HABARI

 

Sunday, September 15, 2013

CHADEMA, CUF NA NCCR-Mageuzi SASA WAMUOMBA RAIS KIKWETE ASISAINI MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA WA 2013

1 Comments
DAR ES SALAAM, Tanzania
VYAMA vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi vimemuomba Rais Jakaya Kikwete asiusaini muswada wa mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, ulipitishwa na bunge hivi karibuni kwa madai kwamba una mapungufu.

Vimemuomba Rais kuurejesha muswadabungeni ili ufanyiwe marekebisho ambayo viongozi wa vyama hivyo wamedai ndiyo yatakuwa yenye kujenga na kuaminiana.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni kushinimkiza matakwa ya vyama vyao, viongozi hao wamesema vyama hivyo vinaanza kuunganisha umma kufanya maamuzi waliyoyaita ya kuunusuru mchakato huo wa katiba kwa kufanya mikutano nchini mzima  kwa kuanzia utakaofanyika Jumamosi ijayo Viwanja vya Jangwani, mjini Dar es Salaam.

Akitoa tamko la vyama hivyo leo mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema vyama hivyo vinadhani muswaada huo una mapungufu hivyo wanamuomba Rais Kikwete asiusaini na aurejeshe bungeni.

Alisema vyama vyao vimeamua kuunda ushirikiano na kuweka pembeni tofauti zao ili kuunganisha nguvu za pamoja kuunusuru mchakato huo wa katiba kwa kile alichokiita maslahi ya taifa.

Profesa Lipumba alisema vyama hivyo vinalaani vilivyokiita ukiukwaji wa kanuni za bunge ambao vinadai ulifanywa wa kuingiza vifungu vipya kinyemela.

Kwa mujibu wa Lipumba, vyama hivyo vinahisi nguvu za wananchi, wadau zinapaswa kuunganishwa kuunusuru mchakato huo.

Naye, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akismama kuunga mkono tamko hilo alisema kusema wataidai Katiba mpya kwa gharama yoyote na wataitafuta kwa njia yoyote licha ya kwamba hakufafanua zaidi.

Alisema katika hoja ya kupata katiba mpya wako tayari kufanya kazi na mtu yoyote.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia naye aliunga mkono tamko lao, akisema, naye pia anatambua kwamba vyma vyao vina tofauti kubwa za kitikadi lakini vinaungana kwa ajili ya hilo la Katiba.

Mape mwandishi wetu alitaka kujua kwamba ikiwa vyama hivyo vinakiri kuwa na tofauti je, vitawezaje kuhakikisha mchakato katika muungano wao huo unafika mbali na wanatambua hasa tofauti zao ni nini?

Wakijibu kwa nyakati tofauti, Lipumba, Mbowe na Mbatia walieleza tu kwamba tofauti zilizopo baina ya vyama hivyo ni itikadi na si vinginevyo.

Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wa kawaida, viongozi wa vyama hivyo walikutana na wahariri katika chumba kile kile cha awali na baada ya kuwa na mazungumzo ya takribani dakika 20, walipata nao chakula cha mchana.

1 Comments:

POSITIVE MIND said...

wasitoe majibu mepesi kwa maswali magumu wabainishe tofauti zao

Post a Comment