HABARI

 

Saturday, August 4, 2012

WAZIRI: CCM NI NGANGARI

0 Comments
ZANZIBAR, TANZANIA
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mansoor Yussuf Himid amesema Chama Cha Mapinduzi kina mwelekeo, viongozi wake wana uwezo wa kuvumiliana na kupima mabadiliko ya nyakati.

Mansoor alitoa matamshi hay oleo wakati akichangia hoja kwenye semina ya mjadala wa mchakato wa ukusanyaji maaoni ya uundwaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muugano Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Mbweni.

Alisema imani yake itabaki ndani ya CCM kinachotokana na vyama vya ASP na TANU na wala haitavia ila anachokihitaji ni kuona Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si ule uliosheni malalamiko ila wenye tija, usawa na haki .

“Ninakiheshimu sana chama changu,ninakipenda,ndicho kilichonilea , bado ni imara sana ,kuna watu wanataka kukichafua, kufika kwetu hapa ni kutokana na utashi wa viongozi wake kuwa na dira na uvumilivu” Alisema

Katika maelezo yake , Mansoor alisema bado ataendelea kuwa muumini wa mfumo wa Serikali mbili chini ya mkataba na si kama ilivyo sasa ili kuipa fursa zaidi Zanzibar kujijenga na kujitegemea kiuchumi.

Alisema si dhambi Zanzibar na Tanganyika  chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zote zikawa na viti viwili katika Umoja wa Mataifa na kuhemea fursa za kiuchumi kwa wananchi wake.

Alieleza kuwa kuna baadhi ya viongozi kwa malengo yao binafsi  wanajaribu kuwajengea hofu wenzao na kuwazuia ili wasitoe maoni yao kwa upana kama raia huru kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Aliongeza kusema kuwa hajawahi hata mara moja kukataa Muungano usiwepo ila mara zote amekuwa akihimiza mabadiliko ya kimfumo katika Muungano huo na kwamba anaamini kuwa  kufanya hivyo si uadui na usaliti.

“Hata NEC ya CCM ilipoanzisha mchakato wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kulienezwa hofu kila mahali ,nashukuru tumefanikiwa kuunda GNU, sasa imesimama na kusomga mbele, kila mmoja anaona fahari, faida na tija ya jambo hilo ” Alisema Mansoor

Alisema awali jambo hilo likiibuliwa na Rais Jakaya Kikwwte kulikuwa na mtazamo hasi kwa baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakiamini kuwa kuundwa kwa GNU kungetoa mwanya wa kuwarejesha watawala waliopinduliwa Januari 12 mwaka 1964, kuporwa ardhi na kulipiziana visasi.

“Hata wenzetu wa CUF kabla ya GNU walikuwa wakipinga kila kitu kizuri cha SMZ ,baada ya kushirikishwa Serikalini hata yale walivyokuwa wakivipinga wakati ule sasa wanayaunga mkono, kuyasimamia na kuyashangilia”Alisema

Akizungumzia umuhimu wa dhana ya  Muungano ulioasisiwa April 26 mwaka 1964 , Mansoor alisema hapendi Muungano huo uvunjike ila mara zote amekuwa akitaka hoja na haja ya Muungano huo kufanyiwa marekebishoya msingi utakaokuwa chini ya mkataba.

Waziri huyo wa SMZ ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM ,alioongeza kusema kuwa ikiwa kuelezea hayo atahesabiwa na chama chake kwamba ametenda dhambi atakuwa tayari kukabiliana na  adhabu yeyote .

“Niko tayari kuadhibiwa kwa kutoa maoni ninayoyaamini kama ni  consructive , nafikiri nimetumia haki yangu ya kikatiba na kiraia, nataka Zanzibar iwe nyenzo zake za kiuchumi kwa maendeleo ya watu wake,sijali na wala sitawasiliza wanaoenezamaneno ya uzushi ”Aliongeza Mansoor

Aidha Mansoor alisema kila mzanzibari anayo haki ya kutoa maoni yake bila ya mtu mmoja kuzuuia utashi na matakwa ya mwenzake huku akisisitiza kuwa hiyo ndiyo demokrasia anayoijua yeye ndani ya chama chake.

0 Comments:

Post a Comment