HABARI

 

Sunday, October 21, 2012

SOHIA SIMBA KURA 716, ANNE KILANGO KURA 310

0 Comments

DODOMA, TANZANIA
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) jana ulikamilisha uchaguzi wake mkuu ambao Mwenyekiti wa zamani Sophia Simba akitangazwa kuwa mshindi kwa kura 716 huku Anne kilango aliyedhaniwa kutoa ushindani mkali akipata kura 310 tu.

Akitangaza matokeo hayo jana saa 7.30 usiku, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Abrahman Kinana alisema mgombea mwingine wa nafasi hiyo Mayrose Majige alipata kura 7.

Baada ya kutangazwa mshindi Sophia Simba alisema uchaguzi huo ulikuwa mgumu lakini wanawake wamekubali kuumpa tena uongozi wa kuongoza Jumuiya hiyo kwa miaka mingine mitano.

Mwenyekiti huyo mpya alihaidi kufanya kazi zake kwa bidii ili kuhakikisha kuwa Jumuiya hiyo inafikia malengo yake.

Hata hivyo aliwataka viongozi wengine hadi wa ngazi za kata kuhakikisha kuwa nao wanajituma kufanya kazi zao katika kuwatetea wanawake.

“Kazi ya kuendelea jumuiya sitaiweza kuifanya pekee yangu bila nyinyi kunisaidia katika kutekeleza majukumu yenu nawaoomba sana kila mmoja kutekeleza wajibu wake ili kuifikisha jumuiya yetu pale tulipotaka ifike’’

Akizungumzia uchaguzi huo msimamizi Kinana alisema pamoja na uchaguzi huo kuwa mgumu kutokana na umuhimu wake lakini waliweza kukamilisha kama ulivyo pangwa.

Kwa upande mwingine akizungumza kabla ya kujiudhuru uenyekiti wa muda wa mkutano huo Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka alisema Jumuiya hiyo ina kakzi kubwa katika kuhakikisha kuwa mauaji ya wanawake vikongwe yanakomeshwa.

Tibaijuka alisema mauaji hayo ya vikongwe kwa taifa ni aibu na ni lazima UWT kuhakikisha kuwa yanaisha haraka ezekanavyo.

“Bado wanawake wengi wanauwawa hovyo na hasa wakina mama kutokana na sababu mbalimbali ambazo hazina msingi hii ni moja ya kazi ya UWT kuhakikisha kuwa wanamaliza tatizo hilo’’ alisema.

Kwa upande wake mgombea Mayrose akishukuru alisema  mamamuzi yaliyofanyika juu ya kumpata Mwenyekiti ni dhati.

Alisema yeye binafsi hana kinyongo na na uchaguzi huo na yupo tayari kushirikiana na Mwenyekiti mpya wakati wowote akihitajika.

Kwa upande wa mgombea Anne Kilango ambaye hakuwepo Mwenyekiti Tibaijuka alisema mgombea huyo alipata msiba wa kaka yake na hivyo hakuweza kuendelea kuwepo wakati wakitoa shukrani hizo.

“ Mgombea wetu anne kilango hakuweza kuwa nasi mida hii kutokana na kupata msiba wa kaka yake na hivyo ameondoka mara baada ya kupiga kura’’ alisema .

 Hata hivyo mkutano huo mkuu wa nane pamoja na mambo mengine ulichagua wawakilishi wa Jumuiya hiyo kwenda katika Jumuiya nyingine ikiwemo ya vijana na wazazi.

0 Comments:

Post a Comment