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita, mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
yameendelezwa na mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Mpango maalumu wa utekelezaji wa Sheria ya Dawa
za Kulevya (Road Map) umeandaliwa;
186
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Hali ya usalama katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Abeid Amani Karume imeimarishwa.
Vifaa vya kisasa ikiwemo “scanner”, Kikosi cha Mbwa
pamoja na choo maalumu kwa ajili ya washukiwa wa
madawa ya kulevya vimewekwa;
(c) Kwa kushirikiana na taasisi zisizokuwa za kiserikali
(NGOs), kazi ya kuhamasisha wananchi kupima afya
zao na kuwapitia ushauri nasaha imetekelezwa; na
(d) Jumla nyumba 13 za kurekebisha tabia za vijana
walioathirika na madawa ya kulevya (Sober Houses)
zimeanzishwa na kuhudumia jumla ya vijana 1,020
Unguja na Pemba.
119. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), SMZ
chini ya uongozi wa CCM, itaendeleza mapambano dhidi
ya madawa ya kulevya kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Utekelezaji wa Sheria ya Madawa ya Kulevya kwa
kuandaa mazingira bora ya utendaji kazi kwa vyombo
husika ili kudhibiti uingiaji na usafirishaji wa Dawa za
kulevya;
(b) Kuendeleza mafunzo na elimu kwa jamii juu ya
athari za madawa ya kulevya na kuandaa mkakati wa
kuwasaidia waathirika na madawa hayo ili kuachana
na utumiaji. Aidha, kitajengwa kituo maalumu cha
kurekebisha vijana walioathirika na madawa ya
kulevya;
(c) Kuendeleza na kuimarisha mashirikiano miongoni
mwa vyombo vinavyosimamia mapambano dhidi
ya madawa ya kulevya kati ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar; na
(d) Kushirikiana na Taasisi za Kimataifa zinazoendesha
mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kudhibiti
usafirishaji na biashara haramu ya madawa hayo bila
kujali mipaka ya nchi.
187
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Demokrasia na Utawala Bora
120. Demokrasia na Utawala Bora ni moja ya nyenzo muhimu
katika ujenzi wa jamii yenye umoja, mshikamano, uadilifu
na uwajibikaji. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
(2010-2015), mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Programu maalumu ya elimu ya uraia juu ya Sera ya
Utawala Bora na Haki za Binaadamu imeandaliwa na
kutekelezwa;
(b) Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi
pamoja na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa imeanzishwa
na kuanza kazi. Aidha, Kanuni za kudhibiti Rushwa
na Uhujumu wa Uchumi zimeandaliwa na kuanza
kutumika;
(c) Mafunzo juu ya mapambano dhidi ya rushwa
yametoelewa kwa wafanyakazi na viongozi
mbalimbali wa Serikali;
(d) Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka, Ofisi Ndogo ya Wanasheria (Mwera) na
nyumba za waendesha Mashtaka wa Mahakama za
Wilaya ya Makunduchi na Mkokotoni (Unguja); na
Madungu na Chake Chake (Pemba) umekamilika;
(e) Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali lilioko Unguja na lile la
Wete Pemba umekamilika. Aidha, mafunzo ya ukaguzi
kwa kuzingatia thamani na mazingira yametolewa
kwa wafanyakazi. Kutokana na juhudi hizo, ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
sasa imefikia kiwango kinachokubalika Kimataifa;
(f) Jengo la Mahakama Kuu Unguja na Pemba, majengo
ya Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Kadhi
yamefanyiwa matengenezo makubwa. Mahakimu
wapya 10 wameajiriwa kati yao, saba (7) ni wanawake
na watatu (3) ni wanaume;
188
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Mafunzo juu ya matumizi ya Teknolojia ya Habari,
uendeshaji na usimamizi wa kesi pamoja na uandishi
wa Sheria yametoelewa kwa Majaji, Mahakimu na
Waendesha Mashtaka;
(h) Sheria ya kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar
imepitishwa na matengenezo ya jengo la Mahakama
hiyo yamekamilika. Aidha, Mahakama ya Watoto
imeanzishwa na kuanza kufanya kazi; na
(i) Ujenzi wa jengo jipya la Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi huko Chukwani umekamilika na kuanza
kutumika kwa ajili ya mikutano na vikao vyote vya
Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
121. Ili kuendeleza Demokrasia na Utawala Bora, katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itahakikisha kuwa, SMZ inatekeleza yafuatayo:-
(a) Utekelezaji wa kazi na majukumu ya Serikali
unazingatia misingi ya Demokrasia na Utawala
Bora kama ilivyoainishwa katika Katiba za nchi na
kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa wananchi;
(b) Kuandaa na kupitisha Sheria ya Maadili ya Viongozi na
kuimarisha mafunzo na elimu ya uraia kwa viongozi
wa taasisi za umma na binafsi pamoja na wananchi
juu ya misingi ya Demokrasia na Utawala Bora;
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu
Uchumi kwa kuiongezea rasilimali watu, mafunzo na
vifaa vya kisasa;
(d) Kuimarisha mfumo wa Sheria kwa kufanya
mabadiliko katika utendaji kazi wa Mahakama, Ofisi
ya Mwendesha Mashtaka, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu, Jeshi la Polisi, Vyuo vya Mafunzo na wadau
wengine wa Sheria ili kuwajengea uwezo katika utoaji
wa haki;
189
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(e) Kuandaa Sera ya Msaada wa Kisheria ili kutoa fursa
kwa wananchi na makundi maalumu ya jamii kupata
haki zao kwa urahisi na kuanzisha mfumo wa kitaasisi
wa masaada wa kisheria;
(f) Kuimarisha Ofisi ya Mrajisi Mkuu wa Serikali na
mifumo ya usajili wa Nyaraka, Biashara, Mali na
Hakibunifu na kudhibiti wizi na uharamia wa sanaa;
na
(g) Kuimarisha huduma za ukaguzi wa Hesabu za Serikali
ili kuhakikisha kwamba miradi inayotekelezwa ina
thamani sawa na fedha zilizotumika. Aidha, mafunzo
ya kada mbalimbali yatatolewa kwa watumishi ili
kuongeza ufanisi.
Serikali za Mitaa
122. Serikali za Mitaa ni chombo muhimu cha kuwashirikisha
wananchi katika kusimamia shughuli za utawala na
maendeleo yao. Serikali za Mitaa zina mchango mkubwa
katika kukuza maendeleo ya wananchi mijini na vijijini na
kuendeleza demokrasia na utawala bora. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2015-2020), mafanikio yafuatayo
yamepatikana:-
(a) Sheria za Serikali za Mitaa na Sheria ya Mamlaka
ya Mikoa zimefutwa na kutungwa Sheria mpya ya
Tawala za Mikoa na Sheria ya Mamlaka ya Serikali za
Mitaa;
(b) Wananchi wamehamasishwa kuunda Kamati za
Maendeleo za Shehia na Majimbo ili kusukuma kasi
ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Jumla ya
Kamati za Maendeleo za Shehia 339 katika majimbo
yote Unguja na Pemba zimeanzishwa;
(c) Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya
yameendelea kupatiwa ruzuku, vitendea kazi pamoja
na watendaji wenye ujuzi. Jumla ya wafanyakazi saba
(7) wamepatiwa mafunzo ndani na nje ya nchi katika
190
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
fani mbalimbali. Wajumbe wa Kamati za Kudumu za
Serikali za Mitaa nao wamepatiwa mafunzo juu ya
masuala ya Fedha, Afya na Sheria;
(d) Mradi maalumu wa Huduma za Jamii (ZUSP)
umeanzishwa ili kuimarisha mazingira ya Manispaa
ya Zanzibar, hifadhi ya eneo la urithi wa Mji Mkongwe
na miji ya Chake Chake, Wete na Mkoani huko
Pemba. Mradi huo umekamilisha kazi ya uwekajiwa
taa za barabarani pamoja na taa za kuongoza magari
zinazotumia umeme wa jua (solar) katika maeneo ya
Mji Mkongwe; na
(e) Baraza la Manispaa la Zanzibar limeanzisha utaratibu
wa kuingia mikataba na vikundi vya kijamii kwa
ajili ya kufanya usafi katika maeneo ya masoko,
bustani, barabara, mitaro na kuondoa taka ngumu ili
kuimarisha usafi wa mazingira ya mji.
123. Ili kuziendeleza Serikali za Mitaa, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha
kwamba, SMZ inatekeleza yafuatazo:-
(a) Kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato
ya Halmashauri za Wilaya, Mabaraza ya Miji na
Manispaa kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato na
kuimarisha ubora wa huduma kwa wananchi na usafi
wa mazingira ya maeneo ya miji;
(b) Kusimamia, kuratibu na kusaidia utendaji kazi wa
Kamati za Maendeleo katika maeneo mbalimbali ili
kusukuma kasi ya maendeleo na kudhibiti vitendo
viovu katika jamii na kusaidia juhudi za wananchi
katika kuimarisha huduma za kijamii na kuwapatia
misaada ya aina mbalimbali; na
(c) Kuendeleza utekelezaji wa mradi maalumu wa
kuimarisha mazingira ya Manispaa ya Zanzibar,
hifadhi ya eneo la urithi wa Mji Mkongwe na miji ya
Chake Chake, Wete na Mkoani Pemba. Aidha, ujenzi
191
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
wa jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Wete
utakamilishwa.
Idara Maalumu za SMZ
124. Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni
vyombo muhimu katika utekelezaji wa Sera za CCM
kuhusu Ulinzi na Usalama hususan dhana ya ulinzi wa
umma ambao unawashirikisha wananchi wote. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), SMZ chini
ya uongozi wa CCM imeimarisha mazingira ya utendaji
kazi na maslahi ya wapiganaji wa Idara Maalumu za SMZ
kwa kutelekeza yafuatayo:-
(a) Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM)
Jumla ya wapiganaji 83 wamepatiwa mafunzo
ndani na nje ya nchi katika fani mbalimbali pamoja
na kuwapatia vyombo vipya vya usafiri na vifaa
vya kisasa. Aidha, ujenzi wa Hospitali ya Kibweni
umekamilika na kuanza kutumika.
(b) Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)
Jumla ya wapiganaji 86 wamepatiwa mafunzo ya aina
mbalimbali. Vijana 2,000 wamepatiwa mafunzo ya
uzalendo, uzalishaji mali pamoja na mafunzo ya amali
kila mwaka. Aidha, jumla ya vijana 900 wamepatiwa
Mafunzo ya Stadi mbalimbali za ufundi katika Chuo
cha Amali cha JKU.
(c) Chuo Cha Mafunzo
Kazi ya ujenzi wa bweni la kulala wanafunzi huko
Kinumoshi imekamilika. Aidha, utaratibu wa
wahalifu kutumikia adhabu zao katika jamii badala
ya Chuo cha Mafunzo umeanza kutekelezwa ili
kupunguza msongamano wa wanafunzi.
192
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kikosi cha Zima Moto na Uokozi (KZU)
Jumla ya wapiganaji 68 wamepatiwa mafunzo ya
zimamoto nje ya nchi. Huduma za Zimamoto na
Uokozi zimefikishwa katika wilaya zote za Unguja
na Pemba. Aidha, huduma za Zimamoto na Uokozi
zimeanza kutolewa katika Bandari za Malindi
(Unguja) na Mkoani (Pemba).
(e) Kikosi Cha Valantia Zanzibar (KVZ)
Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kikosi hicho huko
Mtoni (Unguja) umekamilika na ujenzi wa nyumba ya
maafisa na makaazi ya wapiganaji wa Kikosi hicho
huko Kisiwani Pemba umeanzishwa.
125. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itaielekeza SMZ kuendelea kuziimarisha Idara Maalum
za SMZ kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuimarisha zaidi mazingira ya kazi na utendaji
wa wapiganaji wa KMKM, JKU, KZU na KVZ kwa
kuwapatia mafunzo, vifaa vya kisasa, maslahi
na mahitaji mengine muhimu ili kuwawezesha
kutekeleza majukumu yao ya ulinzi kwa weledi na
ufanisi mkubwa;
(b) Kukamilisha ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya JKU
Mtoni na kukiendeleza Kituo cha Amali cha JKU
kwa kupanua wigo wa mafunzo ya Amali kwa vijana
wanaojiunga na kituo hicho kwa kuzingatia mahitaji
ya soko la ajira na kuwawezesha vijana kujiajiri
wenyewe; na
(c) Kukamilisha ujenzi wa nyumba za maafisa na makaazi
ya wapiganaji wa KVZ Kisiwani Pemba.
193
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kuwaunganisha Wananchi wa Zanzibar
126. Hoja ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar imetokana
na Sera ya CCM ya kujenga umoja wa kitaifa, amani na
utulivu. Bila ya kuwepo mazingira ya amani na utulivu
nchi haiwezi kupata maendeleo na hakuna mwekezaji
atakayekubali kuwekeza. Aidha, wananchi watashindwa
kuendesha shughuli zao za kiuchumi, kijamii na utamaduni.
Katika kipindi cha 2010-2015, Serikali chini ya uongozi wa
CCM, imeifanyia mabadiliko Katiba ya Zanzibar ya Mwaka
1985 (Mabadiliko ya 10) na baada ya Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2010, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye
muundo wa Umoja wa Kitaifa chini ya uongozi wa Mhe.
Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi imeundwa na kufanikiwa kutimiza
malengo yake kwa ufanisi.
127. Ili kuendeleza Sera ya kuwaunganisha wananchi wa
Zanzibar, katika kipindi cha 2015-2020, CCM itandelea
kuwa muumini wa kweli wa amani, utulivu na
kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kwa kuimarisha
mafanikio yaliyokwisha kupatikana na kuielekeza SMZ
kutekeleza yafuayo:-
(a) Kuendeleza jitihada za kuhamasisha jamii juu ya
umuhimu wa amani, umoja na mshikamano ili
kujenga mazingira ya kuaminiana, kuvumiliana na
kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii;
(b) Kuendelea kupiga vita na kudhibiti vitendo vya
ubaguzi vinavyojitokeza katika sehemu za utoaji wa
huduma za kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni
mwa wananchi; na
(c) Kuimarisha mifumo ya taasisi za uratibu na
kushughulikia malalamiko na kero za wananchi kwa
wakati, haki na uadilifu.
194
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kuyaendeleza Makundi Mbalimbali
Watoto
128. Watoto kama Taifa la kesho wanayo haki ya kulindwa kwani
ndio chanzo cha rasilimali watu na mrithi wa Taifa la kesho.
Watoto wanayo haki ya kuishi, kutoa mawazo, kupata lishe
bora, malezi na ulinzi, kupewa elimu na kutobaguliwa
kwa kwa namna yoyote. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010-2015), Serikali chini ya uongozi wa CCM
imeendelea kusimamia maendeleo ya watoto na mafanikio
yafuatayo amepatikana:-
(a) Sheria ya Mtoto pamoja na Kanuni saba za kusimamia
utekelezaji wa sheria hiyo zimepitishwa ikiwemo
miongozo ya uanzishaji na uendeshaji wa nyumba za
kulelea watoto. Aidha, ujenzi wa Kituo cha Kulelea
Watoto cha Mazizini umekamilika;
(b) Jumla ya Mabaraza ya Watoto 239 yameanzishwa
Unguja na Pemba ili kupiga vita ajira kwa watoto
na kazi ya usajili na kuwatambua watoto wanaoishi
katika mazingira magumu imetekelezwa na watoto
12,453 (Unguja 7,711 na Pemba 4,742) wamesajiliwa na
kutambuliwa mahitaji yao. Aidha, kampeni maalumu
ya kupiga vita vitendo vya udhalilishaji dhidi ya
wanawake na watoto imeanzishwa; na
(c) Kiwanja cha kufurahishia watoto cha Uhuru Kariakoo
(Unguja) na Tibirinzi (Pemba) vimejengwa upya
ili kuwapatia watoto maeneo ya kucheza yenye
mandhari nzuri na kuvutia.
129. Katika kipindi cha miaka 2015-2020, CCM itaendelea
kuimarisha haki na maendeleo ya watoto na kuhakikisha
kwamba SMZ inatekeleza hatua zifuatazo:-
(a) Kusimamia uanzishaji na uendelezaji wa Mabaraza
ya Watoto na Kamati za Wazazi katika Shehia, Wilaya
na Mikoa yote ya Zanzibar ili kupiga vita vitendo vya
udhalilishaji dhidi ya watoto;
195
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuendelea kupiga vita ajira za watoto na kusimamia
utekelezaji wa Sheria na mikataba ya Kimataifa
inayohusu Haki, Usawa na hifadhi ya mtoto; na
(c) Kuratibu na kutathmini huduma inazotolewa na
vituo binafsi vya kulelea watoto ili kuhakikisha
vinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria.
Vijana
130. Vijana walioandaliwa vyema na kujipanga vizuri wanao
mchango mkubwa katika kukuza uchumi na maendeleo
ya jamii. Changamoto kubwa inayowakabili vijana mijini
na vijijini ni ukosefu wa ajira, kukosa ujuzi na maarifa ya
kisasa pamoja na mitaji hivyo kushindwa kujiendeleza na
kutekeleza wajibu wao wa kushiriki katika ujenzi wa uchumi
wa kisasa. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-
2015), SMZ chini ya uongozi wa CCM, imechukua hatua
mbalimbali za kuwaendeleza vijana na kupata mafanikio
yafuatayo:-
(a) Baraza la Taifa la Vijana limeanzishwa na jumla ya asasi
za vijana 158 zilipatiwa mafunzo ya aina mbalimbali;
(b) Jumla ya vikundi 258 (Unguja 203 na Pemba 55)
vyenye wanachama 2,285 (Unguja 2,015 na Pemba 270)
vimeanzishwa na kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali
na stadi mbalimbali za maisha. Vile vile, vyama viwili
(2) vya SACCOS za vijana vimeanzishwa;
(c) Mfuko Maalumu umeanzishwa ili kutoa mikopo
yenye riba na masharti nafuu kwa Vijana. Mikopo
yenye thamani ya Shilingi 813,800,000 (Unguja Shilingi
700,000,000 na Pemba Shilingi 113,800,000) imetolewa;
(d) Kwa kupitia mifuko mingine ya Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, jumla ya Shilingi 318,600,000 zimetolewa
kwa vikundi 130 vya vijana Unguja na Pemba.
Kati ya fedha hizo Shilingi 206,950,000 zimetolewa
kwa vikundi 99 vya vijana wa Unguja, na Shilingi
111,700,000 zimetolewa kwa vikundi 31 vya vijana wa
196
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Pemba;
(e) Jumla ya shilingi milioni 100 zimewekwa katika Benki
ya CRDB kama dhamana ya Serikali ili kuiwezesha
Benki hiyo kutoa mikopo kwa vijana; na
(f) Jumla ya Vyama vya Ushirika vinne (4) vyenye
wanachama 72 (wanawake 42 na wanaume 30)
ambao ni vijana waliohitimu vyuo na vyuo vikuu
vimeanzishwa na kuweza kujiajiri wenyewe kupitia
kilimo na usindikaji; na kutoa mafunzo na ukaguzi
kwenye vikundi vya ushirika. Pia vikundi vitatu (3)
vya vijana (Unguja 2 na Pemba 1) vinavyojishughulisha
na kilimo cha mboga mboga kwa kutumia teknolojia
ya umwagiliaji (Drip Irrigation) vimeanzishwa na
kupatiwa msaada wa vifaa vya umwagiliaji maji
vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 21,000 kutoka
Shirika la Kazi Duniani (ILO).
131. Katika kipindi cha mwaka 2015-2020, SMZ chini ya uongozi
wa CCM, itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto za
vijana kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuandaa Programu za Elimu na Malezi Bora kwa
Vijana ili kuwawezesha jumla ya vijana 235,817 kupata
mafunzo ya stadi mbalimbali za maisha pamoja na
kujiajiri;
(b) Kuliendeleza Baraza la Taifa la Vijana ili kuongeza
ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za
maamuzi;
(c) Kuendelea kuimarisha Mfuko Maalumu wa Vijana
ili kutoa mikopo kwa vijana wengi zaidi na kujiajiri
katika kilimo cha kisasa na kuanzisha “Green House”
moja katika kila wilaya;
(d) Kuhamasisha vijana 5,000 waliomaliza vyuo na vyuo
vikuu kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali na utoaji
huduma, kuvipatia mafunzo na mikopo ili waweze
kujiajiri. Aidha, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali
197
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
zitahamasishwa kutoa zabuni za kazi na huduma kwa
vijana hao; na
(e) Kuandaa mikakati ya malezi bora kwa vijana ili kujenga
moyo wa uzalendo, ari ya kujitolea na kuipenda nchi
yao na kuimarisha mahusiano ya vijana ndani na nje
ya nchi.
Wanawake
132. Chama Cha Mapinduzi kinatambua uwezo na nguvu kubwa
ya wanawake katika kusukuma kasi ya maendeleo na kuleta
mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2010-2015), SMZ chini ya uongozi
wa CCM, imechukua hatua mbalimbali za kuwaendeleza
wanawake ili kuwajengea uwezo na uthubutu wa kutumia
fursa za kujiendeleza kiuchumi, kijamii na kisiasa na kupata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Jumla ya vikundi 551 (Unguja 209 na Pemba 362) na
SACCOS 53 (Unguja 24 na Pemba 29) za wanawake
zimeanzishwa. Aidha, wajasiriamali wanawake 129
wamepatiwa mafunzo juu ya ubora wa bidhaa na
masoko;
(b) Kwa kushirikiana na Chuo cha Barefoot College
Tilonia cha India, kituo cha kuwafundisha wanawake
kutengeneza vifaa vya umeme wa jua kimeanzishwa
huko Kibokwa Mkoa wa Kaskazini Unguja;
(c) Waratibu 40 na Makatibu watano (5) wa vikundi
vya wanawake wamepatiwa mafunzo ya uongozi,
umuhimu wa Hati miliki, UKIMWI, Sheria na jinsia.
Pia wanawake 98 wamepatiwa mafunzo juu ya mbinu
za kubaini vitendo vya udhalilishaji na kuepukana
navyo;
(d) Katika jitihada za kupiga vita udhalilishaji wa
wanawake na watoto, Nyumba Salama kwa ajili
ya kuwahifadhi na kuwahudumia waathirika wa
198
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
vitendo hivyo, imeanzishwa. Jumla ya waathirika 26
wa vitendo hivyo wamepatiwa huduma hizo; na
(e) Skuli za Benbella (Unguja) na Utaani (Pemba)
zimeteuliwa kuwa Skuli Maalumu za Sayansi kwa
Wanawake ili kuwashajiisha wanafunzi wa kike
kupenda masomo ya Sayansi na Hisabati.
133. Ili kuendeleza juhudi za kuwawezesha wanawake
kiuchumi kijamii na kisiasa, CCM katika kipindi cha (2015-
2020), itahakikisha kwamba SMZ inatekeleza yafuatazo:-
(a) Kuendelea kusimamia upatikanaji wa Haki
za Wanawake na kupiga vita mila na desturi
zinazowabagua au kudhalilisha wanawake na
kusimamia utekelezaji wa Sheria na Mikataba yote ya
Kimataifa inayohusu ustawi wa mwanamke;
(b) Kuendeleza juhudi za kuhamasisha wanawake na
kuwajengea uwezo na uthubutu ili kushiriki kikamilifu
katika mabaraza ya maamuzi ya ngazi mbalimbali za
uongozi; na
(c) Kuanzisha jumla ya vikundi vya kiuchumi 500 vya
wanawake na kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali na
mikopo ili kujiajiri wao wenyewe.
Wazee
134. Wazee ni hazina na chemchem ya busara katika jamii
kwa kuwa mchango wao katika ujenzi wa Taifa letu ni
wa kutukuka na wa kupigiwa mfano. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2010-2015), SMZ chini ya CCM
imeendeleza jududi za kuwaendeleza wazee na kupata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Jumla ya wazee 91 wameendelea kupatiwa huduma ya
makazi na mahitaji mengine muhimu katika Nyumba
za Wazee za Serikali (Unguja na Pemba). Aidha, jumla
ya wazee 149 wameendelea kupatiwa msaada wa
fedha kwa ajili ya kuweza kujikimu kimaisha kila
mwezi; na
199
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Majengo matatu ya Nyumba za Wazee Sebleni
zikiwemo nyumba mbili na ukumbi wa mikutano
yamefanyiwa matengenezo makubwa. Miundombinu
ya maji na umeme katika majengo hayo pia
yameimarishwa.
135. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itahakikisha kwamba SMZ inaendelea kuchukua hatua
thabiti za kuwatunza na kuwaendeleza wazee kwa
kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuimarisha huduma za kijamii na mahitaji muhimu
kwa wazee wanaotunzwa katika nyumba za wazee;
na
(b) Kuanzisha na kusimamia uendeshaji wa programu
maalumu ya malipo ya pensheni na huduma nyingine
muhimu kwa wazee wote wa Zanzibar zikiwemo
huduma za usafiri na matibabu bure.
Watu wenye ulemavu
136. Watu wenye ulemavu wanayo haki kwa mujibu wa Katiba
ya kutambuliwa utu wao, kuendelezwa, kuheshimiwa na
kulindwa dhidi ya vitendo vinavyoshusha utu wao ikiwemo
ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu. Kwa kutambua
uwezo mkubwa walionao watu wenye ulemavu katika
kujiendeleza na kuchangia uchumi na maendeleo ya Taifa
letu, katika kipindi cha 2010-2015, SMZ chini ya uongozi
wa CCM imewaendeleza watu wenye ulemavu ambapo
pamoja na mambo mengine imeanzisha Mfuko Maalumu
na kuupatia jumla ya Shilingi Milioni 167.6. Aidha, usajili
wa watu wenye ulemavu umefanyika katika wilaya zote
za Unguja na Pemba ili kufahamu idadi yao kwa lengo la
kuwapatia visaidizi pamoja na dawa.
137. Ili kuwaendeleza watu wenye ulemavu, katika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha
kuwa SMZ inaendeleza jitihada za kuimarisha ustawi wa
watu wenye ulemavu kwa kutekeleza yafuatayo:-
200
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa mipango na
programu mbalimbali zenye lengo la kuwaendeleza
watu wenye ulemavu na kuwapatia haki zao za
msingi bila vikwazo;
(b) Kuimarisha Mfuko wa Watu wenye Ulemavu na
kuwapatia huduma ya visaidizi pamoja na dawa bila
malipo; na
(c) Kuendeleza mafunzo na elimu kwa wazazi, walezi na
walimu juu ya makuzi ya mtoto mwenye ulemavu.
Wafanyakazi
138. Wafanyakazi wanao mchango mkubwa katika kukuza
uchumi na maendeleo ya nchi. Ili kuhakikisha kwamba
mchango wa wafanyakazi unaongezeka, katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita (2010-2015), SMZ imeendelea
kuchukua hatua za kuimarisha maslahi yao na kupata
mafanikio yafuatayo:-
(a) Sheria ya Ajira imefanyiwa mapitio na Kanuni kumi
(10) zimetayarishwa na kuanza kutumika. Kanuni hizo
zinahusu maslahi ya wanafanyakazi wa Sekta Binafsi,
usajili na utendaji kazi wa vyama vya wafanyakazi,
mikataba, likizo bila ya malipo na makundi maalumu
ya wafanyakazi. Aidha, Kanuni za Utumishi wa
Umma zimeandaliwa na kusambazwa kwa wahusika;
(b) Mashirikiano ya utatu kati ya Shirikisho la Vyama Huru
vya Wafanyakazi, Waajiri na Serikali yameimarishwa
na majadiliano ya pamoja yameendelezwa. Kwa
kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), Toleo
Maalumu la Sheria za Kazi kwa lugha nyepesi ikiwemo
Sheria ya Ajira, Sheria ya Uhusiano Kazini, Sheria ya
Usalama na Afya Kazini, Sheria ya Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii, Sheria ya Fidia na Sheria ya Usafiri Baharini
limetayarishwa na kuanza kutumika;
(c) Jumla ya wananchi 19,758 wamepatiwa ajira. Kati
yao 5,667, wameajiriwa katika Taasisi za Serikali na
201
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mashirika ya Umma na 7,256 Sekta Binafsi na 6,835
walipata ajira kupitia Vyama vya Ushirika. Aidha,
wananchi 3,400 walijiajiri wenyewe baada ya kupatiwa
mikopo na wengine 4,000 wamepata ajira zisizokuwa
za moja kwa moja;
(d) Ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira
hasa kwa vijana, Kituo Maalumu cha Kutoa Taarifa
za Soko la Ajira kimeanzishwa. Jumla ya vijana 2,473
wameorodheshwa na 1,978 kati yao wamefanikiwa
kuajiriwa nje ya nchi kupitia Kituo hicho;
(e) Maslahi ya Watumishi wa Umma yameimarishwa
kwa kuwaongezea mshahara pamoja na posho katika
mwaka 2011 na 2014; na
(f) Kwa kuzingatia Sheria ya Usalama na Afya Kazini,
Sehemu za Kazi 351 zimesajiliwa na taarifa zake
kuhifadhiwa katika daftari la usajili wa sehemu za
kazi. Aidha, taasisi 1,067 za kazi zimefanyiwa ukaguzi
(Unguja na Pemba) na kupatiwa ushauri na maelekezo
ya kisheria.
139. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itahakikisha kuwa SMZ inaendelea kuimarisha maslahi
ya wafanyakazi kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendeleza mashirikiano ya utatu kati ya Serikali,
Waajiri na Wafanyakazi kupitia chombo chao
(Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi) ili
kuimarisha mahusiano mema;
(b) Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Ajira kwa
Vijana na kuimarisha utendaji kazi katika Utumishi
wa Umma kwa kuandaa programu mbalimbali za
mafunzo na upatikanaji wa rasilimali watu wenye
sifa, kuongeza maslahi ya watumishi ili kuongeza
ufanisi na tija; na
(c) Kufanya ukaguzi katika maeneo 180 na kusajili
taasisi za kazi 140 pamoja na programu mbalimbali
zinazohusu masuala ya kazi.
202
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Hifadhi ya Jamii
140. Katika kuhakikisha kwamba huduma za Hifadhi ya Jamii
zinaimarika, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
(2010-2015), mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Jumla ya wanachama waajiri wa Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii (ZSSF) kutoka Serikali Kuu imefikia 295,
Mashirika ya Serikali 80 na Taasisi Binafsi ni 3,472.
Idadi ya wanachama waajiriwa wa Serikali Kuu ni
133,337, Mashirika ya Serikali ni 10,613;
(b) Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) umeanzisha
mfumo wa uchangiaji wa hiari ili kutoa fursa kwa
wananchi wengi zaidi kunufaika na matunda ya
Mfuko huo. Jumla ya wanachama 4,970 kutoka
vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali, ujasiriamali,
watu binafsi na Wazanzibari wanaofanyakazi nje ya
nchi wamesajiliwa chini ya mfumo huo na jumla ya
shilingi Milioni 122 zimekusanywa;
(c) Ili kutunisha mapato yake na kuongeza fursa za ajira
kwa wananchi, Mfuko umewekeza katika miradi
mbalimbali ya kiuchumi. Miongoni mwa miradi hiyo,
ni ujenzi wa Kiwanja cha kufurahishia watoto cha
Umoja – Kariakoo (Unguja) na Kiwanja cha Watoto
cha Uhuru – Tibirinzi (Pemba) pamoja na ujenzi wa
Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi
ya Zanzibar. Mfuko pia umeweza kutoa mikopo
kwa taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi. Mfuko
pia umenunua jumla ya nyumba 10 katika eneo la
Mbweni Unguja ambazo zimepangishwa kwa taasisi
za Serikali na watu binafsi; na
(d) Mfuko umeimarisha mafao ya wanachama wake
wanaostaafu kwa kuongeza kiwango cha malipo ya
kiinua mgongo na pensheni.
203
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
141. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
kitaielekeza SMZ kuimarisha zaidi huduma za Hifadhi ya
Jamii kwa kufanya mambo yafuatayo:-
(a) Kusimamia Utekelezaji wa Sera na Sheria ya Hifadhi
ya Jamii;
(b) Kuimarisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ili uendelee
kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi
inayozalisha faida kubwa na kukuza mapato ya
mfuko huo; na
(c) Kuhakikisha kwamba Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
unaendelea kuboresha malipo ya pensheni na
kuanzisha mafao mbalimbali kwa wanachama wake.
204
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA SABA
MAENEO MENGINE MUHIMU
Kuimarisha Muungano
142. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka
1964 ambao umedumu kwa kipindi cha miaka 51 sasa,
umekuwa daraja lisilotetereka la kuwafikisha Watanzania
katika azma yao ya kupata maendeleo, amani na ustawi.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuzisimamia Serikali
katika jitihada za kuimarisha Muungano kwa kutafuta
ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoukabili kwa
lengo la kudumisha amani, utulivu na maendeleo.
143. Katika kipindi cha utekelzaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kizisimamia Serikali
zake ili zitekeleze majukumu yake kikamilifu kwa lengo
kuhakikisha Muungano wetu unakuwa imara zaidi na
kwamba amani na utulivu vinaendelea kuwepo kwa
kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar;
(b) Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika
kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizokuwepo kwa
kuweka utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kutatua
changamoto zitakazojitokeza;
(c) Kuendelea kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha
uchumi katika pande mbili za Muungano hususan
katika kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo
kwa manuafaa ya pande zote; na
(d) Kuendeleza harakati za kuulinda na kuutetea
muungano kwa kuzishirikisha asasi zisizo za Serikali
kuimarisha utoaji wa elimu ya uraia mashuleni,
vyuoni na vyuo vikuu pamoja na makundi mengine.
205
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Utawala Bora na Demokrasia
144. Utawala Bora na Demokrasia ni moja ya nyenzo muhimu
katika kuhakikisha Taifa linakuwa na utawala unaozingatia
Sheria, Uwazi na Uwajibikaji ili kutoa huduma bora
kwa wananchi na kutokomeza udikteta na umasikini
katika jamii. Malengo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii
hayataweza kufikiwa iwapo haki, usawa, uwazi na
uwajibikaji vitakosekana. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010-2015), mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Uchaguzi huru na wa haki umeendelea kufanyika
katika ngazi mbalimbali za uongozi;
(b) Hatua zimeendelea kuchukuliwa katika kukuza,
kulinda na kuhifadhi Haki za Binadamu na Utawala
Bora katika jamii;
(c) Serikali zimeendelea kusimamia utekelezaji wa
Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali
kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP).
Aidha, Serikali imeandaa Rasimu ya Muswada wa
Marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma;
(d) Mfumo wa Takwimu Huria umeanzishwa ambao
utakuwa na Tovuti Kuu ya Takwimu Huria, ili
kuwezesha wananchi na wadau wengine kupata
taarifa za uendeshaji wa Serikali kwa urahisi na
kuzitumia katika shughuli na malengo mbalimbali; na
(e) Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya
umeendeshwa na umefikia hatua ya Katiba
Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu
la Katiba ambayo itapigiwa Kura ya Maoni na
wananchi;
(f) Mfumo wa Kujitathmini katika Masuala ya Utawala
Bora (APRM) umeandaliwa na umeanza kufanya kazi;
206
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Katika kupanua demokrasia, Vyama vya Siasa vyenye
usajili wa kudumu vimeongezeka kutoka 17 mwaka
2005 hadi vyama 22 mwaka 2015;
(h) Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeanza zoezi la
kusajili na kutoa vitambulisho vya uraia ambapo hadi
Machi 2015 jumla ya wananchi milioni 5 Tanzania
Bara na 600,000 Tanzania Zanzibar wameshapata
vitambulisho.
145. Ili kuendeleza Utawala Bora, Demokrasia na Uwajibikaji,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM
itahakikisha kuwa, Serikali inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kuendeleza jitihada za kukuza, kulinda na kuhifadhi
Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika ngazi
zote za uongozi;
(b) Kuifanyia mapitio Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma kwa lengo la kuiboresha na pia kutunga Sheria
mpya itakayotenganisha shughuli za uongozi wa
umma na biashara;
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ili iweze kufanya
kazi zake kwa ufanisi na pia kuanzisha Mahakama
Maalumu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi kwa lengo la kuharakisha uchunguzi na
utoaji hukumu kwa makosa hayo;
(d) Kuimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kufanya
maboresho katika utendaji wa vyombo vya maamuzi
ikiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka
na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu;
(e) Kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali ili itekeleze majukumu yake kwa
ufanisi zaidi;
(f) Kuendelea na kukamilisha zoezi la uandikishaji na
utoaji wa vitambulisho vya uraia;
207
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(g) Kukamilisha mchakato wa kutunga Katiba mpya
na kuanza kuitekeleza kwa mujibu wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba; na
(h) Kuendelea kuimarisha Mfumo wa Kujitathmini
Kiutawala Bora (APRM) na kutekeleza mapendekezo
yaliyomo katika ripoti zake za mara kwa mara;
Vyombo vya Ulinzi na Usalama
146. Kwa kutambua kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya
ulinzi na usalama katika kudumisha amani, usalama na
utulivu nchini na kwa kuzingatia umuhimu wa kuendeleza
mafanikio haya, katika kipindi cha Ilani hii (2015-2020),
CCM itazielekeza Serikali zake kuviimarisha vyombo vya
ulinzi na usalama kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kwa
kuviongezea raslimali watu na raslimali fedha kwa
kadri uchumi utakavyoruhusu.
(ii) Kuendelea kuboresha maslahi ya watendaji katika
vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo: makazi,
mafunzo na zana za kazi za kisasa.
(iii) Kuendelea kuweka mazingira yatakayowezesha
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarisha mafunzo kwa
vijana wanaojiunga kwa hiari na wale wanaojiunga
kwa mujibu wa Sheria.
(iv) Kuendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN)
na Umoja wa Afrika (AU) katika kupeleka askari wetu
kushiriki majukumu ya ulinzi wa amani kwenye nchi
mbalimbali duniani ili majeshi yetu yaendelee kupata
uzoefu na mbinu za kisasa za ulinzi wa amani.
(v) Kuendeleza na kuimarisha mpango wa ulinzi
shirikishi na kuwashirikisha wadau mbalimbali
nchini kutoa elimu kwa umma dhidi ya imani potofu
zinazosababisha mauaji ya vikongwe na watu wenye
ulemavu wa ngozi (Albino). Aidha, hatua kali na
208
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
za haraka za kisheria zitachukuliwa kwa wote
watakaobainika kujihusisha na uhalifu wa aina hii,
ujambazi na vitendo vyenye mwelekeo wa ugaidi.
(vi) Kuendelea kushirikiana na Mataifa mengine na Asasi za
Kimataifa katika kupambana na makosa yanayovuka
mipaka hasa ugaidi, uharamia, utakatishaji wa fedha
haramu (money laundering), biashara haramu ya
madawa ya kulevya na usafirishaji wa binadamu.
(vii) Kuimarisha uwezo wa vikosi vya Zimamoto na
Uokoaji kwa kuvipatia mafunzo na zana za kisasa
za kupambana na matukio ya moto, ajali na majanga
mengine ya asili.
Serikali za Mitaa
147. Serikali za Mitaa zimeundwa kwa ajili ya kupeleka
madaraka na huduma karibu na wananchi na kuhakikisha
wananchi wanashirikishwa katika uandaaji na utekelezaji
wa mipango ya maendeleo mijini na vijijini. Katika kipindi
cha 2010-2015, mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Sheria na Kanuni za uendeshaji wa Halmashauri za
Wilaya, Miji na Majiji zimefanyiwa mapitio kwa lengo
la kuboresha mifumo ya usimamizi wa mamlaka hizo;
(b) Kiwango cha ruzuku ya Serikali Kuu kinachopelekwa
katika Halmashauri zote kimeongezeka kutoka
Shilingi bilioni 950 mwaka 2010/2011 hadi Shilingi
trilioni 2.4 mwaka 2014/2015;
(c) Katika usimamizi wa matumizi sahihi ya fedha,
ukaguzi wa mara kwa mara umefanyika na hatua
za kisheria na kinidhamu dhidi ya watendaji
wa Halmashauri waliojihusisha na vitendo vya
ubadhirifu na wizi wa fedha na rasilimali za wananchi
zimeendelea kuchukuliwa.
209
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
148. Ili kuziendeleza Mamlaka za Serikali za Mitaa, katika
kipindi cha 2015-2020 ya Utekelezaji wa Ilani hii, CCM
itahakikisha kwamba, Serikali inatekeleza yafuatazo:-
(a) Kuendelea kuzifanyia mapitio Sheria zote
zinazohusiana na Serikali za Mitaa na Mamlaka ya
Tawala za Mikoa ili kuharakisha mchakato wa kugatua
madaraka kwa lengo la kuziwezesha kutoa huduma
bora zaidi kutoka ngazi ya Kitongoji/Kijiji hadi Kata;
(b) Kuendelea kuzijengea uwezo Serikali za Vijiji
kwa kuzipatia raslimali watu na fedha ili ziweze
kupanga na kusimamia kwa ukamilifu miradi yao ya
maendeleo;
(c) Kuendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kutoka
Serikali Kuu kinachopelekwa kwenye Halmashauri
zote nchini kupitia Bajeti ya Serikali ya kila mwaka
kwa kadri ya uchumi utakavyokua;
(d) Kuendelea kuzihamasisha Halmashauri zote nchini
kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani (own
sources) pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji
na udhibiti wa mapato;
(e) Kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma za
kijamii hususan afya, elimu, maji na miundombinu ya
kiuchumi katika Halmashauri zote nchini pamoja na
kuongeza idadi ya wataalamu wa fani mbalimbali; na
(f) Kuendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu na
kisheria dhidi ya watendaji wa Halmashauri za wilaya
watakaobainika kuhusika na vitendo vya ubadhirifu
na wizi wa mali ya umma pamoja na matumizi
mabaya ya madaraka.
210
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mambo ya Nje
149. Ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi yetu na nchi
nyingine duniani, Chama Cha Mapinduzi kitaihimiza
Serikali kufanya mambo yafuatayo katika kipichi cha
utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020:-
(a) Kuendelea kushiriki kwenye utengamano wa kikanda
na kuendeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kuzingatia
maslahi muhimu ya nchi yetu ili kunufaisha
Watanzania wote;
(b) Kuendelea kuimarisha uhusiano wa Tanzania na
mataifa mengine na taasisi za kimataifa;
(c) Kuendelea kupigania mfumo wa haki wa utawala,
siasa na uchumi duniani;
(d) Kuendelea kuunga mkono jitihada za kulinda amani
na utulivu duniani;
(e) Kuendelea kupigania Diplomasia ya Uchumi na Siasa;
na
(f) Kuendelea kujenga au kununua majengo kwa ajili
ya balozi za Tanzania kwenye nchi ambazo kwa sasa
yanakodishwa ili kupunguza gharama.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
150. Ili kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya
2015-2020, Chama Cha Mapinduzi kitaihimiza Serikali
kufanya mambo yafuatayo:-
(a) Kutekeleza Mpangokazi wa miaka kumi wa kuelekea
katika eneo la Sarafu moja la Afrika Mashariki;
(b) Kutekeleza ujenzi wa mitandao ya reli na barabara
zinazounganisha nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki;
211
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kuendelea na utekelezaji wa hatua za awali za
mtangamano wa Afrika Mashariki za Umoja wa
Forodha na Soko la Pamoja ili kuhakikisha Watanzania
wanaendelea kunufaika na fursa za kibiashara,
uwekezaji na ajira zitokanazo na utekelezaji wa hatua
hizo;
(d) Kuendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki ili wazitumie na kunufaika nazo; na
(e) Kuendelea na majadiliano na utekelezaji wa Ubia
wa Biashara na uwekezaji baina ya Nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki na Marekani, Mkataba wa Ubia
wa Kiuchumi kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki na Umoja wa Ulaya (EAC-EU Economic
Partnership Agreement – EPA) na Kuanzisha eneo
Huru la Biashara la Utatu wa EAC-COMESA-SADC.
Kuhamia Makao Makuu Dodoma
151. Chama Cha Mapinduzi kinatambua jitihada zilizofanywa na
Serikali za kuunganisha mji wa Dodoma na mikoa mingine
kwa njia ya barabara za lami. Aidha, baadhi ya majengo ya
Serikali yameendelea kujengwa Dodoma likiwemo jengo
la Bunge, Benki Kuu, Hazina, Chuo Kikuu cha Dodoma
na Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba kwa ajili
ya makazi ya wananchi. Katika kipindi cha utekelezaji wa
Ilani hii ya 2015-2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kutunga Sheria itakayoutambua mji wa Dodoma
kuwa Makao Makuu ya nchi;
(b) Kusimamia azma ya Serikali ya kuhakikisha majengo
yote ya Wizara za Serikali yanajengwa Dodoma badala
ya Dar es Salaam; na
(c) Kuongeza kasi ya kupima viwanja kwa ajili ya
makazi, viwanda na taasisi; na kuendelea kuboresha
miundombinu ikiwemo maji, umeme na barabara.
212
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)
Dodoma wakipima viwanja kwa kutumia vifaa vya kisasa
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
152. Kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi ni jambo muhimu katika kufikia maendeleo
endelevu. Pamoja na jitihada ambazo zimekuwa
zikichukuliwa katika kukabiliana na uchafuzi wa
mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, bado zipo
changamoto nyingi. Ili kubabiliana na changamoto hizo,
Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha Ilani hii ya
2015-2020, kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kupanga na kuendelea kutekeleza miradi ya upandaji
miti ili kuondokana na hatari ya Taifa kugeuka kuwa
213
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
jangwa kwa kuhakikisha kila Halmashauri inapanda
na kutunza miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka;
(b) Kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinaweka na
kusimamia Sheria ndogo za hifadhi ya mazingira;
(c) Kuweka utaratibu wa kuwaelimisha na kuwashirikisha
wananchi kuhusu usimamizi na utekelezaji wa Sheria
ya Utunzaji wa Maeneo ya Fukwe na rasilimali
zilizopo;
(d) Kuendelea kufanya tathmini ya vyanzo vya maji
vilivyohifadhiwa, kuongeza vyanzo vipya na kufufua
vilivyopotea ama kuharibika ili kuwa na uhakika wa
upatikanaji wa maji safi na salama;
(e) Kuweka utaratibu wa kupunguza bei ya gesi na
majiko yake na kuhamasisha jamii kutumia umeme
na nishati mbadala ili kuongeza idadi ya watumiaji
wa nishati hizo kutoka asilimia 36 mwaka 2015 hadi
asilimia 50 mwaka 2020 ili kupunguza matumizi ya
kuni na mkaa kwa lengo kupunguza kasi ya uharibifu
wa mazingira; na
(f) Kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa shughuli za
viwanda ili zisiharibu mazingira.
Kujenga uwezo wa kukabili majanga
153. Majanga ni matukio yanayojitokeza na yenye uwezo
mkubwa wa kuleta maafa yanayohatarisha maisha ya watu
na mali zao, miundombinu na huduma mbalimbali za
jamii. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020),
katika kukabiliana na maafa, Chama Cha Mapinduzi
kitazielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kusimamia kikamilifu Utekelezaji wa Sheria mpya ya
Kukabiliana na Maafa katika ngazi zote kuanzia Taifa
hadi Vijijini; na
(b) Kujenga Kituo cha Menejimenti ya Maafa na
Mawasiliano ili kuongeza uwezo wa nchi katika
kukabiliana na maafa.
214
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Mapambano Dhidi ya VVU/UKIMWI
154. Katika kipindi cha miaka mitano ya Ilani hii ya 2015-
2020, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali
zake kuendeleza kwa nguvu zaidi mapambano dhidi ya
UKIMWI kwa kutekeleza yafuatayo:-
(a) Kupunguza au kuondokana kabisa na utegemezi
wa wafadhili kwa kuanzisha Mfuko Maalumu wa
UKIMWI (AIDS Trust Fund) ukiwa na lengo la
kuongeza rasilimali kwa ajili ya kuboresha huduma
za UKIMWI zinazotolewa;
(b) Kufanya jitihada za kupunguza kasi ya maambukizi
katika jamii kutoka asilimia 5.1 mwaka 2015 hadi
asilimia 3.0 ifikapo 2020;
(c) Kuimarisha huduma za elimu ya UKIMWI kwa njia ya
mawasiliano baina ya wanafamilia, watu mashuhuri,
programu za mahali pa kazi na viongozi wa dini;
(d) Kuongeza usambazaji wa taarifa zinazohusu kubadili
tabia hatarishi na upatikanaji wa huduma bora kwa
waathirika wa UKIMWI kupitia Vyombo vya Habari;
(e) Kuendeleza tafiti za UKIMWI na kutathmini
vipaumbele kwa ajili ya kufanya maamuzi na kuandaa
programu za UKIMWI; na
(f) Kutoa elimu kwa umma juu ya uhusiano uliopo kati
ya utumiaji wa dawa za kulenya na maambukizi ya
VVU.
Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya
155. Matumizi ya madawa ya kulevya ni tatizo linaloongezeka
si hapa Tanzania tu, bali duniani kote. Madhara ya
matumizi ya madawa ya kulevya ni makubwa hususan
kwa vijana kwani yanapunguza nguvukazi ya Taifa na
kuongeza gharama za kuwatibu na kuwatunza waathirika.
Katika kipindi kijacho, Chama kitaielekeza Serikali
kuongeza jitihada za kupambana na madawa ya kulevya
kwa kutekeleza yafuatayo:-
215
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(a) Kuanzisha Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za
Kulevya;
(b) Kuongeza utoaji wa dawa na matibabu pamoja
na kuanzisha vituo vya kuhudumia wananchi
walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya;
(c) Kushirikiana na asasi za kijamii na kuziwezesha ili
kuinua uwezo wa kushiriki katika kutoa elimu juu ya
athari ya matumizi ya dawa za kulevya katika jamii
zinazowazunguka; na
(d) Kusimamia kwa ukamilifu sheria mpya ya kudhibiti
madawa ya kulevya.
Vyombo vya Habari
156. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
Sekta ya Habari imeimarishwa zaidi na kupata mafanikio
yafuatayo:-
(a) Serikali imeweka mazingira bora yaliyowezesha
kuanzishwa kwa vyombo vingi vya habari nchini;
(b) Matangazo ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC):-
(i) TBC imeendelea kuimarisha usikivu wa Radio na
Televisheni katika maeneo yenye miinuko;
(ii) TBC imefunga mitambo ya kisasa ya idhaa ya TBC
Taifa na TBC FM yenye uwezo wa kusikika kwa
ufasaha bila mikwaruzo katika mikoa mbalimbali
nchini; na
(iii) Shirika limejenga mitambo ya kurushia matangazo ya
Televisheni katika mfumo wa kidijitali katika maeneo
mbalimbali nchini.
(iv) Mitandao mingi ya kijamii imeanzishwa na kuwa
moja ya njia kuu za upashanaji wa habari kwa haraka.
216
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
157. Ili kuendeleza Tasnia ya Habari na Uhuru wa Vyombo
vya Habari, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii
ya 2015-2020, Chama kitaielekeza Serikali kuendelea
kuboresha mazingira ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
kwa kufanya mambo yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kwa
urahisi na kwa wakati kwa mujibu wa Sheria;
(b) Kuharakisha mchakato wa kupitisha na kuanza
kutekeleza Sheria kuhusu uhuru wa Wananchi kupata
habari na uhuru wa Vyombo vya Habari kupata na
kutoa habari;
(c) Kuhakikisha kwamba matangazo ya Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) yanasikika nchini kote kwa
kulipatia uwezo wa rasilimali watu, fedha na vifaa
vya kisasa;
(d) Kuimarisha uwezo wa Idara ya Habari (MAELEZO)
kama msemaji Mkuu wa Serikali;
(e) Kuanzisha Mfuko wa kuwaendeleza Wanahabari
Kitaaluma;
(f) Kuhakikisha kwamba kunakuwepo Uhuru wa
Vyombo vya Habari ili vitekeleze wajibu wake
inavyopasa kwa mujibu wa Sheria; na
(g) Kujenga ushirikiano wa Kizalendo baina ya Vyombo
vya Habari vya Umma na vya Binafsi katika kuitangaza
Tanzania nchi za nje hasa katika eneo la Vivutio vya
Utalii na kujenga Taswira ya nchi.
Utamaduni
158. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
Sekta ya Utamaduni imeendelea kuimarishwa zaidi
ambapo maeneo yote muhimu yanayohusu historia hasa
ya mapambano ya ukombozi ya nchi yetu na Kusini mwa
Afrika yameendelea kutunzwa na kutangazwa kama
vivutio vya utalii.
217
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
159. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015-2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuimarisha
na kuboresha Sekta ya Utamaduni nchini ili ichangie
kikamilifu katika kudumisha utamaduni wa Mtanzania
kwa kutekeleza mambo yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaendelezwa ndani
na nje ya nchi na kutumika kama bidhaa ya soko
na chanzo cha ajira kwa wataalamu na wapenzi wa
Kiswahili. Aidha, kupanua wigo wa misamiati na
istilahi za lugha za Kiswahili kwa kufanya utafiti wa
Lugha za Kijamii;
(b) Kuandaa Sera ya Utamaduni wa Taifa kuhusu masuala
ya Lugha ya Taifa, Filamu, Muziki, Ngoma za Asili na
Sanaa;
(c) Kusimamia Utekelezaji wa Sheria zinazohusu shughuli
za Filamu, Michezo ya Kuigiza, Muziki, Ubunifu kwa
lengo la kulinda haki na Maslahi ya Makundi hayo; na
(d) Kuhamasisha na kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi
katika kuboresha Miundombinu ya Kiutamaduni
ikiwemo ya Tasnia ya Filamu, Michezo, Sanaa ya
Muziki na Ubunifu kwa lengo kulinda haki na Maslahi
ya Makundi hayo.
Michezo
160. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
Sekta ya Michezo imeimarishwa zaidi na kupata mafanikio
yafuatayo:-
(a) Ukarabati wa miundombinu ya michezo nchini
umefanyika ukiwemo uwanja wa Uhuru (Dar es
Salaam), Nyamagana (Mwanza) na Sokoine (Mbeya);
(b) Sekta binafsi imehamasishwa ambapo kampuni
binafsi ya AZAM imeanzisha Kituo cha Michezo na
kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo;
(c) Jumla ya Vituo vya Michezo 75 vimeanzishwa
218
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kwa lengo la kuongeza fursa kwa watoto na vijana
kuonesha vipaji vyao ili viweze kutambuliwa na
kuendelezwa;
(d) Mashindano ya Michezo ya Shule za Msingi
(UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA)
imerudishwa na yanafanyika kila mwaka; na
(e) Mradi wa majaribio wa kufundisha riadha kwa watoto
(KIDS ATHLETICS) umeanzishwa na unashirikisha
shule 98 katika Mikoa minne ya Tanzania Bara na
skuli 18 za Zanzibar.
161. Katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani
hii ya 2015 – 2020, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza
Serikali kuimarisha Sekta ya Michezo ili kuinua kiwango
cha michezo nchini ikiwa ni pamoja na kuifanya Sekta
ya Michezo kutoa fursa za ajira husasan kwa vijana kwa
kutekeleza mambo yafuatayo:-
(a) Kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo
nchini;
(b) Kupanua wigo wa vyanzo endelevu vya fedha za
uendeshaji na ugharamiaji wa maendeleo ya michezo
hapa nchini kwa kuanzisha Bahati Nasibu ya Michezo;
(c) Kuhamasisha na kusisimua Maendeleo ya Michezo
katika ngazi zote hapa nchini kwa kuendeleza
matamasha ya Michezo kuanzia ngazi za Vijiji, Kata,
Wilaya, Mkoa hadi Taifa;
(d) Kuweka vivutio vya kuwavutia wawekezaji na
washiriki wengine kuwekeza na kugharamia shughuli
mbalimbali za michezo nchini;
(e) Kulinda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo
na burudani kwa kushirikiana na makundi ya
wanamichezo, jamii na mamlaka nyingine zilizopo;
(f) Kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, kuanzisha Kituo
cha Kuendeleza Vipaji vya Wanamichezo Mahiri na
219
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kutumika kama kituo cha maandalizi ya wanamichezo
wanaoiwakilisha Tanzania katika michezo ya
Kimataifa (Olympic village);
(g) Kuendelea kufundisha wataalam wa michezo na
kuhakikisha wanapatikana katika ngazi zote;
(h) Kuwahamasisha wanamichezo kujiunga na kunufaika
na fursa zitolewazo na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kwa ustawi na maisha yao ya baadaye; na
(i) Kuendeleza shughuli za michezo mashuleni ili kuibua
vipaji vya michezo mbalimbali nchini.
Tasnia ya Sanaa
162. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-2015),
Serikali imeendelea kuwatambua na kuthamini kazi za
sanaa na wasanii nchini.
163. Tasnia ya Sanaa ikiwemo filamu, muziki, michezo ya
kuigiza inayo nafasi kubwa ya kupanua soko la ajira na
kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kama ilivyo kwa
nchi nyingi duniani. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani
hii (2015-2020) Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali
yake kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuimarisha uwezo wa Bodi ya Filamu
nchini ili isimamie kwa ukamilifu maendeleo ya tasnia
ya Filamu kwa kuendeleza ujuzi katika sekta hii;
(b) Kuanzisha na kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Tasnia
ya Sanaa utakaowezesha upatikanaji wa mikopo
ya masharti nafuu kwa wazalishaji, watengenezaji,
wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo wa
tasnia hii nchini;
(c) Kuwekeza katika mradi wa Ujenzi wa Jumba
Changamani la Uzalishaji wa Filamu (Multipurpose
Filamu Complex);
220
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kuendeleza programu za Ujasiriamali kwa vijana na
makundi mbalimbali kwa kutoa ushauri, mafunzo,
mitaji na huduma za kiufundi kwa wajasiriamali walio
katika tasnia ya sanaa na kuweka msukumo mkubwa
katika maendeleo ya tasnia ya sanaa;
(e) Kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa Sekta ya
Filamu inakuwa na bidhaa zenye ubora, wataalamu
wenye weledi na kuondokana na uharamia wa bidhaa
za filamu;
(f) Kuhakiksha kazi za wasanii zinalindwa ili
zisighushiwe wala kuibiwa;
(g) Kuhakikisha wasanii wanapata maslahi wanayostahili
kutokana na kazi zao kwa kuboresha mazingira ya
kisheria;
(h) Kuweka msukumo katika kuhakikisha kwamba
shughuli na biashara za sanaa zikiwemo filamu,
muziki, ngoma za asili, michezo ya kuigiza na kazi
nyingine za ubunifu zinarasimishwa ili kuendeleza
tasnia hii na wasanii wenyewe;
(i) Kuanzisha maeneo changamani ya shughuli za
utamaduni nchini kwa kujenga miundombinu ya
kisasa;
(j) Kuweka kumbukumbu na kuhimiza matumizi ya mila
na desturi dhidi ya utandawazi kwa kufanya utafiti
wa mila na desturi za jamii ya Kitanzania; na
(k) Kuhifadhi kumbukumbu ya ushiriki na mchango wa
Tanzania katika harakati za ukombozi Kusini mwa
Afrika kwa kuendeleza utekelezaji wa Programu ya
Urithi wa Ukombozi.
221
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kuendeleza Makundi Maalum
Wazee
164. Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwaenzi wazee
kutokana na michango yao katika kulijenga Taifa letu.
165. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya
yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha wazee wanatambuliwa na kupatiwa
huduma za matibabu bila malipo;
(b) Kuhakikisha wazee wanapata haki zao za kisheria na
kupata fursa sawa katika ngazi zote;
(c) Kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili vikiwemo
mateso na mauaji;
(d) Kuwawekea miundombinu na mazingira bora
yatakayowawezesha kwenda wanapotaka na kutumia
vyombo vya usafiri wa umma kwa gharama nafuu; na
(e) Kuweka utaratibu na vigezo vitakaowezesha wazee
wote nchini kulipwa pensheni.
Watu Wenye Ulemavu
166. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba: “Binadamu
wote ni sawa na kila mtu anastahili heshima ya
kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”. Kwa imani
hii, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitazielekeza Serikali kuhakikisha kwamba:-
(a) Walemavu wote nchini wanaendelea kutambuliwa na
kulindwa na vitendo vinavyoshusha utu vikiwemo
ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu;
(b) Kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi
(albino) wanalindwa dhidi ya ukatili na ubaguzi wa
aina yoyote;
222
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(c) Kuhakikisha wanapata elimu kwa kutumia vifaa
maalumu na kushiriki katika nafasi za uwakilishi na
shughuli za kijamii;
(d) Kuwawekea miundombinu na mazingira rafiki
yatakayowawezesha kwenda wanapotaka, kutumia
vyombo vya usafiri na kupata habari;
(e) Kuboresha mahitaji maalumu ya watu wenye ulemavu
kwa kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kwa
urahisi kwa kutumia lugha ya alama, alama mguso,
maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa
au njia nyingine zinazofaa;
(f) Kuhakikisha wanapata ajira na kufanya kazi; na
(g) Kupata huduma bora za afya, uzazi salama,
marekebisho na utengemao.
Wanawake
167. Kwa kutambua kwamba wanawake wanao uwezo mkubwa
wa kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, ipo haja ya
kuendelea kuwathamini, kuwalinda na kuwaendeleza
ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa
maendeleo ya Taifa letu.
168. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuweka utaratibu wa kikatiba na kisheria
utakaowawezesha wanawake kushika nafasi sawa
(50/50) za uongozi katika vyombo vya maamuzi
katika ngazi zote;
(b) Kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za kisheria
na kupata fursa sawa katika ngazi zote;
(c) Kupata haki ya kulindwa dhidi ya ubaguzi,
udhalilishaji, dhuluma, unyanyasaji, ukatili wa
kijinsia na mila potofu; na
223
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(d) Kuhakikisha kuwa ajira za wanawake zinalindwa
wakati wa ujauzito na pale wanapojifungua.
Watoto
169. Kila mtoto ana haki ya kuishi, kukua na kulelewa kikamilifu
ili Taifa kwa siku za baadaye lipate raia wema na waadilifu.
170. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 –
2020, Chama kitaielekeza Serikali kuendelea kutekeleza
mambo yafuatayo:-
(a) Kuhakisha watoto wanalindwa dhidi ya uonevu,
ukatili, udhalilishaji, utumikishwaji na mila potofu;
(b) Kuhakikisha watoto wanapata lishe bora, huduma
ya afya, makazi na mazingira yanayomjenga kimwili,
kiakili na kimaadili;
(c) Kuwapatia haki ya kushiriki katika shughuli
zinazolingana na umri, kuhakikisha kwamba
wanapata malezi na ulinzi kutoka kwa wazazi, walezi,
jamii au mamlaka ya nchi bila ubaguzi wowote; na
(d) Kuboresha viwanja vya kuchezea watoto katika ngazi
za mitaa, vijiji na vitongoji.
Vijana
171. Vijana ni chachu ya maendeleo ya nchi katika nyanja zote
kwani ndiyo nguvu kazi ya Taifa na yenye fikra ya ubunifu
endelevu. Kwa kutambua uwezo na mchango wao jitihada
kubwa zimefanywa na Serikali katika kipindi kilichopita
kuwashirikisha vijana katika shughuli za maendeleo ya
kijamii, kiuchumi na kisiasa.
172. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii (2015-2020),
CCM itaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-
(a) Kuendelea kuwashirikisha vijana kwa kuwapa nafasi
za maamuzi katika ngazi zote kutegemeana na sifa,
weledi na uadilifu;
224
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(b) Kuwaandaa na kuwawezesha vijana kushiriki kwa
ukamilifu katika shughuli zote za Baraza la Taifa la
Vijana;
(c) Kuendelea kutoa elimu kwa vijana kwa kuwatumia
wadau mbalimbali ili kuwajenga kuwa wazalendo na
kuepuka vishawishi vitakavyowaharibia malengo yao
ya baadaye;
(d) Kuvitambua na kuviendeleza vipaji vya vijana katika
nyanja za michezo, sanaa, elimu, ubunifu na uongozi;
na
(e) Kuanzisha uraghibishi kwa vijana waweze kujiajiri
kwa kuthamini kazi nyingine za mikono na utaalamu
kama vile kilimo, ufundi, michezo, sanaa na kazi
nyingine za kitaaluma.
Wafanyakazi
173. Chama Cha Mapinduzi kwa asili yake ni chama cha
Wakulima na Wafanyakazi. Wafanyakazi kwa tafsiri pana ni
waajiriwa na waliojiajiri. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, jitihada zimeendelea kuchukuliwa ili kuboresha
maslahi ya wafanyakazi ambapo mafanikio yafuatayo
yamepatikana:-
(a) Mishahara ya Wafanyakazi:
(i) Bodi za kurekebisha mishahara katika Sekta
Binafsi zimeongezeka kutoka nane mwaka 2010
hadi 12 mwaka 2013 ambapo kima cha chini cha
mshahara katika sekta hiyo kimeongezeka mara
mbili. Aidha, nyongeza ya mwaka 2013 ya kima
cha chini cha mshahara imeongezeka kati ya
asilimia 21 hadi 65 ya viwango vya mishahara
vya mwaka 2010;
(ii) Kodi ya Mapato ya Wafanyakazi (PAYE)
imepunguzwa kutoka asilimia 18 mwaka 2005
hadi asilimia 11 mwaka 2015;
225
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Kima cha chini cha mshahara katika sekta ya
umma kimeongezeka kutoka Shilingi 65,000
mwaka 2005 hadi Shilingi 300,000 mwaka 2015;
na
(iv) Sheria za Kazi zimeendelea kufanyiwa mapitio
ili kuwawezesha wafanyakazi kujiunga katika
vyama huru vya wafanyakazi kwa hiari yao.
(b) Afya na Usalama Mahala pa Kazi:
(i) Jumla ya kaguzi 220,350 zimefanyika ikiwa
ni wastani wa kaguzi 40,000 kwa mwaka kwa
lengo la kuhakikisha waajiri wanafuata Sheria
za Kazi ipasavyo;
(ii) Jumla ya kaguzi za kawaida 26,412 na kaguzi
maalumu 53,807 kuhusiana na Afya na Usalama
kazini zimefanyika. Aidha, wafanyakazi 136,076
walipimwa afya zao ili kubaini matatizo na athari
za kiafya zitokanazo na maeneo wanayofanyia
kazi;
(iii) Maafisa 4,931 wamepatiwa mafunzo mbalimbali
kuhusu Usalama na Afya Mahali pa Kazi;
(iv) Jumla ya sehemu za kazi 5,595 zilisajiliwa na
kupewa vyeti vya usajili; na
(v) Jumla ya sehemu za kazi 398 zilipewa leseni
za kukidhi viwango vya chini vya Sheria Na. 5
ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya Mahali pa
Kazi.
(c) Migogoro Sehemu za Kazi:
(i) Migogoro 10,281 imesuluhishwa ambapo
uamuzi ulitolewa kwa migogoro 6,057 na Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA);
(ii) Wastani wa muda wa kusikiliza na kusuluhisha
migororo ya wafanyakazi umepungua kutoka
226
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
siku 30 hadi siku 12 wakati muda wa kusikiliza
na kuamua umepungua kutoka siku 90 hadi
siku 85;
(iii) Wafanyakazi wapatao 1,908,000 na waajiri 6,890
wamepewa elimu kuhusu Sheria za Kazi;
(iv) Jumla ya Mabaraza ya Wafanyakazi 265
yameundwa katika Taasisi za Umma ikiwa ni
sawa na asilimia 86.6 ya lengo;
(v) Jumla ya vyama saba vya wafanyakazi na
shirikisho moja la vyama vya wafanyakazi
vimesajiliwa kati ya mwaka 2010 na 2015 kwa
lengo la kuongeza na kuboresha wigo wa
ushiriki, majadiliano na utetezi wa haki za
wafanyakazi na waajiri katika sehemu za kazi;
(vi) Vyama vya Wafanyakazi vilivyosajiliwa
vimeongezeka kutoka vyama 24 mwaka 2009
hadi 31 mwaka 2015; na
(vii) Waajiri wameendelea kushirikisha wafanyakazi
katika hatua za maamuzi kwa lengo la kuongeza
ufanisi katika maeneo ya kazi.
(d) Sheria ya Ajira kwa Wageni:-
Sheria ya Ajira kwa wageni imetungwa mwaka 2015
na kuweka mamlaka moja ambayo ni Wizara ya
Kazi na Ajira kuwa msimamizi wa utoaji wa vibali
vya ajira kwa wageni ili kulinda ajira za Watanzania
zisichukuliwe na wageni.
(e) Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
(i) Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi
ya Jamii (SSRA) imeanzishwa mwaka 2010;
(ii) Sheria za mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii
zimefanyiwa marekabisho ili kuipa SSRA
mamlaka ya kusimamia na kudhibiti Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii;
227
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(iii) Kanuni za kukokotoa mafao ya pensheni
zimerekebishwa mwaka 2014 ili kupunguza
tofauti ya malipo ya mafao ya pensheni kwa
wanachama miongoni mwa Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii pamoja na kuanzisha mafao mapya
kwa wanachama;
(iv) Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii kupitia Sheria Na. 5 ya mwaka 2012
yameruhusu wanachama kujiunga na mfuko
wowote wanaoupenda. Aidha, marekebisho
hayo yametoa fursa kwa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii kusajili wanachama kutoka katika sekta
isiyo rasmi; na
(v) Katika mwaka 2014/2015 Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi wanaougua au kuumia kazini
umeanzishwa.
174. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali yake kuendelea kulinda
na kuboresha haki na maslahi ya wafanyakazi kwa
kufanya mambo yafuatayo:-
(a) Kuhakikisha kwamba mfanyakazi atalipwa kima cha
chini cha mshahara kinachokidhi mahitaji muhimu ya
maisha kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa Taifa;
(b) Kuwapunguzia wafanyakazi mzigo wa Kodi ya
Mapato (PAYE) kufikia tarakimu moja (single digit);
(c) Kuboresha na kulinda afya na usalama wa wafanyakazi
wakiwa sehemu za kazi;
(d) Kuridhia mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO)
yenye maslahi kwa wafanyakazi;
(e) Kuboresha mazingira ya utendaji wa wafanyakazi wa
Sekta Binafsi ikiwemo kupewa mikataba kwa mujibu
wa Sheria;
228
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(f) Kuweka utaratibu wa kupunguza pengo la mapato
kati ya wafanyakazi wa ngazi ya chini na juu;
(g) Kuhakikisha kwamba wizi, ubadhirifu, utoro na
rushwa vinakomeshwa kwa lengo la kuongeza tija
sehemu za kazi; na
(h) Kuweka utaratibu maalumu wa kutoa motisha kwa
wafanyakazi wanaofanyakazi katika mazingira
magumu.
(i) Hifadhi ya Jamii:
(i) Kuendelea kutekeleza mikakati mbalimbali kwa
lengo la kuimarisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
ili iendelee kutoa huduma bora na endelevu
kwa wanachama wao; na
(ii) Kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kuanzisha mfuko mkubwa kwa ajili ya kutoa
mikopo kwa wafanyakazi na wajasiriamali
wadogo kwa masharti nafuu.
229
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
SURA YA NANE
CHAMA CHA MAPINDUZI
175. Ilani hii ya Chama Cha Mapinduzi ya kipindi cha mwaka
2015-2020 imejikita katika kupambana na changamoto
kubwa nne ambazo ni: umaskini, ukosefu wa ajira hasa
kwa vijana, rushwa na ubadhirifu wa mali za umma; na
jukumu la kudumisha amani na utulivu. Hii ndiyo ahadi
na nadhiri kubwa ambayo Chama Cha Mapinduzi kinaweka
kwa wananchi endapo watakichagua na kuunda Serikali.
176. Kwa muktadha huo katika kipindi cha Utekelezaji wa
Ilani hii, Serikali zote mbili zitakazoundwa na CCM yaani
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, zitatumia nguvu zote na kwa kushirikisha
Sekta Binafsi zitasimamia mambo yafuatayo:-
(a) Kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi ambayo inategemewa na wananchi walio
wengi nchini;
(b) Kuweka msukumo katika uanzishaji wa viwanda vya
kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi;
(c) Kuweka mipango madhubuti ya kuwawezesha
wananchi kiuchumi na matokeo ya utekelezaji yawe
dhahiri;
(d) Urasimishaji wa raslimali za wanyonge na hasa
upimaji wa ardhi na utoaji Hatimiliki za Kimila kwa
kuweka mfumo madhubuti wa kitaasisi, kifedha na
kisheria.
(e) Kuongeza wigo wa kukusanya mapato ya ndani
yatayotosheleza Bajeti ya Serikali zetu kwa lengo
la kuendelea kupunguza utegemezi wa misaada ya
kibajeti kutoka mataifa ya nje;
230
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
(f) Kuongeza uwekezaji katika kukuza Sekta ya Sayansi
na Teknolojia ambayo ndiyo muhimili wa kuendesha
uchumi wa kisasa wenye tija;
(g) Kuboresha miundombinu ya Barabara, Reli, Bandari,
Nishati, Vyombo vya Majini na Usafiri wa Anga;
(h) Kuimarisha huduma za kijamii, hasa Elimu, Maji na
Afya;
(i) Kuimarisha usimamizi katika Sekta zinazokuwa
kwa haraka kama Utalii, Madini, Mawasiliano,
Huduma ya Fedha na Biashara; na
(j) Kuviimarisha Vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Vyombo vya Kutoa Haki, na Vyombo vya
Udhibiti na Nidhamu.
Kusimamia Utekelezaji wa Ilani
177. Wajibu wa CCM hauishii katika kutoa ahadi kwa wananchi
kupitia Ilani ya Uchaguzi na kuzikabidhi Serikali zake
kwa utekelezaji, bali pia ina wajibu mkubwa wa kufuatilia
utekelezaji wa ahadi hizo. Hivyo, ni muhimu kwa CCM
kuzingatia utaratibu iliyojiwekea wa namna ya kusimamia
na kukagua utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.
178. Tukirejea uzoefu wa miaka ya nyuma, jukumu hili la CCM
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika ngazi
mbalimbali kuanzia Vijijini hadi Taifa, limetekelezwa kwa
kiwango cha wastani, hasa katika ngazi ya Vijiji, Kata na
Majimbo.
179. Kwa utaratibu wa sasa, ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi katika ngazi ya Taifa unafanywa na Wabunge
na Wawakilishi kupitia Kamati zao za Kudumu na pia kwa
Wabunge na Wawakilishi kuwauliza maswali mawaziri
ndani ya Bunge na Baraza la Wawakilishi. Wabunge na
Wawakilishi wanaotokana na CCM wanatakiwa kutoa
taarifa za utekelezaji wa Ilani katika vikao vya CCM,
yaani kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
231
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
kupitia Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Wabunge na
Wawakilishi wote wa CCM. Utaratibu huu unatekelezwa
kwa kiwango cha kuridhisha.
180. Vikao vya Halmashauri Kuu za Wilaya, Kata, Wadi, Jimbo,
na Matawi vinapaswa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi katika maeneo hayo kupitia taarifa kutoka kwa
Wabunge na Wawakilishi wa majimbo husika, na pia kutoka
kwa Madiwani kwa upande wa ngazi ya Kata, Wadi, Jimbo
na Matawi. Katika ngazi za Kata na Matawi, utekelezaji wa
utaratibu huu ni wa wastani.
181. Katika kipindi cha Ilani hii (2015-2020), utaratibu wa vikao
vya CCM kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani kutoka
kwa wahusika utazingatiwa kwa ukamilifu. Utaratibu huu
utakiwezesha Chama Cha Mapinduzi kufanya tathmini ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika ngazi mbalimbali
kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa vikao vya
kikatiba vya CCM.
182. Njia nyingine ya kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Ilani ya
Uchaguzi unaotekelezwa na Serikali zake, ni kwa viongozi
wa CCM kutembelea miradi inayotekelezwa katika maeneo
yao ili kujiridhisha juu ya maendeleo ya utekelezaji wa
miradi hiyo. Utaratibu huu wa viongozi wa CCM wa
Matawi, Kata, Wadi na Majimbo ambako miradi mingi
ndiko iliko, utekelezaji wake bado upo chini.
183. Katika kipindi cha utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani
hii, viongozi wa ngazi zote za CCM ni muhimu wajiwekee
ratiba za kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa
katika maeneo yao. Endapo watakuta utekelezaji unahitilafu,
viongozi hao watoe taarifa haraka kwa viongozi wa Serikali
wa ngazi ya juu yao.
232
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)
akishiriki katika shughuli za kilimo katika moja ya ziara za
kukagua Uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
alizofanya katika Wilaya zote za Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano Mkuu
184. Kama ambavyo Serikali za CCM zinavyowajibika
kutekeleza maelekezo yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi ya
Chama, vile vile CCM inawajibu wa kutekeleza maelekezo
yanayotolewa na Mikutano Mikuu. Mkutano Mkuu wa
CCM wa Taifa wa mwaka 2012 ulitoa maelekezo mengi
yanayotakiwa kuzingatiwa.
Kwa hiyo, kupitia Ilani hii, CCM ina jukumu la kutekeleza
maelekezo yaliyotolewa na Mkutano Mkuu wa Taifa
mwaka 2012. Utekelezaji makini wa maelekezo hayo
utakipatia Chama Cha Mapinduzi uhai na nguvu thabiti ya
kuzisimamia Serikali zake ili zitekeleze kwa ufanisi Ilani hii.
Tukumbuke kaulimbiu isemayo; “Chama madhubuti huzaa
Serikali madhubuti”; na “Chama legelege huzaa Serikali
legelege” (…Mwongozo wa CCM wa 1981).
233
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane
185. Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM wa Taifa uliofanyika
mjini Dodoma tarehe 11-13 Novemba, mwaka 2012
ulipitisha maazimio mengi yenye umuhimu mkubwa
katika kudumisha uhai wa Chama chetu ili kiendelee kuwa
na nguvu na uhalali wa kushika dola. Baadhi ya maazimio
hayo ni kama ifuatavyo:-
(a) Kudumisha Muungano
Mkutano Mkuu wa Taifa ulielekeza kuwa hatua
ziendelee kuchukuliwa za kuuenzi na kuuimarisha
Muungano wetu wa kihisitoria wa Tanganyika na
Zanzibar wenye muundo wa Serikali mbili. Aidha,
changamoto za Muungano huu zitafutiwe majawabu
kila zinapojitokeza ili kuimarisha, kudumisha na
kuendeleza udugu, umoja na mshikamano uliopo
baina ya pande mbili za Muungano.
Katika kutelekeza azimio hili, CCM imeridhishwa
na hatua zilizochukuliwa na Serikali zote mbili
katika kusimamia mchakato wa kupata Katiba
Inayopendekezwa na ambayo hatimaye itazaa Katiba
mpya ya nchi yetu.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba
ndani ya Katiba Inayopendekezwa, kero nyingi za
Muungano zimepatiwa majawabu ya kuridhisha.
Hivyo, iwapo Katiba Inayopendekezwa itapitishwa
hapana shaka itaimarisha Muungano wetu.
(b) Uimarishaji wa Chama
Mkutano Mkuu wa Taifa ulielekeza kwamba jitihada
ziendelezwe za kujenga na kuimarisha Chama Cha
Mapinduzi, na kwamba Viongozi wa Chama wa ngazi
zote waongeze jitihada za kuwa karibu na wananchi
na kuwasemea na kuwatetea. Aidha, mikutano baina
ya Viongozi wa Chama na wananchi ya kufafanua na
kueleza mambo mbali mbali ifanyike mara kwa mara.
234
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Kwa hiyo, katika kipindi hiki viongozi wa ngazi
zote wanawajibika kufanya ziara za mara kwa mara
katika ngazi zote ili kukutana na wananchi, kusikiliza
matatizo yao na kuyatafutia majawabu.
(c) Maadili na Miiko ya Uongozi
Mkutano Mkuu wa Taifa ulikemea tabia ya baadhi
ya viongozi wa umma wanaotumia nafasi zao
kujilimbikizia mali isivyo halali hali inayosababisha
madhara makubwa ya kimaadili na kiuongozi
katika nchi yetu. Mkutano Mkuu uliiagiza Serikali
kuchukua hatua za kuondoa migongano ya kimaslahi
inayojitokeza, kwa kusimamia kwa ukamilifu
Sheria ya Miiko ya Uongozi. Pia iharakishe hatua ya
kutunga sheria itakayotenganisha mtu kuwa kiongozi
wa umma na mfanyabiashara kwa wakati mmoja.
Lengo ni kurejesha dhamira ya kuwa na viongozi
wanaoutumikia umma kwa maslahi ya umma na si
viongozi wanaotumia ofisi za umma kwa maslahi yao
binafsi.
Kwa hiyo, katika kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi
kitazitaka Serikali zake kutekeleza maagizo hayo ya
Chama kuhusu kuimarisha utekelezaji wa Sheria
ya Miiko ya Uongozi na kutunga sheria mpya
itakayotenganisha mtu kuwa kiongozi wa umma na
mfanyabiashara kwa wakati mmoja. Aidha, katika
kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza
utaratibu wa kuwafuatilia na kuwachukulia hatua
viongozi wake wanaokiuka maadili ya uongozi.
(d) Mapambano dhidi ya Rushwa
Mkutano Mkuu wa Taifa ulilaani tabia ya baadhi
ya wagombea wa uongozi kutoa rushwa nyakati za
uchaguzi, na uliagiza Halmashauri Kuu ya Taifa
kuchukua hatua kali dhidi ya watakaothibitika
kujihusisha na tabia hii. Kwa hivyo, Chama Cha
Mapinduzi kinaziagiza Kamati za Usalama na
235
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
Maadili na Kamati za Siasa za kila ngazi kuwafuatilia
kwa karibu wagombea uongozi katika maeneo yao
ili watakaobainika kutoa rushwa wachukuliwe hatua
kwa mujibu wa Kanuni za Chama na Sheria za nchi.
Kukua kwa tofauti kubwa ya kimapato katika
Jamii
186. Mkutano Mkuu wa Taifa ulibainisha tatizo na hatari ya
kukua kwa kasi pengo la mapato baina ya walionacho na
wasio nacho, na kwamba Serikali zote mbili ziliagizwa
kuchukua hatua za kurekebisha hali hii mapema kwani
ikiachwa iendelee itajenga chuki na uhasama baina ya
matabaka haya mawili na kuathiri amani, utulivu na umoja
wa Taifa letu.
Kwa hiyo, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali
zake kuchukua hatua thabiti zenye lengo la kupunguza
pengo la mapato kwa kutumia njia mbalimbali kama kuziba
mianya ya wanaokwepa kulipa kodi, kuimarisha utaratibu
wa Bima ya Afya ili iwafikie wananchi walio wengi na hasa
wanyonge, kuongeza ajira, kuwapunguzia wananchi mzigo
wa ada mbalimbali na hasa wa kipato cha chini.
Chama Kujitegemea Kimapato
187. Uendeshaji wa shughuli za Chama hutumia gharama
kubwa, hivyo moja ya vigezo vya uimara wa Chama ni
kuwa na vyanzo vya mapato vinavyotosheleza mahitaji.
Kwa kuzingatia ukweli huu, katika kipindi hiki, Chama
Cha Mapinduzi kinawaagiza viongozi katika ngazi zote
wabuni miradi itakayokiingizia Chama mapato kwa ajili ya
kugharamia shughuli za uendeshaji.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza suala la ubunifu
wa miradi ya kukiingizia Chama mapato; kwani zipo fursa
nyingi za uanzishaji miradi na kinachohitajika ni ubunifu na
uthubutu kwa kila ngazi. Kwa mfano, mikoa, wilaya, kata
na matawi wanayo majengo na viwanja vyenye Hatimiliki
236
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
UMOJA NI USHINDI
ambazo zinaweza kutumika kama dhamana ya kupata
mitaji kutoka benki ili kuanzisha miradi.
Mafunzo kwa Makada na Viongozi wa Chama
188. Mafunzo kwa makada na viongozi wa Chama ni nyenzo
muhimu katika ujenzi wa Chama na njia sahihi ya kuandaa
viongozi bora. Hivyo, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani
hii, CCM kwa kushirikiana na vyama vya kidugu itaongeza
kasi ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Makada cha Ihemi
(Iringa) na kuanzisha ujenzi wa Chuo cha Tunguu (Unguja)
kwa lengo la kutekeleza azma hiyo.
Jukumu la CCM
189. CCM ina jukumu la kufuatilia kwa karibu utekelezaji
wa Ilani hii kwa kupata taarifa za kila baada ya miezi
mitatu, na pia kwa viongozi kufanya ziara za kutembelea
miradi inayotekelezwa katika maeneo yao. Ili Chama
Cha Mapinduzi kiendelee kukubalika na kuaminiwa
na wananchi ni muhimu viongozi wake wawe karibu
na wananchi kwa kuwatembelea, kusikiliza kero zao na
kuzitafutia majawabu. Ni muhimu kabisa Chama Cha
Mapinduzi kuendelea kuwa msemaji na mtetezi mkuu wa
mwananchi na hasa wanyonge kwani kwa asili yake, CCM
ni Chama Cha Wakulima na Wafanyakazi.

4 comments:

 1. Salamu Kila moja.

  i am Mr Paul Williams binafsi mkopo Taasisi, sisi ni vyombo vya kibinafsi kutoa kila aina ya mikopo kwa watu ambao ni kifedha chini na katika mahitaji ya msaada wa kifedha, sisi kutoa mikopo kwa kiwango nafuu sana bila matatizo yoyote. kampuni yetu ni vizuri kusajiliwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa watu binafsi na kushirikiana miili katika mazingira mazuri. huduma zetu ni haraka na rahisi. kama wewe ni nia ya kupata mkopo kutoka kwetu kindly wasiliana nasi juu ya kampuni yetu email: paulwilliamsfinance@gmail.com

  kutembelea sisi leo kwa ajili ya huduma zetu za kuaminika
  Regards
  Mr Paul Williams.
  Kampuni pepe: paulwilliamsfinance@gmail.com
  Wasiliana nasi sasa.

  ReplyDelete
 2. Salamu Kila moja.

  i am Mr Paul Williams binafsi mkopo Taasisi, sisi ni vyombo vya kibinafsi kutoa kila aina ya mikopo kwa watu ambao ni kifedha chini na katika mahitaji ya msaada wa kifedha, sisi kutoa mikopo kwa kiwango nafuu sana bila matatizo yoyote. kampuni yetu ni vizuri kusajiliwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa watu binafsi na kushirikiana miili katika mazingira mazuri. huduma zetu ni haraka na rahisi. kama wewe ni nia ya kupata mkopo kutoka kwetu kindly wasiliana nasi juu ya kampuni yetu email: paulwilliamsfinance@gmail.com

  kutembelea sisi leo kwa ajili ya huduma zetu za kuaminika
  Regards
  Mr Paul Williams.
  Kampuni pepe: paulwilliamsfinance@gmail.com
  Wasiliana nasi sasa.

  ReplyDelete
 3. Samahani, Nilituma barua pepe hii kwamba alikuja kama unsolicited barua pepe katika folda ya barua taka, nataka tu kutoa taarifa kwamba Daudi Hassan Loan Limited anatoa mkopo 2% kila moja. Kama wewe ni kuangalia kwa baadhi ya fedha, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe: Pattond72@yahoo.com
  Kukamilisha na kurudi ...
  jina:
  nchi:
  Simu ya nambari ya simu:
  Kiasi mkopo:
  Loan Muda:
  Tafadhali usibofye kujibu barua pepe hii, lakini kutuma majibu yote kwa anwani hii ya barua pepe: Pattond72@yahoo.com

  ReplyDelete
 4. Ndugu Wanaotafuta Mkopo

  Wewe katika matatizo yoyote ya fedha? Je, unataka kuanza biashara yako mwenyewe? Hii kampuni ya mkopo ilianzishwa Mashirika ya haki za binadamu duniani kote kwa madhumuni ya kusaidia maskini na watu wenye matatizo ya kifedha ya maisha. Kama unataka kuomba mkopo, kupata nyuma sisi na maelezo hapa chini ya barua pepe: elenanino0007@gmail.com

  jina:
  kiasi mkopo inahitajika:
  Mkopo Muda:
  Namba ya simu ya mkononi:

  Asante na Mungu awabariki
  kujiamini
  Bi Elena

  ReplyDelete