Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina ambaye amewasili mjini Dar es Salaam mchana wa leo, Ijumaa, Desemba 14 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rajoelina, amelakiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na kuwa na mazungumzo, Ikulu.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi wa SADC uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar es Salaam. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana alithibitisha kuwa amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani. Pichani, Rais Kikwete akiwa na mgeni wake, Ikulu (PICHA NA IKULU
0 Comments:
Post a Comment