Siku
ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la
Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya
Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.
Tumezungumza kuhusu
changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata
na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama
na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.
Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na
mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate
thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.
Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama.
Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya
yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda
maana ‘kernel’ yake ina mafuta. Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe Nani anajua matumizi ya Mihama?
IMETAYARISHWA NA DJ SEK BLOG
P.O.BOX
Dar es salaam
IT DEPARTMENT
0 Comments:
Post a Comment