HABARI

 

Saturday, September 14, 2013

KINANA AWASILI SIMIYU LEO

0 Comments
 Wakazi wa kijiji cha Wigelekelo kata ya Masela wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye mkoa huo ikiwa sehemu ya ziara yake inayoanza leo wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Kinana akivishwa skavu na Chipukizi wa CCM baada ya kuwsili Simiyu
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Isanga baada ya kuzindua shina la Muungano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuchanganya mchanga kwa ajili ya kufyatulia matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha N'hami wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha N'hami wilaya ya Maswa  mkoa wa Simiyu.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya N'humi,wilaya ya Maswa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofali kushiriki na fundi kujenga zahanati ya kijiji cha N'humi wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
 Zahanati ya kijiji cha N'humi kama inavyoonekana picha, ujenzi bado unaendelea.
 Balozi wa Shina la Kumalija namba 2 lililoanzishwa mwaka 1983 kata ya Nyakikungu Mzee Elias Sai akimkaribisha Katibu Mkuuwa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika Shina lake ,wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akiwakwenye picha ya pamoja na wanachama wa shina la Kumalija namba 2 kata ya Nyakikungu baada ya Katibu Mkuu kuwatembelea kwenye shina hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM akibadilisha mawazo na balozi wa Shina namba 2 la Kumalija kata ya Nyakikungu Mzee Elias Sai na mwanachama wa shina hilo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana mawazo na vijana wa shina la Ndilizu ambalo kihistoria limeanza mwaka 1977.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na bibi Helena Makeja ambaye ni mke wa Muasisi wa Shina la Ndilizu marehemu Ndilizu , Katibu Mkuu ameanza ziara yake katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

0 Comments:

Post a Comment